Hatimaye Dayosisi mpya ya Mlali yaanzishwa

mtotofisi

Member
Aug 24, 2020
12
19
Mgogoro uliodumu takribani miezi mitatu umesababisha waumini wa kanisa Anglikana kutoka dayosisi ya mpwapwa wa makanisa ya Mlali, iduo,chiwe, nghumbi, ihanda na moleti kupelekea kuanzishwa Leo tarehe 10 Desemba 2023 ikijulikana Dayosisi ya Mlali ikiongozwa na Askofu ELIBARIKI KUTTA

Kiini cha mgogoro huu ni Baada ya kifo cha ghafla cha aliyekuwa askofu wa dayosisi ya Mpwapwa aliyefia Tanga baada ya kuhudumu kwa siku sita tu,ukaitishwa uchaguzi mwingine ambao umeleta mgogoro wa muda mrefu tangu mwezi mei hadi leo hii.

Chanzo hasa cha mgogoro huo ni mmoja wa wagombea aitwaye KUTA kuondolewa kwenye uchaguzi akidaiwa hana vigezo.Kuta anaishi marekani hadi leo na amejipatia umaarufu mkubwa kwa kuwa alikuja na sera tofauti na za kanisa anglikana; kwamba, huduma zote za kikanisa zitafanyika bure,kuanzia ubatizo,kipaimara hadi ndoa,sadaka zote zitabaki makanisani badala ya kutumwa dayosisi.

Baadhi ya dinari na pareshi zilivutiwa na sera zake hadi kupelekea wasiwasi kwa viongozi wa dayosisi na kanisa anglikana kwa ujumla.

Kamati ya uchaguzi iliondoa jina lake tena wakati uchaguzi ukiwa umeshafanyika kwa madai kuwa Kuta hana vigezo,jambo mojawapo lililosemwa ni kuwa bwana Kuta anajihusisha na masuala ya mapenzi ya jinsia moja.Ikumbukwe kuwa Kuta anatokea maeneo ya kanda ya Mlali ambapo ndipo hasa kwenye mgogoro mkubwa,baada ya kuondolewa kwake zaidi ya makanisa 80 yaliyopo kanda hiyo ya Mlali yaliamua kujitoa dayosisi ya Mpwapwa.

Wachungaji,makatekesti na viongozi wengine walioonekana kuwa hawaungi mkono uamuzi wa kujitoa kwenye dayosisi hiyo walifukuzwa makanisani kwa madai kuwa ni wasaliti.Baadhi ya makanisa walibomoa vibao vya mawe ya msingi,na wengine waliandika mabago nje ya kanisa,"TUMEJITOA DAYOSISI YA MPWAPWA".Na wengine wakaenda mbali zaidi wakataka kuunda dhehebu jipya.

Baada ya viongozi wa dayosisi kupata taarifa hiyo walizidisha mgogoro kwa kuwataka wanaojitoa kwenye dayosisi hiyo wahame makanisani kwani majengo hayo ni mali ya dayosisi ya Mpwapwa.

Wachache,angalau kati watu 10-15 wa kila kanisa walioamua kubaki dayosisi ya Mpwapwa ndiyo wanaoruhusiwa kusalia ndani ya makanisa.Wengine ambao ni wengi zaidi wanatumiwa polisi kila jumapili ili kuwafukuza makanisani wkasalie huko wanakojua wao.Mgogoro huu umeshindwa kutatuliwa hadi leo hii hadi kupelekea waliojitoa kuwatishia maisha maisha wale waliobaki makanisani.

Mgogoro huu chanzo chake hasa ni ukabika,kwani wanaotaka kukitoa kwenye dayosisi ni wakaguru wanaolalamika kuwa maaskofu wote wanaovjaguliwa ni wagogo wakati wao kwao(wakaguru) huondolewa kwa kuwa hawana vigezo,hata wale waliobaki na msimamo kwenye makanisa asilimia kubwa ni wagogo,na wakaguru nao wanataka mwenzao ashike hicho kilichokaliwa na wagogo miaka yote.

Waliojitoa Mpwapwa wanataka wapewe dayosisi mpya ya MLALI,jambo ambalo ni gumu.Hivi karibuni wamekuwa wakifanya majdiliano kama wanaweza kuahamia kwa wakaguru wenzao Morogoro lakini pia wamegonga mwamba.

Sasa wameamua kuhamia kwenye majengo ya serikali kama vile magodaoni.

Lakini msimamo wao bado ule ule kuwa kwenye majengo yao wanayofukuzwa na polisi hawataki watu wakasali.

Mkuu wa wilaya ya Kongwa alienda kufanya mkutano na viongozi wa wanaojitoa,lakini mkutano huo haukuzaa matunda na badala yake viongozi wa wanaojitoa walienda kuswekwa rumande kwa takribani siku nne wakituhumiwa kuchochea vurugu.

Hivi karibuni makamu wa rais akiwa kwenye hafla ya kuapishwa kwa askofu mpya wa dayosisi ya mpwapwa,aliagiza uchunguzi ufanyike haraka na taarifa ifike ofisi ya waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom