FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,211
Kwa hiyo uarabu si lugha pekee bali ni sehemu ya uarabu. Desturi Mila, asili, tamaduni na nchi wakati mwingine ndivyo vinajenga utaifa wa mtu. Kwa maana nyingine waarabu ndiyo tuliwaona wakija Afrika na wala si Lugha yao ililetwa Afrika.
Uliwaona Waarabu kwa lugha yao lakini si kwa Utaifa wao. Hao hao Waarabu wana mila na desturi tofauti tofauti na hata dini tofauti tofauti. wana mavazi tofauti tofauti, usichanganye Utaifa na Lugha. na hili halina ubishi.
Wa Sudan, Wa Saudi, Wa Oman, Wa Lebanon, Wa Libya, wa, wa, wa, wa, woote hao ni Waarabu kwa lugha na si kwa Utaifa wala Kabila wala mila wala dini, wana mila zao tofauti, wana kabila zao tofauti, wana mavazi yao tofauti, wana dini tofauti hata makontinenti tofauti, lakini wana Lugha Ya Kiarabu inayowatambulisha kama Waarabu.
Sijui ni kipi kigumu hapo kukielewa?