Wabunge wa Kigoma wana Matatizo gani?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa Kigoma wana Matatizo gani?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KGM, Feb 28, 2009.

 1. K

  KGM Senior Member

  #1
  Feb 28, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naomba nipate michango yenu wanajamii, kutokana na mimi binafsi kutowaelewa Vizuri wabunge wa KIGOMA

  Sijui niseme wanauzalendo sana kwa mambo ya kitaifa au ni vipi, wanashadadia sana mambo mengine lakini MATATIZO ya wana KIGOMA hata hawayaoni.


  Angalia mifano.
  Mh ZIto na mawaswala ya kitaifa na sehemu nyingine kama mambo ya Downs, BUZWAGI, KIWIRA,

  Mh Shelukamba yeye amejikita kwenye utetezi wa mafisadi wote mnajua.


  Bwana Msambya ya yeye ni UDINI, yakija mambo ya OIC na Mahakama ya Kadhi, Bungeni panajimbika.


  SASA wanajamii, mbon matatizo makubwa ya wanaKIGOMA kama Usafiri, Maji na UMEME wala hayawasumbui wako kimyaaaaaaaaaaa, nini TATIZO lao.

  Hivi ndugu zangu kuna mtu asiyefahamu kuwa wana KIGOMA ndio waathirika wakubwa wa usafiri wa Reli ya KATI, mbona wabunge wetu hawakomalii issue za hawa mafisadi wa kihindi walioko pale kwelye shirika la Reli badala yake wanakomalia vitu vingine kabisa?

  Hivi Mh Zito hajui kuwa kigoma wapo GIZA kila siku, mbona hilo halimsumbui badala yake anakomalia mitambo ya Downs ambayo najua kabisa haitawapatia wanakigoma umeme.Kigoma siku zote iko giza, hakuna mbunge wa kigoma anayeinua mdomo kulisema.

  Wanajamii, utashangaa, pamoja na Kigoma kuwa na Ziwa, lakini mji ule hauna maji. Hilo wala halimsumbui ndugu yetu Serukamba, yeye kutwa, kuchwa michango yake ni utetezi wa mafisadi bungeni. Ataongea mpaka utamuonea huruma kwa mishipa na mate kumtoka, nini Tatizo la wabunge wetu? Au ni kwa kwa kuwa wao wenyewe hawaishi kule, au ndio kutaka sifa tu au nini.

  Nisaidieni wanajamii, niko kwenye TUTA.
   
 2. S

  SkillsForever Member

  #2
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana inferiority complex so wanakomaa na issue moja ili iwatoe.wamesahau yaliyowapeleka bungeni ...
   
 3. N

  NTIRU Member

  #3
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo lao, ndugu KGM, ni kwamba Wabunge wa Kigoma hawana ushirikiano katika masuala yanayohusu maendeleo ya kwao Kigoma. Kama ulivyosema Serukamba ni mtetezi mkuu wa Mafisadi na alishiriki kwa nguvu zote kumsimamisha Zito bungeni wakati ule wa suala la Buzwagi. Ndugu yetu Msambya ni mwanasiasa aliyefilisika kimawazo na ndiyo maana uwakilishi wake ni wa udini utadhani wana-Kigoma walimtuma Bungeni kushughulika na maswala ya dini. Katika hali kama hiyo si rahisi Wabunge kama hao kusaidia kuleta maendeleo katika majimbo yao. Zito ni mtetezi wa Watanzania wote kwani ni yeye pamoja na baadhi ya Wabunge kama Dr. Slaa, Mwakyembe, Anna Kilango, n.k. walioibua maovu ya Richmond (Rich-Monduli), EPA, n.k. ambayo madhara yake ni kwa Tanzania yote hata Kigoma. Mimi nafikiri wa kuulizwa zaidi ni akina Serukamba na Msambya kama wananchi wa Kigoma waliwatuma kwenda Bungeni kutetea mafisadi na udini badala ya matatizo sugu ya Kigoma kama usafiri, umeme, maji, n.k. Ushauri wangu kwa wana-Kigoma, hakikisheni Serukamba na Msambya hawarudi Bungeni.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kigoma ilaumuni CCM na si zaidi ya hapo mmejitakia mashida haya wenyewe .Zitto anasimamia Taifa angalau na wengine je ?
   
 5. K

  KGM Senior Member

  #5
  Feb 28, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kidogo ZITO afadhari kwa mambo ya Kitaifa. Ni hata Zito ndugu yangu wapiga kura wake amewasahau kabisa. Hivi unajua wapiga kura wake wamelipwa hela kiduchu sana tena bila hata uthamini kufanyika kupisha ujenzi wa barabara kwenda manyovu.


  Sijamsikia hata akinyenyua mdomo wake mh ZITO. Hajui kama sisi ndio tumempeleka bungeni. watu wameitwa tu kuchukua cheque benk hawajui hata zina shilingi, mh Zito kimya kabisa na niwapiga kura wake kabisaaa.


  LAKINI MAMBO MENGINE ANAONGEA MNO TENA KWA POINT KABISA.
  HEBU ANGALIA SWALA LA DOWNS, ANASEMA NCHI ITAKUWA GIZANI, HIVI SISI KIGOMA TUNA UMEME? HALIONI HILO, HILO SIYO GIZA?.

  HAYA NDIO MATATIZO YA KUCHAGUA WENYEJI WA DSM, ANGEKUWA HAPA KIGOMA GIZA TOTORO TUNALO KILA SIKU HAPA.

  LENGO SI KUMCHAFUA LAKINI KUNA HAJA YA KUTUTETEA NA SISI WAPIGA KULA WAKE

  HIVI KWA JINSI ZITO ALIVYO MSEMAJI MZURI ANASHINDWA HATA KULISEMEA KWA NGUVU SWALA LA USAFIRI WA RELI KWELI?

  USAFIRI KIGOMA UKIENDA DIRISHANI HUPATI TIKETI. KILA SIKU WANAKWAMBIA ZIMEISHA ILI WAZIRUSHE. DAR-KIGOMA DARAJA LA TATU BILA LAKI MOJA HUPATI. HIZO ZOTE NI KERO KWA WANAKIGOMA WANAHANGAIKA KWELI. SASA TUNAHITAJI WATU WATUSEMEE NA WAYAKEMEE HAYA. LABDA KWA KUWA WAKO JIJINI DAR BASI NDIO HIVYO TENA KIMYA TU.
   
  Last edited: Feb 28, 2009
 6. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  KGM;

  Sitasahau, ilikuwa ni mwaka 2005, hapo nilipopata fursa kufika kigoma, hakika nilibaki nimeduaa kama Tahira, nilimuuliza mwenyeji wangu tumefika? akanijibu tumefika, hakika tukashukatoka ndani ya lile gari Moshi na kuelekea Mjini, nikawa najiuliza mjini ndiyo wapi?

  Hakika siku ya kwanza ikapita ya pili ikapita hata nisijui ni wapi panaitwa mjini Kigoma, niliendelea kutazama vile vilima vilivyozunguka pale station, nikaendelea kusawili yale mazingira hali nzuri inayofaa kilimo, cha kushangaza watu wote wanacheza Bao na kahawa nyingi sana.............!!!,

  KGM; nataka nikueleze haya, ninyi ni wengi wa maneno na hamfanyi kazi, Tazama kama umefika pale kwenu mjini hakuna jengo jipya hata moja, majengo unayaona pale Kilimahewa na kule Jeshini, unajua kwa nini ?

  KGM; wabunge wenu wameshawasoma kuwa kutwa nzima nyie mnang'ang'ania habari za dini sasa ni kwanini msitetewe kwenye maswala ya dini tu?

