Vote for Mount Kilimanjaro to become among new 7 wonders

Status
Not open for further replies.

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
WATANZANIA waliopo ndani na nje ya nchi wametakiwa kuonesha uzalendo na kushirikiana kwa pamoja kuupigia kura Mlima Kilimanjaro ili kuhakikisha unashinda na kuwa moja ya maajabu mapya saba ya dunia.

Mwito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Save Mt. Kilimanjaro, Ernest Olotu ambao ndiyo mwakilishi wa kamati ya dunia katika kutafuta maajabu mapya saba ya dunia.

Amesema, Julai 2007 jijini Lisbon,Ureno kulifanyika uzinduzi rasmi wa kutafuta maajabu saba mapya ya asili mpango ambao uliratibiwa na New Open World Co-operation(NOWC) chini ya taasisi isiyo kuwa ya kiserikali ya New 7 Wonders.

Amesema, taasisi hiyo ilitafuta vitu vya asili vinavyoweza kuwa maajabu mapya ya dunia katika nchi 220 duniani, ikiwemo Tanzania na kupata vitu zaidi ya 440 vya kushindanisha ili kupata maajabu saba mapya ya asili mbali na ya zamani.

Olotu amesema, katika mchujo wa kwanza vilibakia vitu 77, ambapo Julai 2009 kamati ya wataalamu ilikaa tena na kupitisha mchujo mwingine wakabaki washiriki 28 ambapo katika Afrika, nchi mbili ziliingia katika shindano hilo ikiwemo Tanzania (Mlima Kilimanjaro) na Afrika Kusini (Milima Meza).

Amesema, tangu 2009 kazi ya kupiga kura imekuwa ikiendelea duniani kupitia mtandao hadi Novemba 11 mwaka huu ambayondiyo itakuwa mwisho wa kutangaza rasmi maajabu hayo mapya.

"Cha kusikitisha mlima Kilimanjaro umekuwa ukipigiwa kura kwa wingi na wageni ambao sio Watanzania, walioufahamu mlima huu kwa kupitia vyombo vya habari, mtandao au waliowahi kuupanda¡ ni jukumu letu sasa Watanzania bila kujali itikadi zetu ,dini, rangi wala kabila kuupigia kura mlima huu," amesema.

Amesema, watu wanaweza kuingia kwenye tovuti ya www.new7wonders.com na kuupigia kura mlima huo pamojana maajabu mengine yatakayofanya yatimie saba...

(FROM HABARI LEO)... Mimi nimeshaupigia kura..bado wewe tu! Ni rahisi kuupigia kura. Tuonyeshe uzalendo! Asanteni!
 
hata tukiipa kura tatizo utawanufaisha mafisadi tu acha tuendelee kukaa hivyo hivyo. utalii wenyewe wala hatuna manufaa nao zaidi ya kenye ndo wanatumia kutangaza utalii kwao sisi huku viongozi wetu wanafikiria kwa kutumia masaburi
 
Nimeahirisha kujenga taifa badala yake napigania upya taifa langu Tanzania
 
Ili ubinafusishwe kama wonders nyingine. Wakenya wataupigia msiwe na wasiwasi. Ukiona mwizi anakufata mara nyingi punguza vivutio ili asipate cha kuiba.
 
Asante sana mkuu. Nadhani hii dhana ya kuchukia maendeleo ya nchi yetu kwa kuwasingizia mafisadi ni potofu na inabidi ifutike. Mimi nimepiga kura yangu
hongera sana... Mkuu umefanya vizuri. Lazima tuitetee nchi yetu.
 
Hebu tuwe na akili, tuache ujinga..! Wewe kwa akili zako unajamba then unajifunika shuka..unafikiri unamkomoa nani? Wakati harufu ya ushuz wako unaipata mwenyewe! Kura zimepigwa na watu ambao sio watanzania, halafu ww mtanzania unaona kuwa ni ujinga! Acheni hizo, kuwa mzalendo. Tuupigie kura..we unafikiri ngorongoro bila kuwekwa katika 7 wonderz ingefanyiwa reserves? Mimi ninapigania nchi yangu kwa kuwa mfano wa kuigwa! Tumkumbuke Nyerere na maneno yake! MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU IBARIKI AFRICA!
 
Haya mambo mengine ni upuuzi tu au mbinu za kibiashara za hayo ma NGO, kwani hizo kura tukipiga zinakwenda pale Moshi kuongeza kitu kwenye huo mlima, kura haziwezi kuubadilisha mlima, mlima upo hivyo na sifa zake wakitaka wautambue au wasiutambue ila ukweli ni kuwa Kilimanjaro ni maajabu ya dunia. Badala kuyaambia mazungu yaache kuharibu mazingira na maviwanda yao ili kulinda barafu iliyopo pale juu tunakaa kujidanganya kupiga kura ili wazungu wauweke kwenye maajabu ya kijinga. Shenzi sana.
 
hata tukiipa kura tatizo utawanufaisha mafisadi tu acha tuendelee kukaa hivyo hivyo. utalii wenyewe wala hatuna manufaa nao zaidi ya kenye ndo wanatumia kutangaza utalii kwao sisi huku viongozi wetu wanafikiria kwa kutumia masaburi

hizo ni akili potofu na zinaonyesha jinsi gani unashindwa kufikiria hata kwa akili ya kuzaliwa. Mkuu, tafuta mawazo za maana zaidi! Hata mtoto wa primary aliyesoma hawezi kuwa na mawazo hayo.
 
Haya mambo mengine ni upuuzi tu au mbinu za kibiashara za hayo ma NGO, kwani hizo kura tukipiga zinakwenda pale Moshi kuongeza kitu kwenye huo mlima, kura haziwezi kuubadilisha mlima, mlima upo hivyo na sifa zake wakitaka wautambue au wasiutambue ila ukweli ni kuwa Kilimanjaro ni maajabu ya dunia. Badala kuyaambia mazungu yaache kuharibu mazingira na maviwanda yao ili kulinda barafu iliyopo pale juu tunakaa kujidanganya kupiga kura ili wazungu wauweke kwenye maajabu ya kijinga. Shenzi sana.
tatizo ni kuriri...Yaani unataka kuniambia kuwa haujui manufaa yoyote ya kuwekwa ktk 7WW? angalia maeneo yote yaliyopo katika 7WW, yapo ktk uangalizi mzuri wa kuyahifadh kuliko maeneo mengine duniani! Eg ngorongoro! Bila kuwa ktk 7WW isingekuwa chini ya uangalizi mzuri. Hebu tuwe wachambuzi wazuri.
 
Tuache kusema mafisadi mafisadi! Hata ww unaweza kuwa fisadi either indirect or direct...! Wewe kama mtanzania, play ur roles as a Tanzanian! Usifikiri kuna mtu atakusaidia kujenga nchi yako kama ww hujitumi!
 
Watanzania umefika wakati tuanze kuitangaza nchi yetu. Hongereni sana kamati ya SAVE MT.KILIMANJARO. Tukiwa hivi tutawaacha wakenya mbali sana.
 
Tupige kura ili tupate watalii wengi wakubwa wa inji hii waendelee kujiSHIMBO!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom