njeeseka
JF-Expert Member
- Oct 19, 2012
- 1,374
- 985
Taarifa nilizopata muda sio mrefu kutoka kwa mdau aliyepo huko boda ya Wajanja Tunduma ni kwamba kuna vurugu zinaanza kutokea kati ya Waislamu na Wakristo kutokana na ng'ombe 9 waliochinjwa jana na wakristo wenyewe. Walioko boda jamani tupeni taarifa zaidi. Hii nchi inakwenda wapi jamani?
hakuna vurugu zozote kwa sasa, kilichotokea ni kwamb leo asubuhi kulitokea mtafuruku machinjioni uliosababishwa na bwana afya. baada ya kugoma kupima nyama iliyochinjwa na wakristu,hivyo kukosa uhalali wa kuuzwa mabuchani. mtafaruku ulihamia mjini baada ya wakristu ambao ndio wengi hapa kusikia mabucha yao yamefungwa sababu nyama haijapimwa....bila busara za diwani wa chadema Freck Mwakajoka huenda hali ingekua mbaya zaidi... haraka sana alitafutwa huyo bwana afya na kulazimishwa kupima nyama na kugonga mihuri chini ya ulinzi mkali wa polisi maana wananchi walikua na hasira sana na bwana afya. tetesi zinasema bwana afya alikua anatimiza maagizo ya mkuu wa wilaya .....mpaka sasa hivi hali ni shwari kabisa.!!!
CC Moderator.