Waandishi waungane kukomesha hii Tabia Chafu ya Haji Manara

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,191
103,716
Ukimsikiliza Afisa Mhamasishaji wa Yanga utaona namna gani anaumizwa na dhihaka anayofanyiwa na Watanzania wenzake ambayo hajawahi kufanyiwa akiwa nje ya Nchi yake pendwa aliyozaliwa na kuipenda.

Kama kuna Watanzania wanamfanyia dhihaka hii bila sababu yoyote, yani anapita tu mtaani unamdhihaki kwa ulemavu wake wanakosea sana sana sana.

Hatupaswi kufanya namna hiyo kwani jamii na familia zetu zinatufundisha kuwa na huruma na watu wenye mapungufu ya kimaumbile kwa namna yoyote ile.

Watanzania wanapaswa kufuata mafundisho mema ya Dini zetu Kuu 2 ambazo zote zinapinga hili kama zinavyopinga mambo mengi maovu yasiyo na maana.

#Mytake
Ulemavu haupaswi kuwa kinga kwa mmoja wetu kufanya dhihaka kwa wengine kisa yeye mlemavu, akidhihakiwa yeye kwa ulemavu wake ama namna nyingine yoyote, aanze kusaka huruma ya jamii.

Afisa mhamasishaji amedhihaki wangapi kwa maumbile yao? Alimdhihaki Makamu Mwenyekiti wa Yanga na kumuita Kilo 800 tena mbele ya Camera za Waandishi Habari, huko alikotembea mwenzetu ile ni sawasawa tu.

Afisa mhamasishaji amemdhihaki mara ngapi mwekezaji wa Simba kwa Uhindi wake? Vipi huko Duniani wanakoenda wenzetu hii haina shida? Wangapi wamedhihakiwa na kuitwa majina yasiyofaa iwe dhahiri au kwa kificho na Bwana huyu ambaye analalamika yeye kudhikiwa?

Ukidhihaki wenzio kwa unayoyaona yanafaa kwako, usiwachagulie wewe wakudhihaki kwa lipi. Dawa ni kutowadhihaki ili nawe wakulindie udhaifu wako.

Vingenevyo kuwa mvumilivu tu bro, kuna walemavu wa ngozi wanapaswa kulalamikia hilo lakini sio wewe au wale wenye tabia kama zako, kwani unaowadhihaki ni Binadamu kama wewe wana wazazi, mioyo, ndugu na familia kama wewe. Wanaumizwa na dhihaka zako ila wanavumilia wao na familia zao, nawe vumilia tu usitangulize ulemavu wako

Mwalimu wa Madrasa anaejua Dini vilivyo hawezi kuwa wa mwanzo kutakia wengine mabaya tena hadharani na kushinda kwenye vilabu vya pombe analewa halafu analalamika jamii yake kukosa Dini. Nani anapaswa kuwa mfano sasa kama sio wanazuoni wa mambo ya Dini?

NB: Ukiishi kwenye nyumba ya vioo usiwe wa kwanza kuanzisha ugomvi wa mawe, wajuba watakupopoa tu bila kujali mambo mengine.

BIN KAZUMARI.
 
Acheni unafiki we Kolowizard mkubwa. Kwa hiyo dhihaka ya Haji umeiona leo kwa kuwa yuko Yanga sc. Mbona alivyodhihaki akiwa kwenu ulikaa kimyaa. Hebu nyamaza na funga mdomo wako mnafiki usiye na haya. Acha AWachambe, si mlimlea? Hayo ndiyo malipo kwenu na mvumilieni tu hakuna namna
 
Simba ndio waliomfundisha Manara kuwa na kidomo domo, akiwa huko kazi yake kubwa ilikuwa ni kudhihaki timu na watu...
 
Acheni unafiki we Kolowizard mkubwa. Kwa hiyo dhihaka ya Haji umeiona leo kwa kuwa yuko Yanga sc. Mbona alivyodhihaki akiwa kwenu ulikaa kimyaa. Hebu nyamaza na funga mdomo wako mnafiki usiye na haya. Acha AWachambe, si mlimlea? Hayo ndiyo malipo kwenu na mvumilieni tu hakuna namna
Sasa wewe unadhani mleta mada ndio analia? Anayelia ni huyo waliye mkebehi kuwa zeruzeru kwa vile anakebehi wengine. Kama unasisitiza aendelee basi aache kulia lia kuomba huruma
 
Mungu hakupi vyote kuna kitu hatakunyima tu duniani maana anajua akikupa vyote utasimanga sana na kusumbua sana watu kuna jambi haji amenyimwa na Mungu nahisi angekipta angesumbua sana hivyo kwa mtu mwenye kuelewa huwezi poteza muda wako kubishana nae wengi hawalijui hilo ndio maana wanaumia kwa maneno yake hata utopox wenyewe aliwaaambia kuwa katika mashabiki wote wa utopox wenye akili wawili 2 ila Leo wanamfuraia wameshasau
 
Aliwai kusema,"ukimtoa babake na mzee wa Msoga mashabiki wote wa Yanga awana akilli"
hii nidhihaka kubwa japo kua ni kweli mashabiki wa Yanga awana akili,lakini akupaswa kusema.
Na rage alituambia nyie makolo ni mbumbumbu
 
Acheni unafiki we Kolowizard mkubwa. Kwa hiyo dhihaka ya Haji umeiona leo kwa kuwa yuko Yanga sc. Mbona alivyodhihaki akiwa kwenu ulikaa kimyaa. Hebu nyamaza na funga mdomo wako mnafiki usiye na haya. Acha AWachambe, si mlimlea? Hayo ndiyo malipo kwenu na mvumilieni tu hakuna namna
Unazidi kuthibitisha kuwa, WENYE AKILI NI WAWILI TU!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom