Waarabu hawakuwa Wakoloni Afrika?

Waarabu hawakuwa wakoloni Afrika. hilo ni jibu tosha.

Usichanganye Uarabu kama ni Taifa fulani, Uarabu ni lugha zaidi ya Taifa. Kama vile Mswahili, mswahili si Taifa. Nadhani umenipata.

Hao wengine wote uliowataja ni mataifa ambayo yanaweza kuwa na koloni lake. Kama si Taifa huwezi kuwa na koloni. Simpo.

Kwanza nashukuru kwa changamoto yako. Mimi niliposema waarabu nilimaanisha waarabu bila yakujali wametoka nchi gani. Hata ukiangalia hao wengine nilitaja wakoloni kisha nikataja na nchi zao. Hapa umeleta kitu kipya kabisa kizuri "nchi" maana hata Afrika wakati huo inatawaliwa sidhani kuna eneo liliwezekanika kuitwa nchi.

Lakini kuna hoja ya msingi hapo ambayo inatakiwa kujadiliwa. Nani na nini hasa hufanya nchi. Huu mfumo tulionao sasa wa "nchi" ndiyo ulikuwa unatumika wakati huo. Hivi tafsiri ya nchi kwa waarabu na wazungu inafanana? Faiza umeleta swali la Kisomi sana.

Labda kweli waarabu hawakuwa wakoloni kwa sababu wao hawakuja Afrika kama nchi!! Utetezi huu unatosha?
 
Kweli biashara ya utumwa ipo mpaka leo lakini waarabu si ndiyo walikuwa wanaongoza kwa biashara hiyo huku Afrika?

Walikuwa wanawauzia kina nani hizo bidhaa za utumwa?

Mkuu unaweza kutuwekea ushahidi wa hayo maneno yako ili tupate kujadili vizuri
 
Walikuwa wanawauzia kina nani hizo bidhaa za utumwa?

Mkuu unaweza kutuwekea ushahidi wa hayo maneno yako ili tupate kujadili vizuri

Kwahiyo hapa unataka kukanusha kwamba waarabu hawakuwa wanafanya biashara ya kuuza waafrika ama unataka kusemaje?

Juzi juzi tumesikia jinsi wakenya (hasa wamnawake)wanavyouzwa huko saudi arabia na kuteswa, huo ni ushahidi mmojawapo wa biashara ya binadamu kuwepo.
 
waarabu walikuwa wananunua watumwa na kuwauza amerika zamani usa ilijulikana kama plantations za waingereza na scotland irish wakapewa sehemu ya mashamba amerika ili wakubali kuungana nao.(waweza google). ndo maana black americans ni wengi huko but not in asia.wote (manza nyanza) wametusumbua waafrika hao WAKOLONI NAO PIA.
 
Walikuwa wanawauzia kina nani hizo bidhaa za utumwa?

Mkuu unaweza kutuwekea ushahidi wa hayo maneno yako ili tupate kujadili vizuri
Hata Uarabuni waafrika walipelekwa lakini sijui walipotelea wapi!!?? Labda wote waliishia Oman.

Afrika kote kulikuwa na tawala lakini hakukuwa na nchi kwa mfumo tunaoufahamu leo. Hata hao waarabu walikuwa na "nchi' kwa mifumo yao ya kiarabu iliyojengwa juu ya misingi Uislamu. Ndiyo maana niliuliza kama tafsiri ya "nchi' ni moja dunia nzima.
 
Kwahiyo hapa unataka kukanusha kwamba waarabu hawakuwa wanafanya biashara ya kuuza waafrika ama unataka kusemaje?

Juzi juzi tumesikia jinsi wakenya (hasa wamnawake)wanavyouzwa huko saudi arabia na kuteswa, huo ni ushahidi mmojawapo wa biashara ya binadamu kuwepo.

Naona unakurupuka kwa jazba sijuhi hata nilochouliza umekielewa
 
Kwanza nashukuru kwa changamoto yako. Mimi niliposema waarabu nilimaanisha waarabu bila yakujali wametoka nchi gani. Hata ukiangalia hao wengine nilitaja wakoloni kisha nikataja na nchi zao. Hapa umeleta kitu kipya kabisa kizuri "nchi" maana hata Afrika wakati huo inatawaliwa sidhani kuna eneo liliwezekanika kuitwa nchi.

Lakini kuna hoja ya msingi hapo ambayo inatakiwa kujadiliwa. Nani na nini hasa hufanya nchi. Huu mfumo tulionao sasa wa "nchi" ndiyo ulikuwa unatumika wakati huo. Hivi tafsiri ya nchi kwa waarabu na wazungu inafanana? Faiza umeleta swali la Kisomi sana.

Labda kweli waarabu hawakuwa wakoloni kwa sababu wao hawakuja Afrika kama nchi!! Utetezi huu unatosha?

Hakuna utetezi hapo, kuna "facts". Kama si nchi huwezi kuwa na koloni, sijui ni kipi kigumu kukielewa. Tuchukulie mfano hai, Obama baba yake ni Mkenya na asili yake ni baba yake na ni Wajaluo, tuseme leo USA ni koloni la Kenya au Wajaluo au Afrika? Fikiri.
 
Mwana JF,
Vitabu ving tu vinaeleza vizuri matokeo ya biashara ya Waarabu na Sub-Saharan Africa ambayo ilipelekea kwa taratibu taratibu kwa pwani za Somalia, Kenya, Tanganika na Msumbiji kuwa makoloni; na Zanziba aidha kutekwa kabisa! Mpaka mwaka 1963, ukanda wa kilometre kumi za pwani ya kenya ilikuwa chini ya Mfalme waZanzibar. Hat hivyo msome Opoku Agyeman kwenye - The Pan African World View; hii hapa sehamu tu ya maandishi yake:
The Arabs played a role in the invasions and conquests that wrought destruction on the ancient Black Kingdoms and empires of North-East Africa, as well as on the West African Black states of Ghana, Mali and Songhay. The Arab slave trade in Africa was a destructive force that raged from the 9th through the 19th centuries in the Eastern seaboard of Africa, both preceding and outlasting even the transatlantic slave trade on the West Coast. The Arabs made depredations on the Sudan through the murderous campaigns of Muhammed Ali at the beginning of the 19th century, and joined in the European Scramble for Africa in the latter part of the same century in an effort, once again, to carve out an African empire for themselves. Through this nexus of social, economic and political assaults, the relations between Arabs and Africans took on the confirmed asymmetry of victimizer and victim. Despite their awareness of the glaring disproportion in the ex- changes between the two races, the Africans, supposedly on the basis of geopolitical considerations flavored with presumptions of Third World solidarity, argued their way vigorously, in the post- World War II era, into a political alliance with the Arabs. As Nkrumah put the case, Africa's freedom "stands open to danger just as long as a single country on the continent remains fettered by colonial rule and just as long as there exist on African soil puppet governments manipulated from afar."[SUP]4[/SUP] The construct involved here is one of a "marriage" founded on the conception that both the Africans and the Arabs on the continent shared identical interests in the independence of Africa — that together they shared the aspiration of liberating Africa from the imperialist encroachments of the Boers to the South and Israelis in the Middle East. To lay bare the essentially expedient nature of this "wedlock", we need only remind ourselves of the core ingredients of Pan- Africanism, and set them against the dynamics of the ideological- political movement of Pan-Arabism. The core ingredients of Pan-Africanism include Afrocentricity; positive racial self-concept, commitment to racial resurgence; racial privacy; positive concep- tion of African history; corporate racial family; and unity. It is necessary to bear in mind the element of Afrocentricity in par- ticular, referring as it does to the Africa of the Africans, of Black people, and decidedly not to a geographical area which includes Africa's invaders — whether they be the Arabs who set foot there over a thousand years ago, or the Dutch who made their incursion some five hundred years ago. In Chinweizu's observation: "The Arab world, even if part of it shares the same land mass with us (Africans), is still the Arab world. Their preoccupation is Pan- Arabism."[SUP]5[/SUP]
 
Zanzibar na pwani yote ya Afrika Mashariki lilikuwa koloni la Oman.

Historia ukiisoma vizuri utakuta Oman na pwani ya Afrika mashariki ilikuwa ni himaya ya Zanzibar. Zenj Empire. Na Oman haijawahi kuwa na koloni Afrika Mashariki.
 
Hakuna utetezi hapo, kuna "facts". Kama si nchi huwezi kuwa na koloni, sijui ni kipi kigumu kukielewa. Tuchukulie mfano hai, Obama baba yake ni Mkenya na asili yake ni baba yake na ni Wajaluo, tuseme leo USA ni koloni la Kenya au Wajaluo au Afrika? Fikiri.
Bi Mkubwa sijakubishia bali ninachotaka kuuliza ni kama tafsiri ya nchi kwa wakati huo inafanana na tafsiri ya nchi kwa wakati huu? Na mifumo ya waarabu wakati ule haukuwawezesha kuwa nchi inayotawala nchi nyingine?
 
Historia ukiisoma vizuri utakuta Oman na pwani ya Afrika mashariki ilikuwa ni himaya ya Zanzibar. Zenj Empire. Na Oman haijawahi kuwa na koloni Afrika Mashariki.

Zenj Empire. Haya lete habari!!
 
Bi Mkubwa sijakubishia bali ninachotaka kuuliza ni kama tafsiri ya nchi kwa wakati huo inafanana na tafsiri ya nchi kwa wakati huu? Na mifumo ya waarabu wakati ule haukuwawezesha kuwa nchi inayotawala nchi nyingine?

Naona hujanielewa, nimekuambia Uarabu sio Utaifa kwa maana hiyo sio nchi. Uarabu ni lugha. Sasa kama Lugha ya Kiarabu imefanya koloni Afrika basi lugha ya Kiswahili imefanya koloni Afrika Mashariki na inaendelea kukuza koloni lake. Sijui umenielewa au?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom