Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

bungeeeeeee.jpg

WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.

Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.

Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.

Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.

Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."

Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.

Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.

"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.

Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.

Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.

Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.

Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.

Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.

"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.

Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."

Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hivi karibuni.

Source: Nipashe
Hawa wabunge wanaolalamika wengi wao wanamiliki fulana za"UKAWA katika ubora wao"
 
Ni kweli mkuu.

Hayo ndio matatizo ya vyeo vya kupewa, lazima utoe ushirikiano vinginevyo unapigwa pending tu...
Hii nchi haikuandaliwa kuwa na Rais ndiyo maana tunaona kunakuwa na maamuzi ya kukurupuka kila sehemu ili kumridhisha mukula
 
Naomba ile picha wakati naibu spika anamkabidhi muheshimiwa ile hundi
 
Na bado wawakilishi nao watadai mgawo wa fedha za shrehe ya muungano.
 
Hivi Bunge linarushaje fedha serikalini, tafsiri yake nini? Kwamba Bunge lina fedha nyingi kiasi kwamba hawana pa kuzitumia kuimarisha ufanisi wa Bunge, wameshindwa kuonesha shughuli za Bunge kwa wananchi halafu wanarudisha fedha serikalini kununua madawati wakati wizara yenye dhamana ipo. Watanzania tuache kuwa mabwe.ge Tukiendekeza vitu vya aina hii vya Mhimili mwingine kujipendekeza kwa muhimili mwingine au muhimili mwingine kuingilia muhimili mwingine itafika mahali kutakuwa hakuta mgawanyo wa madaraka kati ya hii mihimili mitatu na ni hatari sana kwa democrasia ya nchi.
 
Wabunge wanataka kurudisha hela zao walizozipotezea kwenye kampeni. wanataka waende study tours ulaya zisizo na tija kwa wananchi zaidi ya wao kupiga perdiem tu
 
yan huwa swala la fedha na kulilia matumbo! hakuna mbunge mzalendo hata mmoja! hayupoo! Wabunge huu uongozi ni tofauti sana mlikula sana pesa sasa ni zamu yenu kutulia majimboni mwenu! hakuna kuangalia nyumba ulaya wala wapi! Achen mafawati yatengenezwe!..mnalia kabisa hahahahaaaa AIBU
 
pic+mps.jpg

WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.

Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.

Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.

Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.

Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."

Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.

Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.

"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.

Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.

Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.

Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.

Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.

Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.

"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.

Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."

Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hivi karibuni.

Source: Nipashe
nikweli tuunge

nikweli tuunge kubana matmizi
 
Wabunge wengine wao alimradi wajitie kukosoa ili waonekane...ivi hatuoni aibu watoto mashuleni wanakaa chini wao wanajizungusha kwenye maviti yakifahari huku wakibeza jitihada za kuongeza madawati. Verry sad,ivi hawa ndiyo gold au iron...
 
Msigwa analalamika kuwa wabunge wameshindwa kusafiri nje ya nchi kwenda kuangalia balozi? Kila mwaka wamekuwa wanasafiri kuangalia kitu hicho hicho, nchi imepata faida gani? Na kwa 'akili kubwa' ya Msigwa bora wabunge wapande ndege kwenda kushangaa majengo Ulaya kuliko watoto kukaa kwenye madawati? Naomba kuuliza kwenye jimbo la huyo mchungaji shida kubwa waliyonayo wananchi ni wabunge kutokwenda Ulaya?

Bunge limekuwa ni chanzo cha umaskini nchi hii.
 
Hii ni moja wapo ya mbinu za wabunge kushinikiza bunge lirushwe live kwa minajili ya kuuza sura, wameona sasa hailipi kukaa bila kuonekana live, wameanza kuzusha mijadala ili tung'an'anie lioneshwe live kwa mgongo wa kutaka kujua kinachojadiliwa bungeni kumbe ni kwa faida zao binafsi za kujiongezea umaarufu
 
Ukiwa mwana ccm lazima uwe kichaa
Ukiwa CHADEMA sharti uwe na tabia kama wewe...Msigwa anataka kwenda nje ya nchi kuangalia nyumba za mabalozi hahahaha si aende tu kwa mshahara ama kweli wabunge wa CHADEMA ni wa ajabu.
 
Back
Top Bottom