Wabunge wa Kigoma wana Matatizo gani?!

Kifupi ZITO ni mzungumzaji mzuri na anajua kujenga hoja. Sasa kwa nini maswala ya umeme, maji na usafiri ambavyo ni shida kweli KIGOMA haongei, hajengi hoja hata sisi tukaona. kama serikali itatekeleza au la ni swala jingine.

Sikufichi ndugu yangu, kwanza kauri yake kwenye utetezi wa Downs binafsi imenikera sana. Anasema ooooh, nchi itakuwa gizani, ebo, Kigoma tuko gizani kila siku mbona haji kutuhamasisha tukaandamana kuonyesha hasira zetu.
.

Hivi ndugu yangu kwako wewe mbunge mzuri ni yule anayehakikisha kuwa kila anachokifanya kwa jimbo lake ni lazima akiongelee majukwaani/redioani ama kwemye luninga? Then kwako wewe Mbunge mzuri ni Mama Sweety anayengojea kila kitu kifanyike halafu yeye kukimbilia nafasi za kuongea kujionyesha kuwa ndiye aliyefanikisha.

Inaelekea hauko hata huko Kigoma maana kama ungekuweko ama hata kama una mawasiliano na waliopo huko hasa jimboni kwa Zitto ungekuwa unajua juhudi zake katika mambo yote hayo. Inaelekea hata hotuba bungeni huzifuatilii maana katika bunge la bajeti Zitto kama WAZIRI KIVULI WA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU alielezea mengi kuhusu jimbo lake kiasi ya CCM wakiongozwa na KOMBA kuanza kumkekejeli.

Kama una uchungu kweli wa maendeleo ya Kigoma ni vyema ukajaribu hata kuwasiliana na wazee wako ama walio karibu na shughuli za utendaji huko ujue harakati za Zitto kwa miradi mbalimbali inayoendelea huko.

Na kama ni mmoja wa wale katika mchakato ondoa udhia wa kina ROSTAM then subiri wakati wa uchaguzi upate jibu......

By the way inakuwaje unamlaumu Zitto kwa kuwa na msimamo wa kuwa ni muhimu kununu mitambo ya umeme ya Dowans ambayo kiasi fulani itasaidia kuondoa tatizo la umeme Kigoma kwa haraka zaidi kuliko mipango ya muda mrefu iliyokuwepo halafu wakati huohuo unaonyesha kukerwa na tatizo la kukosa umeme huko kigoma?

omarilyas
 
mimi ni mdau wa masuala ya elimu. nataka kujua Zitto amefanya juhudi gani kuinua kiwango cha elimu katika jimbo lake? napenda kujua perfomance ya shule za msingi na sekondari zilizoko jimboni kwa Zitto Kabwe.
 
Sasa kigoma sisi hatuna umeme siku nyingi 2, sasa kukuosa kwetu umeme si ni moja ya kutojengwa viwanda kweli.

Hali ya kigoma ni hali ambayo wangeweza kuungana wabunge wa kule na kutoa tamko au msimamo flani lakini, kimyaaaaaaaa.

Ni kweli you don't have it.lakini kwa taarifa nilizo nazo hapa Kuna project ya Tanesco hapo mto malagarasi ya kuzalisha Megawati 8 then itasambazwa kigoma mjini na wilayani,then matengenezo ya zile mashine za kuzalisha umeme zilizoharibika are in progress.
Inatia uchungu sana ndugu,unajua Kigoma ni mkoa mzuri sana kwa kilimo mazao kama michikichi,kahawa pale manyovu inakubali,na uvuvi pia.Tatizo mkoa huu hauna miundo mbinu kama barabara na umeme wa uhakika ndio maana hakuna shughuli za kueleweka.kabla ya vita ya Congo na Burundi mambo yalikuwa mazuri kidogo watu waliweza kufanya biashara na nchi hizi jirani baada ya vita mambo yakawa mabaya sana mzunguko wa biashara ukafa kabisa.Kama serikali yetu na viongozi wake wangekuwa watu makini wakaacha siasa mkoa huu ni muhimu sana katika uchumi wa taifa hili.soma hiyo article hapo chini.

006-02-28 15:31:04
Na Aziz Issa
Watu 500 watanufaika na ajira katika mashamba na kampuni mpya ya Felisa itakayojishughulisha na kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma.
Ujenzi wa kiwanda hicho unafanyika katika eneo la Mahanga, kata ya Ilagala.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dk. Hamimu Hongo amesema wameazimia kutumia teknolojia ya kisasa kuzalisha nishati ya mafuta aina ya dizeli kutoka katika mbegu za michikichi.
Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hicho, Balozi wa Ubeligiji nchini, Peter Baddens amesema uzalishaji mafuta hayo utakapo anza utapelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama kubwa ya matumizi ya nishati ya dizeli nchini.
Pia ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kutoa ardhi kwa kilimo cha zao hilo na kuweka mitambo ya kutengenezea dizeli.
Mashamba hayo yenye ukubwa wa jumla ya ekari 150, yatatumiwa kwa kilimo cha michikichi, alizeti na pia ujenzi wa kiwanda cha mafuta.
SOURCE: ALASIRI

Projets kama hizi nizinahitaji mioundo mbinu madhubuti kama umeme,maji na barabara bora.maji ziwa lipo.nafikiri serikali imefika wakati iache siasa tupate maendeleo.ukiwekeza kigoma hawato faida kigoma pekee ni Tanzania nzima kwa ujumla.Zitto pigania hili.
 
MTIZAMO WANGU!kigezo sio UBUNGE WA KIGOMA!unapomuangalia zitto,ni MBUNGE MZALENDO,ALIYEWEKA UTAIFA MBELE.kama viongozi weu wa serikali wanazingatia maadili na nidhamu za kazi,ZITTO YUPO SAHIHI SANA kupigania maslahi ya nchi,na taifa zima,kwa sababu automatically kila sehemu,kila kona ya nchi itapata RELIEF!zitto angepoteza sana muelekeo kama angesimama bungeni kuiongelea kigoma PEKEE!

KGM ndugu yangu,wabunge wa sehemu tajwa HAWANA COLLECTIVE PROBLEMS!mmoja anakomaa na OIC,mmoja anatetea ufisadi,na mwingine anaangalia maslahi ya taifa.kila mtu anatenda kadri UTASHI NA BUSARA YAKE INAVYOMTUMA!sasa wewe ndio unatakiwa kuchekecha naaaaaani mbunge bora,na nani BORA MBUNGE!

HALLA!
 
Naomba nipate michango yenu wanajamii, kutokana na mimi binafsi kutowaelewa Vizuri wabunge wa KIGOMA

Sijui niseme wanauzalendo sana kwa mambo ya kitaifa au ni vipi, wanashadadia sana mambo mengine lakini MATATIZO ya wana KIGOMA hata hawayaoni.


Angalia mifano.
Mh ZIto na mawaswala ya kitaifa na sehemu nyingine kama mambo ya Downs, BUZWAGI, KIWIRA,

Mh Shelukamba yeye amejikita kwenye utetezi wa mafisadi wote mnajua.


Bwana Msambya ya yeye ni UDINI, yakija mambo ya OIC na Mahakama ya Kadhi, Bungeni panajimbika.


SASA wanajamii, mbon matatizo makubwa ya wanaKIGOMA kama Usafiri, Maji na UMEME wala hayawasumbui wako kimyaaaaaaaaaaa, nini TATIZO lao.

Hivi ndugu zangu kuna mtu asiyefahamu kuwa wana KIGOMA ndio waathirika wakubwa wa usafiri wa Reli ya KATI, mbona wabunge wetu hawakomalii issue za hawa mafisadi wa kihindi walioko pale kwelye shirika la Reli badala yake wanakomalia vitu vingine kabisa?

Hivi Mh Zito hajui kuwa kigoma wapo GIZA kila siku, mbona hilo halimsumbui badala yake anakomalia mitambo ya Downs ambayo najua kabisa haitawapatia wanakigoma umeme.Kigoma siku zote iko giza, hakuna mbunge wa kigoma anayeinua mdomo kulisema.

