Malori marufuku mchana Mwanza

Malori marufuku mchana Mwanza

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,430
Reaction score
46,158
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakili Kiomoni Kibamba amesema magari makubwa hayatakuwa yakiruhusiwa kushusha mizigo katikati ya Jiji la Mwanza wakati wa mchana, hatua inayolenga kupunguza msongamano wa magari na kuwezesha Wananchi kufanya shughuli zao kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa zoezi la usafi katika eneo la Soko Kuu Jijini Mwanza, Wakili Kibamba amesema magari hayo yatatakiwa kuingia na kufanya shughuli za upakuaji wa mizigo kuanzia saa tatu usiku ili kuondoa usumbufu kwa Watumiaji wa barabara.

Aidha, amewataka Wafanyabiashara wadogo wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa barabara kurejea kwenye maeneo waliyopangiwa ili kuruhusu barabara za katikati ya jiji kubaki wazi na kupunguza msongamano.

Pamoja na hilo, amewataka Wamiliki wa magari kuacha kuyaegesha pembezoni mwa barabara, akitolea mfano eneo la Barabara ya Liberty na maeneo mengine ya katikati ya Jiji ambayo yanapaswa kubaki wazi.

Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuboresha mazingira ya Jiji, usafi na mtiririko wa shughuli za kiuchumi.
 
Hata Dar yanatakiwa kupigwa marufuku Kupiga kazi mchana, yanasabanisha mkwamo bila sababu
 
Wazo langu kwanini Manispaa wasitenge maeneo maalumu kama bandari kavu iwe magari makubwa ya mizigo yanashushia hapo kisha wafanyabiashara na watu wengine wawe wanakuja chukua hapo hii itasaidia kupunguza msongamano na kero pia itasadiia halmashauri kupata mapato, wanashindwaje kutumia changamoto kuwa fursa
 
Back
Top Bottom