Waliosimamishwa KKKT Hai "Wamwaga mboga" mchungaji achana barua ya maombi ya fedha

Jul 30, 2018
13
12
HAI .

VIONGOZI watatu wa kikundi cha Uamsho katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Hai mjini wanaotajwa kusimamishwa kwa madai ya kuvamia na kuvuruga kikao cha uongozi Usharika na Waimbaji wamejitokeza hadharani huku wakimtuhumu Mchungaji wa kanisa hilo ndio chanzo cha mgogoro.

Hili linakuja siku chache baada ya kuripotiwa uwepo wa mgogoro katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Hai mjini kufuatia kusimamishwa kwa baadhi ya Viongozi wa Vikundi vilivyopo chini ya idara za kanisa hilo tayari viongozi hao wamejitokeza hadaharani na kukiri kupkkea barua za kusimamishwa.

Viongozi hao Ndeakomfoo Shoo aliyekuwa Mwenyekiti wa Uamsho ,Mweka Hazina wa Faragha ya Hai mjini ,Clotilda Massawe na Katibu wa Uamsho Joseph Robert wametoa tuhuma nzito dhidi ya mchungaji huyo ikiwemo kuchana Barua ya maombi ya fedha kutoka kwenye mfuko wa kikindi hichjo kwa ajili ya kupaulia nyumba ya maombi.

“Kikundi cha uamsho kiliandika barua kwa Mtunza Hazina kwa ajili ya matumizi ya kupaua nyumba ya maombi ,Barua hiyo imekaa kwa mchungaji kuanzia Februari 23,2023 haijajibiwa chochote,ndipo tukaamua kuuliza sababu za kutokupitishwa, mchungaji aliichana barua hiyo kwa mikono yake na kutuambia twende kokote.” Alisema Ndeakomfoo Shoo Mwenyekiti wa kikundi cha faragha aliyesimamishwa .

Shoo alisema kanisa ni sehemu ya amani,utulivu na upendo ,vurugu kanisani haitakiwi kwani watu wakivurugana nyumbani huwenda kanisani kwa ajili ya upatanisho na anaepatanisha ni mchungaji huku akihoji kama mchungaji anakuwa sehemu ya kuvunja amani inakuwa changamoto sana kwa washarika .

“Kuna kusudio ambalo sio zuri kanisani kwamba viongozi wa faragha wanakusudia kufanya jambo zuri ambalo linaweza kufaa kwa leo na litabaki kanisani kwa vizazi vingi lakini kama mchungaji anakataa vitu vya maendeleo hii inawapa tabu na kuwaacha washarika na viongozi wa Hai Mjini na maswali mengi.”alisema Shoo.

Mtunza Hazina wa Faraghay a Hai mjini Clotilda Massawe alisema sababu ya kinachoendelea Usharika wa Hai mjini ni ripoti ya fedha iliyosomwa mwezi wa Saba na viongozi hao kuona kwamba fedha zao kiasi cha shilingi 4,349,300 hazipo kwenye ripoti hiyo.

“Nilipomuuliza Mchungaji kuhusu kutoonekana fedha hizo kwenye taarifa ,Mchungaji alijibu “Ukichimba Udongo Utakuta Udongo" kauli ambayo sikuielewa na hadi sasa fedha za Uamsho zilizopo ni 7,836,300.”alisema Massawe.

Clotilda alisema Mchungaji amekuwa na tuhuma za kuwanyanyasa akieleza kuwa kitu chochote kinachohusu kanisa hakiwezi kufanyika hata kiwe cha usafi hakitafanyika mpaka ruhusa itoke kwake na kwamba ameamua kuyaweka bayana ili Usharika ujue,na kanisa lijue juu ya unyanyasaji huu.

Mwl.Japhet Robert ni Katibu Msaidizi wa kikundi cha Faragha Usharika wa Hai Mjini alisema barua ya kusimamishwa uongozi imemshtua sana kutokana na kwamba aina ya barua aliyopewa haina maelezo muhimu kutoka kwa mchungaji kiongozi wa usharika wa hai mjini.

“Wakati mchungaji anakaribishwa usharikani hapa alikataa vitu alivyovikuta na kutaka vya kwake vifanyiwe kazi ikiwa pamoja na kusitisha huduma ya maombi hadi saa sita usiku na kusema mwisho wa maombi hayo ni saa mbili usiku.” Alisema Robert .

“Viongozi wa Faragha wameonekana kuja na mawazo ya kuzimu na kuwashangaza viongozi hao kwani mtu kufanya maombi na toba kwa ajili ya Kwaresma je na ilo ni jambo la kuzimu? Mchungaji alizidi kusisitiza kuwa hayo ni mawazo ya kuzimu.” Aliongeza Robart.

Alisema wameendelea na utaratibu wao lakini lolote linalofanyika liwe ni ufunuo wa maombi ya jioni,Mchungaji hataki kusikia wala kuona linafanyika isipokuwa amepewa taarifa na kwamba viongozi hawa kwa saa wamekuwa na changamoto katik autoaji wa huduma.

“Viongozi wa Uamsho wamekuwa na changamoto kwa namna ya kufanya huduma tukitamani kufanya huduma mahali fulani pasipo idhini ya mchungaji haitafanyika na hii imekuwa changamoto kwa viongozi wa Usharika wa Hai Mjini” alisema Robert .

Robert alisema kuna nyumba ya maombi ya utulivu ambayo imekuwa na ukakasi kwa mchungaji kuielewa na hataki kueleweshwavpamoja na kwamba mkutano mkuu na kamati ya jengo kuitambua hiyo nyumba,lakini mchungaji hataki kuielewa nyumba hiyo jambo ambalo linawaacha washarika wa Hai mjini na maswali mengi.

Mchungaji Kiongozi Dominic Mushi wa Usahrika wa Hai Mjini alipotafutwa kuzungumzia tuhuma dhidi yake alisema ufafanuzi wa tuhumza hizo mwandishi akazifuate kwa wale waliomtuhumu na kwamba hawezi zungumzia suala hilo .

“ Si msemaji wa jambo hilo ….huku akiondoka ….msemaji wa jambo hilo labda huyo aliyekueleza , Mh naomba tu uondoke ,hili ni kanisa la utaratibu wake “ alisema Mchungaji Dominic Shoo akimtaka mwandisi kuondoka eneo la kanisa .

Mwisho
 
Video hii inatusaidia KUWEKEWA
 
Attachments

  • 5621854-5566d8c47040be57b0b0cd8dfdfe5991.mp4
    3.3 MB
Mchungaji kagundua kuna upigaji.

Maombi mpaka saa sita itakua inaandikwa ruzuku ya kufuru ndiyo maana hajafuta maombi ila kapunguza muda.

Anataka kujua kila kitu hata cha usafi. Yeye kama incharge kwanini asijue?

Uelewa wangu umeona hivyo
 
Imani ya miaka hii ipo kwenye fedha Mungu amewekwa kando
 
Back
Top Bottom