Wabunge wacharuka! - Uwekezaji siyo kuuza nchi

Hapo sasa tusubili mnamo saa 10 jioni tusikilize bajeti inalipi jipya....kama ni usanii ule ule au lah 'MAISHA MAGUMU KWA MTANZANIA.'
 
Watu wengine mnashangaza! how far are you sure kwamba wabunge walikwenda bila taarifa. Halafu unaposema kwamba watawasumbua wageni waliomo humo hotelini, inamaana hao wabunge wangeonana na huyo bwana kwenye vyumba vya wageni au kwenye ofisi. Watanzania ni watu wa ajabu, wabunge wasipo fuatilia vitu kama hivyo mnasema, ooh tume wapa kula zetu kwenda kukaa bungeni tu na kupata posho sasa wameamua kufanya kazi, ooh wanakwenda bila utaratibu na suti ambazo hazija nyoshwa(matusi) wewe ni mtanzania kweli unaye sema hivyo una masilahi gani pale VIP htl
 
Mutu akishawekeza ni private matter ,hamuwezi kwa kuwa ni wabunge tu mtoke na makoti yenu hata hayajapigwa pasi mtokako mkaingilie sehemu ambayo mtu amewekeza kwa fedha yake ,kuna kitu ni private na kama hiyo ni hoteli basi muwekezaji atakuwa yupo katika mstari na pengine hata nyie mnaotaka kwenda huko akiwemo Raisi hamtoweza kwenda bila ya mipango maalumu,kwani jukumu la usalama na amani ni la huyo muwekezaji ,mpeni taarifa mnaedna saa ngapi,mtakuwepo huko kwa muda gani ,je mtataka muandaliwe chakula mtalipa ,mtalipiwa au muandaliwe free.
Haiwezekani kabisa na si sheria na mnaweza kuitia serikali hasara ikiwa muwekazaji atakuwa na wanasheria wajanja ambao uzembe kama huo uliofanywa na kina Cheo na wenzake kujipeleka kichwa kichwa wanaweza wakautumia na kuomba walipwe fidia.
Katika suite kama hizi ambazo zinakuwa well secured si sehemu za kwenda tu kwa kuwa wewe au nyinyi ni wabunge mukusanyane huko eti mnaenda kuangalia shughuli zinaendeleaji ,hizi si shughuli zenu mmeshakatiwa chenu kaeni pembeni mnataka kwenda pelekeni taarifa msubiri majibu yaani mlifikiri mnaenda kutembelea soko la kariakoo ,hivi atoke mlala hoi na kulekea kwenye jengo la bunge mtamruhusu ? maana hao wabunge amewachagua yeye na wanamuwakilisha yeye na kinachojadiliwa hapo ni kwa ajili yake ,hivi atapata ruhusa ya kuingia ndani na kuangalia shughuli za bunge na wabunge wanavyojadiliana.
Nafikiri hawa wabunge wanahitaji elimu juu ya nini maana uwekezaji naamini kabisa hata Raisi hawezi kwenda hapo bila ya taarifa seuze hawa wabunge masikini za Mungu wanaotoka vijijini hawakuelewa kama kuna mipaka ya kazi zao na sio kuenda popote tu kwa kuwa yeye ni mbunge ,haiwezekani hilo wamefanya ni kosa,na nyie mnaolalamika kuwa wazalendo wanatimuliwa ni lazima watimuliwe kwani hilo eneo limeshakodishwa sasa wao wadai feza inayopatikana huko,mikataba ilitiwa saini huko , wenyewe wanasema na kuandika ,NO TRACE PASSING. yaani mtu akishaweka kibao hicho basi ana haki hata ya kukupiga risasi ujinga ni wako kwa nini hukuenda shule ,waelimisheni wenzenu huko vijijini sio mnakimbilia kuwekeza tu ,halafu mnataka mkate mbuga ,mbona ukikatiza kwenye kambi za jeshi unapelkwa mchura ,naona kuna elimu inahitajika.
Kuna mmoja nimemshangaa amesema kwa nini hawa wabunge hawakutumia power zao ,mbona mimi sijaziona hizo power zao toka liundwe hili Bunge la Tanzania ,nasikia wanaweza kuweka shilingi mbona sijaona na miswada mibovu inapita kila siku tusidanganyane power zao labda kwa mimi mlala hoi wanaweza wakaniitia polisi na kunifunga lakini sio hapo ,huyo mzungu yupo juu ya sheria na wangelijidai kutumia nguvu basi ungesikia jamaa anadai bilioni nyingine anaidai serikali ,serikali itabidi ilipe na fungu jingine anapewa Cheyo.
Kwamba na usomi wao wote wabunge walikurupuka tu hawa kutoa taarifa yoyote, sidhani, msimtete huyo jamaa ni jeuli, na anajua jeuli anaitoa wapi. Wanapo kuja wanakuja mikona nyuma wakishapewa wanagalambuka wanakuwa si waungwana tena. Ndiya maana Mgabe aliwatimua kwa ajili ya mambo kama haya haya.
 