Wanajamii, utashangaa, pamoja na Kigoma kuwa na Ziwa, lakini mji ule hauna maji. Hilo wala halimsumbui ndugu yetu Serukamba, yeye kutwa, kuchwa michango yake ni utetezi wa mafisadi bungeni. Ataongea mpaka utamuonea huruma kwa mishipa na mate kumtoka, nini Tatizo la wabunge wetu? Au ni kwa kwa kuwa wao wenyewe hawaishi kule, au ndio kutaka sifa tu au nini.

Nisaidieni wanajamii, niko kwenye TUTA.

Pengine kuna mambo mawili yaliyokupelekea kupostm thread hii. Aidha hufatilii mtiririko wa shughuli za Bunge au unaongozwa na Bifu juu ya mmoja au zaidi ya Wabunge uliowataja?
Kwa kawaida habari za Bungeni zinazochukua muda na publicize zaidi nimambo makubwa yanayoikabili Taifa kwa ujumla. Fanya utafiti na utaona kuwa habari za majimbo ambazo zitachukua attention ya waandishi nilabda kutokee mapigano, msuguwano, mauwaji na mapambano ya uchaguzi.
Hata kwenye mtiririko wa shughuli za Bunge utaona kuwa Mbunge anasimama na kutishia kutowa Shillingi katika Bajeti kwa sababu ya mradi fulani jimboni mwake na hali ikizidi Waziri Mkuu anasimama na kutowa ahadi ya kufatilia mradi huo na suala humalizika hivyo, sasa nduyu yangu unategemea kuwa publicize ya matatizo ya Kigoma itawapatia Habari ya kuuza waandishi wa Habari? Hiyo ndiyo sababu ya wewe kutowasikia sio wabunge wa Kigoma tu bali hata wa Mikoa mengine.
Suala jengine ni kuwa hawa wabunge unaowataja wao wanatumiwa kama wasemaji wa wabunge wengi ambao hawana ubavu wa kueleza kuchukizwa kwao na mfumo wa serikali kwani kutawaharibia kwenye Chama chao. Hivyo umesahau kuwa labda miaka miwili tu iliyopita Wabunge wa upinzani wakizomewa katika Bunge ili kuwakatisha tamaa na jitihada zao? Ingefanyika hivyo hata sasa haokina Zitto na Slaa wangekuwa wakifungiwa kwenye Bunge kwa "kusema uongo".
Halafu ndugu yangu ivyo umesahau kuwa Mtukufu Rais alishasema huko Kigoma na hivi karibuni Pemba kuwa Wabunge wa Upinzani hawataweza kuleta maendeleo yoyote kwenye jimbo na walio na uwezo na haki ya kuleta maendeleo ni CCM pekee? Hata hivyo Wana Kigoma wenyewe tuwaachie waamue iwapo Wabunge wao hawawakilishi kama walivyowatuma.
 
Kujaribu kumbebesha Zitto lawama ya kutoendelea Kigoma au kutochangamkiwa Kigoma ni kujaribu kukwepa ukweli. Matatizo ya Kigoma hayatokani na Zitto kupiga kelele au kutopiga kelele! Matatizo ya Kigogoma yamefungamana kwa miaka karibu 50 na utawala wa Chama cha Mapinduzi.

Ni chama cha Mapinduzi chenye serikali na chenye sera za sehemu mbalimbali na miradi mbalimbali. Wakati wenzenu Dar wanazungumzia kujengewa Flyovers nyinyi Kigoma hata reli ya kati haijatengemaa! Sasa hivi kutoka Arusha kwenda Mbeya ni karibu kwa masaa kuliko toka Dar hadi Kigoma ingawa kijiografia Kigoma ni karibu na Dar kuliko Mbeya na Arusha!!!

Jinsi unavyozungumza ni kana kwamba Zitto hajawahi kuzungumzia masuala ya Kigoma au wapiga kura wake Bungeni. Naomba utuletee rekodi ya Zitto Bungeni kuhusu masuala haya maana inawezekana wakati anayazungumza hukuyasikia.

Lakini zaidi ni kuwa, kama Kigoma wakitaka mabadiliko ya kweli ni wao wachukue hatua za kurudisha kadi za CCM!! na kuifuta CCM kwenye utawala wa mkoa wao na kuchagua chama ambacho kitakuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia raslimali zenu na chenye kuweza kupiga "kelele" bungeni. Vinginevyo, lawama kwa mtu mmoja kwa matatizo ya mkoa mzima ni kukwepa ukweli kuwa wenye wajibu na wenye kustahili lawama ya kudumaa kwa Kigoma (kama ilivyo Mtwara, Lindi, Tabora n.k) ni serikali ya CCM tu.

CCM ndiyo sababu, Zitto ni kisinigizio!

Mwanakijiji,

Matatizo ya Tanzania hayatokani na CCM, yanatokani na ukoloni uliokuwepo miaka 100 iliyopita kwi kwi kwi!!!!

Mkuu miaka mitano ni mingi mno kuweza kuleta mabadiliko hasa kwa sehemu ambayo maendeleo yako chini mno. Haya mambo ya kulaumu wa nyuma ni ujinga mtupu.

Ukishindwa ku deliver kaa kimya, haya ya nani alikuwa anaongoza miaka 10 au 20 iliyopita
ni siasa za wasanii majukwaani.

Sina data kama mhesh. Zitto ana deliver Kigoma au la ila kuanza kuongelea walioshindwa huko nyuma ni kupoteza muda tu. Yeye alipoamua kugombea aliona ya hao walioshindwa na alienda pale ili kujaribu ku reverse hiyo trend.

Mheshimiwa Zitto chakarika mkuu, charity starts at home! Ndio ni sawa kuhangaika na mambo ya kitaifa lakini pia lazima nguvu kubwa iwekwe kwenye kuendeleza jimbo lako.
 
Tanzania hii ukiifikiria unaweza kulia machozi . Naukumbuka wimbo wa Bob Marley wa" RAT RACE" kuna sehemu anasema " In the abundance of water the fool is thirsty" sasa ndio hawa viongozi wetu. Kigoma imejaliwa vingi Ardhi yenye rutuba, Mbuga nzuri ya wanyama ya Gombe, Ziwa wanalima Mawese ambayo ni zao kuu hata kule Malaysia na ndilo lililowatoa, wanapakana na mataifa mengine kama vile Rwanda, Burundi na DRC kwa hiyo ungetakiwa uwe mji wa kibiashara. Pia Kigoma ni mji wa kihistoria aaah nitalia jamani hii nchi! Inasikitisha sana wajameni Mijitu ikikutana huko bungeni baada ya mijadala ni stori za kwenda Kongwa kunywa na kula nyama na totozz za CBE. Ah ishu kama hizo ni privacy lakini imenibidi niziweke kwa sababu hakuna lolote wanalofanya at least tungeona mabadiliko basi. Angalau Zitto anajitahidi lakini ni wangapi wanaomuunga mkono? Hakuna wanasema aah huyu bwana mdogo mtu wa juzi ataweza nini bwana. Mimi nadhani umefika wakati wa vijana wenye ari sasa. Angalau wanaweza kuleta mabadiliko.
 
Mawazo kuhusu Kigoma yamekuwa mengi lakini mapendekezo/ushauri wa nini kifanyike yamekuwa machache. Mengi yaliyotolewa na wachangiaji ni mambo yanayohusu watu (ambayo kwa hivi sasa Tanzania ndio ya msingi kwa wengi) na hayahusu issues. Na ndio maana wanatajwa zaidi Zitto Kabwe na Peter Serukamba wakati Mkoa una wabunge kibao.

Ili Kigoma iendelee ni lazima ifuate nyayo za mikoa mingine iliyopata mafanikio ya maendeleo kama ifuatavyo:-

1. Kigoma ina uwakilishi wa kutosha katika Bunge.
a) Zitto Kabwe
b) Peter Serukamba
c) Manju Msambya
d) Swanzungwako
e) Kijiko
f) Christopher Chiiza
g) Mporogomy
h) Mhonga
i) Josephine
Kiidadi hao ni wabunge 9 na wanatosha kabisa kuleta maendeleo. Jambo la kwanza la kufanya ili
kuwa effective, ni lazima wawe na forum ya pamoja, waache itikadi zao za kisiasa (CCM na
Chadema), kikabila (uha, utusi, uhutu na umanyema), uzawa (Ukasulu, Ukibondo, Ukigoma) na
kidini (uislamu na ukristo) na wawe na mikutano ya mara kwa mara na kukubaliana ni nini wafanye
kuhusu maendeleo ya Kigoma na jinsi ya kuibana serikali.

2. Kigoma ina rasilimali nyingi, hasa ardhi iliyo safi 100% ya mkoa. Hakuna hata sehemu
moja ya jangwa. Studies nyingi za kichumi zimefanywa kuhusu Kigoma. Agenda kuu ya
ushirikiano huo wa wabunge iwe ni kupitia study hizo na kujiwekea malengo ya
utekelezaji wake hata kidogo kidogo katika muda wa ubunge wao.

3. Wana Kigoma waliopo Kigoma na nje ya Kigoma wasisubiri msukumo wa Serikali kuleta
maendeleo bali waanzishe taasisi zao za kijamii ili waweze nao kuchangia katika
maendeleo yao na hivyo wapate sababu ya kuibana serikali ili nayo itimize wajibu
wake. Anagalieni mikoa mingine. Kila mkoa una jumuia ya wanamkoa ule hapa Dar es
Salaam na mkoani kwao. Jumuia hizi zimefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo ya kiuchumi
mikoani mwao. Pawe na ushirikiano kati ya taasisi hizo na wasaidiane inapobidi. Maana
yangu hapa nikuwa wawe na lengo moja.

4. Wana Kigoma walioko madarakani au katika nafasi za kujulikana nje, watumie nafasi
hizo kupata misaada moja kwa moja toka nje specifically kwa maendeleo ya mkoa
wao. Naona wazungumze na watu kama vile Mungai, Msuya, Mramba etc wajue ni
mbinu gani walizozitumia kusukuma mbele maendeleo ya maeneo yao.

5. Kwa pamoja, wabunge na taasisi za kijamii ziwahamasishe wakazi wa kigoma kuhusu
umuhimu wa uchapaji kazi na waondokane na hali ya sasa ya kukata tamaa na kuona
kama wanaonewa. Wapunguze siasa na waelekezo nguvu zao katika maendeleo ya
kiuchumi.

6. Wote wahusika watambue mithali ya wahenga kuwa "umoja ni nguvu na utengano ni
udhaifu". Na umoja huu utapatikana kama wataachana na tofauti zao zilizopita na
kuanza ukurasa mpya.
 
Jamani, Kigoma tuna taabu, tuna shida, tuna matatizo. Imenichukua muda sana kufikiria namna ya kuchangia hii thread kwa jinsi nilivyo na uchungu maana sijui nianzie wapi. Kwa ujumla nimepata kigugumuzi hadi nikafa ganzi.
Barabara zetu zinawekwa matope (wenyewe wanaita kifusi), baada ya hapo hakuna kinachoendelea. Usafiri wetu: Treni ndiyo hiyo. Mabasi yetu ya ndani na yale yanayokwenda nje ya Kigoma ni lazima udungwe kwanza anti-tetanus kabla hujapanda, vinginevyo unaweza kupata jeraha ndani ya basi bila ya kupata ajali na ukaishia pagumu. Umeme tumeshasahau, ni zaidi ya miezi miwili sasa. Maji ni ndoto ingawa tunalo ziwa kubwa na ambalo lingeweza kuwa "mlango" wa kutokea Kigoma. Hospitali zetu..... mama yangu we!

Tunashukuru kwa kelele za Mh. Zitto Bungeni na kwingineko zinazoonyesha utaifa wake, lakini kwa mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa anapoona hakuna mabadiliko katika jimbo analotoka Mh.
Tunashukuru pia kufahamu kwamba Mh. Zitto ana "things-to-do list" na kwamba ameshakamilisha zaidi ya 99% katika checklist hiyo. Sasa swali: Hivi kukiwa na dharura ya nyumba kuungua moto, ina maana Mh. hawezi kuzima kwa sababu haimo kwenye list?
Sitaki kumlaumu Zitto peke yake - kwa mtazamo wangu Wabunge wa Kigoma hawashirikiani kwa maslahi ya wapiga kura wao. Kukosa mshikamano baina ya Wabunge ni sehemu mojawapo ya kuzama kwa jahazi la maendeleo la Kigoma.
Nakubali kwamba sisi wenyewe wana-kigoma pia ni sehemu ya tatizo km vile wale wanaocheza bao kutwa nzima. Lakini binadamu hatufanani. Wengine wanahitaji kusukumwa ili wajitambue na kujishughulisha kwa maendeleo yao wenyewe. Wengine hadi wachapwe viboko. Basi Wabunge wetu wafanye hata hilo tu (sio kutuchapa viboko). Lakini badala yake wako Dar siku zote. Nakubaliana na mchangiaji aliyesema tumefanya makosa kuchagua Wakazi wa Dar.

Naungana na KGM kuomba msaada wenu wanajamii - hata kwa kupiga kelele tu. Sisi wenyewe sauti zimeshakauka.
 
2006-03-26 09:01:54
By Simon Kivamwo

The Member of Parliament for Kigoma North, Kabwe Zubeiry Zitto, has welcomed the recent pledge by President Jakaya Kikwete that his government was determined to build economic infrastructure in regions styled as forgotten.

The regions are Kigoma, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Rukwa and Tabora.

The MP from the opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) told the Sunday Observer this week that, being the secretary general of the Kigoma-based MPs, he would urge his team to rally behind the President in fulfilling the pledge.

'On behalf of the MPs from Kigoma Region, I promise wholehearted co-operation to the President to make sure that the pledge bears fruit.'


He said Kigoma could not have been in its present state of poverty if previous governments had not neglected it.

...tukiwa tunakaribia kuadhimisha miaka mitatu kamili tangu zilipotolewa kauli hizi, Serikali, wabunge wa Kigoma, na watendaji nanyi msikize vilio vya wana Kigoma katika kugawana 'keki ya taifa.'
 
Kujaribu kumbebesha Zitto lawama ya kutoendelea Kigoma au kutochangamkiwa Kigoma ni kujaribu kukwepa ukweli. Matatizo ya Kigoma hayatokani na Zitto kupiga kelele au kutopiga kelele! Matatizo ya Kigogoma yamefungamana kwa miaka karibu 50 na utawala wa Chama cha Mapinduzi.

Ni chama cha Mapinduzi chenye serikali na chenye sera za sehemu mbalimbali na miradi mbalimbali. Wakati wenzenu Dar wanazungumzia kujengewa Flyovers nyinyi Kigoma hata reli ya kati haijatengemaa! Sasa hivi kutoka Arusha kwenda Mbeya ni karibu kwa masaa kuliko toka Dar hadi Kigoma ingawa kijiografia Kigoma ni karibu na Dar kuliko Mbeya na Arusha!!!

Jinsi unavyozungumza ni kana kwamba Zitto hajawahi kuzungumzia masuala ya Kigoma au wapiga kura wake Bungeni. Naomba utuletee rekodi ya Zitto Bungeni kuhusu masuala haya maana inawezekana wakati anayazungumza hukuyasikia.

Lakini zaidi ni kuwa, kama Kigoma wakitaka mabadiliko ya kweli ni wao wachukue hatua za kurudisha kadi za CCM!! na kuifuta CCM kwenye utawala wa mkoa wao na kuchagua chama ambacho kitakuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia raslimali zenu na chenye kuweza kupiga "kelele" bungeni. Vinginevyo, lawama kwa mtu mmoja kwa matatizo ya mkoa mzima ni kukwepa ukweli kuwa wenye wajibu na wenye kustahili lawama ya kudumaa kwa Kigoma (kama ilivyo Mtwara, Lindi, Tabora n.k) ni serikali ya CCM tu.

CCM ndiyo sababu, Zitto ni kisinigizio!

Hapana, Mkuu. Zitto kama mbunge wa eneo hilo hawezi kukwepa lawama kutoka kwa constituents wake. Ni lazima aonyeshe kufurukuta kwake na kama CCM ndiyo kikwazo, basi hii itawekwa wazi na wananchi wataamua ni chama kipi wakipe dhamana ya maendeleo yao katika uchaguzi ujao!

