Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,890
Ninataka kujua sheria inasemaje juu ya CCM kuwa na Tawi London!

Ni baada ya kuona watanzania tunazidi kugawanyika kwa kiasi kikubwa kisa ni vyama na si maslahi ya Tanzania nimeamua kuchukua hatua za makusudi za kutaka kuijua sheria ya Uingereza inasemaje juu ya kuanzishwa kwa vyama siasa au kuwa na matawi nchini humo.

Nimeshangazwa sana na hatua ya mumewe balozi kuwa kiongozi wa tawi wakati wakijua kabisa kwamba mkewe ni Balozi wa Watanzania wa vyama vyote na wasio kuwa na vyama .Hii ni hatari sana maan nimesha ona matamko hapa kwmaba hata baadhi wanataka kuanza kususia mambo ya TA UK kwa kuwa yana baraka za kisiasa.

Viongozi wote wa TA UK ni wana CCM lakini wanasahau kwamba walichaguliwa na watanzania wote. Kwa habari hii leo balozi atakuwa na wakati mgumu maana tutaanza kumshuku kwa kuwa mumewe ndiyo kinara wa CCM na hatuwezi kusema kwamba wana tofauti hapana .

Mimi naomba msaada wenu pamoja na kwamba nimeanza kuandikia mambo ya Nje ya UK nitawapa na anuani za ofisi hizo na mamlaka zingine waweze kutueleza kama ni haki kuwa na Chama cha Siasa rasmi kama ilivyo CCM.

Watu najua mtasema CUF lakini CUF ni wapenzi tu ambao wana mshikamano. Hawana matawi wala nini na ni wa kimbizi baada ya serikali yetu ya CCM kumwaga damu kule Zanzibar.

Napinga kitendo cha bwana Majaliwa Sharif kuwa kiongozi wa CCM wakati mkewe ni Balozi tutashindwa kuuamini Ubalozi na kufika kusaidiwa na ni vyema watu wa Ubalozini kujitenga na Siasa za aina yeyote wawapo on duty. Mumewe balozi ni kiungi kikubwa hatuwezi kusema tu kwamba si balozi na hafanyi kazi Ubalozini lakini influency je ?
 
Please don't na haina uhusiano kabisa contents ni tofauti sana. Naomba iachwe hapa hapa .Kama unataka kuchangia sema na kama huna la kusema please pita .
 
Jembajemba

Namuunga mkono Lunyungu, havina uhusiano.

Lunyungu

Hapa unataka kujua Sheria za UK au za Uchaguzi Bongo? Mimi sheria sio fani yangu lakini fafanua labda utapata mtaalamu mmoja wapo kati ya hao.

Nimewahi kusikia kitu kama Democrats abroad group wanakutana London kufanya fund raising n.k wao sio similar na hili la CCM?
 
Sina Uhakika na Sheria lakini Nafikiri inaruhusiwa Kwani kwa hao wenzetu kama ingekuwa hairuhusiwi tungelikwisha sikia Muziki wake.


Sina Uhakika na Sheria lakini Nafikiri inaruhusiwa Kwani kwa hao wenzetu kama ingekuwa hairuhusiwi tungelikwisha sikia Muziki wake.


KNKCU

Sio lazima tuwe "tumeshasikia mziki wake", kwani huenda wamesajili kama charity, or Ltd Company or Trust, au labda hawajasajili kabisa n.k sio lazima wasajili kama "Political Party" kama ilivyo CCM yenyewe.

Kuna haja ya kuchunguza, ila mimi sidhani kama wamesajiliwa...nina mashaka sana na hawa jamaa.
 
I believe in those dark days of Apetheid in SA we had ANC established and even in some ways funded by CCM if was not by our Govt directly .Leo CCM kuwa hivi sina chuki kabisa na wao ila wanatugawa . Tunataka kujua sheria inasemaje . yeboyebo wewe umesema kweli hapa kuna watu lakini pia naweka malalamilka rasmi serikalini UK watanijibu tu na nitaweka hapa . Majaliwa Sharif kufanya siasa namna hiyo ni sawa na kazi je ana kibali cha kazi UK . Je akiwa kwenye mikutano hiyo ikazuka vurumai akapigwa na kuumia nini itakuwa position yake ?

Demo na wengineo hata CUF huwa wanafanya wanaweza kuwa na washabik , wapenzi au hata kuwa na Club ni sawa lakini si kuweka kitu official like what you guys did in UK . NO way .Mnatugawa na wacha tuangalie sheria inasemaje .
 
KNKCU

Sio lazima tuwe "tumeshasikia mziki wake", kwani huenda wamesajili kama charity, or Ltd Company or Trust, au labda hawajasajili kabisa n.k sio lazima wasajili kama "Political Party" kama ilivyo CCM yenyewe.

Kuna haja ya kuchunguza, ila mimi sidhani kama wamesajiliwa...nina mashaka sana na hawa jamaa.
Hapo hapana usajili wowote labda kama unieleze hiyo ofisi waliofungua ni Bubu na inafanyakazi kibubu.Hivyo wazee nyeti hazijawafikia kama ipo sheria ya kutoruhusu.Lakini hivi kweli Mama Balozi pamoja na taaluma yake ya sheria na wadhifa wake wa Kidiplomasia anaweza kushawishika kumruhusu Mume kujiingiza kwenye kitu ambacho ni Illegal ktk Nchi ya watu?
 
Lunyungu,

Unajua hata huku kuna vyama vya nchi nyinginezo ambavyo vimehusika na upinzani wa chama tawala. Yaani watu waliokimbia nchi yao (Udiketa) wakajipa ikmbimzi nje na kuuunda ama kuendeleza mapambano ya kifikra wakiwa nje. Mfano ndio kama huo wa ANC lakini sijawahi kuona chama tawala kikifungua tawi lake nje! Sielewi sababu hasa zinazotumika hapo!

Kibaya zaidi kwa hapo London ni kama ulivyosema. Mme wa Balozi kuwa mwenyekiti wa chama ambacho kina wapinzani na pengine naweza sema wakimbizi wa CUF nchini humo. Maamuzi mengi ya kiserikali yanaweza ingiliana na maamuzi ya kichama.
Nadhani wakati mzuri wa kuweka swala hili mezani ilikuwa wakati ule JK alipotembelea UK.. na majibu ya JK ktk swala la wakimbizi wa UK, dhahiri ilionyesha wazi kuwepo ama kujengwa kwa chuki za kichama zaidi ya kitaifa. Ni lazima JK kapewa maelezo kuhusu maisha ya hawa wakimbizi na ilikuwa jukumu la JK kuwakaribisha upya wakimbizi hao na kuwahakikishia usalama wao pindi wakirudi. Yaliyotokea wakati wa Mkapa (mauaji ya Zanzibar 2000) yalikuwa makosa kwa sababu JK mwenyewe anaamini yalifanyika makosa. Huwezi kuwa punish watu ambao walisalimisha maisha yao na pengine kupunguza vurugu zaidi ndani ya nchi, zaidi ya hapo wengi wa wakimbizi hawa ni wakimbizi wa hali ya kimaisha jambo ambalo nchi kama Nigeria, Cuba, China na India ni sehemu ya mikakati yao ya kuiba teknologia ama kuwapa elimu ya juu wananchi wake.
 
Hapo hapana usajili wowote labda kama unieleze hiyo ofisi waliofungua ni Bubu na inafanyakazi kibubu. Hivyo wazee nyeti hazijawafikia kama ipo sheria ya kutoruhusu. Lakini hivi kweli Mama Balozi pamoja na taaluma yake ya sheria na wadhifa wake wa Kidiplomasia anaweza kushawishika kumruhusu Mume kujiingiza kwenye kitu ambacho ni Illegal ktk Nchi ya watu?


