omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 145
Kifupi ZITO ni mzungumzaji mzuri na anajua kujenga hoja. Sasa kwa nini maswala ya umeme, maji na usafiri ambavyo ni shida kweli KIGOMA haongei, hajengi hoja hata sisi tukaona. kama serikali itatekeleza au la ni swala jingine.
Sikufichi ndugu yangu, kwanza kauri yake kwenye utetezi wa Downs binafsi imenikera sana. Anasema ooooh, nchi itakuwa gizani, ebo, Kigoma tuko gizani kila siku mbona haji kutuhamasisha tukaandamana kuonyesha hasira zetu.
.
Hivi ndugu yangu kwako wewe mbunge mzuri ni yule anayehakikisha kuwa kila anachokifanya kwa jimbo lake ni lazima akiongelee majukwaani/redioani ama kwemye luninga? Then kwako wewe Mbunge mzuri ni Mama Sweety anayengojea kila kitu kifanyike halafu yeye kukimbilia nafasi za kuongea kujionyesha kuwa ndiye aliyefanikisha.
Inaelekea hauko hata huko Kigoma maana kama ungekuweko ama hata kama una mawasiliano na waliopo huko hasa jimboni kwa Zitto ungekuwa unajua juhudi zake katika mambo yote hayo. Inaelekea hata hotuba bungeni huzifuatilii maana katika bunge la bajeti Zitto kama WAZIRI KIVULI WA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU alielezea mengi kuhusu jimbo lake kiasi ya CCM wakiongozwa na KOMBA kuanza kumkekejeli.
Kama una uchungu kweli wa maendeleo ya Kigoma ni vyema ukajaribu hata kuwasiliana na wazee wako ama walio karibu na shughuli za utendaji huko ujue harakati za Zitto kwa miradi mbalimbali inayoendelea huko.
Na kama ni mmoja wa wale katika mchakato ondoa udhia wa kina ROSTAM then subiri wakati wa uchaguzi upate jibu......
By the way inakuwaje unamlaumu Zitto kwa kuwa na msimamo wa kuwa ni muhimu kununu mitambo ya umeme ya Dowans ambayo kiasi fulani itasaidia kuondoa tatizo la umeme Kigoma kwa haraka zaidi kuliko mipango ya muda mrefu iliyokuwepo halafu wakati huohuo unaonyesha kukerwa na tatizo la kukosa umeme huko kigoma?
omarilyas