Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,221
WATANZANIA waliopo ndani na nje ya nchi wametakiwa kuonesha uzalendo na kushirikiana kwa pamoja kuupigia kura Mlima Kilimanjaro ili kuhakikisha unashinda na kuwa moja ya maajabu mapya saba ya dunia.
Mwito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Save Mt. Kilimanjaro, Ernest Olotu ambao ndiyo mwakilishi wa kamati ya dunia katika kutafuta maajabu mapya saba ya dunia.
Amesema, Julai 2007 jijini Lisbon,Ureno kulifanyika uzinduzi rasmi wa kutafuta maajabu saba mapya ya asili mpango ambao uliratibiwa na New Open World Co-operation(NOWC) chini ya taasisi isiyo kuwa ya kiserikali ya New 7 Wonders.
Amesema, taasisi hiyo ilitafuta vitu vya asili vinavyoweza kuwa maajabu mapya ya dunia katika nchi 220 duniani, ikiwemo Tanzania na kupata vitu zaidi ya 440 vya kushindanisha ili kupata maajabu saba mapya ya asili mbali na ya zamani.
Olotu amesema, katika mchujo wa kwanza vilibakia vitu 77, ambapo Julai 2009 kamati ya wataalamu ilikaa tena na kupitisha mchujo mwingine wakabaki washiriki 28 ambapo katika Afrika, nchi mbili ziliingia katika shindano hilo ikiwemo Tanzania (Mlima Kilimanjaro) na Afrika Kusini (Milima Meza).
Amesema, tangu 2009 kazi ya kupiga kura imekuwa ikiendelea duniani kupitia mtandao hadi Novemba 11 mwaka huu ambayondiyo itakuwa mwisho wa kutangaza rasmi maajabu hayo mapya.
"Cha kusikitisha mlima Kilimanjaro umekuwa ukipigiwa kura kwa wingi na wageni ambao sio Watanzania, walioufahamu mlima huu kwa kupitia vyombo vya habari, mtandao au waliowahi kuupanda¡ ni jukumu letu sasa Watanzania bila kujali itikadi zetu ,dini, rangi wala kabila kuupigia kura mlima huu," amesema.
Amesema, watu wanaweza kuingia kwenye tovuti ya www.new7wonders.com na kuupigia kura mlima huo pamojana maajabu mengine yatakayofanya yatimie saba...
(FROM HABARI LEO)... Mimi nimeshaupigia kura..bado wewe tu! Ni rahisi kuupigia kura. Tuonyeshe uzalendo! Asanteni!