Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

Vurugu Mwanza: Wamachinga Vs. Jiji - Damu yamwagika

wenye taarifa ya kilichopelekea vurugu watujuze tafadhari
 
Hii kitu inahusiana na maelezo ya Dk Slaa ile juzi? nakumbuka member mmoja DAUGHTER alimwambia Dk Slaa kwamba jiji la mwanza chafu,vioski kila kona, taka nyingi, maachinga kibao, nae akafanya follow-up na akaongea na watendaji na akatupa update!! Vp hii ya leo ina mahusiano yoyote na Ile ya Dakta?? safisha JIJI??


kwa taarifa yako jiji la mwanza kwa miaka 6 mfululizo linashika namba moja kwa usafi.......uliza wakwambie
 
Nakushangaa unauliza jibu! hivi hujui kuwa meya na madiwani wengi wa mwanza ni cdm? unategemea nini?
Kuna watu wengine ukiwajibu unaweza kula ban bure. Na hivi mamod wote sasa hivi na wanaCCM? Kazi tunayo.
 
kuna tetezi kua watu watatu wamepigwa risasi na polisi mwanza eneo la makoroboi.
 
kwa taarifa yako jiji la mwanza kwa miaka 6 mfululizo linashika namba moja kwa usafi.......uliza wakwambie

Historia iko wazi jiji la mwanza lilikuwa na amani wakati wa CCM, hawa CDM wameingia na visasi pia madiwani wao wamegeuza ofisi za jiji vijiwe vya kuzungumzia masuala ya CDM
 
mayoka picha tafadhali......tuwekee
 
Historia iko wazi jiji la mwanza lilikuwa na amani wakati wa CCM, hawa CDM wameingia na visasi pia madiwani wao wamegeuza ofisi za jiji vijiwe vya kuzungumzia masuala ya CDM
Mkuu hili suala la umachinga ni uongozi mbovu wa serikali yetu ya CCM, hivi kila mtu akiwa machinga ni nani atakayenunua vitu, machinga wamekuwa wengi yaani ndio ajira, hii inafanya watu wengi wanakuwa hawana uhakika wa mkate wao wa kila siku. Mkuu viwanda vyote vya Mwanza vipo wapi, mhh kuna ngozi, kuna samaki pamba ipo..., hivi serikali inashindwa kuhakikisha kuna viwanda ili kuongeza ajira kuliko kila mtu kuwa middle man wa kuuza bidhaa za china?
 
Acha uchakavu wa akili wewe,kwani meya na madiwni ndo wanao ua watu??? hujui kuwa mkurugenzi ndo tatizo??


Nakushangaa unauliza jibu! hivi hujui kuwa meya na madiwani wengi wa mwanza ni cdm? unategemea nini?
 
Historia iko wazi jiji la mwanza lilikuwa na amani wakati wa CCM, hawa CDM wameingia na visasi pia madiwani wao wamegeuza ofisi za jiji vijiwe vya kuzungumzia masuala ya CDM

Hakuna chama cha siasa hapa nchini kinachoitwa CDM....Acheni uvivu wa kufikiri!
 
Hivi ni lini wa-Tanzania tutaanza kufuata sheria? Ni mpaka tufukuzwe na polisi hadi kupigwa risasi? Inatakiwa elimu ya kutosha kuwafundisha wamachinga kuwa hawawezi kufanya biashara mahali popote katika miji.
.Kwenye suala ya kukusanya kodi libaki serikalini, ila masuala ya elimu na ajira kwa vijana wetu tuiombe serikali ya Kenya itusaidie hayo.POLENI VIJANA WA MWANZA MNAOUAWA MKITAFUTA NAMNA ANGALAU YA KUPATA MLO MMOJA TU KWA SIKU. SERIKALI YA IK KWA KIPINDI CHAKE CHA MIAKA SITA INAONGOZA AWAMU ZILIZOTANGULIA KUWAUA RAIA WAKE KWA RISASI. HII NI SIFA MOJAWAPO ATAKAYOKUMBUKWA NAYO JK..
 
wenye taarifa ya kilichopelekea vurugu watujuze tafadhari

Kiukweli Mwanz hapakaliki,watu ni mbiombio huku na kule,magari hayafuati tena sheria za barabarani kwa kukimbia vurugu,magari yanapigwa mawe,magari matatu ya wahindi yamechomwa moto,bidhaa nyingi za wahindi zmechomwa moto katikati ya barabara, Jumba la kifahari la wahindi limevunjwavunja vioo,watu wapigwa mawe na kukimbizwa,biashara zot zmefungwa.Hivi sasa ni mpambano wa askari na wamachinga unaendelea,wamachinga wanataka kuchoma msikiti,askari wameuzingira usichomwe. Chanzo ni wamachinga kufukuzwa ktk maeneo ya mji.Sjajua msikiti na wahindi wameingiaje ktk mkasa huu.tutafuatilia zaidi
 
HOFU kubwa imetanda jijini hapa baada ya kundi la wafanyabiashara ndogo maarufu kama Wamachinga, kuvamia mitaa na kufanya fujo, huku wakitaka wafanyabiashara wenye maduka kufunga biashara zao.

Fujo hizo zilizofanyika juzi zilikwenda sambamba na kurusha mawe na kuzuia magari kupita maeneo walimopita wao wakiwa njiani kwenda ofisi za Mkurugenzi wa Jiji. Hali hiyo ilitokana na hasira waliyokuwa nayo, baada ya kuondolewa kwenye maeneo waliyopangiwa juzi kuuzia bidhaa zao.

Tafrani hiyo ilianza saa tatu asubuhi baada ya askari wa mgambo wa Jiji wakishirikiana na polisi, kuwaamuru Wamachinga hao kufunga biashara zao, jambo ambalo awali walitii.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye, upepo uligeuka kwani Wamachinga hao walipita madukani na kuwaamuru wenye maduka kuyafunga au wajiandae kwa vurugu.

Wamachinga hao walidai, kwamba walitaka haki sawa itendeke kwa kufunga biashara zote, badala ya kuzuia watu wa kada fulani huku wengine wakiachwa wafanye shughuli zao, hasa wenye biashara ya maduka.

"Tunasema lazima waturudishe maeneo yetu tuliyopangiwa juzi na Mkuu wa Mkoa Abbas Kandoro, ni kwa nini Jiji watuondoe? Mpaka kieleweke," walisikika Wamachinga hao wakisema huku kundi kubwa likipita Barabara ya Nyerere kuelekea Barabara ya Nkrumah.

Madai ya Wamachinga hao ya kutaka warudishwe Makoroboi, Miti Mirefu na Mirongo yalipingwa na Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe, akisema lazima wahame maeneo hayo kwa kuwa yako katikati ya Jiji.

Jana wakitembea mguu kwa mguu na Kandoro, Meya wa Jiji la Mwanza, Josephat Manyerere na wakuu wengine wa idara walibaini maeneo yanayofaa na kuwapangia Makoroboi, Vitunguu Soko Kuu, karibu na Nyumba ya kulala wageni ya Zimbabwe na Mirongo Community Centre.

Hata hivyo, Kabwe alishikilia msimamo kuwa, mwenye mamlaka ya kupanga wafanyabiashara hao ni ofisi yake na si ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya.

Alisema ni marufuku wafanyabiashara hao kufanyia biashara zao katikati ya Jiji akiwataka kuhamisha mara moja vizimba vya biashara zao na kwenda maeneo waliyopangiwa kisheria.

Hadi gazeti linaondoka ofisi za Mkurugenzi wa Jiji Wamachinga hao wapatao 500 walikuwa wakitaka kuuona uongozi wa halmashauri, ili washinikize kurudishwa kwenye maeneo walikoondolewa.
 
Tatizo la Mwanza ni kubwa sana kuliko linavyochukuliwa, sio tatizo la kuisha haraka. karibu kila siku kuna wahamiaji wengi sana wanaohamia katika jiji hili kujaribu bahati zao, na hasa hii kutokana na utajiri mkubwa sana uliopo mkoani Mwanza, lakini ukiangalia kwa undani zaidi hawa wananchi wa kawaida tu sidhani kama wananufaika na hilo. Mwanza kuna watu wachache ambao ni matajiri hasa na wengine ni maskini wa kutupwa, mfano wahindi, na hili litakuja kuleta mtafaruku mkubwa sana huko mbeleni hasa suala la ubaguzi wa rangi. nachowaomba CDM waangalie mpango wa muda mrefu utakaofanikisha sekta ya ujasiliamali kwa jiji la mwanza, sababu jiji linakua kila siku na idadi ya watu inaongezeka kila siku.
 
Chanzo cha vurugu ni wamachinga kukatazwa kufanya biashara leo katika eneo la Makoroboi ambapo KIONGOZI MKUU WA KIDINI WA BANIANI angepita leo kuelekea katika hekalu lao.

Habari zinasema kuwa wamachinga hao walipewa taarifa kuwa wasifungue biashara zao leo kwa sababu ya msafara huo, hata hivyo walipinga kwa kusema kuwa kama ni misafara inapita mingi na haiathiriwi na biashara zao

Kufika leo asubuhi wamachinga walikuta eneo zima limezungukwa na askari wenye silaha ambao hawakuruhuru wamachinga hao wapasogelee

Vurugu baina ya wamachinga na askari zilianza kidogo kidogo lakini baada ya muda umati wa watu uliendelea kuongezeka, ndipo askari walipoanza kutumia gia kubwa zaidi ya mabomu ya machozi

Vurugu zipokolea zaidi askari walianza kutumia risasi za moto, na hapo raia mmoja alipigwa risasi na kufariki

Kufariki kwa raia huyo mmoja ndiko kulikozua balaa zaidi kwani vurugu zilisambaa zaidi na kuwahusisha wahindi na biashara zao ambazo zilishambuliwa vibaya sana, magari yakichomwa moto, maduka yalivunjwa huku raia wakiendelea kukabiliana na askari, na hadi wakati, watu wengine kadhaa wamesahpigwa risasi na kufariki


Mungu ibariki Tanzania
 
Tatizo la Mwanza ni kubwa sana kuliko linavyochukuliwa, sio tatizo la kuisha haraka. karibu kila siku kuna wahamiaji wengi sana wanaohamia katika jiji hili kujaribu bahati zao, na hasa hii kutokana na utajiri mkubwa sana uliopo mkoani Mwanza, lakini ukiangalia kwa undani zaidi hawa wananchi wa kawaida tu sidhani kama wananufaika na hilo. Mwanza kuna watu wachache ambao ni matajiri hasa na wengine ni maskini wa kutupwa, mfano wahindi, na hili litakuja kuleta mtafaruku mkubwa sana huko mbeleni hasa suala la ubaguzi wa rangi. nachowaomba CDM waangalie mpango wa muda mrefu utakaofanikisha sekta ya ujasiliamali kwa jiji la mwanza, sababu jiji linakua kila siku na idadi ya watu inaongezeka kila siku.

Shomari upo sahihi kabisa, katika miji inayokuwa kwa kasi ya ajabu Africa au duniani kwa ujumla Mwanza ipo juu. Kwa Afrika ni ya kwanza. Maelezo yako yapo sahihi hasa ukizingatia sera mbofu mbofu za MAGAMBA
 
vurugu4.JPG
 
Hivi ni lini wa-Tanzania tutaanza kufuata sheria? Ni mpaka tufukuzwe na polisi hadi kupigwa risasi? Inatakiwa elimu ya kutosha kuwafundisha wamachinga kuwa hawawezi kufanya biashara mahali popote katika miji.

Sidhani kama tunawatendea haki wamachinga kama tukianza kuwalaumu moja kwa moja, kwani eneo hilo halikukatazwa kisheria kufanya biashara, bali walizuiwa ili msafara wa kiongozi wa kidini wa wa-baniani apite...
 
Back
Top Bottom