Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Kukimbilia kufungua mashina ya CCM huku mkiongoza kuwamwagia misifa viongozi wa CCM ambao kila mtu anajua ni incompetent na Corrupt ni kuishiwa hoja ambazo zingeweza kuongoza kujenga taifa letu. Hivi inaingia akilini kweli wakati huu ambao Taifa liko katika wakati mgumu kutokana na viongozi wengi waliotoka CCM ambao wanaongoza kwa ubadhirifu wa mali za umma na rasilimali za nchi, baada ya kukaripia uchafu huu unaoendelea, nyinyi mnaongoza kuwamwagia sifa hawa mafisadi. Ilitegemewa kwamba wasomi kama nyinyi ndio mngekuwa mstari wa mbele katika mapigano ya kuleta haki na kumaliza rushwa hatimaye kuingoza nchi katika kuiletea maendeleo ya kiuchumi. Lakini leo hii ndio kwanza mnajiunga na MAFISADI na kuzidi kuwafanya waone kuwa hata wasomi wanawakubali katika ujambazi wao wanaoufanya nchini mwetu. MNABOA, MNANUKA NA MNATIA AIBU.

Good job Geeque,

mazee naona wamekuboa hadi basi tu! Utakuta watu mambo muhimu ya nchi wako kimya na kusifia ufisadi day in day out. Inaonekana wengine hata kuwa na redio ya internet ni makosa! Kwi kwi kwi yaani kuna watu wanataka kuwe na radio uhuru na RTD pekee ili kumwaga propaganda za Kingunge na wezi wenzake! grrrrrrrrr
 
Speech Ndefu imejaa sifa kwa CCM instead of critising, humbling down, accepting mistakes and showing us the new ways to solve these problems (realistically)..umegusia swala la ufisadi kwa mbali kama kikwete vile...umeacha tuu kusema vijana tuunde tume ya kuhakikisha huu ufisadi kama ni kweli..campaign za kukanda upinzani were for 1995, 2005..saizi kila mtu anajua CCM chafu!!Mayb u can fool those kids in India of which 80% are on govt scholarships so they knw wer their loyalites lie....uchafu wa CCM umetapakaaa..tumechoka hadithi..hata waandishi wa magazeti ya rostam are doing a better job kusaficha chama kuliko nyie vijana wasomi mnaokula hela zetu za kodi India!!

ps: shein labda atakupa u assistant wake mkafungue mabucha na masoko wote!!

Kuongea tu ndio wanajua, muda wanatumia kuandika hotuba mbovu kama hizi wangeutumia kuchambua au kusoma vizuri mikataba ya madini, yale ya Buzwagi yasingetokea!
 
Naona ni kweli mwafrika wa kike hawa watu wanataka tusikilize Radio Uhuru na RTD pekee watupe propaganda zao. Bora hizi radio zetu uchwara lakini zinawafikia wengi katika nchi mbalimbali duniani kwa sababu tunajaribu kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia kuliko wao hata tovuti ya Ikulu inawshinda kutengeneza.
 
Kuongea tu ndio wanajua, muda wanatumia kuandika hotuba mbovu kama hizi wangeutumia kuchambua au kusoma vizuri mikataba ya madini, yale ya Buzwagi yasingetokea!

Amen to that..wasting their skills on the wrong things...kuna wakati ilikuwa sifa kuwa mwanasheria wa serikali lakni saizi ni haibu..utafikiri watu wanaletewa mikataba na kuisign tuu..ndo taifa la kesho hili! TUMEKWISHA!!

Lakini kwa kuandika hotuba za sera za chama aaah ata nyerere haoni ndani..
 
Kwao kutetea maslahi ya CCM ni muhimu zaidi kuliko kutetea maslahi ya Taifa letu. Wako tayari waibe mapato ya nchi yetu na kuwaumiza mamilioni ya Watanzania ili tu Chama chao kifaidike na kuimarika. Wako tayari kutetea na kuwalinda Majambazi na Mafisadi walioko ndani ya Chama chao ili tu walinde maslahi ya chama na si ya Taifa. Wako tayari waone Taifa linadidimia kiuchumi na wananchi kuzidi kuteseka kwa umaskini lakini tu wao wajaze matumbo yao kwenye majumba yao ya kifahari na magari yao ya thamani tele. Halafu unalikuta jitu limesoma lakini bado linawapigia makofi na vigelegele hawa watu.
 
Naona ni kweli mwafrika wa kike hawa watu wanataka tusikilize Radio Uhuru na RTD pekee watupe propaganda zao. Bora hizi radio zetu uchwara lakini zinawafikia wengi katika nchi mbalimbali duniani kwa sababu tunajaribu kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia kuliko wao hata tovuti ya Ikulu inawshinda kutengeneza.

Yaani we acha tu mazee! vidonge vimewashika wakiona bongoradio inapata wasikilizaji kibao huku ikitoa nafasi kwa watanzania wa nje kutoa maoni yao. Kuna watu utadhani wamezaliwa North Korea au Uchina vile! grrrrr

By the way,

Nimesubiria sana uweke bolingo lakini kimya.... hiii taarabu inaimba bongoradio ikiisha basi twende congo au kinondoni kwa wana ngwasumo kidogo!
 
CCM kusifiwa imekuwa kosa
JK kupigiwa makofi imekuwa kosa
CCm kufungua matawi nje imekuwa kosa
JK kupigiwa saluti imekuwa kosa

JE chadema haitofungua matawi nje kama ingeona kuna haja ya kufanya hivyo ?
 
heri yangu mimi nisie na chama kabisaaa, wala sina mpango "kuitoa" kisiasa...kwa kifupi vyama vyote vimejaa mafisadi!!
kwani nani kawakataza ninyi chadema kufungua cha kwenu huko ughahibuni?? pilipili usoila inakuwashia nini?? au ndio mambo ya kupangiana, wajameni, tupo kwenye demokrasia kama watu wanaamua kupoteza muda(kama mawazo yenu yanavyowatuma, of course na mie pia) kina wauma nini?? ni haki yao kufanya vyovyote watakavyo na chama chao!!!
kuna ka-gene ka-udikteta hapa.......haingii kabisa akilini
!!

wanataka ccm ifanye kazi kutokana na matamanio ya nafsi zao na sio kutokana na mitazamo ya chama CCM. Mbaya zaidi nafikiri hupatwa na pressure kabisa pale expectations zao zinapokuwa too high mwishowe "hayafanyiki" waliyokuwa wakiyatamani au yakifanyaika yanakuwa below of what they expected.

Subiri ninwe maji mie ! huku nikisubiri matawi mengine yakifunguliwa. napata uradi kidogo !
 
CCM kusifiwa imekuwa kosa
JK kupigiwa makofi imekuwa kosa
CCm kufungua matawi nje imekuwa kosa
JK kupigiwa saluti imekuwa kosa

JE chadema haitofungua matawi nje kama ingeona kuna haja ya kufanya hivyo ?

Je ni CCM inayofungua matawi nje au Wapambe wa CCM??
Kwasababu kuna wengi tuu bongo madiwani hadi wabunge..lakini hawanasay yoyote ndani ya CCM ndo muwe nyie mlioshindwa maisha ya ULAYA sasa siasa za bongo ndo last resort??
 
hata ikiwa ccm chini ya wapambe wake ndio wanaofungua matawi, KOSA LIKO WAPI ? au watu wanaongea ili mradi waonekane nao wameongea ?
 
Naona kuna mtu anataka sasa kuamulia watu cha kusema. CCM ni mafisadi na watasemwa anytime anywhere by anybody. Kama hutaki kusoma unaweza kwenda hapa:

walewenyekulialiasanakilamaraccmikisemwa.co.kirohochauma
 
kwikwikwi....watakoma basi kama wana vijiba vya moyo, hivi stress zote hizi za nini? waacheni SISIEM na wapambe wao(kama mnavyowaita) wafanya vyovyote watakavyo na chama chao!!

..kuna rumor kwamba SISIEM wanampango wa kufungua tawi kwenye MOON, MARS na lingine kwenye 'international space station'....Kikwete atakuwa mgeni rasmi kote huko na atatumua "souz" toka Kazakhstan!! LOL....sisiem kiboko yao na zidumu fikra sahihi za marehemu nyerere!!!

talking about pumba
.......!!!

babu wee acha tu, tena saluti atapigiwa, tarumbeta ndio usiseme !
Gwaride la nguvu, picha bweleleeeeeee.

Nadhani watu watakufa hapo ! Hata nickson aliwaza kwenda kwenye moon, ccm nashauri waweke matawi hadi huko......(talking about pesa za ufisadi, lol)

Kazakhstan watasema JK alipewa hela za kampeni huko, teh teh teh !

Ndio hapo ninaposhangaa, ccm chama chao na wanaweza kufanya lolote wanachotaka na chama chao ! na asiyependa akanywe uji wa gundi na vioo vya kusaga !
 
Nakuunga mkono kusema tudumishe Utanzania.

Ila nashindwa kujua hofu yako inatokana na nini; Hapo Tanzania kumekuwa na Vyama vingi tangu 1992, sijapata kusikia Tanzania bara kuwa watu hawazikani au hawaowani kwa sababu zao za kisiasi. Kwa nini unahofia hilo litatokea huku kuliko endelea?

Yebo Yebo Wasiwasi wangu mimi ni kuwa tunataka kukimbia wakati hata kutambaa hatujamaliza. Siasa yetu ni changa mno, tujiimarishe kwanza sisi wenyewe kama Taifa then hayo mengine yatafuata. ndo kwanza katika upeo wa masikio yangu tokea Taifa letu lianzishwe ndo juzi tu tumesikia kiongozi wa juu serikalini kujiuzulu kwa tuhuma; safari bado ndefu ukizingatia kuwa kuna watu bado wana fikira za kuwa wamezaliwa ili waitawale Tanzania.
Tujitangaze kama watanzania, tusaidie kulijenga taifa letu changa then ndo baadae ukivuka mipaka ya Tanzania ujitangaze kama mwanaCCM, au CUF. Unaonaje hapo?
 
