Rais Samia: Wanaosema tunakopa sana, waseme pia tunalipa sana

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akishuhudia Sherehe ya Utiaji Saini Mkataba wa SGR LOT 6 (Tabora - Kigoma) katika Ukumbi wa Kikwete Hall - Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Desemba, 2022.


Utiaji saini huo utahusisha kati ya Serikali kupitia Shirika la Reli na Kampuni za ubia wa CCECC na CRCC kutoka China.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla anazungumza:
Hali ya usalama ni shwari, nashukuru kwa Shilingi Bilioni 12.3 ulizotupa za kujenga madarasa 618, nikuhakikishe hakuna mtoto ambaye hatakwenda shule

Dar ndio Jiji la kibiashara, sisi ni wanufaika wa kwanza wa mradi wa SGR, hivi karibuni ulinipa fursa ya Kwenda kuifunza mambo ya usafi Rwanda, wanakushukuru kwa kufungua biashara.

Unayoyafanya yameandikwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, chama cha siasa kazi yake ni kushika dola, unayoyafanya unatekeleza kile kilichopo kwenye ilani.

Ukishaona mtu mzima anacheza michezo ya kitoto kwa mfano ‘hide and see’ au kujipikilisha ujue mambo sio mazuri, juzi tumesikia wenzetu wanachagua Bunge la Mtandao, linaitwa Bunge na lina Spika, sasa hapo tunaona kabisa wanacheza mchezo wa hide and see, wamechanganyikiwa, hii ni kutokana na kazi nzuri unayofanya.

Masanja Kadogosa, Mkurugenzi wa TRC anazungumza:
Utiaji Saini huu wa leo unafanya utimilifu wa reli ya kati, kutoka Dar- Mwanza na Dar-Kigoma, kwingine kote kutakapofuata ni reli za matawi

Mheshimiwa Rais ulisema tuanze kujenga reli kuelekea DRC kwa kuwa tusipofanya hivyo wenzetu watajenga

Kwa ujenzi huu wa jumla wa kilometa 2102 unaifanya Tanzania kuwa Nchi yenye ujenzi wa SGR ndefu kuliko zote Afrika.

Reli ya SGR itaunganisha bandari ya Dar, DRC kupitia bandari ya Kigoma, hivyo katika miji mikubwa ndani ya DRC tutakuwa tumefikia miji mitatu yenye idadi kubwa ya watu, hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara.

Ujenzi wa Tabora-Kigoma una kilometa 506, tutakuwa na station 10, vituo vikubwa vya miziko Uvinza na Katosho.

Thamani ya mkataba ni Dola bilioni 2.21 bila kodi, ukijumuisha kodi inakuwa Dola bilioni 2.7 sawa na Tsh. Trilioni 6.34 na ujenzi huu unatarajiwa kutuchukua miezi 48.

Kwa kusaini kipande hiki, Serikali itakuwa imewekeza Dola Bilioni 10.04, sawa na Tsh, Trilioni 23.3 kwa maana ya awamu ya Dar-Mwanza na Tabora-Kigoma.

Mikataba yote tuliyosaini haitakuwa na mabadiliko ya bei, mfano bei ya vitu vya ujenzi ikibadilika na bei ibadilike, hiyo haitakuwepo. Kama tukekubali hilo inamaanisha kuwa kungekuwa na nyongeza ya zaidi ya Dola Bilioni 1.304.

Hii inamaana kungekuwa na ongezeko la 30.3%, kwa maana ya thamani ya fedha.

Serikali inaendelea na ununuzi wa vitendea kazi, tumenunua mabehewa 59, ambapo tayari mabehewa 14 mapya yameingia, kuna mabehewa 30 na vichwa viwili 'used' vitaingia Machi – Aprili 2023.

Tulikuwa na matatizo na msambazaji wa kwanza wa Uturuki, tuliamua kuvunja mkataba baada ya kushauriana Serikalini, tukampa mtu mwingine aliye Ujerumani kwa ajili ya kumalizia kazi, tulifanya maamuzi hayo kwa nia njema.

Pia tuna vichwa vya treni 17 kutoka Korea Kusini, vitaanza kuingia Juni 2023, tuna seti 10 ya treni za kisasa (EMU), ambapo seti mbili za kwanza zinaingia Juni 2023.

