TANAPA: Ripoti imebaini chanzo cha moto Mlima Kilimanjaro ni shughuli za kibinadamu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
23f73a79-4342-4e1b-9deb-7bcc3c3c65de.jpg

Kamishna William Mwakilema

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetoa ripoti ya kukamilisha uzimaji wa moto uliotokea kwenye maeneo ya Mlima Kilimanjaro huku wakibainisha kuwa taarifa za awali zimebaini kuwa chanzo cha moto ni shughuli za kibinadam.

Kitengo cha usalama cha TANAPA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama linaendelea na utafiti ili kubaini wahusika wa tukio hilo, tayari jalada la uchunguzi limefunguliwa kituo cha Polisi Moshi MOS/RB/9563) 2022 MOS/IR/877/2022.

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), William Mwakilema imesema shirika litachukua hatua stahiki kwa atakayebainika pasi shaka kuhusika na tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.

Imeelezwa kuwa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro ilipokea taarifa ya uwepo wa moto katika Bonde la Karanga (Karanga valley) saa 02:30 usiku, Ijumaa ya tarehe 21.10.2022. Taarifa hiyo ilitolewa na mwalimu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori – Mweka kutokana na eneo hilo kuonekana vizuri kutokea maeneo ya chuo.

TANAPA imeeleza kuwa zoezi la uzimaji wa moto lilianza kufanyika kuanzia 21/10/2022 hadi 28/10/2022 ambapo moto ulidhibitiwa katika maeneo mengi korofi.

Aidha, 29/10/2022 moto ulilipuka tena eneo la Korongo la Mto Karanga na kusambaa kuelekea maeneo ya Umbwe na Baranco kutokana upepo mkali uliosababisha kulipua mioto midogo iliyokuwa kwenye magogo na ardhini (kwenye mboji).

William Mwakilema.jpg

Kamishna William Mwakilema

Kamishna William Mwakilema amesema jitihada za uzimaji moto zimehusisha vyombo vya usalama Nchini ikiwemo Kamati ya Usalama ya Mkoa, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Jeshi la Uhifadhi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto, Jeshi la akiba, viongozi wa chama na serikali, wananchi pamoja na wadau wakiwemo wamiliki wa makampuni ya utalii (waongoza wageni na wapagazi).

Mbinu mbalimbali zilitumika katika kuzima moto zikiwemo kulinda miundombinu ya utalii dhidi ya moto na kutengeneza kinga ya moto ili kupunguza makali na kuuzima.

Moto wa Ubetu / Samanga
Aidha, amesema usiku wa 28/10/2022, moto mpya uliibuka kwenye msitu wa asili eneo la Ubetu / Samanga lililoko Wilayani Rombo. Kikosi cha Askari wa Jeshi la Uhifadhi na wananchi wa Rongai walifika eneo la tukio kwa ajili ya kuukabili.

“Moto huo ulidhibitiwa kwa siku mbili. Chanzo cha moto huo pia kinasadikika kuwa ni shughuli za kibinadamu,” anasema Kamishna William Mwakilema.

Moto wa Mandara karibu na Maundi Crater
Amesema jioni ya 29/10/2022, moto mpya uliwaka eneo la Mandara - upande wa Marangu na ulikuwa unasambaa kushuka kwenye msitu wa asili. Hata hivyo kufuatia upepo kubadili uelekeo mara kwa mara, moto huo ulianza kusambaa kwa kufuata uelekeo wa Kwa-Masheu na Mlima Kifinika.

Kamishna amesema chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana, ingawa inasadikika kuwa ni shughuli za kibinadamu. Juhudi za kuukabili moto huo zilifanywa na askari wa Jeshi la Uhifadhi, Jeshi la Akiba (Rombo na Longido), Jeshi la Polisi (mkoa wa Kilimanjaro) na TPDF. Moto huu uliweza kudhibitiwa tarehe 01/11/2022.

Madhara yaliyosababishwa na moto huo:
Ametaja madhara yaliyotokea kutokana na moto huo kuwa ni;

Kujenga hofu kwa wageni

Kuteketeza kilomita za mraba 34.2 za uoto wa asili wenye mimea aina ya Erica sp., Protea sp., Kniphonia thomsonii, Herichrysum sp, grasses, Bracken ferns (Aquillinum pteridium), Myrica salicifolia, Lobelia deckenii, mountain gladiolus na Senecio kilimanjarica (Kielelezo Na 4). Eneo hili ni sawa na 1.9% ya eneo zima la Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro yenye km2 1,712.

Uharibifu wa mandhari ya ukanda wa juu wa hifadhi

Kuleta taharuki kwa jamii ya watanzania na dunia kwa ujumla

Kuteketeza viumbe wadogo ambao uwezo wao wa kutembea ni mdogo wakiwemo mamalia wadogo


Changamoto zifuatazo zilijitokeza wakati wa kuzima moto;
Uzoefu mdogo wa uzimaji moto katika mazingira ya mlimani kwa baadhi ya wadau hususani ambao hawana uzoefu wa kupanda mlima na kufanya kazi kwenye maeneo yenye mwinuko mkubwa (high altitude)

Umbali mrefu wa maeneo yaliyoathirika, hivyo wazima moto kuchelewa kuyafikia

Kuwepo kwa kipindi cha ukame na upepo mkali kulichangia kwa kiasi kikubwa kusambaa kwa haraka kwa moto mlimani.

Kuwepo kwa makorongo makubwa ambayo ni vigumu kuyafikia kwa miguu hususani makorongo Karanga, Baranco, Umbwe, Lyamungo na Mweka

Kuwepo kwa mimea aina ya “Erica” inayoshika moto kwa haraka

Mlundikano wa mboji kwenye udongo iliyokuwa inahifadhi moto ardhini (underground fire)

Teknolojia hafifu ya uzimaji moto
 
Kwahiyo wameshamaliza kutoa taarifa yao!

Hakuna mikakati ama hatua za kukabiliana na changamoto walizokumbana nazo?

Inakuwa kama ajali za meli na ndege kwenye ziwa victoria.
 
Back
Top Bottom