Wabunge wacharuka! - Uwekezaji siyo kuuza nchi

Fundi Mchundo,'
Usichanganye mambo. Baraza la senate au kamati ya senate hapa Marekani inayo kila haki ya kuwaita viongozi wa Microsoft kama kutakuwepo na utata katika uendeshaji wao. Kwetu wabunge walikuwa na wana na kila haki ya kumwita Mr. Tudor au kutembelea mbuga zake ambazo naamini bado ziko chini ya himaya ya Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania. Unless eneo lake ni himaya mpya isiyo chini ya mamlaka ya Tanzania.
 
Fundi,

Una raise point za maana ile mbaya. Japo kuwa hatari ya kuonekana zinatetea mafisadi. Hongera sana kwa ujasiri.

Unajua, kuna mada zingine kwa kweli ni vigumu sana hata kuchangia kwa sababu hujui nini hasa kinaendelea. Na hili ni kosa la kutokuwa na Press Tanzania.

Hii kamati ilienda hapo kwa mujibu wa makubaliano gani? Walienda kukagua mahesabu au ni vipi? Walikuwa wanazunguka nchi nzima? Walikuwa na mabwana Kodi? Walikuwa wameambatana na Mabwana Afya wa kutafuta mende kwenye majiko na panya kwenye vyumba vya hoteli au vipi? Walianza na Kampuni gani na wamemaliza ngapi? Walikuwa ma inspector wa Wizara za Ujenzi wakitafuta nyufa kwenye ukuta au vipi?




Habari inasema kamati ya Bunge "ilifika huko mbugani kuangalia mambo yanavyoendelea."

Sasa hapo Fundi Mchundo ndugu yangu, kwa information hiyo hapo juu, ukimkosoa Cheyo na kamati yake unakurupuka, na ukimtetea Mfanyabiashara unapambia, fisadi!

Kutokuwa na Media Tanzania ni moja ya mizizi wa matatizo yetu. Hujui kinachoendelea nchini, utaanzae kurekebisha? Fundi, unaweza kutengeneza gari bila kufungua "boneti" kuangalia ndani kulikoni? Zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nimefundishwa kuwaheshimu mafundi wanaojifanya kuweza kujua tatizo la gari kwa kusimama pembeni anakwambia, "haya piga, piga tena, kanyaga mafuta...acha, zima...kabadilishe mafuta ya breki"! Fundi please! Wengine wanaojua diagnosis hawataki hata kukwambia kama anaweza kuli fix gari mpaka umwachie akae nalo.

Huwezi kurekebisha hitilafu ya kitu bila kujua kinachoendelea. Tunahitaji Press!


Bwana Fundi na Kuhani kama uko Marekani jaribu kuwa na mazoea ya kuangalia C-SPAN uone ni jisi gani wenye makampuni uwa wanawekwa kiti moto kwa saa kadhaa na Senate. Najua wengi uwa hamna muda wa kuangalia TV kama unaangalia basi uwa ni channels za sport tu. Kama ulingalia week hii senate walivyowakaanga CEO'S wa makampuni ya mafuta hapa Marekani Exoon/BP/CHEVRON/ N.K. Hivyo senate wakitaka kuja kwenye shughuli zako wanakuja. hiweje huyo mwizi wa wanyama hapo serengeti asifuatwe na wabunge. Hi kudhalau serikali, kama Kikwete angekuwa anasikia matusi ya Bush anayosema baada ya kulamba miguu na omba omba nafikiri, angejitia kitanzi kuliko kuendelea kuishi.
http://www.c-span.org/
 
We Kokolo unaniwekea mimi link ya C-Span?

Ha haa haaaaaaa.... watu wengine bwana! Watu waliochelewa kushtukiwa vitu bwana wana matatizo bwana! Duuuh!

Sasa hao kina Cheyo waliwaita Jamaa Bungeni, au waliwazukia Jamaa sehemu yao ya biashara bila appointment wakatimuliwa! LOL! ha ha haaaaaaaaaaaa
 
Duh!!! Wabunge wametolewa mkuku!!!!!

Mhn!! nao wamezidi!! kwani wao ni wakaguzi wa serikali???? Nadhani wana matatizo ya kimtazamo!! wanavuka mipaka!!!!! mboona hawaendi kukagua mahospitalini, masokoni, magerezani???

Lakini tusilalamike sana, pengine walitaka wakajipumzikie japo ka night kamoja kwa mzungu!!!
 
Bwana Fundi na Kuhani kama uko Marekani jaribu kuwa na mazoea ya kuangalia C-SPAN uone ni jisi gani wenye makampuni uwa wanawekwa kiti moto kwa saa kadhaa na Senate. Najua wengi uwa hamna muda wa kuangalia TV kama unaangalia basi uwa ni channels za sport tu. Kama ulingalia week hii senate walivyowakaanga CEO'S wa makampuni ya mafuta hapa Marekani Exoon/BP/CHEVRON/ N.K. Hivyo senate wakitaka kuja kwenye shughuli zako wanakuja. hiweje huyo mwizi wa wanyama hapo serengeti asifuatwe na wabunge. Hi kudhalau serikali, kama Kikwete angekuwa anasikia matusi ya Bush anayosema baada ya kulamba miguu na omba omba nafikiri, angejitia kitanzi kuliko kuendelea kuishi.
http://www.c-span.org/

Kuna tofauti ya kuwa'summon' kwenye senate hearing na kwenda Houston kudai kuangalia vitabu vya Exxon na wengine! Hawa wanaitwa panapo onekana kuna kaharufu kabaya. Na wana kila haki ya kujilinda na Fifth Amendment au kukataa kwenda kama wanajiamini. Huku kwetu huu ulikuwa mradi wa waheshimiwa kujikusanyia bidhaa adimu wakati kuna upungufu! Au unadhani wangeiita TVT waonyeshe jinsi wanavyomkaanga mwekezaji kule Serengeti?

Huko uliko, ni lazima ujue kuwa private property ni sacrosant. Hata Bush Whawezi kuingia kwa mtu bila kualikwa! Unadai huyo jamaa ni mwizi wa wanyama. Kwa hiyo hao waheshimiwa walienda kuangali kama kweli amewafungia ndani. Wakati wa kuwakemea watu kama hawa ni pale wanapokuja kuomba kuwekeza katika sehemu kama hizi. Hao wabunge hapo ndipo wangesimama kidete kuhakikisha kuwa maslahi ya nchi yanalindwa. leo wanaenda kufunga mlango wakati farasi ameishakimbia!
 
Duh!!! Wabunge wametolewa mkuku!!!!!

Mhn!! nao wamezidi!! kwani wao ni wakaguzi wa serikali???? Nadhani wana matatizo ya kimtazamo!! wanavuka mipaka!!!!! mboona hawaendi kukagua mahospitalini, masokoni, magerezani???

Lakini tusilalamike sana, pengine walitaka wakajipumzikie japo ka night kamoja kwa mzungu!!!

Kiufupi Wakuu wameenda bila appointment!

LOL!
 
We Kokolo unaniwekea mimi link ya C-Span?

Ha haa haaaaaaa.... watu wengine bwana! Watu waliochelewa kushtukiwa vitu bwana wana matatizo bwana! Duuuh!

Sasa hao kina Cheyo waliwaita Jamaa Bungeni, au waliwazukia Jamaa sehemu yao ya biashara bila appointment wakatimuliwa! LOL! ha ha haaaaaaaaaaaa

Siyo lazima waitwe bungeni, wanaweza kwenda kwenye hiyo miradi kwani ni himaya ya Tanzania na siyo Kenya au Uganda. Sijui elimu yako kama ungekuwa na upembuzi kidogo ungejua nachosema ni nini!.
Bunge ndo chombo kikuu cha serikali kuangalia matwakwa ya Nchi kwa ujumla, kama huyo mwekezaji yuko nje ya nchi ya Tanzania na Serengeti siyo Tanzania hapo sina neno, lakini kama Serengeti hiko Tanzania wanauwezo wa kwenda pale na kuangalia shughuli zinazofanywa. Mfano, Kama umeoa na una vyumba 4 na watoto 3 kila mtoto ana chumba chake ukitaka kwenda kuangalia chumba cha watoto wako baada ya kugonga mlambo, unaambiwa na mtoto kwamba uwezi kuingia ndani ng'o utajisikiaje Mr. Jugallo/Porchmonkey. Inabidi urudia Darasa la Saba tena.
 
Kuna tofauti ya kuwa'summon' kwenye senate hearing na kwenda Houston kudai kuangalia vitabu vya Exxon na wengine! Hawa wanaitwa panapo onekana kuna kaharufu kabaya. Na wana kila haki ya kujilinda na Fifth Amendment au kukataa kwenda kama wanajiamini. Huku kwetu huu ulikuwa mradi wa waheshimiwa kujikusanyia bidhaa adimu wakati kuna upungufu! Au unadhani wangeiita TVT waonyeshe jinsi wanavyomkaanga mwekezaji kule Serengeti?

Huko uliko, ni lazima ujue kuwa private property ni sacrosant. Hata Bush Whawezi kuingia kwa mtu bila kualikwa! Unadai huyo jamaa ni mwizi wa wanyama. Kwa hiyo hao waheshimiwa walienda kuangali kama kweli amewafungia ndani. Wakati wa kuwakemea watu kama hawa ni pale wanapokuja kuomba kuwekeza katika sehemu kama hizi. Hao wabunge hapo ndipo wangesimama kidete kuhakikisha kuwa maslahi ya nchi yanalindwa. leo wanaenda kufunga mlango wakati farasi ameishakimbia!

Fundi kila nchi ina sheria zake, sheria za marekani siyo lazima sifanane na za Tanzania/ Russia/UK or Japan. Tanzania Wabunge wanawajibu wa kwenda kwenye miradi yeyote na kuangalia wakati huo huo kwa Marekani Senate wanaweza uwezo kwenda kuangalia hau kuwaita na kuwahoji.
 
Mwekezaji aling'akia Bunge


*Ni Mmarekani anayemiliki hoteli mbugani Serengeti
*Mbunge asema anapewa kiburi na vigogo serikalini



Na John Daniel, Dodoma



WABUNGE wameonesha wazi kukasirishwa na kiburi cha baadhi ya wawekezaji wasiojali utu wa Watanzania na kuitaka Serikali kumchukulia hatua kali na mara moja mmiliki wa hoteli ya Guruneti VIP iliyopo katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani mara.

Mwekezaji huyo anadaiwa kuizuia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kufanya kazi yake kwa madai kuwa wageni wake hawataki usumbufu.

Licha ya kutaka kuchukuliwa hatua kali mwekezaji huyo, pia wameitaka Serikali kulieleza Bunge siri ya kiburi cha raia huyo wa Marekani, hadi kufikia hatua ya kuzuia chombo kikubwa kama Bunge kuingia katika hoteli hiyo jambo ambalo ni dharau kwa Serikali na wananchi.

Wakichangia Muswada wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma wa mwaka 2008, iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustapha Mkulo, wabunge hao walisema kutokana na kitendo hicho, mwekezaji huyo amepoteza sifa za kuwekeza nchini na anastahili kusitishiwa mkataba kwa utovu mkubwa wa nidhamu kwa Bunge, Serikali na Watanzania wote.

“Sasa nchi hii imevamiwa katika sekta ya wanyamapori, CAG angepewa meno ya kuingia katika sekta hii na kuona mapato ya hawa watu, tulikwenda kule Mugumu (5/6/2008) katika hoteli ya Guruneti VIP pale Serengeti, tukazuiwa kuingia.
"Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, sasa katika Tanzania hii wawekezaji wamejikatia ki-Tanzania chao, Serikali itusaidie kueleza huyu mwekezaji ametoa wapi kiburi hiki!,” alisema Bw. John Cheyo ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP).

Kwa upande wake, Mbunge wa Karatu, Dkt. Wilbroad Slaa (CHADEMA), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, alisema ni lazima Serikali iliambie Bunge ni wapi mwekezaji huyo ametoa kiburi cha kudhalilisha Watanzania na kuona Bunge kama chombo ambacho hakiwezi kuingia katika hoteli yake.

“Mimi kwa bahati nzuri nimetembea katika nchi nyingi mpaka huko kwao Marekani, kitu cha kwanza kwa mwekezaji ni kuheshimu Taifa lao, Waziri atusaidie huyu mwekezaji anazungumza na nani, kuna nani nyuma yake, na huko kuna nini?,” alihoji Dkt. Slaa.

Naye Mbunge wa Kwamtipura, Bw. Zuberi Ali Maulid (CCM), alisema: “Tulipotaka kwenda katika hoteli hiyo, tuliambiwa kwamba mwenyewe amekataa kwamba wageni wake hawataki usumbufu, hao watu walitoka katika sayari gani, Jupiter au Saturn?.

“Nashauri sana tuwe makini katika mikataba, haya ni matusi kwetu na tena kwa chombo kikubwa kama Bunge, swali la msingi ni huko kuna kitu gani mpaka hataki tuingie, mkataba alioingia na Serikali ni wa aina gani, hapa lazima Serikali itupatie majibu,” alisisitiza.

Mbunge wa Iramba Mashariki, Bw. Mgana Msindai (CCM), licha ya kulaani kitendo cha mwekezaji huyo, alisema eneo hilo lina utajiri mkubwa wa wanyama aina mbalimbali na kwamba alipokuwa Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori cha Pasiansi, Mwanza, lilikuwa ni eneo maalumu kwa ajili ya mazoezi kwa wanafunzi, hivyo kitendo alichofanya Mmarekani huyo, kinaashiria kuna kitu ndani ya eneo hilo.

Naye Mbunge wa Kibakwe, Bw. George Simbachawene (CCM), alisema licha ya hatua kali ambazo atachukuliwa na Serikali, ni muhimu mkataba wake ukawasilishwa bungeni ili Bunge lijiridhishe kama hauna dosari na kuongeza kuwa kitendo alichofanya ni matusi kwa Watanzania.

Hoja ya mkataba huo kuwasilishwa mbele ya Bunge, iliungwa mkono na wabunge wengine wanne huku wakisisitiza kwamba si rahisi kwa mwekezaji mwenye mkataba wa kawaida kudhalilisha nchi kwa kiasi hicho na kwa kujiamini.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Vunjo, Bw. Aloyce Kimaro (CCM), alitoa siri na kueleza, kwamba kiburi cha mwekezaji huyo kinatokana na urafiki wake na Serikali.

Alieleza, kwamba alipohudhuria katika moja ya chakula cha usiku Marekani ambacho kiingilio kilikuwa dola 1,000 alishuhudia jinsi mgeni huyo alivyokuwa karibu na vigogo kadhaa wa Serikali ya Tanzania.

“Nimesikitishwa sana na mwekezaji kuzuia Kamati ya Bunge kufanya kazi yake, kama amezuia Bunge je wananchi anawafanyeje? Ni lazima anawatesa, taarifa nilizonazo ni kwamba mwekezaji huyu ana jeshi lake kubwa pale na anawasumbua wananchi.

“Huyu Bwana nilikutana naye kule New York, Marekani, na ni rafiki wa Serikali, kiburi alicho nacho ni cha Serikali; ameitukana Serikali sasa hana haki ya kukaa pale, aitwe ajieleze kwa Kamati hii kwa nini alifanya hivyo, Bunge hili ni la kisasa, tunataka kutenda haki,” alisema Bw. Kimaro.

Hata hivyo, kutokana na kauli hiyo ya mwekezaji huyo kuwa na urafiki na vigogo wa Serikali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Bw. Philip Marmo, aliomba mwongozo wa Spika akitumia kanuni ya 68 kifungu kidogo cha kwanza akimtaka Bw. Kimaro atoe maelezo ya kina kuhusu urafiki huo.

Akijibu hoja hiyo, Bw. Kimaro alisema kutokana na maofisa wa Serikali walivyokuwa naye karibu wakati wa chakula hicho cha usiku Marekani na kwa mazingira yalivyokuwa, aliamini kwamba ni rafiki wa Serikali na kuongeza kwamba anazo picha zinazoweza kuthibitisha kauli yake kama zitatakiwa.

Akizungumza na Majira nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Serengeti, Dkt. James Wanyancha, alikiri kwamba mwekezaji huyo anawatesa wananchi na kuongeza kuwa amepokea malalamiko mengi juu ya suala hilo.

“Unajua tatizo ni kwamba yule mwekezaji amejenga ukuta pale na ukitaka kuingia lazima uombe kibali, ana askari wake ambao huwa wanaingia mpaka kwa wananchi kufanya ukaguzi na kuwapiga, swali ni kwamba wanafanya ukaguzi kwa ruhusa ya nani na je nani kampa uwezo wa kisheria kuunda Jeshi?,” alihoji Dkt. Wanyancha.

Awali wakichangia Muswada huo wa Sheria ya Hesabu za Umma wa mwaka 2008, wabunge waliitaka Serikali kumpa meno kisheria na uwezo zaidi CAG, ili aweze kushughulikia tatizo la mapato katika sekta ya utalii, matumizi yasiyo ya lazima kwa Serikali hususan ununuzi wa magari ya kifahari bila sababu na kukamilisha miradi kwa wakati.

Walisema ofisi ya CAG inapaswa kujibu Bunge moja kwa moja na si kupitia Waziri wa Fedha kwa kuwa si rahisi mtu kukaguliwa kisha huyohuyo aliyekaguliwa akabidhiwe taarifa ya ukaguzi kwa ajili ya kuiwasilisha bungeni.
http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6901
 
Kiufupi Wakuu wameenda bila appointment!

pengine wangepewa vyumba, wasingewahi kikao cha bajeti!!! VIP panatisha mzee!!! Kilometa chache toka mugumu (wilayani serengeti), nilishawahi kutia mguu pale, ukweli hotel mgt haina kiburi kama unafata taratibu!!!!
 
Kama umeoa na una vyumba 4 na watoto 3 kila mtoto ana chumba chake ukitaka kwenda kuangalia chumba cha watoto wako baada ya kugonga mlambo, unaambiwa na mtoto kwamba uwezi kuingia ndani ng'o utajisikiaje Mr. Jugallo/Porchmonkey. Inabidi urudia Darasa la Saba tena.

Anha!

Haya nimekuelewa, uchambuzi wako ni mzuri, nimekubali, nilikuwa nakosea!
 
Fundi, unaweza kutengeneza gari bila kufungua "boneti" kuangalia ndani kulikoni? Zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nimefundishwa kuwaheshimu mafundi wanaojifanya kuweza kujua tatizo la gari kwa kusimama pembeni anakwambia, "haya piga, piga tena, kanyaga mafuta...acha, zima...kabadilishe mafuta ya breki"! Fundi please! Wengine wanaojua diagnosis hawataki hata kukwambia kama anaweza kuli fix gari mpaka umwachie akae nalo.

That made me laugh......
 
Mfano, Kama umeoa na una vyumba 4 na watoto 3 kila mtoto ana chumba chake ukitaka kwenda kuangalia chumba cha watoto wako baada ya kugonga mlambo, unaambiwa na mtoto kwamba uwezi kuingia ndani ng'o utajisikiaje Mr. Jugallo/Porchmonkey. Inabidi urudia Darasa la Saba tena.

Mbona unaleta mfano wa kiswahili? Mtoto ana haki ya kulinda eneo lake (his/her space) na mzazi hautakiwi kuingia bila sababu ya maana! Hivi ndivyo ilivyo huko mliko. Kwa hawa jamaa zetu, mfano wako si sahihi maana hawa si watoto wako. Hawa ni wapangaji kwenye nyumba yako. Lakini kwa vile wewe ndiyo baba mwenye nyumba unataka kukaa na funguo ya chumba chao na kuingia kila unapojisikia! Hii, hata kwetu, haikubaliki. Je huyo mpangaji akija dai kuwa kuna vitu vyake vimepotea wakatia umeingia kukagua? Je huyo mwekezaji akija dai kuwa hawa wakuu walitaka takrima ndio maana aliwatolea nje? Ndiyo maana mambo kama haya yanatakiwa yafanyiwe wazi kweupe. Wabunge wana matatizo na mwekezaji, wanamkaribisha katika himaya yao ambapo wana kila uhuru wa kumweka kiti moto tena mbele ya luninga! Ukiwa na wasiwasi na mpangaji unampeleka kwa mjumbe na kama una ushahidi kuwa anakuibia unakuja na mjumbe na mashahidi wengine ndipo unapodai kuingia kwake. Ndivyo ilivyo uswahilini. Msitake kutuchanganya,Wakuu!
 
hao kina mzee cheyo washakagua, pale club 84, mwanga bar au chako ni chako pub(viwanja maarufu kwa wabunge pale Dom)???

Kweli wa TZ hatuwezi stahamili aina yoyote ya kiburi, dharau na jeuri!!! si tu toka kwa mwekezaji bali hata mtanzania mwenzetu. Ndivyo tulivyolelewa hivyo. Hata hivyo yaonekana wabunge hawajui scope ya wajibu wao. Kuwa ktk kamati ya hesabu za serikali haimaanishi unatakiwa kwenda (hata kama unaweza) kwa kila mtu bila taarifa na kwa ubabe. kwa mfano huko VIP walikwenda kukagua nini??? na je TRA, idara ya wanyamapori na bodi ya utalii wafanye nini????

Kwa maoni yangu, Bunge linazidi kukua kichwa!! ni vizuri tukakemea UFISADI huu!! pengine wajifunze sasa toka kwa muhimili mwingine wa dola MAHAKAMA. hawa jamaa wametulia kiasi. Walichofanya wabunge pengine tukifananishe na KUONA KUNDI LA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU, LIMEONGOZANA, BILA HODI WALA TAARIFA LINAENDA PALE KILIMANJARO KEMPISKI HOTEL. LINADAI LUNCH NA VYUMBA. KISHA LIKITOLEWA MKUKU, LINALALAMIKA KUWA ETI LILIENDA KUANGALIA KAMA TARATIBU ZA SHERIA ZINAFUATWA KTK UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA HOTELI!!!!

Wabune wamejiongezea mzigo (mingi ikiwa ya kimaslahi binafsi), pengine ndio maana wanalala hovyo bungeni!!!
 
Fundi kila nchi ina sheria zake, sheria za marekani siyo lazima sifanane na za Tanzania/ Russia/UK or Japan. Tanzania Wabunge wanawajibu wa kwenda kwenye miradi yeyote na kuangalia wakati huo huo kwa Marekani Senate wanaweza uwezo kwenda kuangalia hau kuwaita na kuwahoji.

Unakosea tena. Si wajibu wawabunge wakwenda kwenye miradi yeyote. wakati Chama kilishika utamu na miradi yote ilikuwa ni ya serikali, walifanya hivyo. Leo hizi enzi za soko huria hawana haki hiyo tena. Kwa nini hawaendi huko mawilayani ambako kila siku kuna kilio cha hela za miradi kutafunwa?

Lini umesikia kamati ya senate ya marekani imeenda kwa mwekezaji kumkagua? Hilo haliwezekani kaytika nchi ambayo hata polisi akiingia kwako akakukuta unabwia unga hana haki ya kukukamata kama hukumkaribisha ndani! Angalia hizo C-Span na kuzielewa!
 
"Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, sasa katika Tanzania hii wawekezaji wamejikatia ki-Tanzania chao, Serikali itusaidie kueleza huyu mwekezaji ametoa wapi kiburi hiki!,” alisema Bw. John Cheyo ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP).

Kamati ya Bunge ya HESABU ZA SERIKALI inaenda kumkagua mfanya biashara binafsi. Wanaenda kuangalia kama analipa kodi? Hesabu zipi za serikali walizozifuata huko Serengeti? Halafu wanatueleza kuwa huyu Bwana walikata nae misosi huko ughaibuni ambako kiingilio kilikuwa kijisenti dola alfu (Mheshimiwa alilipa kweli alfu kwa msosi?). Hawa ego zao zimeguswa na wala sio uzalendo. Kila kitu kina mipaka yake. Hapa wamevuka mpaka.
 
Originally Posted by KOKOLO
Kama umeoa na una vyumba 4 na watoto 3 kila mtoto ana chumba chake ukitaka kwenda kuangalia chumba cha watoto wako baada ya kugonga mlambo, unaambiwa na mtoto kwamba uwezi kuingia ndani ng'o utajisikiaje Mr. Jugallo/Porchmonkey. Inabidi urudia Darasa la Saba tena.

Wewe unashindwa kupambanua sasa hao watoto na vyumba vyao huoni kama ni mashirika ya serikali ambayo yamejaa ufisadi na ambayo ndio yanayohitajiwa kugongewa mlango na si kugongewa bali wakuu wanahitajiwa kufanya ziara za kushitukizia tu kama huyo baba mwenye watoto hala fu ndio unamkuta meneja hayupo amechukua gari na kuonekana sokoni akinunua mchicha na samaki si umesikia ile ndege ya jeshi kuanguka ,sababu ilikuwa imepakia majani ya ng'ombe na eti wamewapa lifti wapita njia.

Muekezaji naona umpe heshima ya mpangaji au mtu ambae umemkodisha nyumba ,so far utakachosubiri ni kuletewa kodi yako kila mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka au kila baada ya miezi sita na ukimwamini unaweza kukaa hata miaka miwili hujamuuliza kwani una uhakika atakuletea.
Sasa kama unaona kimya kingi kimepita unaanza kuulizia kulikoni na bila ya shaka ili kutomkera uliemkodisha unaweza kuanza kwa kuulizia majirani vipi mbona fulani simuoni na pia unaweza kumpigia simu na kujua mbona mida imepita na hujaona malipo yeyote.
lakini hili la akina Cheyo kukurupuka utafikiria takukuru naona wamekosea stepu ,wao kama ndio wenye nyumba walikuwa waulizie na wanayo sehemu nzuri tu ya kuulizia ambapo ni hapo Bungeni ,yaani sheria zikiwabana wabunge hawa kuulizwa ni jambo gani lililowapeleka naona wanaweza kunasa vibaya sana tena kwenda pengine bila ya taarifa ,mambo haya maana hata kama ni watu wa kamati ya fedha lakini hiyo kamati itakuwa na utaratibu wa kutaka kujua kwani si wapo watu wanaohusika na mahesabu ya serikali si wangeweza kuwahoji wao.Kuna usumbufu gani mpaka wamekwenda kuaibika huko ni aibu ambayo wanajaribu kuificha kwa kusingizia kuwa kuna vigogo ndio wanaowapa kiburi wawekazaji hao.
Hawa watu wamezoea kusimamisha magari ya walala hoi na kupanda bila ya kutoa nauli,kujipeleka kwenye baa za wazalendo wakinywa bure ,ni mazoea tu ya kupata vya bure ndio yaliyowafanya kuvamia mavitu ya wazungu,hivi ndugu zangu mnaoishi maulaya si mnawajua wazungu kwa bajeti ,kila kitu wanapanga hata awe rafiki yako basi mtapangiana mahesabu ya ununuzi kama jana alikununulia soda basi leo utamnunulia wewe otherwise atakuhesabu ni kupe na siku itakayofuata atanunua yake peke yake ,ndivyo yalivyo maisha ya ulaya.
Sasa hawa wajamaa wameona watapata bure wajipeleke ,ndio tulivyo jamani tusifichiane ,haya ni mazingira yaleyale ya polisi akiwa na unifomu basi anaweza kupanda gari bure tokea mwanza hadi Dar ,ndio yale yale ya kuruhusu kwa vile ni watoto wa shule wapande daladala bure ,mambo haya mumeyaona wapi zaidi ya Tanzania ,mtu anahudumikia daladala yake na wakati mwengine inabidi akope ili alitengeneze leo jukumu la serikali la kuwatafutia mabasi ya shule wanafunzi wanabebeshwa watu binafsi wakati wakaguzi wetu kila wakipata cheo cha juu humega fedha ya Taifa kwa mabilioni fedha ambazo zingeweza kuwapatia wanafunzi mabasi kibao na kila shule ikapatiwa japo mabasi matatu , nashangaa kwamba hata wabunge wa upinzani wapo mstari wa mbele maana hao wawekezaji wakiona mpo msatari wa mbele kuwabana wao badala ya serikali wataona bora hao hao CCM kuliko nyie na ndio wakawa wanaidhamini CCM hata katika shughuli za Uchaguzi sababu wapinzani hawajui kula na vipofu ,hawajapata uongozi wanawafutia kwenye vitega uchumi vyao je wakipata kuongoza nchi si ndio watagonga milango na kusemwa ni vyumba vya watoto wetu !
 
"Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, sasa katika Tanzania hii wawekezaji wamejikatia ki-Tanzania chao, Serikali itusaidie kueleza huyu mwekezaji ametoa wapi kiburi hiki!," alisema Bw. John Cheyo ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP).

Kamati ya Bunge ya HESABU ZA SERIKALI inaenda kumkagua mfanya biashara binafsi. Wanaenda kuangalia kama analipa kodi? Hesabu zipi za serikali walizozifuata huko Serengeti? Halafu wanatueleza kuwa huyu Bwana walikata nae misosi huko ughaibuni ambako kiingilio kilikuwa kijisenti dola alfu (Mheshimiwa alilipa kweli alfu kwa msosi?). Hawa ego zao zimeguswa na wala sio uzalendo. Kila kitu kina mipaka yake. Hapa wamevuka mpaka.

Fundi, kazi kako:
http://www.guardian.co.uk/world/2006/nov/14/usa.ciarendition

http://www.philcooke.com/IRS_investigation
 
Mwiba, Kuhani Mkuu, Fundi, asanteni kwa kazi nzuri maana niliposikia habari hizi nilizua debate kubwa na wenzangu.
I find personally umegaji wa Serengeti na Tudor huko Grumeti distasteful lakini ni lazima tuheshimu rule of law. Kama mlivyosema kama una personal beef na Tudor or some ego issues like Cheyo ni lazima utofautishe na majukumu yako kama mbunge.
Wale wanaotetea wabunge watuletee hapa sheria inayompa haki mbunge kwenda kwenye private entreprise kuikagua without appointment.
Mimi kama private entrprenuer nimekuwa nikiangalia 'ziara' hizi za wabunge na nimechukizwa nazo kwani hata makampuni ya mawasiliano, media houses etc wanatembelewa na kila aina ya kamati na wabunge wanatakiwa kupewa vijizawadi, wazungushwe, wengi wao hata hawaelewi wanachoelezwa kuhusu huduma za hapo alomuradi wamechukua per diem zao. Sasa kama hiyo ya Serengeti wameshachukua per diem kubwa zaidi kwa sababu walisafiri! Katika pitapita zao wakasema hebu tukapaone pale anapopumzika JK ana faidi nini? Basi wakaamua ku-divert!
Wabunge si Miungu watu na tresspassing is tresspassing.
Kuhusu wabunge kutembelea private entreprise naomba nitoe mfano katika kitabu cha Obama "Audacity of Hope"alipotembelea Google offices. ALIOMBA APPOINTMENT na alionana na owner. Lakini alienda kama Obama na alitaka kuelewa zaidi kuhusu uchumi na maswali yake yalilenga kujua IT sector ina challenges gani. He went in to learn more, siyo kukagua vitabu vyao.
 
Back
Top Bottom