  KGM; mshukuru Mola hata kwa kumpata huyu Kijana mbunge (zito) nadhani baada ya kutetea Taifa zima sasa ataelekeza nguvu zake hapo kigoma , naomba usitie shaka siku si nyingi neema itafunguka.
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Nadhani si sahihi kuwajumuisha wabunge wa Mkoa wa Kigoma katika kundi moja kimtazamo kwani huwezi kumfananisha Zitto na Serukamba na hata Kaborou kabla yake, that will be criminal. Zitto anaangalia matatizo ya kimaendeleo kitaifa wakati Serukamba na hata Kaborou kabla yake ni wabunge wa maslahi yao binafsi na ndio maana Serukamba yuko mstari wa mbele kuwatetea mafisadi bungeni kwani huko ndiko anakopata mshiko wake na ndio maana siku Lowassa alipolazimishwa kuachia ngazi juu ya kashfa ya Richmond inasemekana Serukamba alibubujikwa na machozi kwa kuondokewa na mfadhili mkuu!! Kaborou yeye aliwaambia CCM bei yake, wakamnunua na wakamhonga ubunge wa Afrika Mashariki ndio ikawa mwisho wake na watu wa Kigoma!! WanaKigoma Mtakuwa mnajidhalilisha sana tena sana kama mtamrudisha Serukamba bungeni 2010, mnao watu waadilifu wengi watakaoweza kuwarepersent effectively wakujaza nafasi hiyo .
   
 8. K

  KGM Senior Member

  #8
  Feb 28, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  wacheza bao ni waswahili wa pale ujiji, wengine tunachapa kazi mtindo mmoja ndugu yangu.

  Lakini ki ukweli kabisa anyoyatetea zito si mabaya lakini anatakiwa awatetee na waliompeleka pale bungeni.
   
 9. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  KGM;

  Mara ya mwisho kuwa pale kigoma ni lini wewe KGM;? maana nafikiria hata sipati jibu, uliondoka lini kule KG? NAJUA UKO TOWN MKUU..
   
 10. K

  KGM Senior Member

  #10
  Feb 28, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mimi kila mwaka natia mguu pale, nimetoka huko juzi tu na kilio cha mapunjo ya fidia kupisha ujenzi wa barabara nimekishudia mwenyewe.

  Hakuna nyumba hata moja iliyofanyiwa uthamini, wameitwa dirishani tu. Sasa wewe kama mbunge utakaa kimya kweli, na kijijini kwake mhe zito (mwandiga) kiganza----. Kwa kifupi ni jimboni kwake kabisa.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Isatamwita,
  Katika mikoa iliyosahaulika ni Kigoma..yaani duh! sina la kusema..
  Pale ulipofikia mkuu wangu sio mjini ulitakiwa uende Ujiji Kariakoo yao ndiko mjini..
  Aaaah! mambo mengine tuwaachie wenyewe!
   
 12. K

  KGM Senior Member

  #12
  Feb 28, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unakosesa sana unaposema mtuachie wenyewe.

  Kule kwenye Mjadala wa Downs unato michangu na ushauri mzuri kwa mh ZITO. hapa napo unatakiwa umwambie mh ZITO afanye angalau kidogo kwa ajili ya mkoa ule.

  Kigoma kuna vitu vingi sana ambavyo anawezakuvizungumzia bungeni na vikammwinua na kumpatia nguvu kisiasa si kwa wapiga kura wake na kitaifa pia.

  SERUKAMABA YEYE YUKO NA MAFISADI, NA MSAMBYA YUKO NA IOC&KADHI.


  SASA HUYU ZUBERI, KWA NINI ASIZUNGUMZIE MATATIZO YA KIGOMA HASA UMEME NA MAJI.

  JAMANI KIGOMA UMEME HAMNA NI GIZA KILA SIKU, MAJI USISEME, MAJI YA ZIWA TUNAYAANGALIA TU.

  HIVI MH ZITO HANA ANALOWEZA KUPELEKA BUNGENI NA SISI TUKAMUONA KAMA MKOMBOZI.

  USAFIRI NDIO USISEME INATISHA KABISA. UKIPANDA DARAJA LA TATU HATA PA KUWEKA MGUU HUPATI, 2ND NA 1ST CLASS, UTANYEWA NA PANYA MPAKA UNAFIKA. NI USAFIRI AMBAO KWA KWELI ULITAKIWA UPIGWE MARUFUKU KABISA KUTUMIKA.

  TUNAHITAJI MTETEZI WA KUTUTETEA NA HAPA.

