Vurugu za kugombea kuchinja nyama huko Tunduma muda huu

Vurugu za kugombea kuchinja nyama huko Tunduma muda huu

Status
Not open for further replies.
Acheni Kupigana na kubishana nyie, njooni hapa nina Panya Buku wangu mje mnichinjie Pasaka yangu iwe nzuri!!
 
sasa kweli watu wanashangaza mtu kama kachinja ale mwenyewe yanini kumwingilia, mtu hata kama kachinja mbwa ili mradi anakula yeye mwenyewe mimi sioni tatizo
 
Badala ya kugombea kazi za maana wanahangzika na kuchinja bata..hii dini bana
 
Hayo ndio matokeo ya kufanya mazoea kuwa sheri, kawani hakuna sheria ya nchi iliyo muidhinnisha muislamu kuchinja zaidi ya mazoe. Mungu ibariki Tanzania R.I.P cccm2015
Ni kama vile jumamosi na jumapili imefanywa mazoea ya kupumzika kuwa ni sheria.
 
Hawa waislam hela yenyewe ya kununua nyama wanayo au wanaleta fujo tu
 
Mzee Ruksa namkumbuka kwa mengi..mojawapo ni hili
anayekula .... ruksa
anayekula kitimoto riuksa etc
hii ni dunia ya viumbe mbalimbali,tusihukumu dini za wenzetu wala rangi wala jinsia hivyo tumevikuta hatukupata nafasi kuvichagua kabla hatujazaliwa hivyo basi tuheshimu dignities za kila mtu
 
Waislamu wachache waliopo Mbeya wahamishiwe Mtwara au Lindi, halafu Wakristo wachache wa Mtwara au Lindi wahamishiwe Mbeya.

Tungeanza kuwa na eneo moja ambalo ni free from Christians na jingine free from Muslims.
Hii itawapa Waislamu waliopo sehemu nyingine za Wakristo wengi wawe wamepata sehemu ya "kukimbilia" na Wakristo waliopo sehemu za Waislamu wengi wawe wamepata sehemu yao ya kukimbilia.

na sisi waislamu ambao asili yetu ni sehemu hizi za wakristu wengi tufanyeje?
 
Mimi ni mkristo, lakini katika hili nadhani Wakristo wanaoendekeza vurugu za kudai kuchinja wanakosea. Haya ni matokeo ya hisia za kulipiza kisasi, jambo ambalo Yesu alilikemea sana. Acheni Waislamu waendelee kuchinja, kwani tangu tulipoanza kula vilivyochinjwa, hatujawahi kuona dosari kwenye nyama! Mkristo ukitaka, chinja nyumbani kwako. Basi.
daa, yaani hujui tatizo ni nini! Tatizo ni muislamu kumzuia Mkrito asichinje! Hapo Mkristo analipiza kisasi gani? Yesu alikufa si kwa wizi wa kuku! bali kutetea Haki. Na hajawahi kumkemea mtetezi wa Haki hata mmoja! Injili gani unayoihubiri!
 
Kila dini wawe na mabucha yao Waislam wawe na bucha zao na Wakirsto wawe na bucha zao wauze nyama zote wanazotaka pamoja na nguruwe hakuna tatizo.
..na siku za mapumziko zigaiwe kwa kila dini (Ijumaa na Jumapili)
 
Mkuu Manyerere; tangu mwanzo jamii hizi mbili ziliishi bila matatizo bila upande mmoja kuwa na hisia yoyote mbaya dhidi ya mwingine kutokana na issue ya kuchinja. Hii iliwezekana kwa sababu pengine kwa "ujinga" upande mmoja haukujua maana halisi ya kilichokuwa kinafanywa na upande mwingine.

Ni hivi karibuni ilidhihirika kwamba kumbe upande mmoja ulikuwa unatumia nafasi hii KUFANYA IBADA yaani KUMTUMIKIA MUNGU WAO kupitia migongo ya wengine. Labda kama wewe sio mtu wa imani vinginevyo ungefanyaje? Ni mpumbavu tu atakayekuwa tayari kushiriki ibada za wengine kinyume na imani ya dini yake.

USHAURI KWA SERIKALI: Iwe ni marufuku kwa machinjo ya umma kuchinja mifugo kwa ibada ya dini fulani. Pili, kama ilivyo kwenye nchi nyingine ruksa kuanzisha ile nembo ya HALAL atakayependa kwenda huko na aende asiyependa na asiende. Nadhani hii itamaliza tatizo.

Tukimaliza hilo la kuchinja Waislam wanataka kuifuta siku ya Jumapili isiwe tena siku ya mapumziko.

Waislam hapo mwanzo hawakujua kama Jumapili ni siku ya ibada kanisani kwa Wakirsto wanaishauri serikali ifanya Jumanne ndiyo iwe siku ya mapumziko.

Kama itashindikana basi Ijumaa nayo iwe siku ya mapumziko.
 
Kila dini wawe na mabucha yao Waislam wawe na bucha zao na Wakirsto wawe na bucha zao wauze nyama zote wanazotaka pamoja na nguruwe hakuna tatizo.

Hilo ndilo la muhimu. Kuwe na bucha huru na zile zitakazoonesha nyama zilizosongolewa kwa imani za kijini.
 
Kila dini wawe na mabucha yao Waislam wawe na bucha zao na Wakirsto wawe na bucha zao wauze nyama zote wanazotaka pamoja na nguruwe hakuna tatizo.

Hapo ni sawa ila alhamisi na ijumaa iwe ni mapumziko (wiki hii inakua alhamisi na ijumaa wiki inayofata jumamosi na jumapili)
 
Kwa miaka 50 hakuna aliyefahamu kwamba kumbe kuchinja ilikuwa inatumiwa pia kama sehemu ya kufanya ibada hadi hivi karibuni waliporopoka wenyewe na kumwamsha aliyelala.

Kama ni hivyo basi waislam watakuwa na haki ya kukataa kuimbishwa mwimbo wa taifa maana ni ibada kwa wakristo (refer chuo kidogo cha sala), sasa unadhani kuna atakaye baki salama hapo? Lazima tukubaliane pasipo kukubaliana.
 
Tukimaliza hilo la kuchinja Waislam wanataka kuifuta siku ya Jumapili isiwe tena siku ya mapumziko.

Waislam hapo mwanzo hawakujua kama Jumapili ni siku ya ibada kanisani kwa Wakirsto wanaishauri serikali ifanya Jumanne ndiyo iwe siku ya mapumziko.

Kama itashindikana basi Ijumaa nayo iwe siku ya mapumziko.

Haina tatizo kabisa Mkuu. La msingi mkristo apewe uhuru wake wa kuabudu na kupumzika kama anavyoagizwa na dini yake. Vivyo hivyo kama waislamu nao WANAAGIZWA KUPUMZIKA IJUMAA hawana budi kufanya hivyo. Muhimu serikali iandae utaratibu mzuri kufanikisha hilo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom