Wabunge wa Kigoma wana Matatizo gani?!

Nakubaliana na wewe kidogo ZITO afadhari kwa mambo ya Kitaifa. Ni hata Zito ndugu yangu wapiga kura wake amewasahau kabisa. Hivi unajua wapiga kura wake wamelipwa hela kiduchu sana tena bila hata uthamini kufanyika kupisha ujenzi wa barabara kwenda manyovu.

Sijamsikia hata akinyenyua mdomo wake mh ZITO. Hajui kama sisi ndio tumempeleka bungeni. watu wameitwa tu kuchukua cheque benk hawajui hata zina shilingi, mh Zito kimya kabisa na niwapiga kura wake kabisaaa.

LAKINI MAMBO MENGINE ANAONGEA MNO TENA KWA POINT KABISA.
HEBU ANGALIA SWALA LA DOWNS, ANASEMA NCHI ITAKUWA GIZANI, HIVI SISI KIGOMA TUNA UMEME? HALIONI HILO, HILO SIYO GIZA?.

HAYA NDIO MATATIZO YA KUCHAGUA WENYEJI WA DSM, ANGEKUWA HAPA KIGOMA GIZA TOTORO TUNALO KILA SIKU HAPA.

LENGO SI KUMCHAFUA LAKINI KUNA HAJA YA KUTUTETEA NA SISI WAPIGA KULA WAKE

HIVI KWA JINSI ZITO ALIVYO MSEMAJI MZURI ANASHINDWA HATA KULISEMEA KWA NGUVU SWALA LA USAFIRI WA RELI KWELI?

USAFIRI KIGOMA UKIENDA DIRISHANI HUPATI TIKETI. KILA SIKU WANAKWAMBIA ZIMEISHA ILI WAZIRUSHE. DAR-KIGOMA DARAJA LA TATU BILA LAKI MOJA HUPATI. HIZO ZOTE NI KERO KWA WANAKIGOMA WANAHANGAIKA KWELI. SASA TUNAHITAJI WATU WATUSEMEE NA WAYAKEMEE HAYA. LABDA KWA KUWA WAKO JIJINI DAR BASI NDIO HIVYO TENA KIMYA TU.

ZITTO alifanya kampeni yake kisomi zaidi.alikuwa na CHECK LIST ya mambo ambayo angefanya kama akichuguliwa kuwa Mbunge.
Aliwagawia wananchi hiyo Check list na kuwaambia wawe wana 'tick' kila atakachofanya na kama haja fanya wa muulize.
Mpaka mwaka jana alipo kuwa Kigoma 99.5% ya aliyoahidi yalikuwa yamekamilika.
Ktk kipengele cha umeme na mawasiliano haikuwepo kwenye Check list yake na Hata alipo ulizwa kwenye kampeni kuhusu hayo alijibu kuwa yapo nche ya uwezo wake ila atajaribu kuona atafanyaje.
Kwa sasa anapigania DOWANS au umeme wa GRID ya TAIFA kwa sababu anajua hilo likitatuliwa hata KIGOMA itapata umeme wa jenereta kwa uhakika.
Kama mnakumbuka mwaka 2005/2006 Tanzania ilikumbwa na tatizo la umeme lakini KIGOMA hakukuwa na tatizo hilo kwa sababu KIGOMA haitumii GRID yaTAIFA na MAFUTA MENGI YALIELEKEZWA KIGOMA NA MTWARA ili kuendesha mitambo hiyo ambayo haipo ktk GRID YA TAIFA.
Mwisho,ZITTO HAWEZI KULETA MAENDELEO KIGOMA KUPITIA SERIKALI LABDA WAFADHILI BINAFSI KAMA ANAVYO FANYA DR.SLAA,HII NI KUTOKANA NA SERIKALI KUTAKA KUONESHA KUWA UPINZANI HAUWEZI KULETA MAENDELEO BALI CHAMA TAWALA.LAKINI NI JUKUMU LA SERIKALI KUHAKIKISHA MAENDELEO YA JAMII NZIMA.
MKITAKA KUJUA SERIKALI INAHUJUMU MAENDELEO YA WANANCHI ANGALIA KIPINDI HIKI AMBACHO NI ZAMU YA CCM KUONGOZA HALMASHAURI YA KIGOMA,WATAFANYA MAMBO MENGI MAZURI ILI IONEKANE KUWA CHADEMA WALISHINDWA.
Tayari wameshaanza na treni la haraka kutoka DSM-KGM.
KIGOMA MSIFE MOYO CCM INAKARIBIA KUFA KWANI SASA HAINA UELEKEO.KILA MTU ndani ya CCM,ANAFANYA NA KUONGEA MAMBO YAKE.
 
mkuu,unaweza kuyaandika hayo mambo aliyoahidi zito wakati wa kampeni na kuyatekeleza kwa 99.5% kama unavyodai?
 
mkuu,unaweza kuyaandika hayo mambo aliyoahidi zito wakati wa kampeni na kuyatekeleza kwa 99.5% kama unavyodai?

1.kupambana na mikataba mibovu ya ubzwag - kahama
2.kupambana na ufisadi boat.
3.kuanzisha oparesheni sangara
4..
teh teh teh wengine wataongezea
 
wacheza bao ni waswahili wa pale ujiji, wengine tunachapa kazi mtindo mmoja ndugu yangu.

Lakini ki ukweli kabisa anyoyatetea zito si mabaya lakini anatakiwa awatetee na waliompeleka pale bungeni.

Nakuunga mkono kuna umuhimu wa Wabunge wetu kuzungumzia na kutetea mambo mbali mbali ya Kitaifa lakini wakati huo huo wasisahau wapiga kura wa majimbo yao na hata mikoa yao walikotoka. Kuna haja ya Zitto kuongeza utetezi wa Kigoma ambao bado uko nyuma sana kimaendeleo. Kama mtakumbuka mwenzetu mchukia ufisadi alituwekea mapicha ya Kigoma alipokuwa huko hivi karibuni ambayo yalionyesha ni jinsi gani mkoa huo ulivyo nyuma kimaendeleo.
 
1.kupambana na mikataba mibovu ya ubzwag - kahama
2.kupambana na ufisadi boat.
3.kuanzisha oparesheni sangara
4..
teh teh teh wengine wataongezea

duh yani aliwahidi watu wa kigoma kupambana na karamagi buzwagi?swali:zito aliomba lini kura kigoma na karamagi alisaini lini mkataba wa buzwagi?
 
ZITTO alifanya kampeni yake kisomi zaidi.alikuwa na CHECK LIST ya mambo ambayo angefanya kama akichuguliwa kuwa Mbunge.
Aliwagawia wananchi hiyo Check list na kuwaambia wawe wana 'tick' kila atakachofanya na kama haja fanya wa muulize.
Mpaka mwaka jana alipo kuwa Kigoma 99.5% ya aliyoahidi yalikuwa yamekamilika.
Ktk kipengele cha umeme na mawasiliano haikuwepo kwenye Check list yake na Hata alipo ulizwa kwenye kampeni kuhusu hayo alijibu kuwa yapo nche ya uwezo wake ila atajaribu kuona atafanyaje.
Kwa sasa anapigania DOWANS au umeme wa GRID ya TAIFA kwa sababu anajua hilo likitatuliwa hata KIGOMA itapata umeme wa jenereta kwa uhakika.
Kama mnakumbuka mwaka 2005/2006 Tanzania ilikumbwa na tatizo la umeme lakini KIGOMA hakukuwa na tatizo hilo kwa sababu KIGOMA haitumii GRID yaTAIFA na MAFUTA MENGI YALIELEKEZWA KIGOMA NA MTWARA ili kuendesha mitambo hiyo ambayo haipo ktk GRID YA TAIFA.
Mwisho,ZITTO HAWEZI KULETA MAENDELEO KIGOMA KUPITIA SERIKALI LABDA WAFADHILI BINAFSI KAMA ANAVYO FANYA DR.SLAA,HII NI KUTOKANA NA SERIKALI KUTAKA KUONESHA KUWA UPINZANI HAUWEZI KULETA MAENDELEO BALI CHAMA TAWALA.LAKINI NI JUKUMU LA SERIKALI KUHAKIKISHA MAENDELEO YA JAMII NZIMA.
MKITAKA KUJUA SERIKALI INAHUJUMU MAENDELEO YA WANANCHI ANGALIA KIPINDI HIKI AMBACHO NI ZAMU YA CCM KUONGOZA HALMASHAURI YA KIGOMA,WATAFANYA MAMBO MENGI MAZURI ILI IONEKANE KUWA CHADEMA WALISHINDWA.
Tayari wameshaanza na treni la haraka kutoka DSM-KGM.
KIGOMA MSIFE MOYO CCM INAKARIBIA KUFA KWANI SASA HAINA UELEKEO.KILA MTU ndani ya CCM,ANAFANYA NA KUONGEA MAMBO YAKE.

Hivi ndugu yangu train la haraka limeanza leo?, Train hili lilikuwepo toka zamani na halina msaada wowote kwa msafiri. umewahi kusafiri na train wewe?
lini train ya kati ikafika kwa wakati uliopangwa.

Train la haraka ndilo litazuia mabehewa na reli nyenyewe vilivyochoka haswa visianguke njiani?

Train ya haraka ndio itaondoka tiketi za kuruka kigoma au hata hapo dar.(KIGOMA NI ZAIDI)

Jamani kigoma unaijua kweli wewe? unasema kipindi kigoma kulikuwa hakuna kwa sababu ya majenereta, sasa yamekwenda wapi? KIGOMA hakujawahi kuwa na umeme unaoweza kuwaka hata kwa siku mbili mfulilizo.

Hivi mambo ya BUZWAGI na UFISADI kwa ujumla ndio yako chini ya uwezo wa zito.

Eti Downs itatusaidia kigoma kupata umeme KIGOMA Jamani, wewe utakuwa unatania kabisa ndugu yangu.

Anyway yote kwa yote tunacho omba ni msemaji atakaye address matatizo ya wana kigoma. Aseme kwa nguvu na Hoja pia. Kinachokera ni kuwa wako kimyaaaa. wanazungumzia mambo mengine tu why.?

Sasa haya matatizo ya kigoma nani atayasema. kwanini wameridhika hivi.
Mh ZITTO anashindwa kweli kwa uchungu kabisa kuzungumzia matatizo ya mkoa wetu (maana hao wengine ni CCM wameridhika), lakini kazi ya upinzani ni kuibua maovu na mambo yaliyoko kigoma ni maovu pia kwanini haongei.

Sisemi hayo mengine asiseme lakini na mkoa wake auonee huruma aseme.
wewe katafute tiketi ya kwenda kigoma dar hapo reli ya kati uone kama hujaambiwa zipo za mwezi wa tano.

kigoma kuja dar ndio kabisa. sasa hayo nayo yanahitaji ufadhiri gani zaidi ya kuyakemea na kuyasema hadharani ili watu wa kigoma wapate ahueni.

Tunataka mtu wa kusema na kusema na kesemax100., serikali itasikia, kama haikusikia situtakuwa tumeona na kusikia?
 
Nakuunga mkono kuna umuhimu wa Wabunge wetu kuzungumzia na kutetea mambo mbali mbali ya Kitaifa lakini wakati huo huo wasisahau wapiga kura wa majimbo yao na hata mikoa yao walikotoka. Kuna haja ya Zitto kuongeza utetezi wa Kigoma ambao bado uko nyuma sana kimaendeleo. Kama mtakumbuka mwenzetu mchukia ufisadi alituwekea mapicha ya Kigoma alipokuwa huko hivi karibuni ambayo yalionyesha ni jinsi gani mkoa huo ulivyo nyuma kimaendeleo.

Ni kweli BAK niliweka hapa datas za Kigoma mwaka jana.

KGM atembelee hapa chini kuona vitu live:
https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/18654-jamani-maskini-kigoma.html
Lakini kama wengi walivyoshauri, maendeleo ya Kigoma yataletwa na wana Kigoma wenyewe through sanduku la kura. Kadri wanavyochagua SISI M. wajue ndivyo mambo yatakavyendelea kuwawia magumu.
KGM anaonekana ana kampeni binafsi dhidi ya Zitto maana anamsema huyo sana as if yeye ana serikali. Nashangaa kwa nini asikomalie wana sisi M ambao hawasemi hata angalau matatizo ya kitaifa. Jamani huyu Zito sie wate ni mashahidi kapiga kelele mpaka watoto wanaamka kwa hizo kelele na hawawezi kulala. Zito anasema weeeeeeeeeeeeee pamoja na rafikiye DR Slaa mpaka kila mtu sasa hampendi kiasi cha kumtegeshea hata vinasa sauti. Sasa hata akisema tu unadhani atasikika?
By the way KGM unaweza kutuambia kama umepitia Hansard za mkusanyiko huu wanaouita bunge na kuona kuwa Zito hajasema lolote kuhusu mkoa wenu? au shida zimewafanya muwe kama mfa maji? maana mtu aliyezama akiona mtu kaenda kumuokoa basi hutaka amzamishe. Ni hatari kujaribu kumuokoa mtu aliyezama na kesha kunywa glass za kutosha za maji.
Lakini pia wana Kigoma wao kama wao wamejisahau sana. Hawajali lolote hata usafi binafsi ambao hauhitaji serikali kuwahimiza. Lakini pia wanatumia muda wao mwingi kwenye religion fanatism. Hapo maendeleo msahau kabisa!
Kama unadhani nasema uongo wewe nenda popote Tanzania hii uone watu wanakojifanya wakeleketwa wa dini kama wana lolote la maendeleo. Hakuna.
 
Utafiti unaonyesha kuwa mahali palipokaliwa na waislamu wengi huwa hapana maendeleo, mfano Mtwara, Kigoma, Pwani, Zanzibar na kwingineko. Na wabunge wao nao ukiacha wachache kamaakina zito sijui akili zao zimewekwa kutu ya aina gani huwa hawakomalii mambo ya maendeleo ila kutetea udini tu. Kweli Kigoma iko nyuma sana na wabunge wao wameweka mbele udini tu na kutetea mafisadi. Kama nakumbuka vizuri, Serukamba ni mojawapo wa wabunge wenye vyeti feki na Lowasa alimtetea ndo maana na yeye kwa nguvu zote huwa anamtetea hasa na ndo maana alitoa machozi siku amejiuzulu Uwaziri mkuu maana hapo kitumbua kilikuwa kimeingia mchanga. Wabunge wa Kigoma badilikeni acheni udini shughulikieni masuala ya maendeleo huko kwenu.
 
Naomba nipate michango yenu wanajamii, kutokana na mimi binafsi kutowaelewa Vizuri wabunge wa KIGOMA

Sijui niseme wanauzalendo sana kwa mambo ya kitaifa au ni vipi, wanashadadia sana mambo mengine lakini MATATIZO ya wana KIGOMA hata hawayaoni.

Angalia mifano.
Mh ZIto na mawaswala ya kitaifa na sehemu nyingine kama mambo ya Downs, BUZWAGI, KIWIRA,

Mh Shelukamba yeye amejikita kwenye utetezi wa mafisadi wote mnajua.

Bwana Msambya ya yeye ni UDINI, yakija mambo ya OIC na Mahakama ya Kadhi, Bungeni panajimbika.

SASA wanajamii, mbon matatizo makubwa ya wanaKIGOMA kama Usafiri, Maji na UMEME wala hayawasumbui wako kimyaaaaaaaaaaa, nini TATIZO lao.

Hivi ndugu zangu kuna mtu asiyefahamu kuwa wana KIGOMA ndio waathirika wakubwa wa usafiri wa Reli ya KATI, mbona wabunge wetu hawakomalii issue za hawa mafisadi wa kihindi walioko pale kwelye shirika la Reli badala yake wanakomalia vitu vingine kabisa?

Hivi Mh Zito hajui kuwa kigoma wapo GIZA kila siku, mbona hilo halimsumbui badala yake anakomalia mitambo ya Downs ambayo najua kabisa haitawapatia wanakigoma umeme.Kigoma siku zote iko giza, hakuna mbunge wa kigoma anayeinua mdomo kulisema.

Wanajamii, utashangaa, pamoja na Kigoma kuwa na Ziwa, lakini mji ule hauna maji. Hilo wala halimsumbui ndugu yetu Serukamba, yeye kutwa, kuchwa michango yake ni utetezi wa mafisadi bungeni. Ataongea mpaka utamuonea huruma kwa mishipa na mate kumtoka, nini Tatizo la wabunge wetu? Au ni kwa kwa kuwa wao wenyewe hawaishi kule, au ndio kutaka sifa tu au nini.

Nisaidieni wanajamii, niko kwenye TUTA.

Nionavyo, kabla ya kuwalaumu Wabunge mmoja mmoja kuhusu majimbo yao ya uchaguzi, ni bora tukazirudia katiba na sheria za nchi na zile za vyama vyao.

Katiba na sheria za nchi na za vyama, hazitoi uhuru kwa mpiga kura kumchagua mbunge amtakae.

Mgombea anachujwa na kuchaguliwa na chama, anagharamiwa kampeni na chama na anatangaza ilani ya chama, ambayo kimsingi ilani hiyo haishughulikii wala haizingatii matatizo ya jimbo maalumu ya mgombea huyo.

Mgombea huyu kwa hakika akichaguliwa, anakuwa Mbunge wa chama chake na hawi mbunge wa wapiga kura wake. Akienda bungeni, anakwenda kukiwakilisha chama chake na kuigombea ilani ya chama chake. Aendapo bungeni haendi kwa ajili ya kero za waliompigia kura.

Jinsi katiba na sheria za nchi na vyama zilivyowekwa, Mbunge huyu akienda kinyume cha chama chake, chama kinamfukuza na ubunge unapotea.

Ndio maana tunawaona wabunge wanalalama wee, lakini ikifikia kupiga kura wabunge hao hao waliolalama wanapiga kura za kuridhisha vyama vyao badala ya wapiga kura wao.

Tunajidanganya sana tunaposema Zitto ni mbunge wa Kigoma. Zitto anakwenda bungeni kama mbunge wa Chadema, na pale bungeni anaiwakilisha Chadema na anaitetea ilani ya Chadema. Na wabunge wengine wote ni hivyo hivyo.

Kama Kigoma kuna matatizo au kero, basi matatizo hayo yapelekwe kwenye vikao vya Chadema vya Kigoma, ili vipenyezwe kwenye ilani ya Chadema. Vinginevyo ikubalike Zitto hana uwezo wa kuwatetea wapiga kura wake hata kama anataka.

Wanadai mbunge kachaguliwa na chama na kama chama kisingemchagua, wewe mpiga kura ungempigia kura nani? Tunasema kila siku, katiba hii imekaa mkao wa "chama" kula na kwamba hailengi maslahi ya wananchi kwa jumla.
 
Kujaribu kumbebesha Zitto lawama ya kutoendelea Kigoma au kutochangamkiwa Kigoma ni kujaribu kukwepa ukweli. Matatizo ya Kigoma hayatokani na Zitto kupiga kelele au kutopiga kelele! Matatizo ya Kigogoma yamefungamana kwa miaka karibu 50 na utawala wa Chama cha Mapinduzi.

Ni chama cha Mapinduzi chenye serikali na chenye sera za sehemu mbalimbali na miradi mbalimbali. Wakati wenzenu Dar wanazungumzia kujengewa Flyovers nyinyi Kigoma hata reli ya kati haijatengemaa! Sasa hivi kutoka Arusha kwenda Mbeya ni karibu kwa masaa kuliko toka Dar hadi Kigoma ingawa kijiografia Kigoma ni karibu na Dar kuliko Mbeya na Arusha!!!

Jinsi unavyozungumza ni kana kwamba Zitto hajawahi kuzungumzia masuala ya Kigoma au wapiga kura wake Bungeni. Naomba utuletee rekodi ya Zitto Bungeni kuhusu masuala haya maana inawezekana wakati anayazungumza hukuyasikia.

Lakini zaidi ni kuwa, kama Kigoma wakitaka mabadiliko ya kweli ni wao wachukue hatua za kurudisha kadi za CCM!! na kuifuta CCM kwenye utawala wa mkoa wao na kuchagua chama ambacho kitakuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia raslimali zenu na chenye kuweza kupiga "kelele" bungeni. Vinginevyo, lawama kwa mtu mmoja kwa matatizo ya mkoa mzima ni kukwepa ukweli kuwa wenye wajibu na wenye kustahili lawama ya kudumaa kwa Kigoma (kama ilivyo Mtwara, Lindi, Tabora n.k) ni serikali ya CCM tu.

CCM ndiyo sababu, Zitto ni kisinigizio!
 
Ni rahisi sana kutenganisha siasa na maisha ya kawaida hapa Marekani na hata ulaya. Ukawa unaangalia personal interests tu but when you go back to Africa hasa Tanzania now you have to look politics as your mom and dad. kwani uamuzi unaouchukua will cost you severely. Hili tunatakiwa tuwaambie jamaa zetu... Imetucost miaka 40 kurekebisha barabara ya kati tena kwa mikopo itokanayo na shinikizo la akina barrick. wasingekuwepo lol.... Kigoma na mikoa ya kusini chemkeni wote kwa ujumla.
 
KGM USIWALAUMU WABUNGE WENU BALI WALAUMUNI WANANCHI WENU WA KIGOMA KWA KUWA WAPINZANI WA MAENDELEO TANGU ENZI ZA MWALIMU.
Nimepata nafasi ya kukaa Kigoma mwaka mmoja mfululizo,pamoja na shughuli zangu nilifanikiwa kuongea na wazee wa maeneo mbali mbali kama vile MWANDIGA,KASEKE,ILAGALA,MWAMGONGO NA SIGUNGA ambao kwa nyakati tofauti waliniambia kuwa kuna kipindi MWL alikua anahamasisha kilimo cha pamba na alipofika akaoneshwa shamba la majani,wenyeji wanayaita "motomoto" na kuambiwa ni pamba(alifanyiwa sijui ndio kiini macho?).baadae Mwl aligundua kwa alichooneshwa ni majani.
Kipindi cha MKAPA nacho wakamwagia mchanga pale kijiwe cha URUSI MWANGA.
Baada ya kumwagiwa mchanga MKAPA aliahidi kutorudi KG lakini kwa Bahati mbaya alifika kufungua kivuko cha Mto Ilagala.Pamoja na kufika hapo hakuongea na wananchi na alifika kwa ndege na kuondoka siku hiyo hiyo.
Hayo ni baadi ya vitu vinavyo changia KG kuwa nyuma.
Nikiongelea wabunge, MBUNGE HAWEZI KULETA MAENDELEO BALI KUWASILISHA SHIDA ZA WANANCHI SEHEMU HUSIKA ILI ZIWEZE KUTATULIWA VINGINEVYO,MBUNGE ATAFUTE WAFADHILI BINAFSI AMBAO MARA NYINGI HUWEKEZA KWENYE MIRADI MIDOGO KAMA AMBAVYO DR.SLAA ANAFANYA KULE KARATU KWENYE MIRADI YA MAJI.
Zitto anapigania maslahi ya Taifa akiamini ustawi wa Taifa hili ni pamoja na KG kuneemeka.
KG kuna tatizo la umeme kwa sababu ya jenereta chakavu lakini kama unakumbuka mwaka 05/06 Tanzania ilikumbwa na tatizo la umeme lakini KG na MTWARA haikuwa na tatizo kubwa.Hii ni kwa sababu gharama zilizo kuwa ziendeshe mitambo ya gridi ya Taifa ambayo wakati huo haikufanya kazi zilihamishiwa huko kwa ajili ya kununua mafuta na matengenezo madogomadogo ya jenereta.
MWISHO:USIMLAUMU ZITTO KWA KUTOTETEA MASLAHI YA KIGOMA KWANI WAKATI ANAOMBA KURA ALIKUWA NA "CHECK LIST" ALIYO ORODHESHA MAMBO AMBAYO ANGEFANYA NA KUWAAMBIA,"KILA NITAKALOTEKELEZA WEKENI ALAMA YA V",mwaka jana alitembelea wananchi wake na 99.5% alikuwa ametekeleza kwa mujibu wa check list.Aidha ktk list hiyo,umeme na mawasiliano havikuwepo na hata alipo ulizwa alisema yapo nje ya uwezo wake na hawezi kuahidi chochote bali atajitahidi.
PIA NAOMBA UELEWE SERIKALI INA HUJUMU MAENDELEO YA BAADHI YA WANANCHI HASA PALE WANAPO CHAGUA UPINZANI,INAFANYA HIVYO KUWA KOMOA KWA UAMUZI WENU.UKITAKA KUTHIBITISHA,ANGALIA SASAHIVI BAADA YA CHADEMA KUKABIDHI UONGOZI WA HALMASHAURI YA KIGOMA KWA CCM,MABADILIKO YATAONEKANA IKIWA NI PAMOJA NA UPATIKANAJI WA MAJI KWA WINGI KWENYE MABOMBA N.K.HIVI SASA KUNA "TRENI YA MWENDO KASI"kutoka DAR-KG WATAKUAMBIA WAO WAMEWEZESHA!
USIWE na HOFU MATATIZO YA KIGOMA YATAISHA PUNDE KWA SABABU CCM AMBAYO NDIYO KIKWAZO INASAMBARATIKA.USHAHIDI NI NAMNA WANAVYO TOFAUTIANA WENYEWE KWA WENYEWE.
 
...Wajaameni, hebu basi muangalie na uwiano wa wabunge wa Kigoma toka chama tawala na vyama vya upinzani,...naona hapo Mh. Kabwe atakuwa anahukumiwa isivyostahiki jamani, eti...?
hawa wengine wa CCM kama walowatangulia wanawafanyia mema gani wana Kigoma? Kina Dr Walid Kabourou?

kilontsi mporogomyi.jpg
-CCM Kilontsi Mporogomyi, Kasulu magharibi

Felix Ntibenda- Muhambwe.jpg
-CCM Felix Ntibenda, Muhambwe

Christopher Kajoro- Buyungu.jpg
-CCM Christopher Kajoro, Buyungu​

Peter Serukamba-mjini.jpg
-CCM Peter Serukamba, Kigoma Mjini

Salum Msambya- South.jpg
-CCM Salum Msambya, kigoma kusini​

View attachment 3716
-CHADEMA Zitto Kabwe, Kigoma Kaskazini

...anyway, karibuni Kigoma kwa "Dr Livingstone I pressume!"

Kigoma_Airport_04.jpg
 
Isatamwita,
Katika mikoa iliyosahaulika ni Kigoma..yaani duh! sina la kusema..
Pale ulipofikia mkuu wangu sio mjini ulitakiwa uende Ujiji Kariakoo yao ndiko mjini..
Aaaah! mambo mengine tuwaachie wenyewe!

Mheshimiwa Zitto si alisema kule mkoa wa Mara kaona kumbe Tanzania tuko nyuma sana? Ni kama aliona umaskini wa kutisha ambao hajawahi kuuona Kigoma. Aliyesema nyani haoni kundule hakukosea.

Mimi naamini uzalendo unaanzia nyumbani, ni muhimu kutatua matatizo yanayokuzunguka kabla hata kufikiria matatizo ya mbali.

Wabunge wetu wengi wanahangaika na mambo ambayo yanaweza kuwaweka kwenye TZ kila siku na kusahau mambo ya kule wanakotoka. Hata wakienda huko kwao basi wanaongozana na vyombo vya habari ili vitoe taarifa kwamba waheshimiwa wameenda kutembelea majimbo yao. Hivi uliona lini mtu unatembelea sehemu yako ya kazi?
 
Nikiongelea wabunge, MBUNGE HAWEZI KULETA MAENDELEO BALI KUWASILISHA SHIDA ZA WANANCHI SEHEMU HUSIKA ILI ZIWEZE KUTATULIWA VINGINEVYO,MBUNGE ATAFUTE WAFADHILI BINAFSI AMBAO MARA NYINGI HUWEKEZA KWENYE MIRADI MIDOGO KAMA AMBAVYO DR.SLAA ANAFANYA KULE KARATU KWENYE MIRADI YA MAJI.

Haya ndio mawazo ya wasanii wa Tanzania. Ndio mawazo ya watu wasio na jipya na ambao
badala ya kuwa solution ni tatizo kwa Tanzania yetu ya baadaye. Mawazo ya watu wanaofikiria misaada tu vichwani kiasi kwamba wamesau kwamba uongozi ni kuonyesha kwa vityendo na wala sio ubingwa wa kwenda kuwa ombaomba. Ingelikuwa hivyo basi MATONYA angelikuwa rais wa Tanzania.

Mawazo mengine yanatia kichefuchefu kweli kweli, ndio maana wilaya zetu zitaendelea kuwa maskini kwani kama sehemu ya wabunge wetu wanaamini kazi zao ni kusikiliza shida za wananchi na kwenda kuzitupa bungeni au wizarani, hapo tusahau maendeleo kwa nchi nzima.
 
Lakini zaidi ni kuwa, kama Kigoma wakitaka mabadiliko ya kweli ni wao wachukue hatua za kurudisha kadi za CCM!! na kuifuta CCM kwenye utawala wa mkoa wao na kuchagua chama ambacho kitakuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia raslimali zenu na chenye kuweza kupiga "kelele" bungeni. Vinginevyo, lawama kwa mtu mmoja kwa matatizo ya mkoa mzima ni kukwepa ukweli kuwa wenye wajibu na wenye kustahili lawama ya kudumaa kwa Kigoma (kama ilivyo Mtwara, Lindi, Tabora n.k) ni serikali ya CCM tu.

CCM ndiyo sababu, Zitto ni kisinigizio!

...Sawa sawa Mwanakijiji, lakini nikiwaangalia ami zangu kule wete, chakechake, Kengeja, Changaweni na Pemba kwa ujumla wanalitumia sanduku la kura ipasavyo kusema NO kwa CCM, lakini mmmnnhhh... kelele za CUF bungeni baaado kabisa hazijawasaidia... au?
 
Aliyeanzisha hii thread anaongea ukweli kabisa. Mfano umedhihirika hapahapa JF. Zitto kaingia humu ametumia muda wake kujibu hoja za Dowans na TANESCO tu. Huu mjadala unaoligusa jimbo lake hajachangia hata mstari mmoja. Its clear kwamba hili swala la jimbo kwake haliko katika vipaumbele. Ila mimi nadhani wanaotakiwa kuchagua nani awawakilishe ni watu wa Kigoma wenyewe, so iwapo Zitto na wabunge wenzake wa kigoma hawawawakilishi ipasavyo, basi mwakani watapata fursa ya kuchagua wawakilishi wengine. Watakavyochagua ndio kitakua kipimo cha utendaji wa hawa wabunge wa sasa- ofcourse iwapo watagombea tena!.
 
Ingekuwa sijui logic behind haya "malalamiko" ningesema labda Kigoma wawachague "WAFADHILI" wa aina za kina ROSTAM badala ya wawakilishi bungeni ili nao waweze kufadhiliwa kwa kutumia pesa za EPA na UFISADI mwengine ama labda MARANDA atawatimizia mahitaji yao.....

omarilyas
 
...Wajaameni, hebu basi muangalie na uwiano wa wabunge wa Kigoma toka chama tawala na vyama vya upinzani,...naona hapo Mh. Kabwe atakuwa anahukumiwa isivyostahiki jamani, eti...?
hawa wengine wa CCM kama walowatangulia wanawafanyia mema gani wana Kigoma? Kina Dr Walid Kabourou?

View attachment 3717
-CCM Kilontsi Mporogomyi, Kasulu magharibi

View attachment 3718
-CCM Felix Ntibenda, Muhambwe

View attachment 3719
-CCM Christopher Kajoro, Buyungu​

View attachment 3720
-CCM Peter Serukamba, Kigoma Mjini

View attachment 3721
-CCM Salum Msambya, kigoma kusini​

View attachment 3716
-CHADEMA Zitto Kabwe, Kigoma Kaskazini

...anyway, karibuni Kigoma kwa "Dr Livingstone I pressume!"

Unajua wewe nafikiri hujanielewa, hao ni ccm nao tunawajua wamesharidhika.
Zito ni upinzani, na upinzani kazi yake ni kurekebesha pale panapoenda Kombo.
Mimi nachotaka kusema, ni kwamba atutetee sisi wanakigoma kama anavyotetea na kufichua maovu sehemu nyingine.

Hivi umemsikia anavyoitetea Downs kwa nguvu zote? Ulimsikia alivyotoa msimamao wake thabiti kwenye sakata la BUZWAGI mpaka akatimuliwa.

Kifupi ZITO ni mzungumzaji mzuri na anajua kujenga hoja.
Sasa kwa nini maswala ya umeme, maji na usafiri ambavyo ni shida kweli KIGOMA haongei, hajengi hoja hata sisi tukaona. kama serikali itatekeleza au la ni swala jingine.

Sikufichi ndugu yangu, kwanza kauri yake kwenye utetezi wa Downs binafsi imenikera sana. Anasema ooooh, nchi itakuwa gizani, ebo, Kigoma tuko gizani kila siku mbona haji kutuhamasisha tukaandamana kuonyesha hasira zetu.

Anasahau kwamba KIGOMA haina viwanda kwasababu hata umeme hatuna.
Angalia Usafiri wetu, unatia KINYAAA. Hivi kweli kwa ujengaji hoja wa ZITO akipiga kelele hasa watu hamutatuaonea huruma nakusema kweli hawajamaa wanateseka, hata tukiandamana mtatuunga mkono!!!!!!?????????.

Lakini hali ilivyosasa kila mbunge yuko kimya(hata zito mpinzani) kwa hiyo hamjui kama tunateseka.
 
Back
Top Bottom