  ZITO ACHANA NA GIZA LA WANA DSM, ZUNGUMZIA GIZA LINALOTUKABILI KIGOMA.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  KGM,
  katika maendeleo ya mkoa au wilaya mkuu wangu Mbunge hana nafasi kabisa zaidi ya kulia bungeni lakini serikali iliyopo madarakani ndiyo yenye maamuzi yote..
  Ndio maana binafsi huu mpango wa demokrasia ya vyama vingi hata nashindwa kuufahamu unavyofanya kazi kwani hata hapa nilipo wananchi tuna malalamiko kibao yanayohusiana na sehemu nayoishi lakini tunapo mkabiri mbunge wetu hutwambia tatizo hilo linatokana na serikali iliyopo madarakani..
  Kibaya zaidi basi jimbo langu limeshinda chama kinachoitwa NDP wakati mkoa umeshikwa na Liberal na Kitaifa wamekamata Conservative, hivyo matatizo juu ya matatizo..
  Kifupi Zitto hana ubavu.kumlaumu yeye ni kutokuelewa taratibu za utekelezaji wa maendeleo ya wilaya au mkoa..
   
 14. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mkandara mbona Mramba na Msuya waliweza leta maendeleo kwao??
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa sababu Mramba na Msuya hawakuwa Wabunge tu walikuwa pia mawaziri, hivyommaendeleo ya kwao yalipatikana tu kwa sababu walikuwa mawaziri ktk nafasi muhimu sana..Zitto hana ubavu, labda huko kwenye kamati yake...
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kigoma pia si wapo mawaziri?

  Zito hawawezi kushirikiana na mawaziri hao?
   
 17. p

  p53 JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  KGM yuko sawa.Zito hana ubavu wa kupeleka maendeleo kama mnavyosema.KGM yeye kilio chake ni kuona zito anapiga kelele bungeni pia kuhusu matatizo ya wana kigoma na si taifa tu kwa ujumla.KGM anataka azisikie kelele za zito kuwatetea wana kigoma.sasa serikali ya ccm ikitekeleza isipotekeleza hayo yote ni matokeo anayoyategemea KGM.
   
 18. K

  KGM Senior Member

  #18
  Feb 28, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  mkuu mkandara, hata kupiga kelele basi tumsikie, mbona mambo mengine anayashikia bango.

  Kama nilivyoeleza awali mambo mengine wanayajengea hoja na kuyapigia kelele, mbona matatizo ya wanakigoma hayawasumbui.

  Umemsikia zito wakati anajenga hoja juu ya downs, anasema nchi itakuwa giza na viwanda vitaacha kufanya kazi.

  Sasa kigoma sisi hatuna umeme siku nyingi 2, sasa kukuosa kwetu umeme si ni moja ya kutojengwa viwanda kweli.

  Hali ya kigoma ni hali ambayo wangeweza kuungana wabunge wa kule na kutoa tamko au msimamo flani lakini, kimyaaaaaaaa.
   
 19. K

  KGM Senior Member

  #19
  Feb 28, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  yaani wewe umenielewa hasa. Hivi mnakumbuka kipindi kile pale nauli za kwenda kaskazini zilipopanda? Polisi walishinda pale kuzuia upandishazi wa nauli.


  Sasa ndugu zanguni hivi zito na wwabunge wengine wa kigoma, hawaoni ulanguzi wa tiketi za train pale kigoma?

  Unaniambia zito na wenzie, wakishika bango kweli ulanguzi wa tiketi hautaisha?

  Watu wanaweza kusema kwani unamsema zito tu?
  Jibu ni kwa sababu zito amekuwa mbele kutetea mambo mengi ya kitaifa, sasa matatizo ya wananchi pale kigoma hayaoni.? Kwa nini yenyewe ameyafumbia macho.

  Mbunge kazi yake kusema na pia kuhamasisha. Hivi zito alishindwa nini kuwasemea wananchi pale walipolipwa fidia bila hata ya uthamini kufanyika achilia mbali kama serikkali wangeendelea kutekeleza au la.

  Mimi nachotaka waonyeshe watanzania kwamba kigoma kuna matatizo, sio sasa wako kimya au wanazungumza mambo mengine kabisa kana kwamba kigoma hakuna issue za kuzungumzia.
   
 20. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kwenye mambo ya ufisadi wameweza je? kukabiliana nao iliihali hawaongozi serikali?
   
Loading...