Ndugai avuliwe U-spika wa Bunge, kutokana na kuikanyaga Katiba ya nchi kwa kung'ang'ania kuwakumbatia wabunge wa viti maalum wa Chadema

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,159
Tunajua kuwa sheria mama ya nchi hii ni Katiba ya Jamhuri wa Muungano, 1977, ambapo kila mwananchi anapaswa kuiheshimu na kuitii.

Viongozi wakuu wa serikali wanaapishwa kwa kuilinda Katiba hiyo kabla hatujawakabidhi madaraka hayo.

Katika kile tunachokiona watanzania kwa sasa kuona viongozi wetu wa serikaki kuidharau mno Katiba ya nchi na kuiona kama "toilet paper" Spika wa Bunge la nchi, Job Ndugai, amegoma kabisa kutambua mamlaka ya Chama cha Chadema, iliyoamua kuwavua uanachama wao wale wabunge 19 wa viti maalum katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema walichofanya hivi karibuni.

Katiba ya nchi ipo wazi katika suala hilo ambapo inatamka kuwa mbunge yeyote atapoteza ubunge wake pale chama kilichomdhamini mbunge huyo kabla ya kumvua uanachama wake.

Tunaomba Bunge la Jamhuri ya Muungano, ingawa tunajua kuwa ni la chama kimoja cha CCM, lakini katika suala hili inabidi wasimamie Katiba ya nchi na wasipepese macho na wamwambie Spika Ndugai kuwa kitendo chake cha kuisigina waziwazi Katiba ya nchi, ataipeleka nchi hii kwenye machafuko makubwa na wafanye maamuzi magumu kwa kumvua u-Spika wake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jambo jema ni kuwa hata aliyekuwa Spika mstaafu, Pius Msekwa, ambaye ni mwanaccm mwenzie amelifafanua suala hili kwa kutokuwa mnafiki kwa kueleza kuwa hao akina Halima na wenzie, ubunge wao umekoma pale Kikao cha Kamati Kuu kilipofanya uamuzi wa kuwavua uanachama wao.

Ninaloweza kumuuliza Spika Ndugai, hivi kwa kuendelea kuwang'ang'ania wabunge hao, watakuwa wa chama gani?

Kwa kuwa Katiba hairuhusu wabunge binafsi, hatujui hadi hivi sasa wabunge hao wanahesabika kuwa wa chama gani?

Kwa hiyo pamoja na kuelewa kuwa Spika Ndugai ana chuki kubwa na chama cha Chadema, lakini katika hili suala la wabunge wa viti maalum, inabidi akiri kuwa "amebugi step" kwa hiyo itamlazimu Spika Ndugai ajiuzulu wadhifa wake wa U- Spika ili kulirejeshea heshima iliyokuwa nayo Bunge letu na kama hataki basi wabunge wa CCM watende haki kwa kumfukuza Spika Ndugai mara moja, kwa kuwa ameliabisha sana Taifa hili ndani ya nchi na katika Jumuiya ya kimataifa, kwa kuona kuwa Spika wetu wa Bunge haitii na kuiheshimu kabisa Katiba ya nchi.

Kama kweli Taifa hili tunataka kuirejesha heshima yetu kama Taifa linaloheshimu sheria za nchi, Bunge linalazimika kumvua u-Spika Ndugai kwa manufaa mapana ya Taifa letu.
 
Kwa Tanzania mpya hii?

Mara ya mwisho nakumbuka ni mwaka 2008 ambapo waziri mkuu alijiuzuru. Lakini kwa sasa, nchi sidhani kama inaongozwa kwa kufuata katiba kwa 💯% labda kwa 10% pekee.
 
Muda wa kukata rufaa haujapita. Subirini wakate rufaa huenda maamuzi yakapinduliwa na baraza kuu. Wasipopata haki Baraza kuu wataenda mahakamani kuitafuta haki yao. Muda huo wote bado ni wabunge wenu kwa hiyo kuweni wapole.

Hata hivyo Chadema haina cha kupoteza hata kama wakiendelea kuwa wabunge kwani chenyewe hakina mpango wa kuteua wabunge🤣.

Muda utaongea
 
Kwa Tanzania mpya hii?

Mara ya mwisho nakumbuka ni mwaka 2008 ambapo waziri mkuu alijiuzuru. Lakini kwa sasa, nchi sidhani kama inaongozwa kwa kufuata katiba kwa 💯% labda kwa 10% pekee.
Lakini kwa kuendelea kwa Spika Huyu, huoni kama Taifa tunapata aibu kubwa?

Hata Spika mstaafu katamka wazi kuwa, chama ambacho anadai kuwa ndicho kilichomdhamini kuja hapo Bungeni kikatamka tu kimeshamvua uanachama wake, automatically anaupoteza pia na huo ubunge wake..............

Hivi huyu Spika Ndugai anataka kutuambia kuwa hajui kusoma wala kuandika?
 
Muda wa kukata rufaa haujapita. Subirini wakate rufaa huenda maamuzi yakapinduliwa na baraza kuu. Wasipopata haki Baraza kuu wataenda mahakamani kuitafuta haki yao. Muda huo wote bado ni wabunge wenu kwa hiyo kuweni wapole.

Hata hivyo Chadema haina cha kupoteza hata kama wakiendelea kuwa wabunge kwani chenyewe hakina mpango wa kuteua wabunge🤣.

Muda utaongea
Mbona wakati CCM ilipowafukuza uanachama wao wa CCM, akina Sophia Simba, papo hapo walipoteza ubunge wao?

Mbona wakati chama cha CUF kimewavua uanachama wao, wabunge wake wa viti maalum, automatically walipoteza ubunge wao?

Iweje Leo wakati Chadema imewafukuza uanachama wabunge wao, kuwe na "double standard" ya utekelezaji wake?
 
Lakini kwa kuendelea kwa Spika Huyu, huoni kama Taifa tunapata aibu kubwa?

Hata Spika mstaafu katamka wazi kuwa, chama ambacho anadai kuwa ndicho kilichomdhamini kuja hapo Bungeni kikatamka tu kimeshamvua uanachama wake, automatically anaupoteza pia na huo ubunge wake..............

Hivi huyu Spika Ndugai anataka kutuambia kuwa hajui kusoma wala kuandika?
Mkuu, hilo ni tawi tu katika ujumla wa uvunjaji wa sheria na katiba! Na jambo la msingi ni kwamba, kuna mengi yajayo!
 
Mkuu, hilo ni tawi tu katika ujumla wa uvunjaji wa sheria na katiba! Na jambo la msingi ni kwamba, kuna mengi yajayo!
Watanzania wote tunapaswa tulikemee kwa nguvu zote, hili suala la kuvunja Katiba linalofanywa na watawala wetu, ili kuliponya Taifa letu katika anguko kubwa lijalo
 
It is you saying that the King is naked. Despite of the fact, not a single MP will open one's mouth: The King is naked. Ndugai has all the unwavering support from the "Emperor".
 
Muda wa kukata rufaa haujapita. Subirini wakate rufaa huenda maamuzi yakapinduliwa na baraza kuu. Wasipopata haki Baraza kuu wataenda mahakamani kuitafuta haki yao. Muda huo wote bado ni wabunge wenu kwa hiyo kuweni wapole.

Hata hivyo Chadema haina cha kupoteza hata kama wakiendelea kuwa wabunge kwani chenyewe hakina mpango wa kuteua wabunge🤣.

Muda utaongea
Ebu mnijuze. Katiba ya Chadema inasemaje kama mwanachama atakiburuza chama mahakamani?
 
Spika wa Bunge la nchi, Job Ndugai, amegoma kabisa kutambua mamlaka ya Chama cha Chadema, iliyoamua kuwavua uanachama wao wale wabunge 19 wa viti maalum katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema walichofanya hivi karibuni
Hivi cdm wameikana barua ya utambulisho wa wabunge wao
 
Lakini kwa kuendelea kwa Spika Huyu, huoni kama Taifa tunapata aibu kubwa?

Hata Spika mstaafu katamka wazi kuwa, chama ambacho anadai kuwa ndicho kilichomdhamini kuja hapo Bungeni kikatamka tu kimeshamvua uanachama wake, automatically anaupoteza pia na huo ubunge wake..............

Hivi huyu Spika Ndugai anataka kutuambia kuwa hajui kusoma wala kuandika?

Kwanza ni muhimu kujua spika kapatikana kupitia njia zipi pi ndipo uone umuhimu wa kumtoa
 
Hivi cdm wameikana barua ya utambulisho wa wabunge wao
Nijibu swali lako moja kwa moja.

Kama chama cha Chadema "absolutely" wameikana barua hiyo moja kwa moja kuwa haikutoka barua toka kwao, iliyoenda kwenye Tume ya Taifa na baadaye kufikishwa kwa Spika wa Bunge na kuapishwa wabunge hao wa viti maalum
 
Kwanza ni muhimu kujua spika kapatikana kupitia njia zipi pi ndipo uone umuhimu wa kumtoa
Hata kama Spika kapatikana kwa ajili ya uwingi wao hao CCM, lakini bado Katiba ya nchi, ambayo kila viongozi wa nchi anaapa kuitii na kuiheshimu kabla hajaanza kutumikia madaraka hayo, kwa hiyo hana "option" ya kuitii Katiba hiyo bali analazimishwa kuitii Katiba hiyo. OVA
 
Watanzania wote tunapaswa tulikemee kwa nguvu zote, hili suala la kuvunja Katiba linalofanywa na watawala wetu, ili kuliponya Taifa letu katika anguko kubwa lijalo
Tunakemeaje mkuu Mystery?! Tunakemeaje?! Na sasa kuna wizara mpya ya kupambana na ‘freedom of speech’, Mawasiliano na Teknologia ya Habari!’ Hiki ‘kijiwe’ tu hapa, tutafutana, wee subiri tu!
 
Back
Top Bottom