Hivi wewe KNKCU, ccm unawaonaje? Mimi wala sitashangaa kabisa kama ikiwa ni illegal.
 
Whether they are allowed to have a branch or not, thats their issue, cos at the end of the day, the people who will join are CCM followers etc. In my view, the problem comes when every other Tanzanian is assumed to have political interests. The case of JK's first meeting, with CCM hijacking the place, that was so low. We may have differences and no interest in political affiliation, but if the president is visiting, we see him as our Leader, and not a CCM leader. That campaign should stay in bongo. We are intelligent enough to differentiate between party propaganda and genuine Tanzanian concern. Inatia kichefuchefu.......

Having said all that, if the opposition are smart enough, they can actually benefit more if they follow the same path. Infact, its more beneficial for them.....if they cant see that, then kweli bongo hamna opposition. In the UK its a level playing field, and the opposition have more to gain.
 
Defun the issue is not oppositions benefit no .Issue ni CCM kuwa na matawi nje ya Nchi na kufunguliwa na Viongozi wakubwa wa Nchi tena na mtu kama Balozi Malecela ambaye anajua sheria za kibao .Je ni haki ? Je Mumewe Balozi kuwa Mwenyekiti wa Tawi la CCM itanifanya niamini kwamba Balozi ni wa Tanzania badala ya kuwa wa CCM? Wapinzani ambao ni Watanzania na wale amabao hawana vyama lakini wako UK wanawekwa kundi gani kwenye shughuli za Kitaifa kwa kuwa kila shughuli sote tumeona ni CCM kwanza the Tanzania .Naomba msaada wa kuijua sheria wakati mimi naandika Mambo ya Nje na ndani pia UK kuuliza utaratibu wa habari hizi. TZUK kuna ushahidi wa kutosha hakuna la zaidi watakalo taka ili kupata ukweli wa CCM na ofisi UK .Kuna picha hapa pia na link za Forum nawapa mimi .
 
Lunyungu,

Labda nikiweza kuelewa wamejiandikisha kama nini na malengo yao ni vipi, ndio nitaweza kufind out whether its legal or not (and to be honest, sina hata muda wa kufuatilia ishu zao). But am pretty sure, they wont do things kiswahili swahili.

I will also ask a friend of mine (might take a few days, hayupo nchini). Her family live in the UK, wanajishughulisha na siasa nchini kwao kutokea UK, wakifanya mabadiliko nchini kwao, sasa sijui wamejiandikisha vipi. The family is loaded, and organisation is loaded, and they have meetings with people from their country, hapa hapa UK. Mabadiliko na orders zinatokea UK, na mabadiliko yanafanyika taratibu nchini kwao (kwa nia njema). You have the right to ask (I admit I didnt acknowledge that), na mimi ndio maana nasema kwamba (as an addition), opposition wangekuwa wajanja, wange-benefit zaidi. Ila kwavile ni mbio za CCM vs opposition, wacha wengine tukae pembeni tuangalie........Vita Vya Panzi.........

Read this transcript, I picked up the info below;

http://transcripts.cnn.com/TRANSCRIPTS/0108/31/ltm.16.html

'In the USA, you can register with Foreign Agents Registration Act, which will demand any organisation or people raising money for foreign political parties to register with US Justice department'. So I suppose it might be similar thing with UK, just how they register themselves as and their goals.
 
Defun
CCM they are not raising cash ila wanachimba shimo kuweka msingi . Hawasemi kwa nini wanataka matawi . CCM hawawezi kuetegemea pesa za wabeba ma box toka UK maana wanakula pale pale hazina . Unajua wanapa kiasi gani kwa mwezi kisa ni majority ? Sijajua malengo hasa ya CCM na matawi yao kwa kasi . Ni symbolic kwamba wanakubalika ama ni kitu gani hasa kinatakiwa ?Bado nataka kujua sheria inasemaje .
 
Lunyungu,
Kuna issue ya Srilanka imeleta minong'ono hapa UK Parliament na Srilanka penyewe. Am sure utakuwa umesikia kuhusu hii.
Nakupa link;

http://www.asiantribune.com/index.php?q=node/5640

Sasa (forgetting about fundraising), its clear hawa watu wana vyama vyao huku UK, na vinaruhusiwa. Ishu tu ni kwamba, wana extort pesa kwa population yao hapa UK, na pia wakuu kule Srilanka wamekuja juu. Otherwise, nadhani wanaruhusiwa kuwa na some sort of Chama....labda kama NGO. Ndio maana nasema, ukiweza kujua CCM wanajiandikisha kama nini hapa London, ndio utapata jibu la maswali yako yote.
 
Kwa maarifa yangu sioni kama katiba ya nchi yetu inaruhusu matawi nje ya nchi.
kuna watu wamemdanganya Sharif Maajar ili wapate umaarufu kupitia mgongo wa Balozi.

nilisema huko nyuma balozi atajua kama kauvaa mkenge kuanzia matawi ya chama, Miss Tanzania UK, na Yebo Yebo kumdanganya kuwa within a year jumuiya ya Watazania UK itakuwa na Jengo kama la bond street.

Waulize hao ccm so far wamepata wanachama wangapi? jibu hakuna.
Uliza wana Cuf mambo wanayoyafanya utazimia, wao wanapeleka ZNZ sio kuchukua toka Africa kama hao CCM ambao hadi Bendera ya tawi lao wameiandikia write up akapelekewa Malinzi.
 
Hawa CCM wamechemsha sana kwenda kufungua matawi nchi za nje. Kwanza katiba ya CCM na Tanzania zote ziko kimya katika kufungua matawi nchi za nje. Pili sidhani kama waliangalia katiba za nchi husika zinaruhusu vyama vya nchi nyingine kuwa na matawi katika nchi zao. tatu, Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili na Watanzania wanaoishi UK na nchi nyingine zenye matawi ya CCM wana uraia wa nchi hizo. Na hakukuwa na mchujo wowote kuangalia kama waliojiunga na matawi hayo bado ni Watanzania au la. Kwa maana hiyo basi CCM imevunja sheria za nchi kwa kuwa na wanachama ambao si Watanzania.

Nina hakika kabisa kwamba baadhi ya wanachama hao wa CCM ama wana uraia wa nchi hizo ama wako mbioni kufanya hivyo. Baniani mbaya..... Wanataka kukusanya pounds na dollars toka nje wakati huo huo huo bado wanajikanyaga kanyaga inapokuja uraia wa nchi mbili
 
Hao wasri lanka~Tamil Tiger~ndio wanakusanya michango mingi katika nchi mbali mbali za nje ili kwenda "kuikomboa" nchi yao. Wanatumia hata vitisho kwa wenzao ili wachange michango hiyo.

Sasa hivi baadhi ya wasrilanka wamewatolea nje na kwenda kuwashtaki katika serikali mbali mbali za magharibi. Hii imesababisha Tamil Tiger kuwekwa kundi la majasusi na hivyo kupigwa marufuku katika baadhi ya nchi. Naamini si muda mrefu watapigwa marufuku nchi zote za ulaya magharibi na North America.
 
Well I know little on CCM or opposition Politics but I guess hizi ni deal za maopportunist wanaotaka serikali itake note their presence and participation katika shughuli za kichama. Zaidi ya hapo sioni kwa nini chama kinachoshinda kwa 80% kitafute wanachama wengine nje ya nchi. This is just opportunistic move by some "smart fellaz". Ni opportunist kwa sababu wangekuwa na nia njema wangeanzisha foundation ya kuspearhead maendeleo ya nchi katika nyanja mbali mbali nyumbani. In anyway I wish them luck in this!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom