Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,198
18 Aug 2020
Dodoma, Tanzania

WanaCCM waandamana kupinga maamuzi


Vurugu zinaendelea leo 18 agosti 2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma mjini baada ya kupokea majina ya wagombea udiwani ambao wamekatwa licha ya kuongoza.

Jana halmashauri ya CCM mkoa wa Dodoma walirudisha majina ya madiwani waliogombea kupitia chama hicho ambapo kata 7 Kati ya 41 za jiji la Dodoma walioongoza walikatwa na kurudishwa wengine ndipo wakaandamana ofisi za wilaya.

Mmoja wa diwani aliyeshinda CCM lakini jina lake lililokatwa amewaomba wanaCCM wa kata ya Changombe kuwa watulivu wasifanye maandamano wasubiri maamuzi ya Halmshauri ya wilaya CCM watakapotafuta ufumbuzi wa sintofahamu hiyo ndani ya CCM .

Chanzo: Mwananchi digital

Habari za ziada juu ya mtafaruku wa Dodoma kwa kina hapa chini kwa hisani kubwa : source: A.DIGITAL TZ youtube

MGOMBEA ALIA NA CHAMA BAADA YA KUSHINDA NA KUKATWA
Mshindi wa pili katika kura za wajumbe abaki na mshangao taratibu za maamuzi kupingana wakati aliletewa taarifa za kuteuliwa rasmi kuwakilisha CCM. Kuna makundi ndani ya CCM


CCM WAGOMBANA,POLISI WAINGILIA KATI
Wanachama Dodoma wilaya kata ya Ipagala, Nzuguni, Kizota watilia shaka maelezo kuwa hiyo ni taarifa toka juu kuwa washindi wa kura za juu ndiyo wepewe uteuzi kuwakilisha CCM inapingana na maamuzi ya vikao vya Halmashauri ya wilaya ya Dodoma. Wagoma kuondoka mpaka wapate barua zao za kwenda kwa Tume ya Uchaguzi msimamizi wa uchaguzi wa udiwani


WanaCCM washutumu viongozi wenye mishahara makao makuu kwa maamuzi yenye utata wakati wao viongozi wa mitaani wenye kujitolea ndiyo wanajua ukweli wa watia nia wagombea kama wana maadili au la kuliko viongozi wa CCM Mkoa au Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama Makao Makuu CCM Dodoma.
 
Vurugu kubwa zimeibuka leo 18 August 2020 hapa ofisi za CCM wilaya ya dodoma opposite na white House makao makuu ya CCM Taifa, wafuasi watch toka kata ya Chang'ombe walimvamia katibu wa wilaya na kumpa kichapo Hali iliyopelekea police kuwahi kuwatuliza wafuasi hao inadaiwa walienda kumsindikiza kada wao Juma masugu inaedaiwa jina lake limerudi kugombea udiwani wa changombe.

Na aliwakusanya wafuasi wake wengi waende kumescort kufika ofsin wakakuta jina la Bakari fundikira aliyeongoza kura za maoni kwa kutumia wajumbe mamluki wanavyosemaga wao maCCM, bw Masugu anadai Katibu alimpigia simu Jana na kumwambia jina limerudi ila ampe million moja kwanza sijui ilikuwa ya nini pia inasemekana bw fundikira alivyoona chama kata hakimtaki alimpigia simu Katibu mkuu Bashiru baada ya kuongea nae jina lake likarudi na ndo ugomvi ukaibuka leo ofisin na kusababisha kupigwa vibaya Sana.

Katibu wa CCM wilaya bila police kuwahi huenda angefariki,mpaka mda huu vijana wa CCM na wafuasi wao ma bodaboda wametapakaa hapa nje ya ofisi na baadhi ya wafanyabiashara wameanza kufunga maduka yao, police inaonekana wanaogopa wanapata kigugumizi kuwamwagia maji ya washawasha hao wahuni wa CCM kuwatawanya.
 
Back
Top Bottom