yorkshire
JF-Expert Member
- Sep 9, 2016
- 2,445
- 2,956
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada bila kupoteza muda.
Nimekuta ugomvi mkubwa tu ambao umetokana na kichwa cha habari hapo juu, upande mmoja ukipinga vikali mwarabu kuitwa mkoloni na upande mwingine ukimuhusisha mwarabu moja kwa moja kama mkoloni namba moja tena ambaye ni mbaya kabisa.
Labda turudi kwenye maana ya ukoloni, vitabu vingi vinasema kwamba ukoloni ni kitendo cha nchi moja yenye nguvu kiuchumi, kisiasa , kijamii na kiutamaduni kuitawala nchi nyingine ambayo ni dhaifu kwenye vipengele hivyo vinne. Sasa basi kutokana na hivyo vingepele ni dhahili mwaarabu na mreno wanaingia moja kwa moja kwenye kuitawala Tanganyika.
Bahati mbaya sana vitabu vingi haviwataji waarabu na wareno kama wakoloni hasa waarabu wanatajwa kama wafanyabiashara ili hali waliitawala Zanzibar na Pwani ya Afrika Mashariki kwa miaka nenda rudi katika nyanja zote nne muhimu.
Upande wa watetezi waarabu wanadai kuwa wao (Waarabu) hawakuwa wakibeba rasimali kuzipeleka kwao uarabuni walizitumia hapa hapa Afrika Mashariki kwa kuanzisha makazi Pwani na Zanzibar kwa ujumla wakati huo huo kundi la pili linapinga vikali kigezo hicho likirudi kwenye maana nzima ya ukoloni nini maana yake hata hivyo kundi hili la pili wameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa waarabu hawaingizwi kwenye kundi la wakoloni kwa sababu ya mapenzi binafsi ya waandishi wa vitabu kuwa wanashabihiana nao kwenye suala la dini (Uislamu) ndio maana waarabu hawaandikwi hivyo tofauati na wazungu ambao ni Wakristo.