Wakachunguze nini hotelini? Mbona wanachagua kwenye neema tu? Kazi ya kuchungua si ya wabunge, kuna vyombo vinavyotakiwa kufanya hivyo. Kama wana wasiwasi (umesema WANAFUATILIA) na jambo waeleze bayana lakini wasijifanye kuwa wanaenda kuchunguza. Hizi zilikuwa nyenzo za kutafutia ulaji hapo zamani kwenye mashirika ya umma. Sio sasa. Kuna mambo mengi yenye umuhimu zaidi kuliko kukarimiwa hawa waheshimiwa kwenye hizo hoteli. Wasimame kidede kuhakikisha kuwa hatupotezi heritage yetu na si kwenda after the fact kutaka kusumbua watu!

I am not impressed.
 
Loliondo, Vitalu vya uwindaji, VIP hotel, Jim Sinclair ,Buzwagi,Richmond,IPTL,EPA,Kiwira Coal Mine.....................Its boring now.
 
Naye Mbunge wa Kwamtipura, Bw. Zuberi Ali Maulid (CCM), alisema: "Tulipotaka kwenda katika hoteli hiyo, tuliambiwa kwamba mwenyewe amekataa kwamba wageni wake hawataki usumbufu, hao watu walitoka katika sayari gani, Jupiter au Saturn?.
Source: Majira

Mh Zuberi nawe ubunge wako ni wa kutoka sayari gani? Mars au Pluto?
 
Kuna mambo mengi kama watanzania tulio wengi tunatakiwa tujifunze. Dunia imebadilika tena sio mabadiliko madogo big big changes. Na kama hatutaweza kukubali kuna mabadiliko huo ndio utakuwa mwisho wetu. Huwezi kwenda kwa mtu bila kumpa taarifa hata kwangu sio vizuri uje ujimwage tu let the muhusika know!

Kama hawa wabunge hawakutoa taarifa sioni haja ya wao kulalamika! halafu eti wanafika bungeni na kuanaza kuulizana anaoata wapi kiburi wakati wanajua wazi kabisa nani anampa huyu bwana kiburi. ni mara ngapi JK amekwenda huko na kuacha kutumia gari lake akapanda lile la huyu mwekezaji. Wananchi wa mugumu wako barabarani wanapungia gari lenye dereva kumbe msanii wao yupo anafanya usanii wake kwenye gari ya mwekezaji. Kama sijakosea mwaka jana alimpa JK tuzo huko Marekani something to do with conservation. correct me if am wrong.
 
TUmeshauza kila kitu, hata hati miliki ya nchi si ya kwetu tea, tunaishi kwa kupangisha katika ardhi ya wenye pesa. Ngojeni Ukimwi utumalize ili wenye mali warudi kwenye ardhi yenye rutuba mpya!
 
TUmeshauza kila kitu, hata hati miliki ya nchi si ya kwetu tea, tunaishi kwa kupangisha katika ardhi ya wenye pesa. Ngojeni Ukimwi utumalize ili wenye mali warudi kwenye ardhi yenye rutuba mpya![/QUOTE]

Mkuu Rev,kwenye hiyo quote,imenitia majonzi sana,kwani ndiyo ukweli wenyewe huo!.Wala serikali yetu haijishughulishi na chochote juu ya gonjwa hili linalotumaliza!.Hapo ninamaanisha kuwa tumekuwa wategemezi mno wa kila kitu kutoka kwa wazungu.jamani tunashindwa hata kuwa serious na maisha yetu wenyewe!,sembuse mzungu.

ahsante mkuu,inauma sana
 
Kwamba na usomi wao wote wabunge walikurupuka tu hawa kutoa taarifa yoyote, sidhani, msimtete huyo jamaa ni jeuli, na anajua jeuli anaitoa wapi. Wanapo kuja wanakuja mikona nyuma wakishapewa wanagalambuka wanakuwa si waungwana tena. Ndiya maana Mgabe aliwatimua kwa ajili ya mambo kama haya haya.

Hapana ndugu tusiwe wa shamba na mambo ya watu,kwa kufuata jazba ,jambo la muhimu si kwenda kujidai mnataka kuchunguza au kutazama kinachoendelea ,hivi tuwaulize hao wabunge kama ifuatavyo :-

i) Walitaka kwenda huko kwa misingi gani ?

ii) Hiyo hoteli haikushuka hapo kama nyota iliyoanguka ,walikuwa wapi ,kama unakumbuka Muungwana alihoji juzi ,mnakuwa wapi wakati watu wanaaza kufyeka ,kuchimba msingi na kuezeka mpaka wanafikia kuhamia,ndio mnakurupuka kutaka kuwavunjia majumba eti hawakufuata sheria ? Muungwana alilenga mbaali sana ,hivyo kaeni chonjo saa mbaya.

iii) Kama mnaona uwekezaji huwo ulikuwa na mizengwe basi wabunge sio kazi yao kwenda huko hotelini kutaka kuchunguza kinachoendelea ,hivi wameona wapi mfumo wa aina hii ?

iv) Labda kwa lugha ya sasa wameona kuna rushwa imetendeka (katika biashara za mabilioni kipo kiwango fulani anapewa anaeifanikisha dili ) ,hata hivyo wabunge hao kama wangetaka kujua njia zilizotumika kumpata muekazaji huyo na ni namna gani alifanikiwa na kuruhusiwa kupewa eneo ambalo ni mali ya asili basi wakukamatwa ukosi ili aeleze stori yote hiyo ni Waziri husika ,Je wabunge wamewahi kuhoji ?

v ) Unajua Maraisi mawaziri huwa wanasafiri nchi za nje na balozi zetu nazo ziko nje zikituwakilisha, sasa kuna watu ambao huwa wanabuni namna ya kuekeza fedha aliyokuwa nayo ,watu wetu hawa viongozi akiwemo raisi wanaposafiri nchi za nje hupata nafasi ya kuzungumza na watu waliojaaliwa kuwa na vijisenti ,hapo huwa wanabadilishana mawazo na wenye vijisenti hivyo hupata nafasi ya kuwakilisha mbinu au njia ambazo anahisi zitazidi kumpatia vijisenti na moja ni hiyo ya kuulizia au kuwakilisha kitu ambazo angependa kuekeza kwa hao viongozi wetu ,aidha mtu anaweza kumwita pembeni kiongozi au kumualika ili ampe mawazo yake kwa kuogopa kuzitoa mbele ya wengine kunawaweza kuhatarisha mpango wake huo na kunyakuliwa na walio mzidi nguvu.
Nchi yetuimeruhusu uwekezaji ,na jamaa amejaribu kuulizia kama ataweza kuekeza katika mbuga za wanyama ,bila ya shaka amejibiwa inawezekana ,kilichofuata ni dili ya mapato ambayo Tanzania kama ni mhusika mkuu au mwenye kumiliki sehemu hiyo atafadika vipi ? hapo ndio penye mchezo ambao muekezaji yeye haumhusu zaidi ya kukubali au kukataa mapendekezo aliyoletewa na Serikali ,kumbukeni hii au hizi sio hesabu za tenda kama ile ya umeme ,hapa ni mtu ambae alisecure uwekezaji katika mbuga na kutaka eneo la mraba kwa kiasi fulani cha mitamraba au mstatili.
Sasa tukirudi kwenye mahesabu ndio serikali iwajibike(Waziri) kulieleza bunge mahesabu hayo yalifikiwa vipi ukilinganisha na mahoteli ya kitalii yaliyomo ndani ya mbuga hizo ,kwa ufupi makisio na muda wa ukodishwaji ,je serikali itakuwa share holder ,au watalipwa kwa ujazo wa asilimia fulani.
La muhimu hesabu hizi zitakuwa zikipitiwa kila baada ya miaka mingapi ,pia siku hizi kuna aina ya ukodishaji ambao unamkodisha mtu kwa miaka kama 50 au mia na akimaliza ,anahama au mnapnga na kuingia nae mkataba upya.

Wabunge hamjakuwa na sababu kuzuka huko na makoti yenu ,haya mambo yanaenda kisheria tena kama mlikuwa makini zipo sheria za kimataifa ambazo zinajulikana kwenye vifungu vya UN. Kilichotokea Zimbabwe huwezi kulinganisha na hapa unaweza kulinganisha na Zanzibar ambako baada ya Mapinduzi waligawana mashamba na majumba yaliokuwa yakimilikiwa na waarabu au watu wakaribu yao ,mbona mashamba yamewashinda na majumba yanaporomoka kila ufikapo msimu wa mvua.
Hivyo kila jambo na mipango yake ,unaweza kusema mnyamwezi anaweza kulima ekari nyingi tu za shamba na akazitunza vizuri na akafanikiwa kuvuna mazao na kuuza na kujipatia fedha lakini huwezi kwenda kumchukua mtu wa pwani kwenye ufukwe ukampa ekari kama za mnyamwezi .ni kupoteza wakati na mnyamwezi huwezi kumpa mtumbwi ukamuambia aende baharini kuvua arudi na samaki .Na ndio mambo yanavyokwenda usione dobi anapata fedha kwa kukusanya nguo za watu na kuwanyooshea ukaona na wewe kazi hiyo unaiweza .wandugu mtakatika mikono na nguo haijapigika pasi pengine ukimaliza shati tu umechoka maji unaita mee.

Sasa mtu anaposema hataki kiwingi katika shughuli zake basi mumfahamu ,pengine ameahidi sehemu hiyo haitembelewi na watu wasio kuwa watalii ,na pengine sehemu hizo zinakuwa half nude wenyewe wanapunga upepo mnawazukia na mabuti na kugongesha viatu kwenye sakafu ,kuweni wastaarabu ,kama mna wasiwasi basi kamataneni mashati huko huko bungeni .
Mna vijisenti wekeni booking mkapumzike ,harudishwi mtu ,labda mnaweza kudai kwa raia kuwepo na kajipasentage fulani kanaondolewa ili wazawa nao wasitoke denda ,hayo ndio mambo ya kuyaomba na sio kuyadai ,mnaomba kwa maneno mazuri na kutongoza mpaka muekezaji anakubali ,sio mnaingia kijeshi ,mambo hayo sasa yamepitwa na wakati ,kuna watu wanatamani wawekezaji wa aina hiyo waende nchini kwao ,Hebu angalieni Botswana , South Africa nafikiri na Namibia wapo wawekezaji wa aina hiyo ,msione kuwa limefanyika hapa Tanzania mkaona ni jambo jipya.
Vipi nchi itaweza kufaidika na hifadhi hiyo ambayo bila ya shaka itakuwa na huduma za kisasa kiasi cha kuitangaza Tanzania na kuwa Holiday destination ,wageni watakaofika sio kuwa watafika hapo tu na kuwa basi ,watatamani kutembezwa sehemu za miji ya wakaazi na humo watakuwa wakinunua bidhaa za wenyeji hao kama kumbukumbu ,na pia wageni watakuwa wakitumia Airport za Nchi na hivyo kuweza kuingiza fedha ya kigeni ,kinachotakiwa ni kujenga infrastructure nzuri ya barabara na viwanja vya ndege ,muwekezaji anaweza kubanwa asianzishe usafiri wa ndege ,ila panaweza kujengwa kiwanja cha ndege ndogo ndogo ambazo zitaweza kutoa huduma za uhakika kati ya sehemu hizo na viwanja vya ndege vya kimataifa .
Na kwa vile wapo wazalendo wanaomiliki ndege na mambo yakikua na wengine wenye vijisenti watajitokeza kuanzisha safari za ndege na mabasi ya kitalii ya kissa kabisa.

Wabunge mnatakiwa kudai katiba mpya ili kuidhibiti nchi na viongozi wake au na serikali yake. Huyo mwekezaji hana hata habari kama mnaibiana wakati alishamwaga saini na serikali yenu.mkimletea fujo atahama tu aende kwengine awaache na mashamba na majumba kama kule zenji sasa wanayia mifuko ya nayloni na imeshakuwa shida wanafinga kwenye magazeti nayo yameshaana kuwa hayapaitikani.
Tunahitaji uongozi safi na katiba mpya sio kuzukia miradi ya watu mkidai mnaenda kuchunguza si bora kwanza muichunguze serikali yenu na halafu mkimaliza huko mtakuwa mmekwisha jua kila kitu mnakaa na wawekazi mnahadithiana na mambo yanasawazishwa ,halafu na hao viruka njia wanaojipeleka na kukatiza kwenye sehemu zilizotiliana saini na serikali mnastahili kupigwa risasi ,mnakwenda kufanya nini huko kama si kuiba mali ya serikali au mnakwenda kupiga chabo ?
 
Naona sasa wabunge wa upinzani watakosa mabomu ya kulipua bungeni.
Hongera ccm kwa kazi nzuri.

Masaka kwani ni Lazima kila kinachoanzishwa JF kilenge kushindanisha chama fulani na fulani?
Nilidhani kulikua hakuna haja ya kuleta hilo uliloleta lisipotakiwa kuletwa na wewe ukaliweka
 
Mutu akishawekeza ni private matter ,hamuwezi kwa kuwa ni wabunge tu mtoke na makoti yenu hata hayajapigwa pasi mtokako mkaingilie sehemu ambayo mtu amewekeza kwa fedha yake ,kuna kitu ni private na kama hiyo ni hoteli basi muwekezaji atakuwa yupo katika mstari na pengine hata nyie mnaotaka kwenda huko akiwemo Raisi hamtoweza kwenda bila ya mipango maalumu,kwani jukumu la usalama na amani ni la huyo muwekezaji ,mpeni taarifa mnaedna saa ngapi,mtakuwepo huko kwa muda gani ,je mtataka muandaliwe chakula mtalipa ,mtalipiwa au muandaliwe free.
Haiwezekani kabisa na si sheria na mnaweza kuitia serikali hasara ikiwa muwekazaji atakuwa na wanasheria wajanja ambao uzembe kama huo uliofanywa na kina Cheo na wenzake kujipeleka kichwa kichwa wanaweza wakautumia na kuomba walipwe fidia.
Katika suite kama hizi ambazo zinakuwa well secured si sehemu za kwenda tu kwa kuwa wewe au nyinyi ni wabunge mukusanyane huko eti mnaenda kuangalia shughuli zinaendeleaji ,hizi si shughuli zenu mmeshakatiwa chenu kaeni pembeni mnataka kwenda pelekeni taarifa msubiri majibu yaani mlifikiri mnaenda kutembelea soko la kariakoo ,hivi atoke mlala hoi na kulekea kwenye jengo la bunge mtamruhusu ? maana hao wabunge amewachagua yeye na wanamuwakilisha yeye na kinachojadiliwa hapo ni kwa ajili yake ,hivi atapata ruhusa ya kuingia ndani na kuangalia shughuli za bunge na wabunge wanavyojadiliana.
Nafikiri hawa wabunge wanahitaji elimu juu ya nini maana uwekezaji naamini kabisa hata Raisi hawezi kwenda hapo bila ya taarifa seuze hawa wabunge masikini za Mungu wanaotoka vijijini hawakuelewa kama kuna mipaka ya kazi zao na sio kuenda popote tu kwa kuwa yeye ni mbunge ,haiwezekani hilo wamefanya ni kosa,na nyie mnaolalamika kuwa wazalendo wanatimuliwa ni lazima watimuliwe kwani hilo eneo limeshakodishwa sasa wao wadai feza inayopatikana huko,mikataba ilitiwa saini huko , wenyewe wanasema na kuandika ,NO TRACE PASSING. yaani mtu akishaweka kibao hicho basi ana haki hata ya kukupiga risasi ujinga ni wako kwa nini hukuenda shule ,waelimisheni wenzenu huko vijijini sio mnakimbilia kuwekeza tu ,halafu mnataka mkate mbuga ,mbona ukikatiza kwenye kambi za jeshi unapelkwa mchura ,naona kuna elimu inahitajika.
Kuna mmoja nimemshangaa amesema kwa nini hawa wabunge hawakutumia power zao ,mbona mimi sijaziona hizo power zao toka liundwe hili Bunge la Tanzania ,nasikia wanaweza kuweka shilingi mbona sijaona na miswada mibovu inapita kila siku tusidanganyane power zao labda kwa mimi mlala hoi wanaweza wakaniitia polisi na kunifunga lakini sio hapo ,huyo mzungu yupo juu ya sheria na wangelijidai kutumia nguvu basi ungesikia jamaa anadai bilioni nyingine anaidai serikali ,serikali itabidi ilipe na fungu jingine anapewa Cheyo.