Mkuu nakuelewa; Baba wa Taifa alisema ili tuendelee tunahitaji Arthi, Watu, Siasa Safi na Uongozi Bora. Hayo mambo ni LAZIMA yabalance ndio tutaendelea. Sasa Watu tunao, Arthi tunayo; Siasa yetu sio safi kwa sababu inazalisha Viongozi Wabovu. Sasa ni lazima turekebishe hilo kwanza kabla ya yote.

Utakubaliana na mimi kuwa bila uongozi imara Taifa linakosa muelekeo; ndio maana naunga mkono haya matawi kuja huku ughaibuni sababu huku wanaoweza kudangwanywa ni wachache mno (so I hope). Cha kusikitisha ni kuwa Watanzania badala ya Kumkoma Nyani Gilani wao wanaleta majungu na fitina.

CCM leo ipo madarakani na itaendelea kuwepo madarakani mpaka pale Watanzania watapoamua kuwa Serious. Wajenge hoja, sio fitina, majungu na matusi. CCM wamekuja na Tawi, wengine nao waje na njia mbadala ya kupandana na haya matawi lakini fitina na tuhuma za vijiweni hazifiki popote.

Hayo ndio maoni yangu mkuu.
 
Speech Ndefu imejaa sifa kwa CCM instead of critising, humbling down, accepting mistakes and showing us the new ways to solve these problems (realistically)..umegusia swala la ufisadi kwa mbali kama kikwete vile...umeacha tuu kusema vijana tuunde tume ya kuhakikisha huu ufisadi kama ni kweli..campaign za kukanda upinzani were for 1995, 2005..saizi kila mtu anajua CCM chafu!!Mayb u can fool those kids in India of which 80% are on govt scholarships so they knw wer their loyalites lie....uchafu wa CCM umetapakaaa..tumechoka hadithi..hata waandishi wa magazeti ya rostam are doing a better job kusaficha chama kuliko nyie vijana wasomi mnaokula hela zetu za kodi India!!

ps: shein labda atakupa u assistant wake mkafungue mabucha na masoko wote!!

Mkuu Wangu Kapinga,

Nadhani unamaanisha watu wanaodhaminiwa na bodi.Kama ndivyo hilo ni halali yao kama watanzania na sidhani kama CCM wanaweza kuwaletea riwaya zao ndefu ndefu eti kwamba wanawasaidia maanake wakifanya hivyo itakua ni kukiuka sheria na ni ufisadi mwingine.

Suala la kutumia neno 'those kids in India' ni dharau kwa watanzania wasio na chama na wale ambao wana mawazo kinzani na CCM.Leo hii hapa tuna mjadala mkali kuhusiana na haya matawi.Mimi sipingi suala la matawi kufunguliwa huku na ndio maana tumeamua kufungua ya opposition ili tupambane nao kwa hoja na hii ni habari mbaya kwa Chama tawala na wale wote wanaopenda kujipendekeza kwa chama kilichoshindwa kubeba dhamana waliyopewa na watanzania
 
Mkuu nakuelewa; Baba wa Taifa alisema ili tuendelee tunahitaji Arthi, Watu, Siasa Safi na Uongozi Bora. Hayo mambo ni LAZIMA yabalance ndio tutaendelea. Sasa Watu tunao, Arthi tunayo; Siasa yetu sio safi kwa sababu inazalisha Viongozi Wabovu. Sasa ni lazima turekebishe hilo kwanza kabla ya yote.

Utakubaliana na mimi kuwa bila uongozi imara Taifa linakosa muelekeo; ndio maana naunga mkono haya matawi kuja huku ughaibuni sababu huku wanaoweza kudangwanywa ni wachache mno (so I hope). Cha kusikitisha ni kuwa Watanzania badala ya Kumkoma Nyani Gilani wao wanaleta majungu na fitina.

CCM leo ipo madarakani na itaendelea kuwepo madarakani mpaka pale Watanzania watapoamua kuwa Serious. Wajenge hoja, sio fitina, majungu na matusi. CCM wamekuja na Tawi, wengine nao waje na njia mbadala ya kupandana na haya matawi lakini fitina na tuhuma za vijiweni hazifiki popote.

Hayo ndio maoni yangu mkuu.

Kwi kwi kwi Matawi ya CCM kuja Ulaya kutasaidia kupata viongozi bora? Are you dreaming?

Jumuia kama JF, Tanzanet na zingine zitasaidia kupata viongozi safi lakini sio hayo matawi ya CCM ambako ndiko wahalifu wanakojificha na kutaka kupata nafasi ya kushikana mikono na viongozi wa kitaifa.
 
Sio kila mtu anaweza kuja hapa forum, Tanzanet na kwingineko kutoa michango.

Wao ni wanasiasa, majukwaa yao sio humu ni kule mitaani na majukwaani kuomba kura na kuahidi maendeleo kwa kila Mtanzania.

Nashindwa kuelewa mkuu kwa nini hutaki kuthamini na kuheshimu fani za watu wengine?
 
Back
Top Bottom