Nadhani biashara ya utumwa unaisoma kijujuu, utumwa ilikuwa ni biashara ya dunia nzima. Enzi hizo kulikuwa hakuna neno, "mfanya kazi", mfanya kazi ni Mtumwa tu au mtumishi siku hizo, na walikuwepo wa kila namna na kutoka kila Taifa. Walikuwa wanahitilafiana thamani zao zao kwa wayajuwayo.
Kuna Waafrika walikuwa na watumwa kutoka Uropa na hali kadhalika kulikuwa kuna Wa Uropa walikuwa na watumwa kutoka Afrika.
Somo la utumwa na historia yake ni ndefu kuliko unavyofikiria, samahani kwa kukuambia kuwa, kwa maandishi yako machache naweza kusema hujaingia ndani kuisoma historia kama hobby au somo na nnauhakika, hukufanya vizuri mitihani ya historia kama lilikuwa ni moja ya kati ya masomo uliyofundishwa.
Nakuomba tafadhali sana wacha kuchanganya mambo twende taratibu utafaidika sana, kama ulivyofaidika kule kwa Mohamed Said, unajuwa, mashule duniani huifundisha historia ya mwanzo mashuleni kutokana na wanavyotaka wao wanafunzi wawe na ufahamu upi. Ukiondoka stage hiyo ukifikia kutaka kuingia ndani kwa kina, kiila utavyo zama utakutana na pembe tofayti za historia zitazokufanya uwe na uelewa mpana zaidi.
Umeanza na ya Waarabu, hujayamaliza unarukia ya Utumwa. Tumalize ya ukoloni wa Waarabu kwanza, hilo pekee ni somo tosha na amabalo hulielewi na ndio maana ukaliuliza> Kaa tupeanae darsa, si lazima tukubaliane kwa yote lakini mwisho wa siku tutakuwa tumeondoka tumefaidika sote. Au unasemaje?