Mkuu Mwiba.
Naamini hapa utakuwa unakufuru. Mbunge hata kama akitoka bila koti kupigwa pasi bado ni mbunge ndiyo namaanisha Mwakilishi wa Wananchi. Na bado ana dhamana ya kuwakilisha wananchi. Kwa hiyo huyo mwekezaji hata kama atakuwa anafanya upupu basi aachiwe tu aendelee kufanya eti kwa sababu ni muwekezaji. Yaliyotokea Greenland Bank hayawezi kufumbiwa macho.
 
THE problem is, wanacharuka wakati nchi imeshauzwa. Labda sasa hivi waanze kufikiri namna ya kuinunua kutoka kwa hao waliouziwa.
 
Mkuu Mwiba.
Naamini hapa utakuwa unakufuru. Mbunge hata kama akitoka bila koti kupigwa pasi bado ni mbunge ndiyo namaanisha Mwakilishi wa Wananchi. Na bado ana dhamana ya kuwakilisha wananchi. Kwa hiyo huyo mwekezaji hata kama atakuwa anafanya upupu basi aachiwe tu aendelee kufanya eti kwa sababu ni muwekezaji. Yaliyotokea Greenland Bank hayawezi kufumbiwa macho.
Sasa kama mbunge hapigi pasi sio msafi unategemea unategemea akasimamie au achaguliwe waziri ,si ndio unaona watu wanavyopukutika kwa ukimwi ,sababu hawa watu hawana mpamgo na waliowachagua ,walikwenda huko kusaka njia ya kurudisha takirima tu.
Sasa nikirudi naona hatujafahamiana ,na tatizo mnalikataa na mnataka kumuandama muekezaji aliejitenga porini. Kama kweli muna wasi wasi na e hakufuata sheria kwa nini msiwabake hao mawaziri hapo bungeni ,na kwa nini musiwasilishe hoja binafsi na kwa nini msitumie nguvu ya shilingi na kwa nini na kwanini na kwa nini ,?
Aidha mtakuwa na choyo kama kile cha vigogo wa Zimbabwe tofauti hapa nyinyi ni wapinzani kule wenzenu ni watu wa serikali ,nashangaa mnapoilaumu CCM kuwa ndio wavunjaji sheria ,wakati kwenda kumfuata na kutaka kuingia katika eneo la muekezaji mnaona mnafuata sheria.
kama kuibana basi kwa vile tumo katika mapambano ya kufuata demokrasia na utawala bora ,wapinzani humo bungeni wakiwemo pia wa CCM ambao wanatakiwa wawe wapinzani waisakame serikali kuhoji na kujua kiini chake au kugundua palipokosewa na kumegwa sio kwenda kumfuata muwekezaji ,sasa mkitumia njia mlizotaka kutumia za kuuvamia mtaji wa mwekezaji kwa kuwashawishi au wananchi kushawishika na kuona kweli jamaa hana haki ya kuwekeza ,wakavuruga na kuiba kila kitu ,mtasemaje ndio mnajenga nchi muwe kama marekani ? Upinzani gani huo ? mliuona wapi ? Au ndio sasa mnawaona kama waZimbabwe walifanya sawa ? Mnataka kuiga ,haya waigeni maana mnaumwa sana na uzalendo ,zile mbuga ziko mika mingapi mbona hamuihoji serikali mpaka hii leo imepata kiasi gani ? Haya mambo ya wabunge kuvamia mtaji wa mwekezaji ni uvunjwaji wa sheria mnataka kusababisha yale yale yaliokimba serikali na Richmod ,jambo ambalo serikali mpaka leo inalipa na anaelipwa hajui fedha inaendea wapi ?
 
Ndiyo Faida au hasara ya rushwa!!

Jaribu kufikilia Investors anatoka nje ya Marekani na Kuja hapa Marekani, Masenata wanamtembelea tena kwa kufanya appointment, wakifika uwafukuze, sijui hiyo biashara utaifanyia wapi!!, ni siku hiyo unafunga virago vyako. Huyo Investor anafanya makusudi kwa vile Kikwete keshapata zake 10% kuuza sehemu hiyo, ndo maana kila baada ya dakika chache utamsikia Kikwete yuko Marekani. Na hicho ndo kinampa kiburi sana huyo mwekezaji.

Pia tabia ya Raisi kuwa omba omba, sijaona Raisi yeyote Duniani anayekuja mara kwa mara hapa Marekani kama si huyo Jakaya Kikwete. Elimu zetu zingekuwa zinatusaidia kufikili angalau kidogo tu tungekuwa mbali. Fikiria Budget ya Tanzania ni Trilion 7.2 Tshs ambazo ni sawa na US$7billion. Hii budget ni sawa na nusu ya mishahara ya WAFANYAKAZI WA Walmart/Kellog/Kroger/BP/GE/ etc. Ni sawa na budget ya wilaya moja hapa Marekani, ni sawa ni nusu ya net profit ya kampuni kama HONDA/SUZUKI , NI SAWA na net profit ya kampuni ndogo ndogo za hapa Marekani. Jamani nchi kubwa kama Tanzania yenye Maziwa, madini(Almasi. dhahabu, Rubi, Tanzanite etc) kwa kweli hapo kuna kazi. Sijui hawa viongozi walisoma wapi?.

Tabia ya kuomba omba inakufanya uwe mvivu wa kufikili, ukifilia omba omba ni kama Investment.

Toka nije hapa Marekani Miaka 8, Raisi wa Denmark/Swis/ German/ Russia/Japan/ walishafika mara moja au mbili tu, lakini Jakaya ni kila Mwezi yuko hapa kupangusa miguu ya Bush na kuomba omba kama hana akili nzuri vile.
 
Ndiyo Faida au hasara ya rushwa!!
...
Toka nije hapa Marekani Miaka 8, Raisi wa Denmark/Swis/ German/ Russia/Japan/ walishafika mara moja au mbili tu, lakini Jakaya ni kila Mwezi yuko hapa kupangusa miguu ya Bush na kuomba omba kama hana akili nzuri vile.

mkuu hii hata miye nishawahi kuiulizia kwenye moja ya threads lakini naona
haikuwanasa wengi. jamani raisi zaidi ya mara tatu kwa mwaka marekani! hii inatia hofu na lazima tujiulize, marekani kunani kwa mkuu wa kaya?
 
Jaribu kufikilia Investors anatoka nje ya Marekani na Kuja hapa Marekani, Masenata wanamtembelea tena kwa kufanya appointment, wakifika uwafukuze, sijui hiyo biashara utaifanyia wapi!!, ni siku hiyo unafunga virago vyako. Huyo Investor anafanya makusudi kwa vile Kikwete keshapata zake 10% kuuza sehemu hiyo, ndo maana kila baada ya dakika chache utamsikia Kikwete yuko Marekani. Na hicho ndo kinampa kiburi sana huyo mwekezaji.

Usitudanganye Mkuu! Umesikia lini kamati ya senate inaenda Seattle kuikagua Microsoft. Mbunge kutembelea, kwa makubaliano si kitu cha ajabu lakini si kamati iende ati kumkagua mtu binafsi. Hata huyo Steve angewatupa nje. Wafanyabiashara wa kibongo (kama huyo kiongozi wa msafara) wengi wamefilisika kwa kuwatetemekea wanasiasa badala ya kuangalia wateja! Nakumbuka simulizi ya Tony Blair kuwa alikuwa kwenye ndege ya BA inakaribia kuruka akapigiwa simu na malkia. Rubani akatuma ujumbe kuwa simu zote zikatwe na alipoambiwa kuwa ni mheshimiwa anaongea na malkia alijibu kuwa hata kama ni f*****(hapa pengine nimeongeza chumvi) mama akate simu. Tony akakata simu mara moja bila kumuaga Malkia. Tony alisimulia hii hadithi kuonyesha jinsi watu makini walivyo, wanatekeleza wajibu bila kuogopa mtu. Sio kwetu.

Hizi kamati za bunge zimekuwa zikitembelea kukagua mashirika ya umma kibao na hamna la maana walichofanya kuyanusuru yasifilisike. Leo waende kwa mwekezaji na kudai kukaa na meneja kujadili namna anavyoendesha biashara yake na kuangalia vitabu vyake! Mbona mnatutania wenzenu?
 
Usitudanganye Mkuu! Umesikia lini kamati ya senate inaenda Seattle kuikagua Microsoft. Mbunge kutembelea, kwa makubaliano si kitu cha ajabu lakini si kamati iende ati kumkagua mtu binafsi. .... Wafanyabiashara wa kibongo (kama huyo kiongozi wa msafara) wengi wamefilisika kwa kuwatetemekea wanasiasa badala ya kuangalia wateja!

...Hizi kamati za bunge zimekuwa zikitembelea kukagua mashirika ya umma kibao na hamna la maana walichofanya kuyanusuru yasifilisike. Leo waende kwa mwekezaji na kudai kukaa na meneja kujadili namna anavyoendesha biashara yake na kuangalia vitabu vyake! Mbona mnatutania wenzenu?

Fundi,

Una raise point za maana ile mbaya. Bila kuogopa hatari ya kuonekana zinatetea mafisadi. Hongera sana kwa ujasiri.

Unajua, kuna mada zingine kwa kweli ni vigumu sana hata kuchangia kwa sababu hujui nini hasa kinaendelea. Na hili ni kosa la kutokuwa na Press Tanzania.

Hii kamati ilienda hapo kwa mujibu wa makubaliano gani? Walienda kukagua mahesabu au ni vipi? Walikuwa wanazunguka nchi nzima? Walikuwa na mabwana Kodi? Walikuwa wameambatana na Mabwana Afya wa kutafuta mende kwenye majiko na panya kwenye vyumba vya hoteli au vipi? Walianza na Kampuni gani na wamemaliza ngapi? Walikuwa ma inspector wa Wizara za Ujenzi wakitafuta nyufa kwenye ukuta au vipi?

Habari inasema kamati ya Bunge "ilifika huko mbugani kuangalia mambo yanavyoendelea."

Sasa hapo Fundi Mchundo ndugu yangu, kwa information hiyo hapo juu, ukimkosoa Cheyo na kamati yake unakurupuka, na ukimtetea Mfanyabiashara unapambia, fisadi!

Kutokuwa na Media Tanzania ni moja ya mizizi wa matatizo yetu. Hujui kinachoendelea nchini, utaanzae kurekebisha? Fundi, unaweza kutengeneza gari bila kufungua "boneti" kuangalia ndani kulikoni? Zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nimefundishwa kuwaheshimu mafundi wanaojifanya kuweza kujua tatizo la gari kwa kusimama pembeni anakwambia, "haya piga, piga tena, kanyaga mafuta...acha, zima...kabadilishe mafuta ya breki"! Fundi please! Wengine wanaojua diagnosis hawataki hata kukwambia kama anaweza kuli fix gari mpaka umwachie akae nalo.

Huwezi kurekebisha hitilafu ya kitu bila kujua kinachoendelea. Tunahitaji Press!
 
Masaka kwani ni Lazima kila kinachoanzishwa JF kilenge kushindanisha chama fulani na fulani?
Nilidhani kulikua hakuna haja ya kuleta hilo uliloleta lisipotakiwa kuletwa na wewe ukaliweka

Huyu bwana masaka ni idiot sana, sijui mbegu zingine zilitengenezwa vipi, Jamani kuweni mbali na hii familia la sivyo mutapata watoto wenye utindio wa ubongo kama huyu jamaa. Nadhani ni Family history. Kwa wale ambao hawajaoa au kuolewa watch out, jaribu kuwa mbali la sivyo ni disaster kwa generation yako.
 
Kokolo,'
Si umesikia wameongezewa bajeti? Sasa lazima huyu aonyeshe anastahili mshahara atakaoongezwa.
 
Back
Top Bottom