Vurugu za kugombea kuchinja nyama huko Tunduma muda huu

Status
Not open for further replies.
mimi nasema leo kinachopiganiwa si imani bali ni ujira. unajua mimi sioni mantik ya kupigania kuchinja maana wanaopigania kwamba wana haki huwa hawafanyi hiyo kazi bila malipo sasa imani hiyo iko wapi. nashauri Raisi atoe tamko na washauri wake wamshauri vizuri kwani naona dalili ya uongozi wake kuishia pabaya. Lowasa alisema kuna bomu la ukosefu wa ajira washabiti wenye mwono wa karibu wana simama na kusema amekurupuka sasa haya ndiyo madhara ya kuwa viongozi watumia uzoefu wa umri kuongoza badala ya tafiti
 
Du! Sasa wakristo wakichinja wanakuwa wamevunja katiba au sheria yoyote??
 
Kwani Kuchinja ni kosa jamani? Mbona mimi nimejichinjia kuku wangu mwenyewe kwa ajili ya pasaka!
 
Taarifa nilizopata muda
sio mrefu kutoka kwa mdau aliyepo huko boda ya Wajanja Tunduma ni kwamba
kuna vurugu zinaanza kutokea kati ya Waislamu na Wakristo kutokana na
ng'ombe 9 waliochinjwa jana na wakristo wenyewe. Walioko boda jamani
tupeni taarifa zaidi. Hii nchi inakwenda wapi jamani?
Wanaoanzisha fujo watakuwa wamekosa ujira wa kuchinja ambayo ni nyama ya shingo. njaa hii!
 
Mimi ni mkristo, lakini katika hili nadhani Wakristo wanaoendekeza vurugu za kudai kuchinja wanakosea. Haya ni matokeo ya hisia za kulipiza kisasi, jambo ambalo Yesu alilikemea sana. Acheni Waislamu waendelee kuchinja, kwani tangu tulipoanza kula vilivyochinjwa, hatujawahi kuona dosari kwenye nyama! Mkristo ukitaka, chinja nyumbani kwako. Basi.
 
Haya mambo yako huko bara huku pwani watu walishastarabika toka zamani.ukafiri na ushetani una nguvu.
Naona Maaskofu wamewatuma muanze kuwagawanya Waislamu wa Pwani na Wabara sasa!

MMeshindwa na mtashindwa! Mpwani au Mbara anayesema Laailaaha illa llaah wote huunganishwa na tamko hili.

Huu ndio mwanzo wa mwisho wa MfumoKristo Tanzania.
Bye bye MfumoKristo!
 
Kwani Kuchinja ni kosa jamani? Mbona mimi nimejichinjia kuku wangu mwenyewe kwa ajili ya pasaka!

Kama unachinja na kula mwenyewe na familia au ndugu zako hakuna taabu. Tatizo ni pale unapochinja kibudu chako then kupeleka bucha na kuanza kuuza jumla kwa watu wote. Naamini tatizo ndio liko hapo!
 
Mimi ni mkristo, lakini katika hili nadhani Wakristo wanaoendekeza vurugu za kudai kuchinja wanakosea. Haya ni matokeo ya hisia za kulipiza kisasi, jambo ambalo Yesu alilikemea sana. Acheni Waislamu waendelee kuchinja, kwani tangu tulipoanza kula vilivyochinjwa, hatujawahi kuona dosari kwenye nyama! Mkristo ukitaka, chinja nyumbani kwako. Basi.

hatuwezi kuendelea kula nyama zilizosomewa dua ambazo hatuzijui.
 
Kama unachinja na kula mwenyewe na familia au ndugu zako hakuna taabu. Tatizo ni pale unapochinja kibudu chako then kupeleka bucha na kuanza kuuza jumla kwa watu wote. Naamini tatizo ndio liko hapo!

Kauli za aina hii ndizo zinazoibua na kukomaza mgogoro. Nyama iliyochinjwa na mtu timamu haiwezi kuwa kibudu! Kejeli na dharau ndiyo mafuta kwenye cheche za udini. Ziacheni-Waislamu kwa Wakristo!!
 
hamna aliyekulazimisha kununua!
 
Kwani lazima ukanunue,njaa tu zinawasumbua
Kama unachinja na kula mwenyewe na familia au ndugu zako hakuna taabu. Tatizo ni pale unapochinja kibudu chako then kupeleka bucha na kuanza kuuza jumla kwa watu wote. Naamini tatizo ndio liko hapo!
 
Mimi ni mkristo, lakini katika hili nadhani Wakristo wanaoendekeza vurugu za kudai kuchinja wanakosea. Haya ni matokeo ya hisia za kulipiza kisasi, jambo ambalo Yesu alilikemea sana. Acheni Waislamu waendelee kuchinja, kwani tangu tulipoanza kula vilivyochinjwa, hatujawahi kuona dosari kwenye nyama! Mkristo ukitaka, chinja nyumbani kwako. Basi.

ushindwe na ulegee kwa jina la Yesu (si Isa)! Why nichinjie kwangu? Nijifiche kitu gani?
 
Kauli za aina hii ndizo zinazoibua na kukomaza mgogoro. Nyama iliyochinjwa na mtu timamu haiwezi kuwa kibudu! Kejeli na dharau ndiyo mafuta kwenye cheche za udini. Ziacheni-Waislamu kwa Wakristo!!

wanadai ndiyo wenye haki ya kuchinja pekee, niwaulize hiyo haki ya kuchinja kwa ajili ya wakristo ni nani kawapa?
 
Hausadii!
Uamuzi mzuri ni kuwahamisha Wakristo waliopo sehemu za Waislamu na kuwapeleka sehemu za Wakristo.

Waislamu waliopo sehemu za Wakristo nao wahamishiwe sehemu za Waislamu.
Ni MPUMBAVU tu anayeweza kuwa na mawazo ya aina hii.
 
Jamaaa jamaaa!!!!!!!!! Tutaona roho Yarabi! Mwisho wa kugombea kuchinja nyama itakuwa kuchinjana Binadamu!Ngomb'e watashukuruje! Mola tuepushie!!!!!!!!!
 
Uptodate:ameenda kuitwa mtu anayekagua afya ya nyama,kitu ambacho sijaelewa huyu atalimaliza vipi hili kwani majukumu yake ni kukagua usafi na afya ya nyama,waislamu wameamua kufunga butcher za wakristu,kuna tension kiasi kwani watu wanasubiria kitoweo cha pilau na butcher ndo zimefungwa,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom