Kuanzia saa 2 hii asubuhi kumezuka mapigano kati ya police na machinga maeneo ya katikati ya jiji watu wanakimbizwa huku na kule.
Maduka yamefungwa, sokoni hakuendeki! Watu watano wameripotiwa kupigwa risasi na wawili kati yao wameripotiwa kufa, magari yamechomwa moto huku nako misikiti ya kati imeharibiwa sana.
Source: Mimi mwenyewe nimeona
==============
UPDATES:
Leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi kumezuka vurugu jijini Mwanza kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi Mwanza kwa wafanyabiashara hao kudai kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.
Kamanda Sirro akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani.
Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.
Friji ikiteketea..
Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market nakisha kuchoma friji ilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuiteketeza.
Kusanyiko la shaka-shaka.
Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza haliiliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa..
Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.

Kona ya kuingia barabara ya Msikiti wa Ijumaa kutokea barabara ya Nyerere risasi zimelia nao wananchi wakikimbia kujihami na mabomu ya machozi.
Market Street hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji.
Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.
Machinga na jiwe lake mkononi tayari kulirusha..Hali imekuwa tete kwa watanzania wenye asili ya kiasia kwani imekuwa wakionekana tu wanafanyiwa kitu mbaya.
Ni moja kati ya hasara zilizojitokeza kwa jengo hili ambalo wamiliki wake ni watanzania wenye asili ya Kiasia lililoungana na msikiti wa Hindu.
Mpaka sasa hivi ikiwa ni saa 6:15 barabara ya Nyerere haijatulia kwani kuna umati mkubwa wa watu eneo hili mawe yakirushwa nayo mabomu ya machozi yakisikika mitaa ya Makoroboi, Alhamini, Maketi na Msikiti wa Ijumaa kuwatawanya waandamanaji.
Usalama wa Taifa unaanza kwa hatu moja kama hii hapa,Jana tarahe 6/07/ nilichangia thread ya
Bungeni kumechachamaa,Msigwa awambia ukweli Usalama wa Taifa kuwa ni usalama wa CCM.[Bofya]. nikasema Watanzania Nchi yao kuwa kwenye hati ya usalama wa Taifa hatarini sio mpaka uhaini,bali inaanza kwa picha kama hii,vijana hawana kazi,wanapojishikisha mamlaka zinakuja kuwakulupua,na kama binadamu anapokosa hatima ya kuwa atakula nini na chakula ni uhai,basi uwa ana cha kupoteza kinachofuata ni kanuni ya msituni [Survival of the fittest],ambayo kwa ulimwengu wa sasa si sahihi kwa kuwa binadamu amestaarabika na kwa kuwa tunaishi kama binadamu wenye utashi kanuni hiyo,inakuwa controlled na vyombo muhimu vya umma kuleta haki sawa kwa watu wote.
Na kwa Nchi yoyote Usalama wa Taifa ndio msimamizi sahihi wa kuakikisha kanuni hii HAITUMIKI vibaya na baadhi ya RAIA dhidi ya Raia wengine.Nilisema vijana watakapokosa kazi kinachofuata ni hayo yanayotokea Mwanza,yaani HAWANA UHAKIKA NA UHAI WAO TENA.Kwa gharama yoyote watatafuta nafais ya kuwa na UHAKIKA wa Maisha yaani UHAI wao na vizazi vyao vijavyo.
Na watakapo pata mwanya mzuri wa kuimarika watawasaka mmoja baada ya mmoja ,nyumba kwa nyumba,wale wote walioshiriki kuuza na kukwapua mali yao ya umma.Na ole wako uwe ni mtu ambae jamii imekuwa ikikutaja kwenye taarifa za waliokwapua mali ya umma,wewe na familia yako na jamaa zako mtaingia hatiani kwa hukumu ya umma.Haya si Maneno yangu hii ni kanuni ya maaumbile toka zama hizo,Mapinduzi ya Ufaransa ,Mapinduzi ya umma ya Nchi za Kiarabu sasa hivi, ni
kanuni ya what goes around comes around.Historia zipo jamani kwanini hatuendeshi nchi japo kwa kujifunza toka kwenye historia.
Mwalimu amesema kwenye kitabu chake cha
Man and Development,
Maskini wakiwa wengi uhai wa
Matajiri uko hatarini. Haya ni maneno ya Mtu ambae Watanzania wamempa jina la Baba wa Taifa.Tuyaheshimu maneno hayo.
Wahindi wa Mwanza wamewindwa kuibiwa,kuchomewa ,kupigwa n,k.ndio ni Watanzania kama Watanzania wengine,pengine huyo Mhindi atakae athirika au ameadhirika na tukio hili au lile jamani amekuwa raia mwema na mtenda haki kwa Watanzania wenzie. Ila kwa kuwa kuna baadhi ya Wahindi wenzie kwa kutumia ujanja wa kuwa na ufahamu [Exposure] ya kimataifa wameamua kulihujumu Taifa kwa kushirikiana na Watawala wasio onekana kwa dhahiri kwenye wigo wa wizi,basi hukumu yote ya UMMA [Ambayo mara nyingi ndio hukumu kali kuliko mahakama yoyote ya sheria katika Nchi yoyote ile] inchukua mkondo wake.
Tufike sehemu Taifa mbele jamani,tujifunze kupitia Mataifa mengine kama Misri, Tunisia,Yemenn n.k. Ndio tutateseka sana pengine Watanzania wengine watapoteza maisha lakini dhambi kubwa sana hata kwa MUNGU itakuwa dhidi ya viongozi aliwowapa dhamana kupitia binadamu wenzao wenye imani tofauti tofauti kukuchagua wewe kiongozi kuwaongoza.Kiongozi utakuwa na hukumu ya wanadamu na hukumu ya Mungu,pia utaacha kizazi chako kwenye utando wa dhambi juu ya dhuluma ambayo itawaandama wao na watoto wao.
Ni ufahari gani kuishi kitajiri miaka kumi au ishirini ya kiduniani, kisha kuacha watoto wako na kizazi chako kwenye maisha choka mbaya na lawama za kizazi na vizazi.
USALAMA WA TAIFA KUWA NA HATIHATI UNAANZIA HAPA.
Sio jukumu la usalama kutafuta wahusika wa tukio hilo,hiyo ni kazi ya Police.Kazi ya USALAMA WA TAIFA ni kuijiuliza na kutafuta majibu ni kwani na kwa vipi Umma huo umefikia hatua hiyo ya maamuzi hayo.Maswali ya Msingi ya kujiuliza
1: Nini Chanzo?
2: Nani wanahusika katika swala zima hilo [Wananchi,Serikali,Municipal,Mtu binafsi,Polisi,nk]?
3: Hatua zipi zilizopatwa kuchuliwa toka chanzo cha mgogolo mpaka hatua ya tukio?
4: Nani kasimama upande upi kati ya Umma na huyo ambae umma unaghadhabu nae juu ya mgogolo?
5: Waliohadhilika kabla na baadaya ya mgogolo?
6: Yupi anastaiki tuzo juu ya mgogolo huo kabla ya tukio na hata baada ya tukio?
7: Kisheria tatizo lilikuwa liko kwenye ngzi ipi na maamuzi gani yalikwisha tolewa
8: Watendaji wana uelewa gani juu ya maamuzi yao kulinganisha na utashi wa umma?
9: Je Umma unahaki na kama si haki,Je Umma ni zaidi au walio upande tofauti na umma ndio zaidi.[Ustawi]?
10: Kuna hujuma, Rushwa,au upendeleo wowote kwenye tukio zima?
11: Au je ni haki imecheleweshwa mpaka hatua ambayo umma umeamu kuchukua sheraia mkononi?
12: Nani waathirika wa tukio zima kabla na baada ya tukio?
13: Nani kawajibika wapi na maamuzi yake yamechangia nini katika swala zima kabla na baada ya tukio hili?
14: Kiwango gani cha nguvu au pingamizi kilitumika kabla na bahada ya tukio zima [Matumizi ya vyombo vya Dola,kuzuia]?
15: Je wadau wa tukio hili yani stakeholders walipewa nafasi sawa?
16: Jambo hili liko kwenye hatua [Level] gani kimaamuzi,Wilaya ,Municipal au Taifa
12: Na maswali mengineyo lukuki yenye nia ya kuleta ustawi bora wa hao wananchi wenye kuchukua sheria mkononi.