Tawi la India nadhani ni kampeni za Nape katika kuja kukamata madaraka ya UVCCM
Mie sioni kosa kwa watu kujiunga na CCM ila suala la kuwa na matawi huko nje ni njia ya ulaji tu!
tuipige vita tabia hii
Naona ni kweli mwafrika wa kike hawa watu wanataka tusikilize Radio Uhuru na RTD pekee watupe propaganda zao. Bora hizi radio zetu uchwara lakini zinawafikia wengi katika nchi mbalimbali duniani kwa sababu tunajaribu kwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia kuliko wao hata tovuti ya Ikulu inawshinda kutengeneza.
Sio kila mtu anaweza kuja hapa forum, Tanzanet na kwingineko kutoa michango.
Wao ni wanasiasa, majukwaa yao sio humu ni kule mitaani na majukwaani kuomba kura na kuahidi maendeleo kwa kila Mtanzania.
Nashindwa kuelewa mkuu kwa nini hutaki kuthamini na kuheshimu fani za watu wengine?
Ndugu yangu Gembe na wengine wote wanaodai ni ULAJI hebu tuelezeni kwa uwazi na mifano ulaji gani huu/huo???
Swala la Nape kwamba wadai ni kampeni kutaka UVCCM,nani kati ya walio India ni mpiga kura kwenye mkutano wa UVCCM na je wengine nchi zingine wanataka UV gani?? Tujenge hoja sio vioja...
Wakuu,heshima kwenu.......
Maneno mengi hapa kama vile twajifurahisha tu, mtu mmoja aliwahi kusema...hasira hata iwe kali vipi,haiwezi kuivisha chakula...maneno haya hata kama makali vipi hayawezi kuwazuiya CCM kufungua matawi nje..na ukiona asiyekutaka analalamika kwa wewe kufanya jambo ujue hilo jema kwako na umemshika pabaya mbaya wako....KWANINI KUANDIKIA MATE NA WINO UPO?BEN NA WENZAKO FUNGUENI MATAWI INDIA HATA CHINI YA MWAMVULI WA MUUNGANIKO WA VYAMA VITANO MNAVYOSHIRIKIANA..NA WENGINE KOTE WALIPO KAMA MNAWEZA FUNGUENI MTOE SERA MBADALA BADALA YA KULALAMIKA TU HAPA JF...
Wacha ninywe maji,ntaleta stori ya mbweha wa tano waliofungwa mikia yao pamoja ukawashwa moto mikiani wakaambiwa kimbieni.....mhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!
Yebo Yebo,
Unataka niamini utapeli na misheni mjini? Utajipima uongozi kwa wanachama 20? Si afadhali hata Tanzanet au TA vyombo ambavyo japo vina wanachama wengi?
Nimekaa Nje miaka mingi na Watanzania tulikuwa tunaongoza kwa mshikamano lakini sasa yanaanza mambo ya vyama, tutaishia kuwa kama Wakenya tu. Huyu CCM, yule CUF nk.
Hakuna anayemkataza mtu kuwa mwanachama wa chama lakini kuanza kufungua matawi nje ni ulaji tu ambao kwa mtu yeyote mwenye lengo la kusaidia jamii hawezi kuhangaika nayo.
Kama sio kulegalega kwa hiyo TA pengine leo kusingekuwa na CCM London....
Sitaki kukushawishi; ila naona unahitaji kuhudhuria hiyo mikutano ya CCM London ujionee mwenyewe idadi ya wanachama walionao. Sina la zaidi mkuu
Yebo Yebo,
Unataka niamini utapeli na misheni mjini? Utajipima uongozi kwa wanachama 20? Si afadhali hata Tanzanet au TA vyombo ambavyo japo vina wanachama wengi?
Nimekaa Nje miaka mingi na Watanzania tulikuwa tunaongoza kwa mshikamano
lakini sasa yanaanza mambo ya vyama, tutaishia kuwa kama Wakenya tu. Huyu CCM, yule CUF nk.
Hakuna anayemkataza mtu kuwa mwanachama wa chama lakini kuanza kufungua matawi nje ni ulaji tu ambao kwa mtu yeyote mwenye lengo la kusaidia jamii hawezi kuhangaika nayo.
Kwa maneno haya nakubaliana nawe kabisa .CCM kuweka matawi nje and then the same people wanakuwa viongozi wa Umoja wa Watanzania na vingozi wa CCM inaleta mgawanyiko na tunakuwa Taifa la watu walio changanyikiwa .JK anaenda London watu wanamuona anaenda ki CCM na watanzania wengine wanakaa mbali .Balozi anapo amua kufanya kazi za CCM openly sijui anataka wasio na vyama waende wapi .Mwalimu angaliyafanya haya Tanzania leo tusingalikuwa hapa JF kwa umoja huu , bali tungalikuwa kama Kenya .CCM wanatugawa nasi tuna shangilia jamani amkeni .Ukiwa kiongozi wa CCM basi jiondoe uongozi kwenye umoja wa Watanzania .
Hili ndio nimekuwa nalisema wakati wote kuhusiana na hawa wapambe wa CCM wanapoamua kuendelea kuanzisha haya mashina yao.Inajulikana kabisa ni haki yao kuwa wanachama wa chama chochote na hakuna anayepinga kuhusiana na hili lakini suala linalogomba hapa ni Judgement na nia yao ya kuanzisha haya matawi. Ina maana hawa watu hawaelewi uchafu wote unaofanywa na CCM mpaka wao kuamua kuvutiwa na kuzidi kufungua matawi huku ughaibuni. Sijawasikia hata siku moja wakitoa matamko ya kulaani ufisadi unaofanywa na wananchama wenzao kwa sababu siku zote kazi yao kubwa ni kukenua midomo na kupiga vigelegele na kushangilia kidumu chama cha Majambazi bila ya kuhoji muelekeo wa chama au matendo ya viongozi wengi wa juu wa CCM. Unajua wengi tunategemea watu ambao wameenda shule na kupata exposure wawe hawaangalii au kufanya maamuzi ya juu juu bila ya kutafakari kwa kina.Yebo Yebo,
Unataka niamini utapeli na misheni mjini? Utajipima uongozi kwa wanachama 20? Si afadhali hata Tanzanet au TA vyombo ambavyo japo vina wanachama wengi?
Nimekaa Nje miaka mingi na Watanzania tulikuwa tunaongoza kwa mshikamano
lakini sasa yanaanza mambo ya vyama, tutaishia kuwa kama Wakenya tu. Huyu CCM, yule CUF nk.
Hakuna anayemkataza mtu kuwa mwanachama wa chama lakini kuanza kufungua matawi nje ni ulaji tu ambao kwa mtu yeyote mwenye lengo la kusaidia jamii hawezi kuhangaika nayo.
Je haya matawi yanayofunguliwa ughaibuni yana malengo gani? Ni jinsi gani wanachama wake wanaweza kushiriki katika siasa nyumbani?.
Kwa maoni yangu naona kwamba kuanza kuwepo kwa matawi ya vyama vya kisiasa ughaibuni kutaanza kuleta mgawanyiko kwa Watanzania waishio huku. Hata siku moja sijawahi kusikia au kuona kama kuna matawi ya Republicams, Democrats, Labour, Conservatives, CDU au Forza Italia katika nchi zingine! Au huu ni mtindo mpya wa siasa za kimataifa ambao unahamishia siasa za ndani ya nchi, kwenda nchi zingine? Ikumbukwe kuwa, nauliza tu.
Lunyungu,
Unalolisema "nadhani" ndilo lililokuwa nia ya wajanja wachache wakati Tawi la London linaanzishwa lakini; ila kwa sasa ninavyojua mimi hakuna mfanyabiashara anayefadhili chama tawi la London kwa hela nyingi kuliko wanachama. Nimedadisi kwa karibu nikagundua kuwa asilimia kubwa Tawi linaendeshwa na wanachama wa kawaida kama mimi na wewe..sasa hawa ndugu zetu wana nia gani; time will tell.
Mkuu Heshima yako,
Unatoa tuhuma hewani bila kujua kuwa huku tupo ughaibuni. Hapa una hoja unauliza kama ilivyo. Unaposema rent ya ofisi ya Shina North London inalipwa na chama; una ushahidi wowote? Maneno yako sio tu kwamba yanalenga kuleta mfarakano kati ya mwenye Cafe na Viongozi wa shina bali pia inaonyesha ni jinsi gani usivyotaka kupata data za uhakika. Hiyo ofisi sana sana itwakuwa inatumiwa kwa sababu mwenye Cafe amejitolea itumiwe na Chama. Kama nilivyosema hapo awali chama (UK) kinaendeshwa na wanachama, mwenye senti za kutoa anatoa, mwenye petroli za kwenda kufungua mashina anatoa, mwenye printer ya rangi ya kuprint nyaraka za chama anatoa n.k
Hakuna mjomba anayefadhili chama kama ambavyo mnataka wanabodi hapa waamini; na iwapo atatokea na kuonekana ana malengo yake binafsi basi mimi kama mwanabodi hapa nitakuwa na wajibu wa kuwaambieni ukweli; kwa sasa fungueni akili wekeni maswali na hoja zenye mashiko za kwa nini haya matawi yawepo huku ughaibuni.
Mkuu hebu niambie kosa lao hasa nini? kama nikutengeneza cv kwa njia halali za kufanya kazi ya chama chao na ikaonekana na kutambuliwa kosa lao nini???Nikama mtu anasoma apate labda degree ili agombee urais kama ndio kigezo kilichowekwa kosa lake nini hasa??Kama kuna mtu anadhani hana sifa ni bora kwenda kushindana kwa wananchi kuwaeleza kwamba huyu hatoshi badala ya kumsema anapojitafutia cv yake.Kama huelewi, wenzako wanachotengeneza ni CV. Ni sawa na wale wenye Ph.D fake. Hata wao wanajua ni fake ila wanachotaka ni hiyo Dr. kwenye CV.
Ukiandika ulikuwa Mwenyekiti wa CCM London, kwa mtu wa kule Musoma anaweza kuamini wewe ni mkali kweli kweli, kumbe hakuna kitu na ulikuwa na wanachama 10.
Soma CV ya Nape wakati anagombea UVCCM labda ndio utaelewa maana yake.
Mwenye CAFE Anajiweza kama sikosei hadi mwaka 2003 alikuwa na nyumba tatu UK
Moja ipo karibu sana na uwanja wa manchester city
Ila ni bahili sana
Lakini pia wakuu, ngoja tujaribu kuchambua sababu za msingi zilizowafanya CCM warudishe utaratibu huu.Ikumbukwe utaratibu huu kauanzisha Julius na si kama wanavyodai waungwana hapa eti wakati wa Julius haukuwepo,huo ni uongo...tena wakati huo ulikuwa mkubwa na mgumu kuliko sasa kwani moja ya kazi za balozi zetu nje ilikuwa ni kuratibu mashina na matawi haya ya CCM nje waliko,so walichofanya CCM kwasasa ni kuyaanzisha upya lakini kwa stail ya kuyatoa ofisi za ubalozi na kuya weka kwa wanachama wenyewe...ni kama ilivyo dini,hivi leo waislamu au wakristo au wapagani wakikutana na kuunda umoja wao wa mahali flani kosa lao nini?? njia bora ni wale wa dini nyingine waanzishe yao nao,badala ya kupondana.Mbona wenye Umoja wa dini flani hatusemi kama wanawagawa watz nje???