Maandamano Tunduma tena kuhusu kuchinja nyama

Maandamano Tunduma tena kuhusu kuchinja nyama

Morick

Senior Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
114
Reaction score
17
Kwa habari nilizozipata hivi punde kutoka eneo la tukio Tunduma( boda la wajanja) zinasema kuwa jensi la polisi limeamu kutumia mabomu kuwatawanya waandamanaji walioandamana kupinga kauli ya mkuu wa wilaya aliyoitoa jana baada ya kukutana na maaskofu na mashehe katika suala la uchinjaji kitoweo.

Inasemekana kuwa mkuu wa wilaya huyo alitoa kauli kuwa waislamu ndio wenye haki ya kuchinja hivyo wao ndio wanastaili kuchinja. kauli hiyo iliinua hisia za hasira upande wa wakristo mpaka kufikia maandamano makubwa sana yanayoendelea mpaka sasa ninavyoandika.

Hali hii imelazimu shule kufungwa kwa muda ili kupisha vurugu hizo.

Updates zitafuata baadae
 
hapo lazima watasema CDM imeshiriki -- ha ha ha
 
Kuna mtu hapa JF aliwahi kusema Raisi KIkwete ana majini yanayotaka damu za wananchi,hivi naanza kuamini kuwa ni kweli swala hili alipaswa kuliweka vizuri juzi alipohutubia taifa hivi kweli anadhani bila nguvu za ziada za kimapatano kuwapatanisha wakristo na waislamu lazima inaweza,hivi mbona yeye anachukulia vitu vizito vinavyoweza haribu tunu yetu kama upepo utapita.

Nchi nzima tayari kumekuwa na mganyiko watu wanachinja na nyama zinauzwa makanisani anadhani hilo litapita bila kuweka mapatano. Tunduma ina wakristo robo tatu ya wakazi leo uambie hawana haki ya kuchinja unataka amani kweli, nguvu ya dola haijawahi kushinda hili la nyama litaleta mtafaruku mkubwa nchini.

Nani amwambie Raisi Kikwete aache kucheka na akina Ruto huko serengeti arudi aweke sawa hili la nyama. Kikwete hatutaki wewe uhalalishe vurugu kwenye nchi yetu. Kikwete mbona umeutafuta uraisi kwa miaka 10,na una miaka saba madarakani ni nini kinakushinda kuipatanisha jamii ikawa moja wewe unainjinia jamii itawanyike.

ikwete wewe ni hatari sana ,nakuweka kwenye maombi pepo la ubaya ulilonalo likutoke.
 
Huyo mkuu wa wilaya hata haangalii upepo unavyokwenda!
 
JK(Serikali+CCM) Mnakotupeleka siyo kuzuri hata kidogo mchumia janga ula na wakwao.
 
Viongozi wa Tanzania wanahitaji hekima ya Mungu kuliko wanayotumia sasa. Nani anayelazimishwa kushiriki ibada ya Imani isiyomhusu. Wakristo si mabwege kiasi hicho.
 
Kuna wakuuu wa wilaya siku hizi, zamani wakuu wa wilaya walikuwa wanateuliwa hawa wa siku hizi wanatamkwa tu. No mchakato. Dada yako mzuri unamtambulisha kwa viongozi wa chama, unaukwaa ukuu wa wilya. Unajua sana kulopoka matusi kwa viongozi wa chadema unapewa ukuu wa wilaya. Una babu yako mganga wa kienyeji ukuu wa wilaya unachagua wilaya ya kwenda. Na the rest ni ukabila na siasa zisioandikwa za CCM. Kwa wadada, wao ni kukubali kutengana na nguo na mtu wa umri wa baba yako unapewa.
Sasa huyu aliropoka akidhani anamfurahisha JK na Kandoro kumbe ndoo anawasha moto. Na Tunduma pale akae chonjo hawakawiii kumfuata kwake.
 
Mwenyezi mungu baba wa rehema uliwapigania shedraki, meshaki na abelnego, pia ulimpigania mussa akiwatoa wana wa israeli misri na wengine walio wengi. Tazama wana wako wa tanzania wameinua macho yao sasa wakikuomba uinue mkono wako na kuwaokoa na majanga haya kwa kuwa damu isiyo hatia ndiyo imwagikayo kila uchao. Kama ulivyo muadhibu farao ndivyo utuonyeshe sisi kuwa upo pamoja nasi.
 
Hivi nimedokezwa tena kuwa mkuu wa wilaya amewaambia maaskofu kuwa japo Tunduma waislamu ni 1/8 ya wakkristo wote lakin wao ndio watakao endelea kuchinja na kwamba amri nyingine naye hana mamlaka nazo sababu zinatoka juu.

MY TAKE; anamaanisha nini hapo kwenye red?
 
Hapa tunakiwa kujiuliza kwa nini sasa?Wakristo walikyuwa wapi kudai kuchinja mpaka wakakumbuke sasa wakati wa JK?Rais wetu na wanaomshauri wanatakiwa kutumia busara ya kutatua tatizo hili si kwa hotuba zilizokuwa na "solution" kama ya JK juzi.

Wanachokifanya ni kufunika moshi kwa lengo la kuzima moto.JK na wenzake wanajua walipokosea,waombe msamaha watu watawaelewa tu!
Tuna zaidi ya miaka miwili ya kuwa na serikali hii, ni mangapi mabaya yataibuka kama hawa jamaa hawatajirekebisha au kuachia nchi mapema?

Hata hawa Wakuu wa wilaya hawatumii bussara zao hata kama wanatumwa.Haki za watanzania si zipo kwenye katiba?Wapo palipotoa haki ya waislamu kuchinja.Huwezi kumpa mtu haki bila kurejea kwenye katiba ambayo ndio muongozo wa kutoa haki na hukumu.

Mh.JK atafakari na achukue uamuzi wa busara kabla mambo hayajawa magumu zaidi.
 
Ivi serikali inapata ugumu gani kusema wakristu chinjieni pale nanyi waislam palejust simple like zet. Tatizo mzee wa kaya kaelement kaudini anako ila ni bingwa wa kubisha kwenye media tu. Ha ha ha ha ha ha ha hahaaaaaaaa..............pipoooooooooooooooozi........!
 
mimi naomba kuuliza swali, hivi aliyewapa haki ya kuchinja nyama waislamu ni nani hapa Tanzania? Na je nchi nyingine ulimwenguni kote waislamu wanayo haki hii na je waislamu wa nchi hizo hawali nyama zilizo chinjwa na wakristo?
 
Nchi ya wapumbvu...sasa naona huu ni ushenz...nizi zinzomwagika ni damu za watu, Tanzania melaaniwa, kwa hali hii huyo mkuu wa wilaya ni kam dampo, unampangia nani amchinjie nani, walitakiwa wadili na huyo mkuu wa wilaya. na hii damu iwe juu yake
 
bahati mbaya Kabisa juzi ktk speech yake hakuzungumzia maamuzi mabovu yanayofanywa na viongozi wake pamoja na yeye mwenyewe, hizi hotuba za kupewa dk 10 kabla ya kuzisoma zitatugharimu sana.
 
Mwenyezi mungu baba wa rehema uliwapigania shedraki, meshaki na abelnego, pia ulimpigania mussa akiwatoa wana wa israeli misri na wengine walio wengi. Tazama wana wako wa tanzania wameinua macho yao sasa wakikuomba uinue mkono wako na kuwaokoa na majanga haya kwa kuwa damu isiyo hatia ndiyo imwagikayo kila uchao. Kama ulivyo muadhibu farao ndivyo utuonyeshe sisi kuwa upo pamoja nasi.
na pia utujalia hekima na busara kuisha kwa amani kwa watanzania wote
 
Back
Top Bottom