Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

Tatizo ni kwamba serikali haitaki kuwaandalia sehemu nzuri ya biashara yenye wateja. Hapo kati kati ya mji ndiyo kwenye wateja, kama ambavyo VIONGOZI WA SERIKALI HAWATAKI NAO KWENDA DODOMA kwa sababu kuna njaa ikilinganishwa na Dar es Salaam, kwanini wawalazimishe wamachinga kwenda kwenye njaa. Tafakari Chukua Hatua.
 
FaizaFoxy my dear, lini utakuwa positive? Hata kama jiji linaongozwa na cdm lakini
haiwafanyi polisi kuua watu. This is very bad!

unamvimbisha kichwa huyu mpuuzi.....yuko kwenye mzunguko wa mwezi
 
msafara wa baniani na biashara zinaingilianaje..... kwani hizi biashara si zinatozwa kodi ..... wafunge ili washindwe kulipa kodi ..... hii nchi bana ..... !
 
itakuwa kwa ajili ya jamaa flani hivi maana anatoka dini inayosali humo msikitini

Hapana. Kilichoshambuliwa sip Msikiti wa kiislamu, ni hakalu (au msikiti) wa wa-baniani. Wakati vurugu zinatokea wahindi walianza kuwajia juu wamachinga... acha veve, acha veve... hawakujua kuwa wenzao washapoteza temper...
 
Kama imelazimu, silaha za moto zitatumika. Hilo ni jambo la kawaida.
Muhimu ni kulinda amani ya walio wengi dhidi ya wakorofi wachache.
Tuwaunge mkono vyombo vya usalama kwa usalama wetu, si kulaumu kwa haja potofu.

WEWE mzima kweli? kwani hao machinga walikuwa wanafanya biashara au walikuwa wanavunja amani. leo wao kesho wewe. shwaini.

hivyo ni vyombo vya usalama au vya uhasama?
 
CHANZO CHA VURUGU NI HIKI

Chanzo cha vurugu ni wamachinga kukatazwa kufanya biashara leo katika eneo la Makoroboi ambapo KIONGOZI MKUU WA KIDINI WA BANIANI angepita leo kuelekea katika hekalu lao.

Habari zinasema kuwa wamachinga hao walipewa taarifa kuwa wasifungue biashara zao leo kwa sababu ya msafara huo, hata hivyo walipinga kwa kusema kuwa kama ni misafara inapita mingi na haiathiriwi na biashara zao

Kufika leo asubuhi wamachinga walikuta eneo zima limezungukwa na askari wenye silaha ambao hawakuruhuru wamachinga hao wapasogelee

Vurugu baina ya wamachinga na askari zilianza kidogo kidogo lakini baada ya muda umati wa watu uliendelea kuongezeka, ndipo askari walipoanza kutumia gia kubwa zaidi ya mabomu ya machozi

Vurugu zipokolea zaidi askari walianza kutumia risasi za moto, na hapo raia mmoja alipigwa risasi na kufariki

Kufariki kwa raia huyo mmoja ndiko kulikozua balaa zaidi kwani vurugu zilisambaa zaidi na kuwahusisha wahindi na biashara zao ambazo zilishambuliwa vibaya sana, magari yakichomwa moto, maduka yalivunjwa huku raia wakiendelea kukabiliana na askari, na hadi wakati, watu wengine kadhaa wamesahpigwa risasi na kufariki

Mungu ibariki Tanzania
Kwa hiyo sasa huyo Baniani kapita salama juu ya damu ya watu tujuvye tafadhali.
 
Tumegeuka watumwa kwenye nchi yetu hivi kikwete, kakobe au Shabani Simba akienda nchi za wenzetu huwa masoko yanafungwa ili apite...
 
kuwa wanaodai ati wahindi wamehonga hela kwa wakurugenzi wa jiji ili wamachinga waondolewe na biashara za wahindi ziendelee vizuri hali hiyo ndo imesababisha vurugu kubwa leo hadi kufikia kuchoma moto magari kadhaa ya mmoja wa wahindi hapa jijini na kupora mali, hali hii itahusishwa kisiasa tu na watu wengina maana jiji la Mwanza linakaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo.
 
Kama imelazimu, silaha za moto zitatumika. Hilo ni jambo la kawaida.
Muhimu ni kulinda amani ya walio wengi dhidi ya wakorofi wachache.
Tuwaunge mkono vyombo vya usalama kwa usalama wetu, si kulaumu kwa haja potofu.

an enemy of God and infidel indeed
 
Akili za watawala zimefika ukingoni,kwani kuzuia machinga mpaka risasi na mabomu zitumike?...Wameamua kutawala kwa mabavu baada ya kujua kuwa hawakubaliki kwa walio wengi....
 
....haya mambo yataisha lini!!!
Siku utakapoacha kujificha nyuma ya kee bodi na kwenda frontline

..............................................................
avatar32154_1.gif
 
Akili za watawala zimefika ukingoni,kwani kuzuia machinga mpaka risasi na mabomu zitumike?...Wameamua kutawala kwa mabavu baada ya kujua kuwa hawakubaliki kwa walio wengi....
Mkuu, inasikitisha sana kuona serikali inatumia risasi za moto kama ngao yao lakini haya mambo yana mwisho ..Arusha tuliambiwa, tulipigwa risasi kwasababu tulikuwa tunaenda kuvamia kituo cha polisi na kulikuwa na silaha nzito, Mbeya wanachi walipochoma lori na kupigwa risasi waliambiwa ni wahuni, Nyamongo tuliambiwa ni majambazi na leo Mwanza sijui tutaambiwa je...
 
Watasema wazurulaji chama tawala kina vocabulary ya maneno special kwa matukio kama haya subiri utawasikia.
 
kwa nini watumie live ammunations,je jeshi letu wameshindwa kutumia rubber bullet (kama kulikuwa na ulazima) na water canon kama lengo lao ilikuwa ni kutawanya watu, mpaka lini damu ya watu wasio na hatia itaendelea kumwagika wakati wauwaji(jeshi la polisi) hawachukuliwi hatua yoyote,ziko wapi haki za binadam, wapi misingi na utawala bora sheria......
 
Back
Top Bottom