Nilimshangaa FaizaFoxy aliposema Zanj Empire ni Zanzibar ya leo nikabaki nimeduwaa. Tatizo lake FaizaFoxy ni "usomi' wa Historia "sahihi" inayotolewa kuonyesha kwamba duniani kuna mfumo maalum wa kuuangamiza Uislamu!!
Tatizo lako ni kuwa hutaki kusoma, unafikiri toka kichwani, si mbaya lakini tazama, ngoja nikufahamishe kuhusu maana ya halisi ya "zenj":
Zenj imetafsiriwa na wengi kuwa ni "Black" au "Mweusi" lakini hiyo ni maana ya ujumla wa kuchangisha maana, maana halisi ya neno zenj ni 'pua pana" au "pua kubwa" au "pua iliyo bambataa" na hii ilihusishwa na watu weusi na ndio ikatafsiriwa kiujumla kumaanisha watu weusi, usahihi ni kuwa kila mwenye pua pana, au pua iliyobabataa huwa ni Zinji. Hiyo ndio maana ya zenj. Na ndio maana hata tangawizi kwa kiarabu inaitwa "Zanjabil", sio kwa ajili imetoka Zanzibar, hapana, kwa ajili ya ilivyokaa, tazama pua zetu zilivyokaa halafu tazama tangawizi mbichi utanielewa.
Maana ya Bar, ni rahisi sana kwa msemaji wa kiswahili kuielewa, maana ya Bar ni Bara (bara Arabu) kwa pamoja ndio tunapata neno Zenj Bar au Bara la wenye pua nene (iliyo babataa), ni sifa ya watu wengi wa Afrika, kwa watu kutaka kuifanya Afrika ("Afrika" yenyewe ni neno la Kiarabu) ni exclusively kwa watu weusi (ama kwa kutokujuwa kwao ama kwa kupoteza maana halisi) wakaitafsiri Zenj kuwa ni mtu mweusi, mtu mweusi Kiarabu ni "Sudan" linatokana na neno "Aswad" (Black).
Ndugu yangu jina Zanzibar linatokana na Zenj Bar. Na hiyo ndio inayojulikana kihistoria kama Zenj Empire, na Zenj Empire ilikuwa na utawala mkubwa sana na haukuishia visiwa vya unguja tu, ndio maana Zanzibar si jina ya kisiwa fulani, visiwa vinavyotambulika leo kama Zanzibar ni vya Pemba, Unguja, Tumbatu na vinginevyo vidogo vidogo, lakini si kisiwa fulani. Na anaposema mtu kulikuwa kuna soko la utumwa Zanzibar, hakosei, kwani Zanzibar ilikuwa ni himaya kubwa sana, Bwagamoyo, Mombasa, Mrima, Kilwa, mpaka Congo, mpaka Somalia, mpaka Mozambique (sofala) na si ajabu mpaka Afrika Kusini na Zimbabwe, pia si ajabu ikiwa ni Afrika Nzima, jee hakuna ma "Zenj" Afrika nzima?
Unaposikia "revolt" au "rebellion" ya "Zanj" usifikiri ilimaanisha Zanzibar unayoijuwa leo hapana inamaanisha watu "Zanj" ni "plural" ya "Zinj", panuka kidogo kuelewa maana kwa uhalisia wake na si kwa muono wako.
Nakuambia tena na tena, nisikilize vizuri, utapata mengi sana kuhusu hili somo, nashkuru sana napata kulitolea darsa hapa ni somo nilipendalo na nnalijuwa kiasi changu. Tartiiibu tutafika. Hii ni amana na ukija kuitaka siwezi kukunyima.