Amandla.......
 
Kutokana na mtizamo wangu...
Maendeleo ya eneo husika yanaletwa na wakazi au wananchi wa maeneo husika cha muhimu ni ushirikiano wenu wananchi katika maswala ya msingi katika maendeleo....
Angalia mfano mzuri Jimbo la Ubungo lipo mahala ambapo wakubwa kwa wadogo wanaingia jiji hili la Dar es salaama lakini pita pembeni utaona barabara mbovu afadhari hata hizo za Kigoma....Ubungo hapo hapo kuna tank la maji la Dawasa na ndipo ofisi na wizara ya maji ofisi zao zilipo cha kushangaza na kusikitisha eneo hilo hata maji ni shida tupu wananchi wanauzunguka maeneo ya Kibo,Msewe,Baruti,Coner n.k wanapata sana shida ya maji lakini wizara ipo eneo hilo hilo la Ubungo hiki kilio chao watapeleka wapi????
Kuna kipindi hata kata kata ya umeme inawaathiri sana hawa wakazi na mitambo kibao ya umeme ipo pale Ubungo....nachelewa kusema ''KWENYE MITI MINGI HAKUNA WAJENZI''
 
Isaya Mwita unapoandika kuhusu mkoa tofautisha ujiji na mkoa wa Kigoma wewe umeenda Kigoma ujiji na vitongoji vyake umefika Kasulu na Kibondo ukawakuta wanacheza bao?nafikiri unamatatizo katika kutoa hoja mimi nimefika Musoma kama unaitwa Mwita sioni tofauti ya Musoma na kigoma.
 
Mtoa maada anaelekea kuamini kwamba ili mbunge awe makini katika maswala ya jimbo lake, inabidi aache kutetea maswala ya kitaifa.

Ingawa kwa kiasi fulani hili lina ukweli (ukipewa dakika thelathini kuongea, unaweza kuelezea vizuri zaidi kama unaamua kuelezea mambo ya jimbo au mambo ya kitaifa) lakini kwa upande mwingine mimi tatizo langu siyo kwamba wabunge wanaongea mambo ya kitaifa (nahitaji waongee mambo ya kitaifa) bali ni kwa nini hawaongelei mambo ya jimboni kwao.

Kwa maana nyingine mbunge anatakiwa awe ana uwiano mzuri katika masuala yake, akitoa muda muafaka kwa mambo ya kitaifa na ya kijimbo. Akienda sana kwenye mambo ya kitaifa, ingawa atakuwa anafanya kazi nzuri, anaweza kuwapunja wapiga kura wake kwenye nyanja fulani.

Akienda sana kwenye mambo ya jimbo lake, anakuwa small minded na anaweza kuikosa "the big picture.
 
...
Wabunge wa Kigoma wana Matatizo gani?!
...ni hoja inayofaa kujibiwa na wabunge wote wa Kigoma, hata kama kuna wasemaji wao humu ndani ya JF. Naamini mh.Zitto Kabwe jana ulipokuwa online, ulichungulia pia mada hii, na ni hiari yako kujibu kwa wakati muafaka ili kuwaondoshea duku duku wana Kigoma wanao oppose na wanao propose maendeleo ya Mkoa huo, au ku "pass", ...binafsi nilitegemea utasema lolote, anyway; 'subra yavuta kheri'
 
Tehe teh teh, wana kigoma wenyewe wametulia tuli, na wanasubiri mwaka 2010 wawape wabunge wao kura tena. kwa mara ya kwanza kufika kigoma 2006 nilishock airport haina tofauti na airstrip.

Cha kushangaza sana sisi wapita njia tunasikitika sana ila wenyeji wako safi kabisa na hawana mpango wa kulalamika waletewe vitu muhimu.

this time kuna haja ya kutoa kura kwa upinzani tu! tuone mabadiliko
 
Sio kigoma tu, ni sehemu zote ambazi waarabu waliharibu hali ya hewa, yaani walileta harufu mbaya ya kuuza na kupitisha watumwa, ni kama kumelaaniwa, na hakutakuja kuendelee. mtu mwingine angefikiri kuwa sehemu ya East african long distance route(Bagamoyo,Mpwapwa and kondoa irangi,Tabora,Kigoma to Ujiji), kungekuwa na maendeleo kwasababu ndiko walianza biashara na watu wa nje mapema sana kwa maeneo ya hinterlands. lakini kinyume chake, maeneo hayo ndo yamelaaniwa utafikiri yalimwagiwa sumu. ndio maeneo ya waswahili wanaopenda kucheza bao saa sita mchana wakisubiri azana wakaswali. maeneo yamekuwa makame kabisa na ndo yanaongoza kwa umasikini na kukosa chakula kila mwaka. hata maeneo kama kigoma ambako at least ungesema ardhi ni nzuri, hakuna mvuto wa maendeleo kwasababu ya hali ya hewa waarabu waliharibu. watu wanajali zaidi kuoa wake wengi na kuzaa watoto wengi bila kuwa na uwezo kuwatunza na kuwapeleka shule au kuwalisha. wanaishia uchawi na kuvaa msuli tu asubuhi hadi jioni wakisubiri kwenda kulala.

kwa wale wanaofanya selikalini ambao walishawahi kufanya kazi Tabora mjini,kigoma,mpwapwa na kondoa, wanajua hili. watu wazima wenye nguvu wanakufuata wanakuomba hela. sio ombaomba barabarani lakini ni masikini hana kitu, anafikiri unayepata mshahara wa selikali una pesa. mawazo yao na uelewa wao uko chiiniiiii, na wanaweza wakapelekwa na aina yoyote ya upepo. hivyo, hata wabunge wao wanahitaji kukombolewa kwa kiasi kikubwa. wajifunze kwa wabunge wenzao wanachofanya. wanapigania maslahi ya taifa na hapohapo maslahi ya jimboni kwao. wao kalaga baho.
 
kama kuna mtu humu alishawahi kufanya kazi kwa mwarabu au akafanya naye joint venture/partnership kibiashara akatajirika anyoshe mkono. kazi yao kubwa ni kuiba nyota za watu wanaofanya nao kazi, kukupa pesa hewa utakazotumia kihasara, na kutukuza dini yao tu.
 
Sio kigoma tu, ni sehemu zote ambazi waarabu waliharibu hali ya hewa, yaani walileta harufu mbaya ya kuuza na kupitisha watumwa, ni kama kumelaaniwa, na hakutakuja kuendelee. mtu mwingine angefikiri kuwa sehemu ya East african long distance route(Bagamoyo,Mpwapwa and kondoa irangi,Tabora,Kigoma to Ujiji),...wanaopenda kucheza bao saa sita mchana wakisubiri azana wakaswali. maeneo yamekuwa makame kabisa na ndo yanaongoza kwa umasikini na kukosa chakula kila mwaka

...MwanawaMungu, nikirejea hotuba ya Mheshimiwa Zitto kabwe bungeni kuhusu maeneo yaliyo na umasikini mkubwa, na maeneo yaliyo na 'afueni' Tanzania, yanapingana na maeneo uliyoyataja hapo juu. Nani msema kweli hapa?

Mheshimiwa Spika, naomba niwasilishe hali ya umasikini kiwilaya kwa wananchi kwa kigezo cha idadi ya wananchi walio katika Umaskini wa kutupwa (% of households below basic needs poverty line)

Wilaya masikini Zaidi

Bunda 68%
Musoma 64%
Geita(vijijini) 62%
Mbarari 13%
Serengeti 61%
Singida(vijijini) 56%
Namtumbo 55%
Meatu 53%
Kisarawe 51%
Babati 50%

Wilaya zenye Ahueni

Bukoba Mjini 11%
Arusha Mjini 12%
Mbeye Mjini 12%
Morogoro Mjini 14%
Kinondoni 14%
Nyamagana 15%
Lushoto 16%
Ilala MC 16%
Tanga Mjini 17%

source; http://www.bunge.go.tz/bunge/docs/mipango.pdf
 
Back
Top Bottom