Waarabu hawakuwa Wakoloni Afrika?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Vitabu vingi vya Historia na Fasihi viwe vimeandikwa na waafrika wenyewe au watu wa kutoka nje ya bara la Afrika, mara zote vinawataja Wareno,Waitaliano, Wajerumani, waingereza, Wadachi, na Wafaransa kama wakoloni, lakini mimi sijawahi kukutana na kitabu kinawataja waarabu kama wakoloni. Najiuliza kama waarabu hawakuwa wakoloni sifa yao ilikuwa ni nini hasa? Wavamizi, wafanyabiashara, waeneza dini au wao walikuwa pia wanatawaliwa na hao tunaowaita wakoloni?
 
Sifa yao kubwa ilikuwa ni biashara ya binaadamu (biashara ya utumwa)
 
Hao uliowataja ndio hasa waliokutana kwenye ule mkutano maarufu (Berlin Conference - 1884) ambao lengo kuu lilikuwa "Scramble for and Partition of Africa" na hatima yake ikawa kuigawanya Afrika kwa mipaka iliyopo leo. Katika mkutano huo mwarabu hakuwepo wala hakujuwa kilichokuwa kinaendelea. Yeye kazi yake kuu ilikuwa kuwinda binadamu wenzake kama swala.

Kwa ufupi, nadhani hiyo ndio sababu kuu waarabu hawaoenekani kwenye vitabu vya historia kama wakoloni ila kwenye historia ya utumwa mwarabu anaongoza.
 
Waharabu..?!
Nani hajawai ona kitabu cha darasa la nne kama sio cha tano cha historia(michoro)..
Namna Babu zetu walivyofungwa na minyororo shingoni mithiri ya n'gombe na kama haitoshi kuwatoboa visigino..
Nadhani umeanza kupata picha waharabu ni akina nani katika hstoria yetu..
Wakatili kulikoni, Wezi na wanyanganyi, wauza watu na hao wengine walikuwa wanunuzi..
Siyo watu wazuri kabisaaaaaa..!
 
mbona hakukuwa na movement za blacks arabuni?? Islam ilikomesha biashara ya utumwa karne ya 7, baada ya hapo hakukuwa na biashara ya utumwa arabuni

alikua ni mwingereza na vibaraka wake wa kiarabu wa oman walofanya biashara ya utumwa so mwarabu hakutawala ila alikua just ni kibaraka
 
Mtafuteni mohamed said anajua sana haya mambo ya waarabu na jinsi walivyokuja pale gerezani kariakoo.
Nina hamu kama nitajua waarabu tuwaweke kundi gani. Wakoloni au watawaliwa na wakoloni?
 
Ila walitawala hawa jamaa,hasa eastafrika,kuanzia karne ya 17 hadi 19,mfano ni z'bar
Walitawala kwa hiyari ya watawaliwa bila ya ghiliba? kwa Karne zote hizo tuwaite wakoloni au hawastahili kuitwa wakoloni?
 
hao waliwauza babu zetu mithili ya ng'ombe, hawafai hata kidogo ni zaidi ya wakoloni wa kizungu
 
Kigarama,

Swali zuri sana nakusifu kwa kuliuliza ila mie sitachangia kwanza wacha tumalizane kule ila nawaomba Moderator waipandishe kule sticky kwasababu hili ni jambo lengine linalotatiza historia ya Tanganyika na Tanzania kwa ujumla.
 
Vitabu vingi vya Historia na Fasihi viwe vimeandikwa na waafrika wenyewe au watu wa kutoka nje ya bara la Afrika, mara zote vinawataja Wareno,Waitaliano, Wajerumani, waingereza, Wadachi, na Wafaransa kama wakoloni, lakini mimi sijawahi kukutana na kitabu kinawataja waarabu kama wakoloni. Najiuliza kama waarabu hawakuwa wakoloni sifa yao ilikuwa ni nini hasa? Wavamizi, wafanyabiashara, waeneza dini au wao walikuwa pia wanatawaliwa na hao tunaowaita wakoloni?

Waarabu hawakuwa wakoloni Afrika. hilo ni jibu tosha.

Usichanganye Uarabu kama ni Taifa fulani, Uarabu ni lugha zaidi ya Taifa. Kama vile Mswahili, mswahili si Taifa. Nadhani umenipata.

Hao wengine wote uliowataja ni mataifa ambayo yanaweza kuwa na koloni lake. Kama si Taifa huwezi kuwa na koloni. Simpo.
 
Haya mambo anayajua Faiza foxy na bwana ake mohamed said jinsi waarabu walivyotawala pwani na pembe ya afrika

Heshima ni kitu cha bure, wala si uungwana kututukana. Naomba sana tuheshimiane, waja wema huwa na kauli njema.
 
hao waliwauza babu zetu mithili ya ng'ombe, hawafai hata kidogo ni zaidi ya wakoloni wa kizungu

teh teh teh! Waarabu wabaya sana coz walishiriki kuwauza Maniga huko ufaransa,uingereza,marekani{kwa mabwana zenu wazungu ambao mnawaona wema }lakini aliogopa kuwapeleka kule arabuni coz biashara hiyo ilikuwa haramu.. Lakini Waarabu ndo wakoloni pekee walo"zaa" na dada zenu weusi na kuish nao kama wake zao...
.
.
Namaliza kwa kusema kuwa waarabu walikuwa wakoloni "waungwana" walotuletea Uislam
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom