Milima 10 mirefu duniani

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
MILIMA 10 MIREFU DUNIANI; HIZI NDIO NCHA ZA JUU KABISA ULIMWENGUNI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Saturday-04/06/2022
Kilimanjaro National Park Marangu Mtoni, Kilimanjaro Tanzania

Jana niliweka andiko kuhusu mlima Kilimanjaro, Mlima wa nne kwa urefu duniani, tulipata maswali mengi kuhusu Mlima Kilimanjaro na wadau kutaka kujua milima mingine iliyo mbele ya mlima Kilimanjaro.

Imetupendeza leo hii nakuletea orodha ya milima 10 mirefu zaidi duniani, katika list hiyo bara la Afrika limetoa mlima mmoja tu ambao ni Mlima Kilimanjaro unaoshika nafasi ya 4 kati ya milima 10 mirefu duniani.

Yes, hizi ndio ncha za juu Kabisa ulimwenguni, milima hii ndio vivutio vyenye upekee duniani, kwa bahati hiyo Tanzania imebahatika kuwa na ncha ya juu kabisa Afrika.

Hivyo basi ifuatayo ni orodha ya milima 10 mirefu duniani, tutaanza na namba 10 kushuka chini.

Ok, twende pamoja Sasa.....

10 Puncak Jaya.

Mlima Puncak Jaya au Piramidi ya Carstensz yenye urefu wa mita 4,884 ndio kilele cha juu kabisa cha Mlima Carstensz katika Safu ya Milima ya Sudirman ya nyanda za juu za kati magharibi mwa mkoa wa Papua, huko nchini Indonesia.

Mlima huu Puncak Jaya upo katika kisiwa cha New Guinea, huku mlima huo ukiwa na mwinuko wa 4,884 mita (sawa na 16,024 ft).

Ndicho kilele cha mlima mrefu zaidi kilichopo katika kisiwa Duniani.

Mtu wa Kwanza kupanda mlima huu alikuwa ni Colijn, Dozy, na Wissels mwaka 1936, kisha wakafatia wengine mwaka 1962 ambao ni Harrer, Temple, Kippax, na Huizenga

9 Vinson Massif.

Mlima Vinson Massif ndio mlima mrefu zaidi katika bara la Antaktika, ukiwa katika safu ya milima ya Sentinel, na safu ya Milima ya Ellsworth, ambayo yote kwa pamoja inasimama juu ya Rafu ya Barafu ya Ronne karibu na usawa aridhi wa Peninsula ya Antaktika.

Mlima Vinson Massif aligunduliwa mwaka 1958 na ndege ya Jeshi la Wanamaji wa Marekani, Mnamo January 1961, jina la Vinson Massif ulipewa na Kamati ya utafiti ya Marekani inayojihusisha na utafiti huko Antaktika inayoitwa US-ACAN.

Jina hilo la Vinson Massif limetokana na jina la mbunge wa Marekani kutoka jimbo la Georgia bwana Carl G. Vinson, ambae ndie aliyetoa msaada wa utafiti huko Antarctic.

Mlima Vinson Massif una urefu wa mita 4,892 sawa na futi 16,050.

Mlima huo ulipandwa mwaka 1966 na bwana Nicholas Clinch, ndio mtu wa kwanza kupanda Kilele cha mlima huo.

8 Pico de Orizaba.

Mlima Pico de Orizaba, au Citlaltépetl, ni mlima wa stratovolcano, ndio mlima mrefu zaidi nchini Mexico, na mlima wa tatu kwa urefu Amerika Kaskazini.

Una urefu wa mita 5,636 (futi 18,491), mlima huu upo kwenye mpaka kati ya majimbo ya Veracruz na Puebla.

Mlima Pico de Orizaba, ni mlima wa Volcano iliyo tulivu, mlipuko wa mwisho unatajwa kutokea katika karne ya 19.

Pico de Orizaba ni kilele cha pili maarufu cha volkeno duniani baada ya Mlima Kilimanjaro uliopo Afrika, nchini Tanzania.

Upandaji wake ulifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1848 na bwana F. Maynard pamoja na bwana William F. Raynolds.

7 Mlima Elbrus.

Mlima Elbrus ni mlima wa volkano tulivu (dormant volcano mountain) mlima huu upo katika safu ya milima ya Caucasus, huko ukanda wa Kabardino-Balkaria na Karachay-Cherkessia, nchini Urusi karibu na mpaka wa nchi ya Georgia.

Kilele chake ni cha juu zaidi katika safu ya milima ya Caucasus, na ndio kilele cha juu zaidi nchini Urusi.

Mlima Elbrus una urefu wa mita 5,642 (18,510 ft) juu ya usawa wa bahari, ni mlima wa asili ya volcano ulio juu zaidi katika Eurasia, yani ulaya na ukanda wa ulaya ya kati

Mlima Elbrus ina vilele viwili, vyote vikiwa ni volkeno tulivu (dormant volcano mountain), Kilele kirefu katika mlima Elbrus ni kile cha magharibi ambacho kina urefu wa mita 5,642 (18,510 ft).

Kilele cha pili ni kile cha mashariki chenye urefu wa mita 5,621 (ft 18,442 ).

Mtu wa kwanza kupanda Kilele cha mashariki kwa mara ya kwanza ilikuwa ni tarehe 10 Julai 1829 na mtu aliyepanda alitwa Khillar Khachirov, na kilele cha magharibi ulipandwa kwa mara ya kwanza mwaka 1874 na msafara wa Uingereza ulioongozwa na F. Crauford Grove akiwa pamoja na Frederick Gardner, Horace Walker na mwongozo wa Uswizi Peter Knubel.

6 Pico Cristóbal Colón.

Mlima Pico Cristóbal Colón ndio mlima mrefu zaidi nchini Kolombia, unaokadiriwa kuwa na urefu wa mita 5,700 (futi 18,700).

Mlima huu umepewa jina kurejelea jina la Christopher Columbus, mtu wa kwanza kutoka ulaya kufika bara la America ya kusini.

Mlima huu ulipandwa kwa mara ya kwanza mwaka 1939 na bwana W. Wood, A. Bakerwell na bwana E. Praolini.

Hata hivyo kwa miaka mingi ufikiaji wa milima huu ulikua mgumu sana kutokana na machafuko ya wenyeji wenye uhasama, walanguzi wa dawa za kulevya na waasi FARC.

Kufatia hilo safari nyingi zilizuiliwa kwa upandaji wa mlima huo mpaka mwaka 2015 pale Safari iliyoongozwa na bwana John Biggar ilikuwa mojawapo ya safari za kwanza kupanda katika mlima huo kwa miaka mingi, na alifanikiwa kufika kilele cha Pico Colón tarehe 13 Desemba.

5 Mlima Logan.

Mlima Logan ndio mlima mrefu zaidi nchini Kanada na kilele cha pili kwa urefu Amerika Kaskazini, baada ya Mlima McKinley (Denali).

Mlima huu ulipewa jina kutoka kwa Sir William Edmond Logan, mwanajiolojia MCanada na mwanzilishi wa taasisi ya Geological Survey of Canada (GSC).

Mlima Logan uko ndani ya Hifadhi ya Kitaifa ya Kluane, na Upandaji wake ulifanyika mwaka 1925 kwa mara ya kwanza, mtu wa kwanza kupanda alikuwa ni bwana A.H. MacCarthy.

Mlima Logan una urefu wa mita 5,959 (19,551 ft).

4 Mlima Kilimanjaro.

Mlima Kilimanjaro, pamoja na safu zake tatu za volkeno za Kibo, Mawenzi na Shira ndio mlima mrefu zaidi Afrika.

Pia mlima Kilimanjaro ndio Mlima mrefu kuliko yote duniani uliosimama peke yake "unaojitegemea" (Single Free standing).

Mlima Kilimanjaro una urefu wa mita 5,895 (19,341 futi) juu ya usawa wa bahari na karibu mita 4,900 (16,100 ft) juu ya msingi wake wa miinuko.

Mlima Kilimanjaro ni mlima wa nne kwa urefu duniani na wa kwanza kwa urefu Afrika, ndio mlima pekee duniani uliopo ukanda wa Tropical wenye theruji mwaka mzima kwa vipindi vyote.

Mlima Kilimanjaro uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo unaweza kufikika kupitia njia za wilaya ya Rombo, Hai na Moshi.

Kilele cha Kibo kina urefu wa futi 19,340 (mita 5,895) ambacho ndio killele kilefu katika mlima Kilimanjaro.

Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), ilianzishwa mwaka 1973 pia mlima Kilimanjaro uliteuliwa kuwa eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO mwaka 1987.

Kijiolojia Kilimanjaro ni mlima wa volkeno iliyolala (dormant volcano).

Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani.

Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani, Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

3 Mlima McKinley.

Mlima McKinley, au Denali (Koyukon Athabaskan yani "The High One"), Mlima huu huko katika eneo la Alaska, Alaska ni jimbo la Marekani hivyo mlima huu upo Marekani, ndio mlima mrefu na kilele cha juu zaidi nchini Marekani na bara la Amerika Kaskazini.

Mlima huu una urefu wa mwinuko wa futi 20,320 (sawa na mita 6,194) juu ya usawa wa bahari.

Kihistoria, watu wa jamii ya Koyukon walioishi eneo karibu na mlima waliuita mlima huo jina la "Denali" kwa karne nyingi.

Lakini mnamo mwaka 1896, mlima ulibadilishwa jina na kuita "mlima McKinley" kurejelea jina la rais wa Marekani wakati huo bwana William McKinley, jina hilo baadae lilikuwa jina rasmi lilotambuliwa na serikali ya shirikisho la Marekani kuanzia mwaka 1917 hadi 2015.

Lakini mnamo Agosti 2015, miaka 40 baada ya jimbo la Alaska kutaka mabadiliko ya majina ya asili maeneo yake, wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani ilikubali Mabadiliko ya mlima huo na ilitangaza kubadilishwa kwa jina rasmi la mlima huo kuwa mlima Denali.

Mwaka 1903, James Wickersham alirekodi jaribio la kwanza la kupanda mlima Denali, ambapo hata hivyo halikufaulu kufika kileleni.

Mwaka 1906, Frederick Cook alijaribu kupanda mlima Denali, lakini upandaji wake mlima haujathibitishwa na uhalali wake kufika kileleni unatiliwa shaka.

Watu wa kwanza wanaotajwa kufika kilele cha mlima Denali na Upandaji wao kuthibitishwa ilikuwa ni mnamo Juni 7, 1913, na wapanda mlima hao walikuwa ni Hudson Stuck, Harry Karstens, Walter Harper, na Robert Tatum, ambao walipitia njia ya Kusini (south corridor).

2 Aconcagua.

Mlima Aconcagua ndio mlima mrefu zaidi barani Amerika wenye urefu wa mita 6,960.8 (futi 22,837.3).

Mlima huu upo katika safu ya milima ya Andes, katika mkoa wa Mendoza, nchini Argentina, na mlima huu upo kilomita 112 (70 mile) magharibi kaskazini mwa jiji la Mendoza.

Kama nilivyosema hapo juu kuwa huu ndio mlima mrefu zaidi katika bara la Amerika, na ndio mlima mrefu duniani nje ya bara la Asia.

Pia ndio mlima mrefu ulio juu zaidi ulio Kusini mwa dunia (south hemisphere) ambao una mwinuko wa mita 6,961 (ft 22,838 ), unaoufanya kuwa Mlima wenye Kilele kirefu cha pili duniani.

Mwaka 1897 bwana Matthias Zurbriggen aliweka rekozdi ya kuwa mtu wa kwanza Kukwea na kupanda mlima Aconcagua.

1 Mlima Everest/Qomolangma.

Mlima Everest au Qomolangma ndio mlima mrefu zaidi duniani, wenye kilele cha mita 8,848 (sawa na 29,029 ft) juu ya usawa wa bahari.

Mlima huu upo katika sehemu ya safu za milima Mahalangur katika safu kuu ya milima ya Himalaya.

Mlima huu upo katikati ya mpaka wa nchi ya China na Nepal, hivyo mpaka wa kimataifa kati ya China na Nepal umepita katikati ya Mlima Everest ambao unatenganisha nchi mbili za Nepal na jimbo la Tibet lililopo ndani ya nchi ya China.

Kwa matiki hiyo Mlima huu upo chini ya umiliki na usimamizi wa nchi mbili za Nepal na China.

Mlima Everest huvutia wapandaji wengi, kutia ndani wapanda milima wenye uzoefu mkubwa, Kuna njia kuu mbili za kupanda mlima Everest, moja ni ile inayopitia kutoka kusini mashariki mwa Nepal (inayojulikana kama "njia ya kawaida") na nyingine kutoka kaskazini mwa jimbo la Tibet.

Hata hivyo mlima Everest una hatari kubwa Katika upandaji wake kulinganisha na Milima mingine duniani, kwani mlima Everest una hatari ya hali ya hewa na upepo mkali, hatari zinazotokana na maporomoko ya theluji pamoja na miamba na mashimo ya theruji.

Mwaka 2019, zaidi ya watu 300 walipoteza maisha kwenye mlima Everest, wengi wao miili yao imesalia mlimani kutokana na mazingira magumu kuondoa miili yao huko.

Jina lasmi la Mlima Everest ni mlima Qomalangma, jina hili ni jina kutoka lugha ya Kitibeti, jina hili Qomolangma humanisha ("Mama Mtakatifu").

Jina la Qomalangma lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye maandishi ya Kichina kwenye Atlasi ya Kangxi ya mwaka 1721 wakati wa utawala wa Mfalme Kangxi wa nasaba ya himaya ya Qing Uchina, na kisha jina hilo likaonekana tena huko kwenye makumbusho ya Tchoumour Lancma kwenye ramani ya mwaka 1733 iliyochapishwa huko Paris na mwanajiografia Mfaransa D'Anville.

Jina hilo liliidhinishwa rasmi kama jina rasmi na serikali ya Jamuhuri ya Watu China Mei 1952, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uchina ilitoa amri ya kupitisha jina Qomalangma kama jina pekee rasmi kuitambulisha mlima Everest.

Mnamo 1849, uchunguzi wa Uingereza kutafuta jina moja linalotukia sana ulianza kufanyika chini ya Andrew Waugh, Mtafiti Mkuu wa Uingereza nchini India.

Bwana Waugh alianza utafiti huo wa kutafuta jina au kupata jina lolote linalotumiwa sana, ili aweze kupata jina la eneo hilo, Ilimpa shida sana kutokana na Nepal na Tibet kuwatenga wageni kufika eneo hilo.

Waugh akahitimisha kwa kusema kuwa kwa sababu kulikuwa na majina mengi ya kienyeji kutambulisha mlima huo, itakuwa vigumu kupendelea jina moja juu ya mengine yote, mfano China (Tibet) huita mlima huo Qomalangma huku Nepal huuita Sagarmāthā pia kusini mwa Tibet huita Mlima Deodungha.

Kwasababu hiyo Waugh akaamua mlima huo huitwe Mlima Everest kurejelea jina la mtafiti Mwingereza Sir George Everest, mtangulizi wake aliyekuwa Surveyor General of India.

China na Nepal walipinga jina lililopendekezwa na Waugh waliwasilisha mapingamizi yao mbele ya kamati ya Royal Geographical Society mnamo mwaka 1857 kwamba "Everest" haikuweza kuandikwa kwa Kihindi, Kinepal wala kichina wala kutamkwa na "wazaliwa wa India, Nepali wala China".

Jina lililopendekezwa la Waugh lilishinda licha ya pingamizi hizo, na mnamo 1865, Jumuiya ya Kijiografia ya Royal society ilipitisha rasmi jina la Mlima Everest kama jina rasmi la mlima mrefu zaidi duniani.

Hii ndio milima 10 mirefu duniani, ndio ncha za juu kabisa ulimwenguni, mlima Everest ndio baba wa milima yote ulimwenguni.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.
 
Attachments

  • FB_IMG_1654322875480.jpg
    FB_IMG_1654322875480.jpg
    130 KB · Views: 87
MILIMA 10 MIREFU DUNIANI; HIZI NDIO NCHA ZA JUU KABISA ULIMWENGUNI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Saturday-04/06/2022
Kilimanjaro National Park Marangu Mtoni, Kilimanjaro Tanzania

Jana niliweka andiko kuhusu mlima Kilimanjaro, Mlima wa nne kwa urefu duniani, tulipata maswali mengi kuhusu Mlima Kilimanjaro na wadau kutaka kujua milima mingine iliyo mbele ya mlima Kilimanjaro.

Imetupendeza leo hii nakuletea orodha ya milima 10 mirefu zaidi duniani, katika list hiyo bara la Afrika limetoa mlima mmoja tu ambao ni Mlima Kilimanjaro unaoshika nafasi ya 4 kati ya milima 10 mirefu duniani.

Yes, hizi ndio ncha za juu Kabisa ulimwenguni, mlima hii ndio vivutio vyenye upekee duniani, kwa bahati hiyo Tanzania imebahatika kuwa na ncha ya juu kabisa Afrika.

Hivyo basi ifuatayo ni orodha ya milima 10 mirefu duniani, tutaanza na namba 10 kushuka chini.

Ok, twende pamoja Sasa.....

10 Mlima Elbrus.

Mlima Elbrus ni mlima wa volkano tulivu (dormant volcano mountain) mlima huu upo katika safu ya milima ya Caucasus, huko ukanda wa Kabardino-Balkaria na Karachay-Cherkessia, nchini Urusi karibu na mpaka wa nchi ya Georgia.

Kilele chake ni cha juu zaidi katika safu ya milima ya Caucasus, na ndio kilele cha juu zaidi nchini Urusi.

Mlima Elbrus una urefu wa mita 5,642 (18,510 ft) juu ya usawa wa bahari, ni mlima wa asili ya volcano ulio juu zaidi katika Eurasia, yani ulaya na ukanda wa ulaya ya kati

Mlima Elbrus ina vilele viwili, vyote vikiwa ni volkeno tulivu (dormant volcano mountain), Kilele kirefu katika mlima Elbrus ni kile cha magharibi ambacho kina urefu wa mita 5,642 (18,510 ft).

Kilele cha pili ni kile cha mashariki chenye urefu wa mita 5,621 (ft 18,442 ).

Mtu wa kwanza kupanda Kilele cha mashariki kwa mara ya kwanza ilikuwa ni tarehe 10 Julai 1829 na mtu aliyepanda alitwa Khillar Khachirov, na kilele cha magharibi ulipandwa kwa mara ya kwanza mwaka 1874 na msafara wa Uingereza ulioongozwa na F. Crauford Grove akiwa pamoja na Frederick Gardner, Horace Walker na mwongozo wa Uswizi Peter Knubel.

9 Puncak Jaya.

Mlima Puncak Jaya au Piramidi ya Carstensz yenye urefu wa mita 4,884 ndio kilele cha juu kabisa cha Mlima Carstensz katika Safu ya Milima ya Sudirman ya nyanda za juu za kati magharibi mwa mkoa wa Papua, huko nchini Indonesia.

Mlima huu Puncak Jaya upo katika kisiwa cha New Guinea, huku mlima huo ukiwa na mwinuko wa 4,884 mita ( sawa na 16,024 ft).

Ndicho kilele cha mlima mrefu zaidi kilichopo katika kisiwa Duniani.

Mtu wa Kwanza kupanda mlima huu alikuwa ni Colijn, Dozy, na Wissels mwaka 1936, kisha wakafatia wengine mwaka 1962 ambao ni Harrer, Temple, Kippax, na Huizenga

8 Vinson Massif.

Mlima Vinson Massif ndio mlima mrefu zaidi katika bara la Antaktika, ukiwa katika safu ya milima ya Sentinel, na safu ya Milima ya Ellsworth, ambayo yote kwa pamoja inasimama juu ya Rafu ya Barafu ya Ronne karibu na usawa aridhi wa Peninsula ya Antaktika.

Mlima Vinson Massif aligunduliwa mwaka 1958 na ndege ya Jeshi la Wanamaji wa Marekani, Mnamo January 1961, jina la Vinson Massif ulipewa na Kamati ya utafiti ya Marekani inayojihusisha na utafiti huko Antaktika inayoitwa US-ACAN.

Jina hilo la Vinson Massif limetokana na jina la mbunge wa Marekani kutoka jimbo la Georgia bwana Carl G. Vinson, ambae ndie aliyetoa msaada wa utafiti huko Antarctic.

Mlima Vinson Massif una urefu wa mita 4,892 sawa na futi 16,050.

Mlima huo ulipandwa mwaka 1966 na bwana Nicholas Clinch, ndio mtu wa kwanza kupanda Kilele cha mlima huo.

7 Pico de Orizaba.

Mlima Pico de Orizaba, au Citlaltépetl, ni mlima wa stratovolcano, ndio mlima mrefu zaidi nchini Mexico, na mlima wa tatu kwa urefu Amerika Kaskazini.

Una urefu wa mita 5,636 (futi 18,491), mlima huu upo kwenye mpaka kati ya majimbo ya Veracruz na Puebla.

Mlima Pico de Orizaba, ni mlima wa Volcano iliyo tulivu, mlipuko wa mwisho unatajwa kutokea katika karne ya 19.

Pico de Orizaba ni kilele cha pili maarufu cha volkeno duniani baada ya Mlima Kilimanjaro uliopo Afrika, nchini Tanzania.

Upandaji wake ulifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1848 na bwana F. Maynard pamoja na bwana William F. Raynolds.

6 Mlima Logan.

Mlima Logan ndio mlima mrefu zaidi nchini Kanada na kilele cha pili kwa urefu Amerika Kaskazini, baada ya Mlima McKinley (Denali).

Mlima huu ulipewa jina kutoka kwa Sir William Edmond Logan, mwanajiolojia MCanada na mwanzilishi wa taasisi ya Geological Survey of Canada (GSC).

Mlima Logan uko ndani ya Hifadhi ya Kitaifa ya Kluane, na Upandaji wake ulifanyika mwaka 1925 kwa mara ya kwanza, mtu wa kwanza kupanda alikuwa ni bwana A.H. MacCarthy.

Mlima Logan una urefu wa mita 5,959 (19,551 ft).

5 Pico Cristóbal Colón.

Mlima Pico Cristóbal Colón ndio mlima mrefu zaidi nchini Kolombia, unaokadiriwa kuwa na urefu wa mita 5,700 (futi 18,700).

Mlima huu umepewa jina kurejelea jina la Christopher Columbus, mtu wa kwanza kutoka ulaya kufika bara la America ya kusini.

Mlima huu ulipandwa kwa mara ya kwanza mwaka 1939 na bwana W. Wood, A. Bakerwell na bwana E. Praolini.

Hata hivyo kwa miaka mingi ufikiaji wa milima huu ulikua mgumu sana kutokana na machafuko ya wenyeji wenye uhasama, walanguzi wa dawa za kulevya na waasi FARC.

Kufatia hilo safari nyingi zilizuiliwa kwa upandaji wa mlima huo mpaka mwaka 2015 pale Safari iliyoongozwa na bwana John Biggar ilikuwa mojawapo ya safari za kwanza kupanda katika mlima huo kwa miaka mingi, na alifanikiwa kufika kilele cha Pico Colón tarehe 13 Desemba.

4 Mlima Kilimanjaro.

Mlima Kilimanjaro, pamoja na safu zake tatu za volkeno za Kibo, Mawenzi na Shira ndio mlima mrefu zaidi Afrika.

Pia mlima Kilimanjaro ndio Mlima mrefu kuliko yote duniani uliosimama peke yake "unaojitegemea" (Single Free standing).

Mlima Kilimanjaro una urefu wa mita 5,895 (19,341 futi) juu ya usawa wa bahari na karibu mita 4,900 (16,100 ft) juu ya msingi wake wa miinuko.

Mlima Kilimanjaro ni mlima wa nne kwa urefu duniani na wa kwanza kwa urefu Afrika, ndio mlima pekee duniani uliopo ukanda wa Tropical wenye theruji mwaka mzima kwa vipindi vyote.

Mlima Kilimanjaro uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo unaweza kufikika kupitia njia za wilaya ya Rombo, Hai na Moshi.

Kilele cha Kibo kina urefu wa futi 19,340 (mita 5,895) ambacho ndio killele kilefu katika mlima Kilimanjaro.

Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), ilianzishwa mwaka 1973 pia mlima Kilimanjaro uliteuliwa kuwa eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO mwaka 1987.

Kijiolojia Kilimanjaro ni mlima wa volkeno iliyolala (dormant volcano).

Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani.

Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani, Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

3 Mlima McKinley.

Mlima McKinley, au Denali (Koyukon Athabaskan yani "The High One"), Mlima huu huko katika eneo la Alaska, Alaska ni jimbo la Marekani hivyo mlima huu upo Marekani, ndio mlima mrefu na kilele cha juu zaidi nchini Marekani na bara la Amerika Kaskazini.

Mlima huu una urefu wa mwinuko wa futi 20,320 (sawa na mita 6,194) juu ya usawa wa bahari.

Kihistoria, watu wa jamii ya Koyukon walioishi eneo karibu na mlima waliuita mlima huo jina la "Denali" kwa karne nyingi.

Lakini mnamo mwaka 1896, mlima ulibadilishwa jina na kuita "mlima McKinley" kurejelea jina la rais wa Marekani wakati huo bwana William McKinley, jina hilo baadae lilikuwa jina rasmi lilotambuliwa na serikali ya shirikisho la Marekani kuanzia mwaka 1917 hadi 2015.

Lakini mnamo Agosti 2015, miaka 40 baada ya jimbo la Alaska kutaka mabadiliko ya majina ya asili maeneo yake, wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani ilikubali Mabadiliko ya mlima huo na ilitangaza kubadilishwa kwa jina rasmi la mlima huo kuwa mlima Denali.

Mwaka 1903, James Wickersham alirekodi jaribio la kwanza la kupanda mlima Denali, ambapo hata hivyo halikufaulu kufika kileleni.

Mwaka 1906, Frederick Cook alijaribu kupanda mlima Denali, lakini upandaji wake mlima haujathibitishwa na uhalali wake kufika kileleni unatiliwa shaka.

Watu wa kwanza wanaotajwa kufika kilele cha mlima Denali na Upandaji wao kuthibitishwa ilikuwa ni mnamo Juni 7, 1913, na wapanda mlima hao walikuwa ni Hudson Stuck, Harry Karstens, Walter Harper, na Robert Tatum, ambao walipitia njia ya Kusini (south corridor).

2 Aconcagua.

Mlima Aconcagua ndio mlima mrefu zaidi barani Amerika wenye urefu wa mita 6,960.8 (futi 22,837.3).

Mlima huu upo katika safu ya milima ya Andes, katika mkoa wa Mendoza, nchini Argentina, na mlima huu upo kilomita 112 (70 mile) magharibi kaskazini mwa jiji la Mendoza.

Kama nilivyosema hapo juu kuwa huu ndio mlima mrefu zaidi katika bara la Amerika, na ndio mlima mrefu duniani nje ya bara la Asia.

Pia ndio mlima mrefu ulio juu zaidi ulio Kusini mwa dunia (south hemisphere) ambao una mwinuko wa mita 6,961 (ft 22,838 ), unaoufanya kuwa Mlima wenye Kilele kirefu cha pili duniani.

Mwaka 1897 bwana Matthias Zurbriggen aliweka rekozdi ya kuwa mtu wa kwanza Kukwea na kupanda mlima Aconcagua.

1 Mlima Everest/Qomolangma.

Mlima Everest au Qomolangma ndio mlima mrefu zaidi duniani, wenye kilele cha mita 8,848 (sawa na 29,029 ft) juu ya usawa wa bahari.

Mlima huu upo katika sehemu ya safu za milima Mahalangur katika safu kuu ya milima ya Himalaya.

Mlima huu upo katikati ya mpaka wa nchi ya China na Nepal, hivyo mpaka wa kimataifa kati ya China na Nepal umepita katikati ya Mlima Everest ambao unatenganisha nchi mbili za Nepal na jimbo la Tibet lililopo ndani ya nchi ya China.

Kwa matiki hiyo Mlima huu upo chini ya umiliki na usimamizi wa nchi mbili za Nepal na China.

Mlima Everest huvutia wapandaji wengi, kutia ndani wapanda milima wenye uzoefu mkubwa, Kuna njia kuu mbili za kupanda mlima Everest, moja ni ile inayopitia kutoka kusini mashariki mwa Nepal (inayojulikana kama "njia ya kawaida") na nyingine kutoka kaskazini mwa jimbo la Tibet.

Hata hivyo mlima Everest una hatari kubwa Katika upandaji wake kulinganisha na Milima mingine duniani, kwani mlima Everest una hatari ya hali ya hewa na upepo mkali, hatari zinazotokana na maporomoko ya theluji pamoja na miamba na mashimo ya theruji.

Mwaka 2019, zaidi ya watu 300 walipoteza maisha kwenye mlima Everest, wengi wao miili yao imesalia mlimani kutokana na mazingira magumu kuondoa miili yao huko.

Jina lasmi la Mlima Everest ni mlima Qomalangma, jina hili ni jina kutoka lugha ya Kitibeti, jina hili Qomolangma humanisha ("Mama Mtakatifu").

Jina la Qomalangma lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye maandishi ya Kichina kwenye Atlasi ya Kangxi ya mwaka 1721 wakati wa utawala wa Mfalme Kangxi wa nasaba ya himaya ya Qing Uchina, na kisha jina hilo likaonekana tena huko kwenye makumbusho ya Tchoumour Lancma kwenye ramani ya mwaka 1733 iliyochapishwa huko Paris na mwanajiografia Mfaransa D'Anville.

Jina hilo liliidhinishwa rasmi kama jina rasmi na serikali ya Jamuhuri ya Watu China Mei 1952, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uchina ilitoa amri ya kupitisha jina Qomalangma kama jina pekee rasmi kuitambulisha mlima Everest.

Mnamo 1849, uchunguzi wa Uingereza kutafuta jina moja linalotukia sana ulianza kufanyika chini ya Andrew Waugh, Mtafiti Mkuu wa Uingereza nchini India.

Bwana Waugh alianza utafiti huo wa kutafuta jina au kupata jina lolote linalotumiwa sana, ili aweze kupata jina la eneo hilo, Ilimpa shida sana kutokana na Nepal na Tibet kuwatenga wageni kufika eneo hilo.

Waugh akahitimisha kwa kusema kuwa kwa sababu kulikuwa na majina mengi ya kienyeji kutambulisha mlima huo, itakuwa vigumu kupendelea jina moja juu ya mengine yote, mfano China (Tibet) huita mlima huo Qomalangma huku Nepal huuita Sagarmāthā pia kusini mwa Tibet huita Mlima Deodungha.

Kwasababu hiyo Waugh akaamua mlima huo huitwe Mlima Everest kurejelea jina la mtafiti Mwingereza Sir George Everest, mtangulizi wake aliyekuwa Surveyor General of India.

China na Nepal walipinga jina lililopendekezwa na Waugh waliwasilisha mapingamizi yao mbele ya kamati ya Royal Geographical Society mnamo mwaka 1857 kwamba "Everest" haikuweza kuandikwa kwa Kihindi, Kinepal wala kichina wala kutamkwa na "wazaliwa wa India, Nepali wala China".

Jina lililopendekezwa la Waugh lilishinda licha ya pingamizi hizo, na mnamo 1865, Jumuiya ya Kijiografia ya Royal society ilipitisha rasmi jina la Mlima Everest kama jina rasmi la mlima mrefu zaidi duniani.

Hii ndio milima 10 mirefu duniani, ndio ncha za juu kabisa ulimwenguni, mlima Everest ndio baba wa milima yote ulimwenguni.

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 2250320View attachment 2250323View attachment 2250321View attachment 2250322View attachment 2250325View attachment 2250324View attachment 2250328View attachment 2250326View attachment 2250327
Table mountain, kumbe ujinga mtupu
 
Ni kipengele cha "above sea level" ndio kinafanya Mount Everest kuitwa mlima mrefu
Lakini kama unaongezea neno "duniani", Mount Mauna Kea ndio mlima mrefu duniani....

Vinson Masif kwenye atlas kipindi hicho mbona nakumbuka niliona ina mita nyingi kuliko Kilimanjaro?

Halafu huo namba tano mbona una mita nyingi kuliko namba nne kwanini iwe hivyo ilivyo?
 
Siyo kweli mlima Kilimanjaro ni wa 29 kwa urefu duniani siyo wa nne kama ulivyoonyesha, ni wa kwanza katika Afrika.
Sijui ni wa ngapi ila siku moja nilikuta mamilima mengi sana yenye urefu kuliko Kilimanjaro sasa huwa sielewi hii kusema namba 4 ni takwimu inayotokaga wapi
 
Back
Top Bottom