Tuna mabehewa ya mizigo 1430 kutoka China, yataingia Nchini Septemba 2023, kuna vifaa kutoka Korea Kusini, hivyo uwekezaji huu kwa jumla unafanya kuwa na thamani ya jumla Dola milioni 557.731 sawa na Tsh. Trilioni 1.29

Niweke wazi pia tenda ya ununuzi ilitangazwa mara mbili lakini hatukupata mtu wa uhakika, tukaamua kwenda kwa mzalishaji moja kwa moja.

Kuna kampuni kutoka Urusi, Korea Kusini, Japan, Ujerumani, Uholanzi, Malaysia ambazo zilifuata taratibu zote na mwisho tukapata 'lowest evaluated bidder' lakini kwa kujali ubora na kujali mahitaji yetu tuliyowaambia.

Hivyo, yanayozungumzwa kuhusu bei ni mambo ya mitandaoni tu.

Pamoja na ujenzi wa miundombinu, TRC kwa kushirikiana na TANESCO tunajenga line ya umeme wa kujitegemea, kwa maana tutakuwa na line ya kwetu haitaingiliana na line yoyote kwa ajili ya kupata umeme wa uhakika.

Tunafurahi kwa kuwa ndani ya siku mbili hizi tutakuwa na mchakato wa kujaza maji kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere, na sisi tutaenda.

Rais Samia Suluhu Hassan anazungumza:
Namshukuru Mungu kutupa idhini ya kukutana hapa kushuhudia utiaji saini kati ya TRC na kampuni zilizotajwa za kichina, na tuombe Mungu atupe idhini ya kushuhudia kukamilika kwa mradi huu.

Mabehewa tumeyaona na mengine tumeambiwa yanakuja. Hii inafanya gharama za uwekezaji kufikia Bilioni 10.04. Fedha hizo zote ni mikopo, wanaosema awamu hii imekopa sana, waseme pia awamu hii imejenga sana, wasijifanye kama wanaume wa kiislamu, Quran inaruhusu waoe wanawake wanne lakini hawaendelei mbele kusoma inasemaje?

Mfano mwezi huu kuna vijimaneno serikalini hakuna pesa, ni kweli. Mikopo imechelewa kuja, na mikopo miwili ime mature kwa pamoja ilibidi tulipe.

Mikopo hii lazima tulipe, huo ndiyo uungwana. Kuna wakati tutaomba msamaha, bado hatujawa wa kuomba msamaha. Lazima tulipe.

Uvinza kwenda msongati kwenye nickel napo mambo yakiwa tayari tutasaini.

Ndugu wananchi, serikali kwa upande wake itaendelea kujenga miradi hii ya kimkakati ili kuendelea kukuza uchumi. Uwekezaji unakwenda pande zote, kwenye SGR pia tunafufua reli za zamani ili kuunganisha bandari zote na reli zote.

Lengo la serikali ni kufanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji na biashara. Nawataka wote wanaohusika na usimamanizi wa ujenzi wa miradi hii kufanya wajibu wao kama inavyotakiwa.

Mradi huu wa SGR umetoa ajira zaidi ya watu 20,000, pia serikali imekusanya kodi bilioni 949 kutoka local content.

Tanzania tumewekwa pahali pazuri na Mwenyezi Mungu, tuna bahari, maziwa makubwa, mito na nchi yetu inapakana na nchi 8. Nataka kusisitiza kwamba fursa hii haiwezi kunufaisha taifa kama hatutaitumia vyema. Tutumie fursa yety hii kijografia.

Niendelee kuitaka wizara, bodi ya wakurugenzi na TRC kuendelea kusimamia miradi hii ikamilike kwa wakati unaotakiwa.

Tumeoneshwa mabehewa hapa, hata kama ya kukarabati, si mabehewa yanayotumika sasa hivi. Niliwahi kupanda treni daraja la kwanza, mabehewa hayo siyo hata hadhi ya tatu ya mabehewa ya sasa. Niwaahidi kwamba serikali yenu tutaendelea kufanya mambo mazuri zaidi.

Nawashukuru, namuomba Mungu aibariki nchi yetu.
 
Mambo mazuri kama haya yatakiwa yawe yanelezewa kwa kina na watendaji kwa maana ya wizara na wengine ili wananchi wawe wanelewa kwa kina jitihada zinazo fanywa na Rais wetu.

Ufafanuzi kwa lugha rahisi ili mwananchi wa kawaida aelewe, kuna baadhi ya misamiati ikitumika inawababaisha sana wananchi kama LOT n.k epukeni
 
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushuhudia utiaji saini Mkataba wa SGR LOT 6 (Tabora - Kigoma), Ikulu, Dar e Salaam, leo Jumanne Desemba 20, 2022

Utiaji saini huo wa Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya SGR, kipande cha Tabora – Kigoma utahusisha kati ya Serikali kupitia Shirika la Reli na Kampuni za ubia wa CCECC na CRCC kutoka China.
Hawa wachina si walizingua hawa
 
Mambo mazuri kama haya yatakiwa yawe yanelezewa kwa kina na watendaji kwa maana ya wizara na wengine ili wananchi wawe wanelewa kwa kina jitihada zinazo fanywa na Rais wetu.

Ufafanuzi kwa lugha rahisi ili mwananchi wa kawaida aelewe, kuna baadhi ya misamiati ikitumika inawababaisha sana wananchi kama LOT n.k epukeni
Umenena pointi muhimu.
 
Bado najiuliza sipati majibu, ...kama tumeamua kujenga reli ya kisasa, SGR_TZ .... Pembeni ya reli ya zamani MGR_TZ:

1.Reli inakamikima, Kwa nini tuliamua kununua mabehewa ya mitumba badala ya mapya? Kulikuwa na haraka gani ya kuagiza mitumba badala ya kutoa order yanunuliwe mapya?

2. Kama zimeagizwa Rolling Stock 5 mpya za kutumika kwenye reli mpya, kwa nini chaguo letu lilijikita kwenye treni zenye speed ya hadi kilometra 160 kwa saa? Kwa nini hatukuchagua kilometa 250-300 au hata zaidi, kwa maana ya kisasa zaidi, ukizingatia ukubwa wa nchi yetu yenye zaidi ya kilometa 900 elfu za mraba?

3. Wametumwa vijana wa kitanzania kwenda Korea ya kusini kujifunza namna ya kuendesha na kuhudumia wasafiri wa reli na treni yetu ya kisasa, Je,ni teknolojia ipi wanaenda kujifunza? ni hii ya MGR au SGR ?

Baada ya miaka kumi tutawatuma kujifunza tena baada ya hii teknolojia ya sasa tuliyochagua kuwekeza kupitwa na wakati?.

Maswali niliyonayo ni mengi mno kwenye uwekezaji huu....natamani kusoma maoni ya wengine kwenye uzi huu kwanza! 🤔
 
Ujinga kama hizi bado ziko Afrika kwa mtu mweusi tu. Kwanini tunataka mambo makubwa ya kizungu halafu tunayaendea kiswahili, weka reli ya kisasa weka treni mpya za kisasa za spidi kubwa ili watu walipe bei zako kubwa kwa kuwa watawahi wanakokwenda!

Weka reli mpya weka na mabehewa mpya hatutaki uchafu wa mabehewa wachina washayajambia weee!!mabehewa mapya yatadumu muda mrefu na kukuepusha na hasara za kufanya maintenance kila siku ujinga mtupu.

Treni mwendo wa konokono km 160 kwa saa eti ulivyo bwege unaweka bei za safari za ndege yani bei za SGR ni kubwa maradufu kuliko bei za bus elfu 10 tu Dar Moro halafu mwendo wake wa jongoo!!

Nani atalipa nauli sijui Dar - Moro 30,000 tsh kwa treni inakimbia km 160 kwa saa hata Bajaj inawahi mjini Moro, Waziri wa uchukuzi achana na akili za kimaskini vunja kibubu weka kichwa kipya cha treni ya SGR spidi km 250 - 500 kwa saa.

Mi nikiri nimezaliwa mjini baba yangu afisa wa sirikali nimekunywa chai ya maziwa tu nikiwa mdogo sasa nachukia sana maamuzi ya kishamba na kijinga ya nchi hii inayokamua maskini matozo kibao na hii maamuzi mengi ya kijinga ni sababu mabosi wengi bongo wamezaliwa kijijini wana akili za kimaskini mamlaka makubwa , huko bush wamelala njaa , viatu vya kushea ukoo mzima, nguo nzuri pea moja ya kuendea kanisani, maji ya matope ya kuchota kisimani kijiji cha jirani, mwanga wa kibatari umeme hamna, kupikia kuni kwenda kuziokota porini na kukimbizana na mafisi na ngiri, hawa policy makers wa bongo wengi ni wabush vijiji haviwatoki kichwani hata wakiwa makamishna wa TRA au BoT.

Tuleteeni SGR kama ulaya sio ubabaishaji mnatumia kodi zetu Mungu anawaona mjue! Mama SSH unafanya kazi iliyotukuka nakukubali sana nakuombea kila siku ila naomba nikukumbushe hili ' kila mtu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga' tuwekee SGR ya kiwango cha juu!

Hivi mbona hawa watu wajinga wafanya maamuzi hawaishi serikalini? Hawafi tu tupate maendeleo? Miaka 60 ya uhuru bado mabosi wajinga wapo tu!!
 
Kama mabehewa ya treni ya umeme tunategemea kuyapata juni 2023 kwa maana iyo sgr itaanza utendaji wake kuanzia mwakani katikati au mwishoni 2023 na si vinginevyo
 
Hizi kazi mnawapa wachina ziende sambamba na maendeleo ya watu.

Tusishangilie tu kusaini mikataba huku hawa wachina tunaishia kuwalipa hela na wao na kuwafanya watu wetu watumwa kwa kuwalipa ujira mdogo, kutozingatia usalama kazini, kutowapa mafunzo, kufanya kazi kienyeji kiasi cha watu kutokuwa nachakujifunza, unyanyasaji uliokithiri nk.
 
Kwanini hizo pesa ambazo tunalipa sana tusiache kukopa tukalipa nusu na nusu nyingine tukafanya yale ambayo tumekopa kuyafanya ?!!!

Kukopa sio Sifa wala sio Ujuzi hata Matonya angeweza kukopa let alone kuomba...

By the way sentensi sahihi ni wanakopa sisi tunalipa....
 
Nimefarijika kuona hiyo reli inaenda Kigoma, kwa lengo kuu la kusafirisha malighafi kutoka DRC.

Serikali ianze mikakati mapema ya kunufaika na malighafi kutoka Congo. Ikewezekana wajenhe mapema masoko ya madini ya kutosha tu huko Kigoma. Lakini pia wajenge mitambo ya kuchenjua hayo madini, ili yakitoka hapo; ni sokoni moja kwa moja.

NB: Relo iishie mpakani tafadhali. Utakuwa ni ujinga wa hali ya juu iwapo serikali itakubali kushirikiana na hizo nchi kwenye ujenzi wa reli ndani ya nchi zao. Maana sisi tunajenga kwa jasho letu.

Kamwe tusikubali madudu kama yale ya TAZARA! Yaani yale majamaa ni mavivu, na muda wote yanawaza starehe tu! Na mtazamo wangu, nahisi yanachangia karibia 60% kwenye kuizorotesha hiyo reli.

Na chakushangaza, sijui Wachina waliingia mkataba wa aina gani na hizi nchi mbili! Maana sioni sababu ya nchi zote mbili kuendelea kushirikiana kuiendesha hiyo reli ya TAZARA. I wish kila nchi ingejitegemea kuendesha reli yake.
 
NB: reli iishie mpakani tafadhali. Utakuwa ni ujinga wa hali ya juu iwapo serikali itakubali kushirikiana na hizo nchi kwenye ujenzi wa reli ndani ya nchi zao. Maana sisi tunajenga kwa jasho letu.

Rejea #Ushiriki wa Tanzania kwa nchi nyingi za Afrika kupata uhuru!. Hili lilituchekewesha.
 
Asante sana Dkt Hangaya , sasa tueleweshe kwenye kipengere kidogo tu hiki chenye utata , naomba niongee kwa sauti ya chini sana , ni hivi , KAMA TUNALIPA MBONA DENI LAZIDI KUPAA ?

Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom