Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

wana CDM wenzangu,2subili tamko la Wenje,ila nahic uongoz wa Cdm mwanza hawajaelewana,kuna mgogoro umetokea kati yake juzi akiwataka wa machinga waendelee kufanya biashara kwani nae ndo alikotokea,huku uongozi wa jiji ukipinga nae vikali. As i said tusubiri tamko lake! Ila hawa polisi wao cjui amri hiyo wametoa wapi,ya kuua raia
Kwa IGP ili amfurahishe Kikwete maana kikwete anaendesha nchi hii kwa visasi kwani juzi alipoenda kufungua barabara moja hapo mwanza wakazi wa mwanza walitoka na Bendera za CHADEMA na alipo pita walimnyoshea vidole viwili yaani V alama inayotumiwa na CHADEMA....
 
this is not fair kwa watanzania wenzetu wenye asili ya kiasia. Tanzania ni yetu sote, na katiba imetoa uhuru wa kuabudu chochote mtu apendacho. Tanzania haijawahi na haitakuja kuwa nchi ya dini mbili tu ukristo na uislam, bado kuna mamilioni wanatambika, wapagani na wenye dini nyingine ndogo. Tuwe na utulivu kwenye kulitazama hili jambo.

Mi ningependa kujua huyo kiongozi wa mabaniani ni wa level gani? Je ni supreme leader wa baniani wote duniani au hawa wa humuhumu nchini?

Je kama hawa baniani walifuata taratibu zote za kuomba kibali cha kufunga barabara?

Na je hicho kibali kilieleza muda wa kufunga na kufunguliwa hiyo njia?

Je hao "wamachinga" au wawakilishi wao walishirikishwa kwenye kupanga hiyo ratiba?

Baada ya hapo, ndio tuanze kujiuliza communication failure ilikua wapi ili kuzuia hili tukio lisijirudie tena.

naunga mkono mkuu alwatan!!!!
 
Historia iko wazi jiji la mwanza lilikuwa na amani wakati wa CCM, hawa CDM wameingia na visasi pia madiwani wao wamegeuza ofisi za jiji vijiwe vya kuzungumzia masuala ya CDM

Hebu nijaribu kuweka akili kwenye meseji yako badala ya ushabiki.

Kabla ya uchaguzi, Mji wa Mwanza na Moshi haukuwa na machinga kando ya barabara. Uchaguzi ulipofika Polisi wote wa majiji na viongozi wote waliambiwa wawe wapole. Pale Moshi nasikia hata wazembe hawakupewa barua za onyo, waliambiwa hayo yote baada ya uchaguzi. Hayo yanawahusu CCM. Ilikuwa ruhusa ya kutaka wapendwe.

Sasa uchaguzi umekwisha na bahati mbaya miji kama Mwanza CCM wana hasira nao. wanajua hawakuchaguliwa si unaona hata safari za Kikwete Mwanza zimekoma! Sasa machinga wanaambiwa waondoke. Miezi zaidi ya sita baada ya kuwaruhusu.


Polisi wameitwa na nani na ni nani kawaambia Machinga wana siraha za kupambana nao? Kwa nini waende na Risasi za moto?
 
Asante MUNGU VITA DHIDI YA MAPONJORO IMEANZA,GOOO.....GOOOOOO ....GOOOOO MAPONJORO....BOMBAY IZ WAITING FOR U LEAVE OUR NATION U PONJORO LEAVE IT......


Huo ni uchochezi usio na mantiki
 
Asante MUNGU VITA DHIDI YA MAPONJORO IMEANZA,GOOO.....GOOOOOO ....GOOOOO MAPONJORO....BOMBAY IZ WAITING FOR U LEAVE OUR NATION U PONJORO LEAVE IT......
Tatizo siyo "MAPONJORO" ni serikali ya CCM unataka kuniambia Arusha, Mara walisababisha...
 
ila ipo siku isiyo na jina,serikali iliyopo madarakani isipoangalia hili la "tabaka" akti ya watu asili ya waasia vs wabongo!!tutachapana sana tu,siku iyo itakua hakuna kuogopa risasi wala nini,sijui ndiko tunakotaka kufika???why uchape mtu risasi kavu?rubber bullets zilishindikana!!haaa
ni kweli wahindi/wazungu/waarabu mwanza na wabongo mwanza kuna utofauti mkubwa wa maisha,kwanza wahindi wananin'ginia nhc town na maduka yao kibao na iyo misikiti yao ndo ipo iyo mitaa ya wamachinga sipati picha palikuweje na uyo kiongozi wao baniani!!chuki imezaliwa upya hapa!!
how i hate it God forbid!!
 
Nakushangaa unauliza jibu! hivi hujui kuwa meya na madiwani wengi wa mwanza ni cdm? unategemea nini?

Kwa hiyo Bunduki zilizo ua ni za madiwani wa CDM? Hao wanaowakimbiza wamachinga ni madiwani wa CDM?
CCM labda ina agenda ya siri kwa kuua raia katika kila jiji lililochukuliwa na CDM!
 
Historia iko wazi jiji la mwanza lilikuwa na amani wakati wa CCM, hawa CDM wameingia na visasi pia madiwani wao wamegeuza ofisi za jiji vijiwe vya kuzungumzia masuala ya CDM
Utakuwa unawaza kwa kutumia makalio au tumbo na siyo akili yako...
 
Acha ndoto za mchana Kbd.
Ukombozi wa Tz ulishafanywa na TANU.
Kilichobaki kwako chapa kazi halali ujenge nchi, si kubwabwaja upuuzi.

Mpuuzi nani kati yako na mshikaji aliyeota ukombozi' TANU IMELETA UHURU WA BENDERA,uhuru wa KIUCHUMI na kisiasa bado! Wachache ndio wanaamua dhidi ya wengi hakuna ushirikishwaji wa wadau.
 
This is not fair kwa watanzania wenzetu wenye asili ya kiasia. Tanzania ni yetu sote, na katiba imetoa uhuru wa kuabudu chochote mtu apendacho. Tanzania haijawahi na haitakuja kuwa nchi ya dini mbili tu Ukristo na Uislam, bado kuna mamilioni wanatambika, wapagani na wenye dini nyingine ndogo. Tuwe na utulivu kwenye kulitazama hili jambo.

Mi ningependa kujua huyo kiongozi wa mabaniani ni wa level gani? Je ni supreme leader wa baniani wote duniani au hawa wa humuhumu nchini?

Je kama hawa baniani walifuata taratibu zote za kuomba kibali cha kufunga barabara?

Na je hicho kibali kilieleza muda wa kufunga na kufunguliwa hiyo njia?

Je hao "wamachinga" au wawakilishi wao walishirikishwa kwenye kupanga hiyo ratiba?

Baada ya hapo, ndio tuanze kujiuliza communication failure ilikua wapi ili kuzuia hili tukio lisijirudie tena.
kimsingi nakubaliana na wewe 100% na inaelekea hukusoma bandiko langu vizuri....
 
Chanzo ni kipi hasa... hizo hapo juu

chanzo ni hiyo habari ya kwanza....hiyo ya pili ya huyu jamaasijui anazungumzia vurugu zipi!! vurugu zimetokea leo yeye anasema juzi.......
 
Madiwani wa CDM Pamoja na Mayor wanapinga kuwa hamisha wamachinga kabla ya kuandaa mazingira ya wanakopelekwa! INAONEKANA HAUFATILII MAMBO!

hata wewe hujui chanzo.uandhani chanzo ni kuhamishwa?!!!
 
HII HABARI HAPO CHINI NI MAELEWANO BAINA JIJI NA WAMACHINGA !!





Machinga kuendelea kutesa Mwanza

By
Dullonet Tanzania
– January 25, 2011Posted in: Biashara na Uchumi





Na Daud Magesa, Mwanza

HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza imeridhia wamachinga waendelee kufanya shughuli zao katika baadhi ya maeneo katikati ya jiji.Mvutano baina ya halmashauri hiyo na wamachinga ulimalizika Alhamisi wiki iliyopita baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Abass Kandoro, na viongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza kukutana na uongozi wa wamachinga na kufikia makubaliano hayo.

Muafaka wa kufanyia shughuli zao katikati ya jiji ulifikiwa kwa amani na utulivu baada ya uongozi wa serikali ya mkoa, halmashauri ya jiji kukutana na viongozi wa wamachinga na kubainisha maeneo yanayofaa kwa wafanyabiashara hao bila kuchafua mazingira wala kuvunja sheria zilizopo.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji wa halmashauri ya jiji, Bw. Henry Matata alikiri kufikiwa kwa muafaka kati ya uongozi wa jiji na wamachinga hao, muafaka ambao uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Abass Kandoro.

Bw. Matata alisema maeneo sita yameruhusiwa wamachinga kuyatumia kufanyia biashara zao na kuyataja kuwa ni Mirongo Community Centre na Mlango Mmoja ambako kuna baadhi ya wamachinga wameendelea kufanyia shughuli zao tangu yalipotengwa.

Magari yote yaliyokuwa yakitumia eneo la Mirongo Community yamezuiwa kutumia eneo hilo tena, huku Mlango Mmoja ambako mmoja wa maofisa wa jiji aliyeziba choo na kukigeza vyumba vya maduka akiamuliwa kuyavunja na kuacha kitumike kwa
wafanyabiashara.

Maeneo mengine yaliyoruhusiwa kutumiwa na machinga ni pamoja na eneo la soko la vitunguu (nje ya soko kuu), Miti Mirefu (nyuma ya nyumba ya wageni ya Zimbabwe) na Mkuyuni kuelekea relini. Eneo jingine ni la mtaa wa Makoroboi (kuacha eneo la Misikiti ya Wahindi)

Matata alisema kuwa kulingana na makubaliano hayo wamachinga hawataruhusiwa kufanyia biashara zao katika barabara kuu za Nyerere, Kenyatta, Pamba, Lumumba, Nkuruma, Rufiji, Uhuru na nyinginezo kama ambavyo wamekuwa wakifanya kabla ya mazungumzo hayo kufanyika umpya mwishoni mwa wiki.

Vile vile wamachinga wanaweza kwenda kufanyia biashara zao katika maeneo ya Buhongwa, Sabasaba, Igoma, Igogo, Nyakato NHC, Kitangiri, Kiloleli, Kayenze, Mkolani na Magomeni Kirumba ambayo awali walipangiwa.

Mbali na Kandoro kuongoza zoezi hilo ambalo lilizua vuta nikuvute kati ya wamachinga na uongozi wa jiji, Meya wa Jiji Bw. Josephat Manyerere na Naibu wake Bw. Chales Chinchibera, walihudhuria shughuli hiyo, wakiwemo Wabunge wa majimbo ya Nyamgana na Ilemela, Bw. Ezekia Wenje na Highness Kiwia na Mwenyekiti wa Mipango Miji Bw. Matata na baadhi ya Madiwani.

Source: Majira
 
iliwahi semwa hapa kuwa jeshi hili (machinga) linalokua kila uchao na kuachwa na mamlaka husika kwa sababu za kisiasa kwamba ni "time bomb" na kuwa ni wakti tu litalipuka, tatizo ni sikio la kufa... Tunisia ni machinga mmoja alilipuka, sote twajua kilichofuatia. Mungu ibariki TZ.
 
Wadau nimedokezewa habari ya kuwa kuna vurugu kubwa jijini mwz kati ya polisi na machinga. Yeyote mwenye habari atuletee hapa jamvini.
 
sasa tuna sababu za kutosha kuandamana nchi nziama
 
Back
Top Bottom