Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

Kayoka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
2,239
1,884
Kuanzia saa 2 hii asubuhi kumezuka mapigano kati ya police na machinga maeneo ya katikati ya jiji watu wanakimbizwa huku na kule.

Maduka yamefungwa, sokoni hakuendeki! Watu watano wameripotiwa kupigwa risasi na wawili kati yao wameripotiwa kufa, magari yamechomwa moto huku nako misikiti ya kati imeharibiwa sana.

Source: Mimi mwenyewe nimeona

==============
UPDATES:

Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.
vurugu4.JPG

Kamanda Sirro akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani.


vurugu13.JPG

Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.


vurugu12.JPG

Friji ikiteketea..

Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market nakisha kuchoma friji ilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuiteketeza.

vurugu3.JPG

Kusanyiko la shaka-shaka.


vurugu5.JPG

Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza haliiliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa..


vurugu7.JPG

Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.



Kona ya kuingia barabara ya Msikiti wa Ijumaa kutokea barabara ya Nyerere risasi zimelia nao wananchi wakikimbia kujihami na mabomu ya machozi.


vurugu6.JPG

Market Street hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji
.

vurugu14.JPG

Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.


vurugu10.JPG

Machinga na jiwe lake mkononi tayari kulirusha..Hali imekuwa tete kwa watanzania wenye asili ya kiasia kwani imekuwa wakionekana tu wanafanyiwa kitu mbaya.


vurugu9.JPG

Ni moja kati ya hasara zilizojitokeza kwa jengo hili ambalo wamiliki wake ni watanzania wenye asili ya Kiasia lililoungana na msikiti wa Hindu.


vurugu1.JPG

Mpaka sasa hivi ikiwa ni saa 6:15 barabara ya Nyerere haijatulia kwani kuna umati mkubwa wa watu eneo hili mawe yakirushwa nayo mabomu ya machozi yakisikika mitaa ya Makoroboi, Alhamini, Maketi na Msikiti wa Ijumaa kuwatawanya waandamanaji.
 
Kisa nini?, machinga wanazuiwa kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi au?, endelea kutujuza.
 
kisa machinga wanazuiwa kufanya biashara maeneo ya mjini kama vle makoroboi wanaambiwa waende nje ya jiji ambako hakuna wateja. Kwa sasa hali ni mbaya sana watu wanakimbia, njia zote zmefungwa magari hayaendi mjini. Milio ya risasi kila kona, police wanatembeza virungu, watu wanavuja damu..!?
 
Mkuu tujeze nasikia hali ni mbaya sana huko.. Nimeongea na jamaa huko.
 
watu3 wamepigwa risasi na kufariki papohapo katikati ya jiji la Mwanza.Askari wanafyatua risasi za moto na mabomu ya machozi kukabiliana na wamachinga.K

atikati ya jiji ni taharuki na hofu,watu wanakimbia huku na kule yaani kiujumla hali ni mbaya na ukizingatia damu imemwagika! HAKUNA AMANI! Kunaduka maeneo ya soko kuu linawaka! Makoroboi hakufai. Kazi mjini zimesimama.

Taarifa zaidi baadaye.

RAI YANGU:

Mh.Wenje ahirisha bunge la leo wapigakura wako huku wanakufa wakitetea mkate wao. Mh.Kikwete muondoe huyu mkurugenzi W.Kabwe.
 
Yap wanafanya mpaka barabarani....Maeneo rasmi hawaendi....wanasema hakuna wateja..na wateja wakiwakosa sehemu ambayo si rasmi naamini watawafata kuliko rasmi...kitengeneza jiji yataka moyo.
 
poleni wana Mwanza.nimeongea na jamaa zangu wanasema hapakaliki vurugu tupu.mabomu yatasaidia hata siku moja katika nchi hii.
 
Hilo la misikiti vp?
ni kweli msikiti wa masingasinga na baniani iliyopo hapa makoroboi imepigwa mawe na kurushiwa makaa ya moto. Kisa wahindi walikuwa wanasema wacha veve vacha veve.
 
Nimesikitika sana kwa taarifa hizo........na mbaya sana viongozi wetu hawajali. Lakini nasikia harufu ya ukombozi kwa taifa hili.......muda mchache ujao. Mungu yuko upande wetu. Poleni sana ndugu zangu wa mwanza.
 
habari zaidi zinasema idadi ya walipigwa risasi na kufa hapo hapo ni watu wa5. Nashindwa kuwapa pcha kwani nipo na sehemu mbaya.
 
Wadau kunataarifa za machafuko katika jiji la mwanza kati ya machinga na dola asubuhi hii.mwenye habari zaidi atujuze.
 
Back
Top Bottom