Vurugu zazuka Kanisani la KKKT Dayosisi ya Konde Mbeya, Ibada yavunjika, Polisi wakamata viongozi

KKKT watumie busara kumsimamisha huyo mchungaji kwa muda (iwe ndo imetoka hiyooooooo) ili kupoza waumini
 
Wakati mgogoro ukizidi kufukuta kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Aprili 17, 2022 baadhi ya waumini wa usharika wa Mbalizi wamemzuia mchungaji wao, Atupele Mlawa kuingia kanisani na kusababisha kuvunjika kwa ibada.

Kutokana na vurugu hizo, Jeshi la Polisi mkoani humo limefika kanisani hapo na kukamata baadhi ya viongozi wa kanisa hilo.

Vurugu hizo zimetokea leo Jumapili Aprili 17 wakati Wakristo kote duniani wakisherekea siku kuu ya Pasaka.

Baadhi ya waumini waliozungumza na Mwananchi kanisani hapo wamesema vurugu zilianza baada ya baadhi ya waumini kufunga milango kumzuia mchungaji Mlawa kutoingia ndani kuendesha ibada wakidai kutumia vibaya mali za kanisa hilo.

Taarifa zaidi zimesema waumini wanaompinga Mchungaji Mlawa, wanamtaka Mchungaji Lusajo Sanga aliyechaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi uliofanyika Machi 22 chini ya Kiongozi wa Kanisa hilo nchini, Dk Fredrick Shoo.

Hata hivyo, waumini wengine walipinga kitendo cha kufunga milango ya kanisa wakitaka mchungaji Mlawa aendelee na kazi yake na ndipo vurugu zilipozuka.

Akizunguka katika eneo la kanisa hilo, mmoja wa waumini, Jane Msingwa amesema baadhi ya waumini walisimama mlangoni wakipinga mchungaji Mlawa kuingia kanisani.

"Leo kilichotokea ni sintofahamu, mchungaji alikuja kuendesha ibada lakini watu wakakaa mlangoni hadi msaidizi wake akaingilia kati ila hali ilikuwa mbaya," amesema Jane.

Kwa upande wake Godfrey Mwasuku amesema wameamua kukaa mlangoni hapo kutokana na kukaidi kwa mchungaji huyo maelekezo kwani alishaandikiwa barua ya kuondoka kanisani hapo.

"Hiki kilichotokea leo ni kutokana na uongozi tulionao, ilipangwa ratiba ya ibada na huyu mchungaji Mlawa tulishamuandikia barua kuondoka, imeshangaza tunamuona amekuja ndio maana tukasema hatumtambui," amesema Mwasuku.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa vurugu aliwatuma askari wake kwenda kumaliza mzozo.

"Msimamo wetu Jeshi la Polisi tumewaambia hao viongozi tuliowakamata nini cha kufanya, waende mahakamani wamalize mgogoro ili mwenye haki apewe, tusichotaka kusikia ni uvunjifu wa amani kwa raia sehemu yoyote," amesema Matei.

Viongozi wanaotajwa kukamatwa na Polisi ni pamoja na Askofu wa dayosisi ya Mbeya Magharibi, Judith Kajela, Mchungaji Atupele Mlawa na Mchungaji Lusajo Sanga.

Chanzo: Mwananchi
KKKT watajuta kukabidhi mamlaka ya Kanisa kwa mangi.

Na baado.

Hapo sababu Ni MASLAHI/MATEMA BEACH
 
Kwahiyo ukiacha ule mgogoro wa kugombea kuamishwa kwa makao makuu ya jimbo huu ni mgogoro mwingine? Tena kwenye jimbo lile lile?
 
Hata kama walikuwa na tatizo naye. Kumtakaza mchungaji kwenda kuongoza ibada siyo jambo jema na zuri. Wajitathimi
Hiyo ndiyo nzuri mkuu, wewe huwajui viongozi wa kidini.

Bahati mbaya hao ni sehemu ndogo sana ya ubadhirifu unaofanywa na hao sijui makasisi, maaskofu, wachungaji nk, yaani kuna madudu huko kwenye makanisa ayayayayaaa.
 
Mkiambiwa Roman Catholic ni taasisi imara kibinadamu na kiroho msiwe mnakuwa wabishi. Hiyo ni laana ya kuasi kanisa la Kristu, na hii ni kwa all Protestants (they protested)
Umetoka nje ya mada bwasheee ....Tukiambiwa na nani??
 
Hata kama walikuwa na tatizo naye. Kumtakaza mchungaji kwenda kuongoza ibada siyo jambo jema na zuri. Wajitathimi
Kwanini akaidi? Wapi ulisikia Yesu anajipendekeza kwa wasiomtaka kwamba walimfukuza akalazimisha kukaa nao.

Ukikaidi utapigwa tu
 
Wakati mgogoro ukizidi kufukuta kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Aprili 17, 2022 baadhi ya waumini wa usharika wa Mbalizi wamemzuia mchungaji wao, Atupele Mlawa kuingia kanisani na kusababisha kuvunjika kwa ibada.

Kutokana na vurugu hizo, Jeshi la Polisi mkoani humo limefika kanisani hapo na kukamata baadhi ya viongozi wa kanisa hilo.

Vurugu hizo zimetokea leo Jumapili Aprili 17 wakati Wakristo kote duniani wakisherekea siku kuu ya Pasaka.

Baadhi ya waumini waliozungumza na Mwananchi kanisani hapo wamesema vurugu zilianza baada ya baadhi ya waumini kufunga milango kumzuia mchungaji Mlawa kutoingia ndani kuendesha ibada wakidai kutumia vibaya mali za kanisa hilo.

Taarifa zaidi zimesema waumini wanaompinga Mchungaji Mlawa, wanamtaka Mchungaji Lusajo Sanga aliyechaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi uliofanyika Machi 22 chini ya Kiongozi wa Kanisa hilo nchini, Dk Fredrick Shoo.

Hata hivyo, waumini wengine walipinga kitendo cha kufunga milango ya kanisa wakitaka mchungaji Mlawa aendelee na kazi yake na ndipo vurugu zilipozuka.

Akizunguka katika eneo la kanisa hilo, mmoja wa waumini, Jane Msingwa amesema baadhi ya waumini walisimama mlangoni wakipinga mchungaji Mlawa kuingia kanisani.

"Leo kilichotokea ni sintofahamu, mchungaji alikuja kuendesha ibada lakini watu wakakaa mlangoni hadi msaidizi wake akaingilia kati ila hali ilikuwa mbaya," amesema Jane.

Kwa upande wake Godfrey Mwasuku amesema wameamua kukaa mlangoni hapo kutokana na kukaidi kwa mchungaji huyo maelekezo kwani alishaandikiwa barua ya kuondoka kanisani hapo.

"Hiki kilichotokea leo ni kutokana na uongozi tulionao, ilipangwa ratiba ya ibada na huyu mchungaji Mlawa tulishamuandikia barua kuondoka, imeshangaza tunamuona amekuja ndio maana tukasema hatumtambui," amesema Mwasuku.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa vurugu aliwatuma askari wake kwenda kumaliza mzozo.

"Msimamo wetu Jeshi la Polisi tumewaambia hao viongozi tuliowakamata nini cha kufanya, waende mahakamani wamalize mgogoro ili mwenye haki apewe, tusichotaka kusikia ni uvunjifu wa amani kwa raia sehemu yoyote," amesema Matei.

Viongozi wanaotajwa kukamatwa na Polisi ni pamoja na Askofu wa dayosisi ya Mbeya Magharibi, Judith Kajela, Mchungaji Atupele Mlawa na Mchungaji Lusajo Sanga.

Chanzo: Mwananchi
Vitu vya aibu sana!! Sidhani kama wapo kumtumikia Mungu kweli! Wapo kumtumikia matumbo yao! Na hayo ndiyo watakayovuna!!
 
Mkiambiwa Roman Catholic ni taasisi imara kibinadamu na kiroho msiwe mnakuwa wabishi. Hiyo ni laana ya kuasi kanisa la Kristu, na hii ni kwa all Protestants (they protested)
Ukikuta katika jamii hakuna migogoro ni either watendwa wamekubali kuwa kondoo au vinginevyo.
Hivi unajua mbinguni penyewe Mungu alikua na mgogoro na shetani?!
So upepo kutokuuona kwa macho namna unavyovuma haina maana upepo hauvumi
Jitahidi kuwa mdadisi.
 
Huenda ameshakula baadhi ya kondoo hapo, si unajua tena akina Atuganile walivyo jazia lazima tu pastor kawala
Sasa asipokula kondoo unata ale nini nyasi au? Kondoo wanakula majani kondoo wakinona mchungaji anakula kondoo hii ndio cycle ilivyo.
 
Wakati mgogoro ukizidi kufukuta kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Aprili 17, 2022 baadhi ya waumini wa usharika wa Mbalizi wamemzuia mchungaji wao, Atupele Mlawa kuingia kanisani na kusababisha kuvunjika kwa ibada.

Kutokana na vurugu hizo, Jeshi la Polisi mkoani humo limefika kanisani hapo na kukamata baadhi ya viongozi wa kanisa hilo.

Vurugu hizo zimetokea leo Jumapili Aprili 17 wakati Wakristo kote duniani wakisherekea siku kuu ya Pasaka.

Baadhi ya waumini waliozungumza na Mwananchi kanisani hapo wamesema vurugu zilianza baada ya baadhi ya waumini kufunga milango kumzuia mchungaji Mlawa kutoingia ndani kuendesha ibada wakidai kutumia vibaya mali za kanisa hilo.

Taarifa zaidi zimesema waumini wanaompinga Mchungaji Mlawa, wanamtaka Mchungaji Lusajo Sanga aliyechaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi uliofanyika Machi 22 chini ya Kiongozi wa Kanisa hilo nchini, Dk Fredrick Shoo.

Hata hivyo, waumini wengine walipinga kitendo cha kufunga milango ya kanisa wakitaka mchungaji Mlawa aendelee na kazi yake na ndipo vurugu zilipozuka.

Akizunguka katika eneo la kanisa hilo, mmoja wa waumini, Jane Msingwa amesema baadhi ya waumini walisimama mlangoni wakipinga mchungaji Mlawa kuingia kanisani.

"Leo kilichotokea ni sintofahamu, mchungaji alikuja kuendesha ibada lakini watu wakakaa mlangoni hadi msaidizi wake akaingilia kati ila hali ilikuwa mbaya," amesema Jane.

Kwa upande wake Godfrey Mwasuku amesema wameamua kukaa mlangoni hapo kutokana na kukaidi kwa mchungaji huyo maelekezo kwani alishaandikiwa barua ya kuondoka kanisani hapo.

"Hiki kilichotokea leo ni kutokana na uongozi tulionao, ilipangwa ratiba ya ibada na huyu mchungaji Mlawa tulishamuandikia barua kuondoka, imeshangaza tunamuona amekuja ndio maana tukasema hatumtambui," amesema Mwasuku.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa vurugu aliwatuma askari wake kwenda kumaliza mzozo.

"Msimamo wetu Jeshi la Polisi tumewaambia hao viongozi tuliowakamata nini cha kufanya, waende mahakamani wamalize mgogoro ili mwenye haki apewe, tusichotaka kusikia ni uvunjifu wa amani kwa raia sehemu yoyote," amesema Matei.

Viongozi wanaotajwa kukamatwa na Polisi ni pamoja na Askofu wa dayosisi ya Mbeya Magharibi, Judith Kajela, Mchungaji Atupele Mlawa na Mchungaji Lusajo Sanga.

Chanzo: Mwananchi
Makubwa
 
Wangewnda kukamata Askofu Shoo inavyoonekana ndiye chanzo
 
Naona jina Judith kajela kuwa ndo Baba Askofu mbeya magharibi, hili jina Judith ni mwanamke Sasa iweje ndo baba Askofu?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hii nguvu ya waumini wa KKKT tukiitumia kwa CCM mbona itakuwa raha Sana.
 
Back
Top Bottom