mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Vyama vya Siasa nchini vinatakiwa kuweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia watu wenye changamoto ya kusikia na kuongea ili kutimiza haki yao Kikatiba ya kushiriki katika mchakato mzima wa kushiriki uchaguzi bila kuwepo kwa vikwazo.
Kutokuwepo kwa mazingira rafiki kwa kundi hili maalum, kunaweza kuwa chanzo cha wao kutowapata viongozi ambao watasimamia maslahi yao na ya wengine wenye uhitaji maalum. Watu wenye ulemavu wanapaswa kupewa kipaumbele ikiwemo kuweka mazingira wezeshi yatakayosaidia kushiriki mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua za awali.
Hii itawasaidia ushirikishwaji wa kina kwani watapata uelewa zaidi wa hotuba na midaharo itakayokuwa inatolewa na wagombea mbalimbali na vyama vya siasa kwa ujumla, hivyo kuwawezesha kufanya maamuzi wakiwa na taarifa sahihi.
Kwa ajili ya ustawi wa demokrasia nchini, suala hili haliepukiki.
Asanteni.