Mkuu hili lifanyie utafiti kwanza kabla hujapingana na Thiong'o. Vyama vingi vimeanzishwa 1995 Nyerere aliondoka madarakani 1985 sasa hebu rudi nyuma zaidi ya hiyo 1992.
Umoja huo wa Watanzani uliokuwepo kabla awi la CCM halijaazishwa Februry/March 2007 ni upi? Pia, hebu tuambie umoja huo umeadhirika namna gani tangu Februry/March 2007 baada ya CCM London kuanzishwa.
Sasa hao watu wanafanikiwa kwa sababu mtu kama wewe na wengine wenye mawazo kama yako hawajitokezi huko kwenye mikutano kuwapinga wasiwe viongozi. Na kama unaona huwezi kwenda kwenye mikutano kwa sababu wewe sio CCM basi kwa nini usiwaachie wana CCM wachague viongozi wao wanaowaona wanafaa. Kama huyu kiongozi ukimuona hafai katika chaguzi za ngazi za juu una uhuru wa kupigia kura mgombea wa Chama kingine.
Mimi naamini bila CCM imara Taifa letu liko mashakani na nina imani hapa UK kuna watu wanaweza kwenda kujiunga na CCM na kubadilisha mambo kwa nfasi zao kama ambavyo Mbunge Anne Kilango au Dr Mwakyembe wamefanya mpaka sasa.
Yebo Yebo,
Uhuru wangu hauishii kwenye kupiga kura, ni pamoja na haya tunayopinga sasa. Process ya kupata kiongozi wa taifa ni ndefu mmno, kama unavyojua garbage in garbage out. Ni muhimu kupinga yale ninayoyaona hayafai mapema kabla hata ya kufika huko kwenye uchaguzi. Hayaishii hapa, tutawapinga hata hiyo 2010, ndio maana ni muhimu kukusanya dossiers zao.
Tumeona madhara ya hawa watu ambao wako tayari kutumia kila njia ili kujijengea mazingira ya kutwaa uongozi Tanzania. Nyerere alisema ogopa mtu anayekimbilia Ikulu kwa njia zote, wengine tunasema ogopa watu ambao wako tayari kutumia njia zozote kupata ubunge Tanzania.
Kuhusu umoja, tatizo la watu wengi ni kuangalia mazingira waliyopo tu. UK kuna matatizo mengi kabla hata ya matawi ya CCM kuanzishwa. Kuanza kwa hayo matawi kunazidisha kubomoka kwa haraka kwa umoja ambao Nyerere alitumia nguvu zote kutuhakikisha tunakuwa nao. Wengine tumeishi nchi nyingi zaidi ya UK, hasa Europe, kwasababu wao mara nyingi wanakuwa wachache kuna umoja mkubwa na mafanikio kuliko hapa UK.
Nani kakuambia sihudhurii mikutano ya Watanzania UK? Nilichosema sitahudhuria ni hiyo mikutano ya CCM nje ya nchi.
Kuhusu matawi ya CCM nje ya nchi, labda wewe na huyo Thiongo ndio leteni
ushahidi. Huko nyuma nimewahi kuwa kiongozi wa vyama vya wanafunzi hapa Europe, hakuna mahali popote hata kwenye historia ya hivyo vyama panapoonyesha wananchi wa nje walikuwa na matawi ya vyama au walikuwa wanaweka UCCM mbele. Chama kilikuwa kinashika hatamu na ili uje nje ilikuwa lazima uwe mwana CCM lakini hapo ndio ulikuwa mwisho wake, ukifika nje wote tulikuwa Watanzania.
Ukiangalia haya mambo ya vyama, washabiki wakubwa ni watu waliokuja nje miaka ya 2000. Ni matokeo ya mgawanyiko wa Watanzania huko nyumbani na wanauleta hata Ulaya. Huko nyuma umoja wa Watanzania nje ya nchi ulikuwa muhimu sana, hakukuwa na mawasiliano ya kuaminika na nyumbani, hakukuwa na JF, hata kuongea na nyumbani ilikuwa shida. Mshikamo ilikuwa ni kitu muhimu mno kwa Watanzania na ndio maana mpaka leo watu waliokuja siku nyingi nje ya nchi wanaheshimu umoja wa Watanzania kuliko waliokuja miaka ya karibuni.
Huko tunakokwenda na kadri Watanzania wanavyozidi kuwa wengi nje ya nchi, hata ukabila utaanza kukua na tutaishia kuwa kama Wakenya tu. Usipozuia jambo moja, mengine huzaliwa.