Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

JF ni ukumbi huru wa kuhabarishana, kuelimishana, kuburudishana, na kitu kikubwa zaidi, kusaidiana. Kama kuna kitu unakijua, na unaona kinafanyika ndivyo sivyo, unajitolea kusaidia, na hiki ndicho ninachofanya hapa, kwa kuendelea na zile makala zangu elimishi kuhusu Maslahi ya Taifa.

Declaration of Interest
Mimi ni kada wa chama cha siasa, ila ninapoandika hapa, siandiki kama kada, bali naandika kama Mtanzania Mzalendo, ukinisoma with preconceived opinions kuwa huyu ni kada wa chama fulani, hutaweza kuiona the rationale behind bandiko hili, hivyo nakushauri bora uishie hapa.

Vyama vya Siasa Tanzania ni Public Parties
Japo vyama vya siasa ni mali ya wanachama na kuhudumiwa na michango ya wanachama, kwa Tanzania, vyama vya siasa ni private parties vya wanachama, wakati wa kuanzishwa tuu, lakini vikiisha ingia kushiriki uchaguzi na kushinda, status ya vyama hivyo ina change from private parties za wanachama into public parties za umma na ndio maana vinalipwa ruzuku ya serikali. Fedha za serikali ni public money, yoyote anayelipwa by taxpayers money ni public entity, kufuatia viongozi wa vyama hivyo kuchaguliwa na wananchi, the public, to hold a public office, serikali za mitaa, udiwani, ubunge hadi urais, walio wachagua ni public ya Watanzania na sio wanachama wao pekee, hivyo hivi vyama vyote vya siasa vyenye viongozi waliochaguliwa na wananchi ni public parties.

Kufuatia status hii ya vyama vya siasa kuwa ni public parties, then maamuzi yoyote ya chama kuhusu uchaguzi, lazima yazingatie the public interest na sio the selfish motives ya viongozi wake, na kiukweli baadhi ya viingozi wa baadhi ya vyama vyetu, ni watu wajinga wajinga, na wengine ni vichaa kabisa! Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?

Kutokana baadhi ya vyama kukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura, viongozi wamekuwa very bitter kwa kujidanganya na kujiaminisha walishinda uchaguzi ila wamepokwa ushindi!.

Miongoni mwa walioshinda, ni baadhi ya wapinzani. Inasemekana vyama vyao vimepanga kuwazuia kuwatumikia wananchi waliowachagua!. Huu sio tuu ni ujinga uliopitiliza, huu ndio ukichaa ninao uzungumzia.

Japo mgombea lazima adhaminiwe na chama cha siasa kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, kwa maoni yangu, udhamini una lengo zuri la kupata viongozi safi, lakini pia huu ni ujinga na ni kinyume cha katiba, japo ujinga huu sasa umehalalishwa na kuchomekewa ndani katiba yetu kinyume cha dhamira ya mtunga katiba.

Lakini huyo mgombea akiisha chaguliwa kwa kura za wananchi kuwa kiongozi, status yake ina change from mdhaminiwa wa chama cha siasa into a public service, kiongozi huyu sasa anakuwa ni kiongozi wa umma na sio mgombea wa chama. Uwezo wa chama cha siasa kumfukuza uanachama mwanachama wake ambaye ni kiongozi wa umma, bila kosa lolote, au kosa lake ni yeye kuchaguliwa kuongoza eneo lake, wakati vigogo wa chama chake wameshindwa na kupigwa chini na wananchi wao, huu ni ujinga na kutowatendea haki wananchi wa eneo husika walio onyesha imani yao kwa mgombea huyo na kumchagua!.

Baadhi ya Viongozi wa Vyama ni Insane, Hawajui Watendalo!
Wanabodi, naomba kutanguliza kuomba radhi kwa haya ninayoyaandika kuhusu baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwa ni insane bila ya wao kujijua they are insane, ila ni kweli baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ni insane na utawajua kwa mawazo yao, maneno yao na matendo yao. Kuna kauli za ajabu ajabu zinatolewa na baadhi ya viongozi wetu, mtu hadi unajiuliza kama vingozi hawa wana akili timamu!

Ili kuielewa hii dhana ya viongozi insane, katibu hapa ili umjue insane ni nani na utamtambuaje na kumtofautisha na mtu mwenye akili zake timamu Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?

Insanity Inawapataje Viongozi wa Siasa?.
Kama nilivyoeleza pale juu, mtu kuwa insane ni hali tuu, kwa Kiswahili kizuri ni kughafilika. Mtu unaweza kuwa timamu kabisa, lakini ukatibuliwa na jambo fulani, ukachukua maamuzi ya hamaki, hasira na kufanya kitendo ambacho sio cha kawaida sometimes hata kuua!, halafu ukiisha tulia, ndipo unajiuliza umefanya nini na kuanza kuujutia uamuzi wako.

Lengo la chama cha siasa, ni kushika dola, hivyo viongozi wanaogombea nafasi mbali mbali kwa lengo la kushika dola (urais), kushika jimbo (ubunge), kata (udiwani), na mitaa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sasa katika kugombea, kukijitokeza umati mkubwa wa watu katika mikutano yako, kunakupa matumaini ya kukubalika, hivyo mgombea unakuwa na too great expectation ya kushinda, kumbe ni just some false hopes, hivyo uchaguzi ukifanyika, matokeo yakaonyesha umeshindwa, unapagawa, unachanganyikiwa unakuwa huamini matokeo, hivyo unaghafilika, unarukwa na akili, una despair, hiyo hali inakusababishia hali inayoitwa preudo insanity, hivyo unatoa maamuzi ya ajabu ajabu, kwanza ni hatua ya kwanza inaitwa denial, hukubali matokeo, unaamini ulishinda ukaibiwa kura, hivyo una wamobilize wafuasi wako muingie barabarani!, this is insanity kutaka kuwafolenisha watu kuwaingiza barabarani ili iweje?!.

Hatua ya pili ni kutoa taarifa kuwa hukubali matokeo, hii ni kawaida kwa kila asiyakubali kushindwa. Hatua ya tatu ni kusema huwatambui walioshinda. Unaweza usiwatambue kwa muda, lakini walioshinda wakiisha apishwa, kutowatambua ni muendelezo wa insanity!. Hatua ya nne ni kususa, na kutaka kuwazuia wengine walioshinda kihalali, au kususia kutoa ushirikiano kwa walioshinda, kama hili la kugomea kutoa majina ya wabunge wa viti maalum!.

Kuna wanaoshindwa na kubakia kuwa stable, lakini kuna wanaoshindwa na kuchanganyikiwa hadi kurukwa akili, sasa hawa walioshindwa na kurukwa akili wakitoa maamuzi ya ajabu ajabu, wenye akili timamu mkiwafuata, wote mtaonekana insane!

Mtu Kuwa Insane Sio Kosa, ni Hali Tuu, Lakini Kikundi cha Watu, Chama, Kikao au Wanachama Wote Kukubali Kufuata Ushauri wa Isane, Wote Mtaonekana Insane!. Wale Wasio Insane, Wasikubali Maamuzi ya Isane!.
Uchaguzi umekwisha, walioshinda, wameshinda, walioshindwa wameshindwa, zipo taarifa za baadhi ya viongozi walioshindwa kutaka kuwazui a walioshinda wasitumikie wananchi waliowachagua!, this is insanity!.

Kuna taarifa za chama fulani kugomea kuteua wabunge wa viti maalum kwa hoja za kususa, this too is insanity!.

Wito wangu kwenye hivyo vyama, kama kuna viongozi ambao sio insane, please stop this madness ndani ya vyama vyenu, vinginevyo wote mtaonekana ni insane!.

Jee Kila Uamuzi wa Kugomea Jambo au Kususia Kitu ni Ujinga, Insane?
Hapana, sio kila kugomea jambo au kususia jambo fulani ni ujinga. Kugomea jambo fulani ili kutuma ujumbe mzito kwa watawala, kuwa this is not right, kunakubalika, hivyo maandamano ya kutuma ujumbe, demonstrations au industrial actions kwa wafanyakazi, kudai haki zao, ni migomo halali na ina justification kwa ajili ya kutimiza malengo fulani.

Kipimo cha kususia jambo fulani au kugomea fulani, kipi ni uamuzi sahihi na kipi ni ujinga na uendawazi, ni kipimo cha kutumia matokeo, jee ukigomea jambo fulani, una goma ili kuachive nini?, kama unagoma tuu ili mradi kugoma, au unasusa tuu ili mradi kususa, kwa kugoma huko, huta achieve anything, huku ndio kugoma kwa ujinga na uendawazimu, viongozi wa vyama wanaohimiza vyama vyao kususa huku na kugoma huku ambapo there is nothing they'll achieve kwa kususa huko au kugoma huko, huu ndio uendawazimu ninaouzungumza hapa! Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Huwezi kususa kumtambua rais wa nchi- aliyeshinda urais kwenye uchaguzi Mkuu wa kidemokrasia huru na wa haki. Huu ni uendawazimu!. Mgombea ameshinda, huwezi kumzuia asitumikie wananchi walio mchagua- huu ni uendawazimu!. Chama kinastahili kupata idadi fulani ya wabunge wa viti maalum, kugoma kupeleka majina NEC ni uendawazimu!, unasusa ili iweje?.

Hitimisho.
Kwa vile vyama vya siasa ni public parties, viongozi wa vyama, mna wajibu wa kuviendesha vyama vyenu kwa kutanguliza mbele maslahi ya umma na sio maslahi binafsi ya viongozi wenu, msiruhusu ignorance, insanity, selfishness ya baadhi ya viongozi wenu wabinafsi, kuviangamiza vyama vyenu kwa ignorance, insanity, selfishness yao, wakati miongoni mwenu sio wote mko insane.

ACT Wazalendo, acheni ujinga wa ignorance, insanity, selfishness ya viongozi wenu insane!, pelekeni jina la Makamo wa Kwanza wa Rais kwa Dr. Mwinyi!

Chadema acheni ujinga wa ignorance, insanity, selfishness ya viongozi wenu insane!, pelekeni majina ya wabunge wa viti maalum NEC
Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali
 
Makada mnalalamika nini?
Makamanda hatutaki kuwa pamoja ninyi,shangilieni mfrahi maana sasa chama kimeshika hatamu

Vyama vya Act ACT wazalendo na CHADEMA ni Mali yetu hivyo maamuzi yetu ya heshimiwe

Halafu vile vitisho vya ofisi ya Msajili bwana Mutungi na Sisty Nyahoza imeishia wapi?
Si avifute usajili tuone kama nyie ni wanaume?

Nadhani ndio hii fursa ya kuvifutia usajili hivi vyama viwili na lipumba pia.

Sory kwa kuchangia ,japo ulitaka tusicomment
 
IMG_20201105_040501.jpg
 
Hauna adabu kabisa.

Hao unaowaona wana akili ndio wangetengeneza kura feki kizembe vile? atleast wangeiba kisayansi ningewaona wamaana, but not that way, wamechoka kabisa akili hawastahili kuendelea kuliongoza hili taifa.
 
Kuwaita viongozi waliodhurumiwa haki zao Insane wakati wewe mwenyewe ukijijua ni Idiot ni kutojitendea haki. Jitambue kwanza Uzuzu ulionao na Ulambamwiko, kujipendekeza na kujikomba hakukusaidii zaidi ya kukushusha.

Umeshiriki kura za maoni ukaongeza ujinga, safari hii unapata uteuzi ambao umeulilia kwa kutukana wenzio, utakapopata ndo utakamilisha kabisa mzunguko wa upumbavu.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom