Vyama 7 vilivyojitoa uchaguzi wa mitaa vyatoa tamko la pamoja

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Nimesikia viongozi wa vyama vya upinzani wakiwaambia watu watege masikio ili wasikie maamuzi yatakayotolewa na viongozi wao kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani serikali ya CCM wamekuwa wakijiamulia kufanya wanayotaka.

Sasa hapa si ajabu ukasikia viongozi hao wamekamatwa kwa kutoa maneno ya uchochezi.

------
TAMKO LA VYAMA VYA ACT-WAZALENDO,CHAMA CHA KIJAMII (CCK), CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA),CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA (CHAUMMA),NCCR-MAGEUZI,NLD NA UPDP-KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, 2019.

UTANGULIZI

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulitangazwa kufanyika tarehe 24.11.2019 na baada ya tangazo hilo Vyama vyetu vilishiriki kwenye michakato mbalimbali ikiwemo kuandikisha wapiga kura, kuteua wagombea na wagombea kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali .

Ilipofikia zoezi lakuchukua fomu ndipo maeneo mengi ya nchi tukashuhudia wagombea wa vyama vya upinzani wakinyimwa fomu za kugombea kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kufungaofisi na kuondoka na au kuwaambia kuwa wanasubiri kupatiwa fomu kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi.

Kwenye baadhi ya maeneo ambako wagombea walifanikiwa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali ilipofika siku moja kabla yasiku ya uteuzi tulianza kushuhudia wagombea wetu wakienguliwa bila kufuatwakwa Kanuni na taratibu za uchaguzi, wengine fomu zao kughushiwa kwa kuongezewa herufi mbele ya majina yao waliyokuwa wamejaza kwenye fomu au tarakimu kwenye kipengele cha tarehe za kuzaliwa nk

Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walitumia sababu mbalimbali ambazo walizisababisha wao kwa kuharibu fomu za wagombea kama kigezo cha kuwaengua bila hata kusubiri wagombea hao kuwekewa mapingamizi na wagombea wa vyama vingine jambo lililopelekea zaidi ya asilimia 95% ya wagombea wetu wote waliofanikiwa kurejesha fomu kuenguliwa kugombea nchi nzima .

Baada ya hali hiyo vyama vya Chadema,ACT-Wazalendo, Chaumma,CCK,NCCR-Mageuzi,CUF, UPDP na NLD vilitoa matamko ya kujitoa kwenye uchaguzi huo kutokana na Ukiukwaji Mkubwa wa Kanuni na Sheria zinazosimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Baada ya Vyama tajwa kujitoa kushiriki uchaguzi huo, serikali kwa upande wake ilitoa matamko mbalimbali ambayo yalikuwa yakitofautiana na kujichanganya pamoja na ukweli kuwa yalikuwa yakitolewa na mtu mmoja ambaye ni Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleman Jaffo.

Baada ya wagombea wa vyama tajwa kujitoa kwenye uchaguzi huo wagombea wake waliwajulisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuhusu kujitoa kwenye uchaguzi na kwa ngazi ya Taifa baadhi ya Vyama vilimjulisha waziri wa TAMISEMI kwa barua
kuhusu kujitoa kwao katika kuendelea na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019.

Baada ya vyama kujitoa ilisababisha wagombea ambao watasalia katika uchaguzi huu kuwa wa chama kimoja pekee cha CCM nchi nzima .


MAELEKEZO YA KANUNI ZA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA NGAZI YA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA ZA MWAKA 2019.

  • Kanuni ya 18 na 19(1)imeweka utaratibu kuwa endapo siku ya uteuzi kutakuwa na mgombea mmoja aliyejitokeza katika kuomba nafasi ya uenyekiti na mwombaji huyo akateuliwa , msimamizi msaidizi wa uchaguzi atamtangaza mwombaji huyo kuwa ni mshindi wa nafasi aliyoomba kugombea kwa kupita bila kupingwa
  • Kanuni ya 19(2)inaeleza hivyo hivyo kwa wajumbe wa serikali ya mtaa au kijiji kuwa
  • watatangazwa kupita bila kupingwa endapo hakutakuwa na wagombea wa vyama vingine .
  • Kanuni ya 20(1) imeweka utaratibu wa wagombea kujitoa baada ya uteuzi kufanyika . Nanukuu “Endapo ,baada ya uteuzi kufanyika ,mgombea aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Mtaa atajitoa,Msimamizi msaidizi wa uchaguzi atatengua uteuzi wa mgombea huyo…..’
  • Kanuni ya 20(2) inaweka wazi kuwa, ‘Endapo ,baada ya uteuzi kufanyika ,mgombea aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Mtaa atajitoa na kubaki mgombea mmoja wa nafasi hiyo,Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi atamtangaza mgombea aliyebaki kuwa mshindi wa nafasi iliyoombwa kwa kupita bila kupingwa’
  • Kanuni ya 20(3) imeweka utaratibu kama huo kwa wagombea wa nafasi za ujumbe wa serikali za Mitaa na Vijiji wa kupita bila kupingwa.
  • Kanuni ya 27(2) imeweka utaratibu wa kuvitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo kuwasilisha ratiba za kampeni kwa msimamizi wa uchaguzi siku saba (7) kabla ya siku ya kampeni .Baada ya vyama vyetu kujitoa hatukuwasilisha ratiba za kampeni na hivyo hatupo kwenye ratiba hiyo.

MSIMAMO WA VYAMA VYETU

  • Hatutashiriki kwa vyovyote vile kwenye Kampeni na uchaguzi huu unaoenda kinyume na kanuni za uchaguzi, na hivyo tunawataka wanachama , wafuasi na wapenda amani wote katika taifa letu kutokushiriki katika kampeni na kinachoitwa uchaguzi .
  • Uchaguzi huu ufutwe na mchakato wake uanze upya kwa mustakabali wa amani ya taifa letu.
  • Tunauomba Umma wa watanzania ujiandae kwa maelekezo yoyote yatakayotolewa baada ya mashauriano yanayoendelea miongoni mwa Vyama na makundi mengine ya kijamii .
  • Tunataka mchakato wa kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia chaguzi zote nchini uanze mara moja.
  • Tumetambua kauli na wito uliotolewa na baadhi ya viongozi wastaafu na viongozi wa dini nchini , hivyo tunawaomba wachukue hatua za kuingilia kati mapema kuinusuru amani ya Taifa letu.
Tamko hili limetolewa leo tarehe 16, Novemba 2019.
 
Nimesikia viongozi wa vyama vya upinzani wakiwaambia watu watege masikio ili wasikie maamuzi yatakayotolewa na viongozi wao kuusu mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani serikali ya ccm wamekuwa wakijiamulia kufanya wanayotaka,
Sasa hapa si ajabu ukasikia viongozi hao wamekamatwa kwa kutoa maneno ya uchochezi.
Huu nao ni uchochezo maama umeamua kuilisha serkali maneno
.
State agent
 
Nimesikia viongozi wa vyama vya upinzani wakiwaambia watu watege masikio ili wasikie maamuzi yatakayotolewa na viongozi wao kuusu mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani serikali ya ccm wamekuwa wakijiamulia kufanya wanayotaka,
Sasa hapa si ajabu ukasikia viongozi hao wamekamatwa kwa kutoa maneno ya uchochezi.
Hebu kunywa maji kwanza tulia, kidogo kisha andika tena, mbona una paparapupa wakimbilia wapi kwani?

Tuambie tamko linasemaje, kisha tuambie tamko linasemaje na kwanini watakamatwa kwa uchochezi?
 
Hebu kunywa maji kwanza tulia, kidogo kisha andika tena, mbona una paparapupa wakimbilia wapi kwani?

Tuambie tamko linasemaje, kisha tuambie tamko linasemaje na kwanini watakamatwa kwa uchochezi?

Subiri tu, wakati utaeleza vizuri
 
Kuanzia sasa viongozi waliotoa tamko wajiandae kusakwa na siro.kwa maoni yangu wasijirahisishe kwenda kwenda polis, polis kwa sasa ni tawi rasmi la ccm.
 
Naiona TLP ya Mrema ikirudi kwenye makali yake
Nikimuangalia Mrema nakumbuka usemi wa biblia kuhusu "kushusha mvi kaburini na aibu".
Yaani unakuwa mzee unakosa/unapoteza heshima yako hadi unashushwa kaburini kwa fedheha itokanayo na kukosa busara.
 
Zama zile kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 watu walikuwa wanafuatilia sana haya matamko ya vyama vya upinzani ila sasa hivi watu wanafuatilia sana matamko ya serikali. Poor upinzani wa Tanzania hawajui kusoma alama za nyakati, na kwa sababu vyama vyenyewe vilundwa bila kuwa na sera maalum wamejikuta wakikosa kwa kuegemea baada ya plan zao kwenda mlama.

 
Nimesikia viongozi wa vyama vya upinzani wakiwaambia watu watege masikio ili wasikie maamuzi yatakayotolewa na viongozi wao kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani serikali ya CCM wamekuwa wakijiamulia kufanya wanayotaka.

Sasa hapa si ajabu ukasikia viongozi hao wamekamatwa kwa kutoa maneno ya

Natabiri,vyama vyote vilivyojitoa kwenye uchaguzi,viongozi wake watakuwa sell kabla ya tarehe yenyewe kufika
 
Naiona TLP ya Mrema ikirudi kwenye makali yake

Tafuteni vyama vyote villivyojifia mvipe viti vya kutosha kama nyie ccm mnavyojipa, lakini hata mfanyaje wananchi sasa hivi tunajitambua, hatuna muda wa kushiriki ushenzi wowote. Na viongozi wowote watakaopata madaraka kupitia zoezi hili la kihuni wasitegemee kupata ushirikiano wowote wa maana kutoka kwa umma.
 
Dar es Salaam. Siku moja kabla ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanza, vyama saba vilivyojitoa katika mchakato wa uchaguzi huo vimetoa tamko vikiwataka Watanzania kujiandaa kwa maelekezo mengine yatakayotolewa baada ya kumalizia mashauriano.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Novemba 16 baada vyama vya CHADEMA, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, CCK, NCCR Mageuzi, UPDP na NLD kutoa msimamo wao.

Akiongea kwa niaba ya vyama hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Profesa Abdallah Safari amesema vyama hivyo vilishatoa matamko ya kujitoa kwenye uchaguzi huo kutokana na ukiukwaji wa kampuni na sheria.

Amesema baada ya vyama hivyo kujitoa kushiriki uchaguzi, serikali kwa upande wake ilitoa matamko mbalimbali yaliyokuwa yakitofautiana na kuchanganya, licha ya kuwa yalikuwa yakitolewa na mtu mmoja ambaye ni Waziri wa TAMISEMI.

"Baada ya wagombea wa vyama hivyo kujitoa kwenye uchaguzi huo, waliwajulisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuhusu kujitoa na kwa ngazi ya Taifa baadhi ya vyama vilimjulisha waziri wa TAMISEMA kwa barua,” amesema Profesa Safari.

Baada ya kushauriana vyama hivyo vimeazimia kwa pamoja havitashiriki kwa vyovyote “kwenye kampeni na uchaguzi unaoenda kinyume na kanuni za uchaguzi” na vimewataka wanachama na wafuasi kutoshiriki.

Aidha vyama hivyo vimetoa wito “uchaguzi huo ufutwe na mchakato wake uanze upya kwa mustakabali wa amani ya Taifa.”

"Tunatoa wito kwa umma na Watanzania wajiandae kwa maelekezo yoyote yatakayotolewa baada ya mashauriano yanayoendelea miongoni mwa vyama na makundi mengine ya jamii," amesisitiza Profesa Safari.

Maazimio mengine ni pamoja na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi zote nchini.

Amesema vyama hivyo vimetambua kauli na wito uliotolewa na viongozi wastaafu na viongozi wa dini nchini na kuwaomba kuchukua hatua za kuingilia kati mapema ili kunusuru amani ya Taifa.

Akizungumza katika mkutano huo, Kiongozi wa ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Watanzania wanatakiwa kuwa tayari na kutega masikio wakati vyama hivyo na makundi mbalimbali yakiendelea na mashauriano.

"Hatutakubali kuendelea kupingwa kwa miaka minne mfululizo. Tunawataka Watanzania kuendelea kutega masikio wakati hatua zikiendelea ikiwemo mashauriano na makundi mbalimbali," amesema Zitto.

Mwenyekiti wa Chaumma, Hashimu Rungwe ametumia mkutano huo kufafanua taarifa zinazoelezwa kuwa vyama vingine vilivyojitoa havikuweka wagombea, akisema si za kweli na akashauri zipuuzwe.

"Mimi niliweka wagombea 25O ambao walitolewa wote wanaosema sikuweka wagombea muwapuze," alisema Rungwe

CHANZO: Mwananchi
 
naona jafo akichungulia huu uzi kwa jicho moja..

huku akimsihi Lipumba nae asijitoe

Naona hapa kuna viongozi wengine wenye nafasi kubwa serikalini wanatumiwa vibaya na mabeberu ili kuchafua sifa ya Dr Rais Magufuli!! some leaders in sensitive positions are incognito being used by armyworms who are not happy with the current Aggressive efforts of revamping the Tanzanian economy! In certain vernacular it is literally translated as “THEY ARE ACTING LIKE HEADLESS GRASSHOPPERS”!!Yetu macho! The simplest advice is for the President to get rid of such headless grasshoppers!
 
Back
Top Bottom