BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Kata ya Kasingirima, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwantumu Mgonja amemtangaza Mlekwa Kigeni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata kura 437 dhidi ya mshindani wake wa ACT-Wazalendo, Alumbula Khalidi aliyepata kura 233.
Ni katika uchaguzi mdogo uliofanyika leo Jumatano Machi 20, 2024.
Mwantumu amesema jumla ya vyama 12 vimeshiriki uchaguzi huo. Idadi ya walioandikishwa ni 1,960, idadi halisi ya waliopiga kura 713, kura halali 699 huku kura zilizoharibika ni 14.
Mgonja amesema katika uchaguzi huo vituo vya kupigia kura vilikuwa sita na wagombea wengine ni Salumu Hassani wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye alipata kura saba na mgombea wa UDP, Hassani Yungura amepata kura tano.
Mgombea wa Chaumma, Fikirini Selemani, Mussa Nkumila wa Ada Tadea na Hassani Rashidi wa Demokrasia Makini waliupata kura moja kila mmoja.
Diwani mteule, Kigeni mbali na kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumpa ushindi, ameahidi kufanya kazi bega kwa bega na wananchi ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika kata hiyo.
Uchaguzi wa kata hiyo umefanyika kufutatia aliyekuwa Diwani wake, Abdallah Kiembe kuajiriwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Pia soma > ACT Wazalendo wakamata Kura Feki uchaguzi Mdogo Kata ya Kasingirima Kigoma, Zikiwa zimepigwa kwa Mgombea wa CCM