Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,095
- 43,305
necessity is a mother of all inventions..tukianza kuona kuwa vitu fulani could be simplified.. ungeshangaa..
necessity is a mother of all inventions..tukianza kuona kuwa vitu fulani could be simplified.. ungeshangaa..
Huyo watson sio baba wa dna kama unavyodhani mama wa dna anaitwa franklin rosakind, na hao wakina watson waliiba tuu kazi a huyo mama, hakuna chochote kipya walichokifanya, mengine nitakujibu kesho............
Unajua huyu Game Theory ana material si kitoto, akiamua kukata ishu hadi utapenda yaani anaongea points kwa kumwaga datas pia ! Keep it up Game Theory !
angetumia huo mfano hapo juu mwanakijiji asikwambie mtu, waafrika wangewatoa nishai wazungu haki ya nani, si unajua waafrica wanavyojua kusoma na kuelewa, tokea kipindi kile kusoma usiku na vibatari lakini mtu still anamanage kufanya vizuri achilia mbali hawa waliozoea study lamp, na still wanafanya poor darasani, sasa uniambie wote wapate breakfast ya nguvu asubuhi, computer, wanalaza ubavu wao kuzuri kitandani ndani na kyoyozi, wazungu watatafuta pa kukimbilia nakwambia !
Pasingekuwepo na tofauti yoyote as far as the skin color is concerned! Na kama ingekuwepo ni very insignificant.
Nyinyi wote humu ndani mnaomuunga mkono huyo jamaa hamna akili, kwani IQ manake nini??? kama ingekua sisi hatuna akili kiasi hicho na kama huyo msenge masatu anavyosema basi waafrika wanaomaliza sekondary africa wasingeweza kusoma ktk vyuo vikuu ulaya kwa maana wangefeli muhula wa kwanza, madaktari wa afrika wasingeweza kufanya kazi ulaya, baadhi ya makampuni makubwa yasingeweza kuongozwa na waafrika.
Sidhani kuwa huyu Watson anakijua anakiongea, IQ inahusisha vitu vingi, nilifikiri atajua zaidi, mtoto wake mwenyewe ana kichaa (schizophrenic). Hata hivyo wazungu wengi wanaelekea kutojua historia ya dunia.Watu wa kwanza kuanzisha science walikuwa waafrika wa Egypt na nubia, 4000BC( Soma African origin of Civilisation,Myth or reality, by cheikh anta diop).Wazungu enzi hizo walikuwa wanaishi kwenye mapango!!!Wagiriki wenyewe walijifunza science, falsafa, n.k Egypt, wakina Pythagoras, archmedes, na wanasayansi karibu wote wa kigiriki walisema wazi kwamba walijifunza kutoka kwa waafrika wa Misri. Soma Herodotus histories.
In actual fact wazungu ni watu wa mwisho kujua science , falsafa n.k .Kati ya wazungu,walianza wagiriki na hawa walijifunza kutoka Egypt around 500BC!! Mamia ya miaka baada ya wamisri. Na hawa wazungu walikuwa watumwa huko misri kwa miaka zaidi ya 3000!
Kinachotuaribu waafrika na kinachotufanya tuonekane na IQ ndogo ni watu kama Jakaya Kikwete, (Ilikuwaje tukamchagua mtu mwenye fikra finyu kama huyu?) ambao kila siku wanaenda ulaya kuomba misaada baada ya kukaa chini na kuendeleza sayansi kwenye shule na vyuo vikuu vyetu na kuimarisha government admistration. Kama kuna rushwa na government admistartion mbovu hata tukipewa mabilioni, pesa zote hizo zitayeyuka!
Je hao watu wenye akili kukuzidi wasingemchagua mtu kama joji bush.....ambaye alishinda kwa kura nyingi tuu mara ya pili ingawaje hao watu unaowaabudu walijua fika kwamba jamaa ni bomu kichwani, wasingekubali kuishi ktk nchi ambayo inatumia pesa zao za kodi kwenda kuvamia nchi nyingine kwa manufaa yasiyo ya taifa bali ya watu binafsi,wasingekubali kuishi ktk nchi ambayo asilimia 5 ya wananchi wanashikilia uchumi wa nchi nzima, wasingekubali kuishi ktk nchi ambayo matajiri tuu ndio wana bima ya maisha ingawaje watu wote wanalipa kodi, wasingekubali kusihi ktk nchi ambayo maskandali kama ya enroni ambapo mtu mmoja au wawili ametumia fedha na kufirisi moja kati ya mashirika makubwa dunia na kuteketeza akiba za uzeeni za watu zaidi ya 10,000 kwa manufaa yake binafsi kama wao wangekua na akili haya yote na mengineo mengi yasingetokea.... itaendeleaLabda watu wenye akili wasingemchagua mtu kama Kikwete....