Mke wa Kafulila awaponza wabunge wa CHADEMA mashindano ya Afrika Mashariki

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Ijumaa njema wadau,
Wiki iliyopita yule mwanadada maarufu katika mtandao wa kijamii wa instagram anayeishi nchini marekani, Mange Kimambi aliandika kwenye akaunti yake ya instagram kuwa David Kafulila na mke wake Jesca Kishoa wameonekana wakila bata katika hoteli ya slip in iliyoko Kariakoo ambako Jesca amefikia pamoja na wabunge wenzake wa chadema kwa ajili ya kushiriki mashindano ya michezo ya wabunge wa Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Dar es salaam. Chanzo cha taarifa ya Mange ni mbunge mmoja mwanamke wa chadema kwani kwa style ya uandishi wa mwanadada huyo huanza kwa kunukuu maneno ya mtu aliyempa taarifa.

Habari za uhakika zinasema kuwa ni mbunge huyo ambaye ndiye chanzo cha taarifa hiyo na ambaye inasemekana yuko karibu sana mh. Mbowe alimpigia simu Mbowe na kumuelea hali hiyo na jinsi ambavyo wabunge wengine hawakufurahishwa na kitendo cha kishoa kwenda na mumewe hotelini hapo kwa mbwembwe huku akijua kabisa amekisaliti chama. Mbowe aliahidi kulifanyia kazi suala hilo

Ikumbukwe kuwa mara tu baada ya Kafulila kujiondoa chadema, mke wake aliitisha vyombo vya habari na kukanusha sababu alizozitoa mumewe za kujiondoa chadema huku akimuona mtu asiye na msimamo. Ni mange kimambi aliyemtaka Jesca Kishoa kuvunja ndoa yake na Kafulila kama kweli aliyoyasema mbele ya vyombo vya habari alikuwa anayamaanisha kweli, la sivyo ilikuwa ni janja tu ya kutaka kuwapa imani chadema. Ili wasimchukulie hatua ambazo pengine zingekuwa ni pamoja na kumfujuza chama . Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alishaonesha dalili za Kishoa kufukuzwa uanachama kutokana na andiko lake kwenye mtandao wa twitter.

Kutokana na sakata hilo la Kafulila, Jesca Kishoa na chadema, jana kamati kuu ya chadema imeazimia wabunge wote wa chama hicho wanaoshiriki mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki kujiondoa mara moja katika mashindano hayo kwa kisingizio cha kupinga kile ambacho wenyewe wanakiita ukandamizaji wa demokrasia, sababu ambayo haina mashiko kwa sababu kelele zao za ukandamizwaji wa demokrasia zimeanza tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani mwaka 2015 na wakati wanawaruhusu wabunge wao kushiriki mashindano hayo walikuwa wanalijua hilo.
 
Ccm na hizi siasa zenu za kuokoteza tumaneno. chama chenu mtakifikisha pabaya na itaendelea kuonekana ccm ni chama wahuni.
 
Ijumaa njema Wadau,
Wiki iliyopita yule mwanadada maarufu katika mtandao wa kijamii wa Instagram anayeishi Nchini Marekani, MANGE KIMAMBI aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa DAVID KAFULILA na mke wake JESCA KISHOA wameonekana wakila BATA katika Hoteli ya Slip In iliyoko Kariakoo ambako Jesca amefikia pamoja na Wabunge wenzake wa CHADEMA kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Michezo ya Wabunge wa Afrika Mashariki yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Chanzo cha taarifa ya MANGE ni Mbunge mmoja. mwanamke wa CHADEMA kwani kwa Style ya uandishi wa mwanadada huyo huanza kwa kunukuu maneno ya mtu aliyempa taarufa.

Habari za uhakika zinasema kuwa ni Mbunge huyo ambaye ndiye chanzo cha taarifa hiyo na ambaye inasemekana yuko karibu sana Mh. MBOWE alimpigia simu Mbowe na kumuelea hali hiyo na jinsi ambavyo Wabunge wengine hawakufurahishwa na kitendo cha KISHOA kwenda na Mumewe Hotelini hapo kwa mbwembwe huku akijua kabisa amekisaliti chama. MBOWE aliahidi kulifanyia kazi suala hilo
Ikumbukwe kuwa mara tu baada ya KAFULILA kujiondoa Chadema, mke wake aliitisha vyombo vya habari na kukanusha sababu alizozitoa Mumewe za kujiondoa CHADEMA huku akimuona mtu asiye. na Msimamo.Ni Mange Kimambi aliyemtaka JESCA. KISHOA kuvunja Ndoa yake na KAFULILA kama kweli aliyoyasema mbele ya Vyombo vya habari alikuwa anayamaanisha kweli, la sivyo ilikuwa ni janja tu ya kutaka kuwapa Imani CHADMA. ili wasimchukulie hatua ambazo pengine zingekuwa ni pamoja na kumfujuza chama . Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alishaonesha dalili za Kishoa kufukuzwa uanachama kutokana na andiko lake kwenye mtandao wa twitter.

Kutokana na Sakata hilo la Kafulila, Jesca Kishoa na Chadema, Jana Kamati Kuu ya CHADEMA imeazimia Wabunge wote wa chama hicho wanaoshiriki mashindano ya Wabunge wa Afrika Mashariki kujiondoa mara moja katika mashindano hayo kwa kisingizio cha kupinga kile ambacjo wenyewe wanakiita ukandamizaji wa demokrasia, sababu ambayo haina mashiko kwa sababu kelele zao sa ukandamizwaji wa demokrasia zimeanza tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani mwaka 2015 na wakati wanawaruhusu Wabunge wao kushiriki Mashindano hayo walikuwa wanalijua hilo.
Kwa hiyo unaona kwa akili yako hawako sawa chadema wakati wabunge wao wansota rumande wamenyimwa dhamana Na hao wanaoshiriki uchaguzi ulikuwa uonevu mkubwa tena washirikiane hata kitu chochote Na ccm
 
YAANI wewe ukiendelea hivi kuonyesha umbumbumbu wako na maneno ya kipumbavu au tuseme siasa majitaka nitakuwa na uhakika ni miongoni mwa wanasiasa mafelia aliowasema mzee wetu Magufuli
 
Ndoa Na siasa. Wapi Na wapi. Watu mke simba Mme Yanga. Kenya kuna familia mke jubilee Mme NASA. CHADEMA mnataka kutuketea nini nchini?
 
Chadema bana,michezo ni afya haina itikadi
Itafikia siku watapangiwa yupi wa kulala nae
Hakuna kamati kuu ya kihuni kama ya chadema,kila mtu ni mjumbe wa kamati kuu,hata ukiingia leo chadema unaukwaa ujumbe wa kamati kuu
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Hata mimi sikuona umuhimu wa wabunge wa UKAWA na upinzani kwa ujumla kushiriki hayo mashindano kwa sababu kwanza hawaheshimiwi na kiti cha spika kama wabunge. Ona Lissu yupo hospitalini lakini uongozi wa bunge hauna habari naye. Nyie wapinzani msimsaliti mwenzenu jamani. Mnashirikianaje na Job wakati mwenzenu Lissu ameumizwa lakini uongozi wa bunge umemtelekeza?
 
Back
Top Bottom