Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,746
- 40,899
Leo wabunge wameanza kuonesha makeke yao pale walipomcharukia mmoja wao aliyejitokeza kutetea kitendo cha Mwekezaji wa Hoteli ya Kimataifa ya Serengeti ambaye aliipiga "full stop" Kamati ya Bunge inayoongozwa na Mhe. Cheyo (UDP) ambayo ilifika huko mbugani kuangalia mambo yanavyoendelea.
Mwekezajji huyo aliwapiga wabunge full stop akidai kuwa wageni wamelala na hawataki kusumbuliwa. Wabunge hawakufurahishwa na hilo na leo Wizara husika imejaribu kutoa maelezo ambayo hayakuwaridhisha wabunge hata pale mmoja wa wabunge wakongwe (jina limenitoka) alipojaribu kuitetea serikali kuwa huyo mwekezaji amewekeza fedha nyingi sana kwa hiyo kitendo chake kinaeleweka, akiiashiria kwamba mwekezaji mwenye pesa nyingi hastahili "kusumbuliwa" na watu wadogo kama wabunge.
Lakini nyuma yake ni maneno ya Bw. Cheyo ambaye alinung'unika kuwa mtindo huu usipokoma basi kila Rais akitoka madarakani atakuwa anaandamwa na kashfa. Kuna tetesi ambazo zinadai kuna kauhisiano ka aina fulani kenye maslahi kati ya huyo mwekezaji na Rais kiasi kwamba yeye kama vile Sinclair anapata kiburi.
Wabunge wengi waliozungumza walionesha kukasirishwa na mwelekeo huo wa mawazo (kuwa wawekezaji wana special status) na Dr. Slaa alidai wazi kuwa hakuna bei katika hadhi na utu wetu na mwekezaji yeyote asijione kuwa kwa vile amewekeza mabilioni basi ana ka ujiko ka aina fulani hadi kuweza kuwapiga stop wawakilishi wa watu.
Hii ni siku ya pili tu ya kikao cha Bunge ambacho kinatarajiwa kuchukua karibu miezi miwili....