Vurugu za kugombea kuchinja nyama huko Tunduma muda huu

Vurugu za kugombea kuchinja nyama huko Tunduma muda huu

Status
Not open for further replies.
Jamani vurugu bado zinaendelea, waislam wanazuia nyama kuuzwa. Defender za polusi naambiwa zimeingia mjini kutuliza ghasia.

Swali:
Hivi kwanini ung'ang'anie kuchinja nyama ambayo hutokula wewe?

Kama ni ibada si nenda kafanyie nyumbani kwako?

Kwanini ulazimishe kila mtu atii imani yako na huku unajua wazi kuwa imani ziko nyingi?
Tatizo serkali ilisha tangaza kua mwenye haki ya kuchinja ni muslim, kilicho kua hapa wakrsto hawatii amri ya serkali (wanaham ya vita ya kidini)
 
Akili yako haina tofauti na jina lako! Yaelekea umekalia jina lako

Acha mipasho lete mistari kutoka kwenye dini yako ku-justify kwa nini upumzike. Bahati mbaya sana kwako huo mstari haupo. Otherwise, shut up your mouth.
 
Hausadii!
Uamuzi mzuri ni kuwahamisha Wakristo waliopo sehemu za Waislamu na kuwapeleka sehemu za Wakristo.

Waislamu waliopo sehemu za Wakristo nao wahamishiwe sehemu za Waislamu.

wazo la ovyo kabisa na barabara, magari na viwanja vya ndege, biashara nk zote utatenganisha?
 
Hv zaidi ya miaka 50 walikuwa wapi kupinga kula nyama zilizo chinjwa na waislam hadi leo wanataka kupambana kwa ajili ya jambo hili!!
Lazima waumini wa kikristo waliangalie kwa jicho la pili hili suala ,huenda wakawa wanatumiwa kwa maslahi ya watu flani chini ya mwamvuli wa dini.
Hawakujua kuwa mnapochinja mnafanyia ibada za Alah hizo nyama.
 
Huyo achana naye Mkuu. Laiti angejua dunia ina amani kwa sababu ya ukristo. Vinginevyo ingekuwa Jehanamu kama huko Solmalia, Northern Nigeria, Mali, Iraq, Iran, Kashmir, Pakistan, Bangladesh, na kwingineko dini ilikoota mizizi.
Hao wana matatizo yasio fanana na yakwetu. Usiamini eti matatizo ya waislam yana fanana dunia nzima. Jitahidi angala kutumia akili yako japo kwa dakika mbili tu.
 
nina kangurue kangu namwomba mwislamu anichinjie

Mimi mwenyewe nawashangaa hao wanapiga tararira huko mm nina washkaji kibao waislam na tunagonga nao NOAH na bia mwanzo mwisho. Wananiambia wameichunguza, wakaichunguza sana hii nyama hawajaona ubaya wake wameona waendelee tu.hao wanaogombania kuchinja wakachinje nyama za waislam wenzao hizi za wakristu tutachinja na kununua wenyewe na wao wafanye hivyo hivyo. Kuna haja gani kusumbuana bana.
 
Dr.slaa alisema 2010 kuwa kuichagua CCM ni kuchagua janga sasa yamekuwa majanga.
Usisahau kua alisema kua nchi haita tawalika, na kweli anatumia mpaka makundi ya kigaidi ili nchi isitawalike
 
Hv zaidi ya miaka 50 walikuwa wapi kupinga kula nyama zilizo chinjwa na waislam hadi leo wanataka kupambana kwa ajili ya jambo hili!!
Lazima waumini wa kikristo waliangalie kwa jicho la pili hili suala ,huenda wakawa wanatumiwa kwa maslahi ya watu flani chini ya mwamvuli wa dini.

waislamu walikuwa wapi kwa miaka 50
kupinga mfumo kristo itakuwa nao wanatumika na JK
 
Mimi ni mkristo, lakini katika hili nadhani Wakristo wanaoendekeza vurugu za kudai kuchinja wanakosea. Haya ni matokeo ya hisia za kulipiza kisasi, jambo ambalo Yesu alilikemea sana. Acheni Waislamu waendelee kuchinja, kwani tangu tulipoanza kula vilivyochinjwa, hatujawahi kuona dosari kwenye nyama! Mkristo ukitaka, chinja nyumbani kwako. Basi.
Manyerere Jackton, hili suala ni zaidi ya kuchinja... watu wanatafuta mahali pa kutolea hasira zao
 
Last edited by a moderator:
Tatizo wakristo walisha zoea kuipeleka puta serkali, sasa Raisi wasasa kawadharau ndio maana wanamuona hafai, hebu angalia madai yao eti wanadai kuchinja? Miaka yote walikua wapi? Acheni unafki tufanye kazi kwa bidii tulijenge taifa letu.
 
Ujinga HALISI, kamwe haufutwi kwa kukaa darasani na kusoma miaka mingi!

ILA

Ni kwa kupitia maumivu makali!

Sidhani watanzania wa leo wataelimika kwa hotuba za kisiasa au za kidini au kwenye lecture huko chuo kikuu ILA
kwa maumivu ya vita, mateso na kunyukana kabisa kabisa ... hadi mioyo ya waisalam na wakrsto IRIDHIKE kuwa hakuna mshindi na wote wataishi Tanzania kama amabavyo imeshakuwa hivyo siku zilizopita.

Somalia sasa wanaheshimiana,

Rwanda sasa wanaheshimiana,

mifano ni mingi, lakini ghrama zake ???? Ni hapo sasa ... inafikia mahali hakuna kurudi nyuma hadi UJINGA ufutike kwa Maumivu ya kumwaga Damu, vita kali na KIFO KUWA KITU CHA KAWAIDA KWENYE SEREKALI TAWALA!!!

Hakuna jipya ambalo waasisi wa Taifa hili hawakuliweka mkazo kwa ajili ya Taifa lenye amani na uhuru wa kweli. Lakini kizazi hiki hakitaelewa Umuhimu wa waasisi wa Taifa hili kwa mihadhara na mafundisho ya mitandaoni ... NI KWA MAUMIVU YA MINYUKANO NA KUMWAGA DAMU ...sioni Tanzania kuliepa hilo. Bora kujiandaa!!!NANI ANABISHA???!!

Nani mwenye akili Timamu Tanzania leo hii Kuweza Kuzuia Vita kati ya Wakristo na Waislamu, Vita ya Kitaifa iliyoko hapo mbeleni kidogo tu?

Niambie yuko wapi?

Kashechukua hatua gani?

Kama kashakua hatua ... auhueni ya Tatizo iko wapi?

Nauliza yuko wapi Mtanzania mwenye busara na akili ya kuepusha vita vya Dini Tanzania???
 
Mkuu madai ya msingi ni kwamba hiyo ni ajira yao; Hivyo basi wakristu wakichinja wenyewe watakuwa wamepoteza ajira zao; ukizingatia shule na elimu zao ni utata mtupu, wataishije hapa mjini?
Utata ktk elim munao wakristo, mfano Mulugo ona kamdhulumu kijana wa kiislam (hamim) ili apate elim ya Sec hapo aitoshi kafoji mpaka cheti cha ualimu ili apate ajira hiyo tu yapaswa uamini kua ni utata alio fanya mkiristo mwenzio. Sasa hebu nipe mfano wa muislam japo mmoja tu, (hapo sijaenda kwa mwigilu)
 
nchi yetu ina tatizo kubwa sana, kuanzia ombwe la uongozi, kutojitambua wanajamii na kuamrishana mambo yasiyo na kichwa wala miguu, yafaa tupate muafaka wa jambohili mapema sana. Wasira kama waziri wa mahusiano anatakiwa awaite viongozi wa dini zote , kukaa meza moja na kufikia muafaka.La zaidi ni kila dini kuchinja na pia bucha hizo kutambuliwa na pia wakaguzi wa nyama/aafisa afya kusimamia mazoezi hayo,pia bucha zibandikwe lebo bucha ya kikristo na bucha ya kiislam (HALAL MEAT BUTCHERY) na zisiwe mahala pamoja, kama vile bucha za kitimoto zisivyo kwenye same stalls as beef butcheries

Ni kansa ya akili kujiona kama mtu ni halali na mwingine haram. Na ndiyo sababu ya mgogoro. Wengine kujiona wana haki ya kuwalisha wenzao aya za shetani. Nao hawataki sasa kwa nini uwalazimishe.
 
waislamu walikuwa wapi kwa miaka 50
kupinga mfumo kristo itakuwa nao wanatumika na JK
Madai hayo ya waislam yalikuapo kabla ya Uhuru wa nchi hii, ndio maana walipambana kumuondoa mkoloni. Tatizo lao walibugi pale walipo mpa kafili mwengine (nyerere) wao wakizani atapambana na mfumo kumbe ni kinyume chake. (yeye aliendeleza pale walipo achia wakoloni)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom