Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom njooni muwekeze wilayani mbogwe kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo nyakafulu tunapata shida sana ya mawasiliano kupiga simu mpka tupande kwenye mti Kuna wakazi zaidi ya elfu 10 hakuna internet minala iko mbali sana tusaidieni huduma
 
TUSUA SPOTI..mchezo wa kubahatisha unao endeshwa KITAPELI.

Nasema kitapeli sababu ya kwamba mnatumia maneno ya kilaghai kwa mteja huku mkijua kabisa sivyo ilivyo huo ni wizi.

Mfano ukisema watu washindane kukimbia na mshind wa kwanza ata jishindia elfu 60 mfano alafu,asa mtu akimbie na baada ya kua wa kwanza ndio muongeze neno jipya na sheria nyingin ala mtu ajikute amekua wa kwana na asipate zawadi yoyote huo ni ulaghai ( UTAPELI ).

Maelezo ya tusua spoti yanasema.
"Unatakiwa kuchagua majibu sahihi kwa haraka kwa kila mechi 14 zilizochezwa.Utashinda kama utajibu kwa usahihi maswali 6 au 7 ya kwanza,au maswali 11,12,12 au 14 utakayopokea.kiasi cha Tsh.50,000,000 kutolewa kila siku."

Tuachane na izo million kadha ambazo mnasema mnatoa kila siku.ila tayari mmesha ahidi kua utashinda ata ukipatia majibu 6 tu ya mwazo utashinda sio utaweza kushinda ni utashinda ndivyo maelezo ya navyo sema.

Ukishiriki tu bahati nasibu hii unapata meseji nyingine inasema hivi.

"WASHINDI DROO YA SAA wa leo wenye majibu sahihi 14 watapata kiwango cha chini Tsh 50,000 na 13: Tsh10,000 na 12: Tsh2,500 & 11: Tsh 500!

Endelea kucheza ushinde zawadi kabambe!"

Yani ayo maelezo yako wazi washindi wenye majibu 14 sahihi wata pata kiwango cha chini Tsh.50,000.ya ni maana yake wote watapata maana maelezo ayajasema atapata, bali watapata ata kama wako 10.na sio chini ya elfu 50.ndivyo maelezo ya navyoeleza.

Mimi nikashiriki mara kadha na nikafanikiwa kupatia mjibu yote ya mechi 14 nikapata msg hii.

"Umefanya vizuri!
Umejibu kwa usahihi maswali 14
Kwenye spoti slip kwa tiketi namba 15.
Utaingia kwenye droo saa 10:00:00 na washindi wote waliojibu maswali 14 kukomboa zawadi ya Tsh50,000"

Maelezo ya nasema ukipatia majibu 14 sahihi unapata elfu50 na apo pia mmesema washindi wote,na sio mmoja wao wote.na sio ataweza hapana ni wamekomboa nini maana ya kukomboa yani ni kama kitu akikua chako au ulikiweka lehani sasa umekikomboa yani kimekua chako..kwa maelezo hayo nikwamba ata mkichezesha iyo droo na sijafanikiwa kupata ayo ma million tayari mimi nimekomboa Tsh50,000 kama maelezo yenu yote ya navyo sema aijalish tupo wangapi mmesema wote.

Asa nashindwa kuelewa baada ya hiyo droo naambiwa tiketi inayo fata ni bure umeshinda Tsh500 isiyo hamishika ila unaweza ichezea tiketi inayofata yani iyo Tsh500 siwez ata ichukua mana yake nimepatia mechi zote 14 na nimeambulia tiketi ya bure wakati nilihakikishiwa elfu50.naiyo tsh500 ni anastahili apatiwe yule aliye patia mechi 11 tu kwa mujibu wa maelezo yenu kuhusu mchezo huu.

Alafu cha ajabu zaidi ata iyo tiketi ya bure siwezi cheza maana mmeniwekea Tsh 425. Na tiketi ni Tsh 500. Huku kiwango cha chini kuweka ela kutoka mpesa ni Tsh1000 manayake akuna na mna yoyote naweza itumia iyo Tsh 425.

Kwaiy kwa sasa mimi nawadai Tsh50,000 kwakupatia majibu sahihi 14 kwenye spoti slip id15.

Kama mtabadiri sheria za mchezo na maelezo mbadiri ila mkishanipatia zawadi yangu niliyoshinda
 
Nipe maelezo ya makato haya
IMG-20210904-WA0000.jpg
 
Voda com ...mtandao wenu ni wakidua sana ...aiwezekani mteja ana emegency anawapigia simu harafu mnaweka ki voice note cha kipuuzi ....eti "Kwa kingereza bonya 1 kwa kwa huduma nyingine za kiswahili subiri"harafu ukisubiri " mnajibu tumeshindwa kutambua chaguo lako" huu si upuuzi kabisa.

Nimetuma hela tangu saa sita kwenda Halopesa mpaka sasa mtu hajapata fedha tena yupo hospitali kwa ajili ya matibabu hazijafika mpaka sasa saa 21:46 pm.....Harafu ampokei simu? Mseme basi kama customer care yetu huwa mnafanya mwisho ijumaa tu weekend huwa mnaenda Samaki samaki ili tuelewe tutafute mitandao inayotoa huduma 24/7
 
Harafu voda com ....nimekuwa nikifatilia salio kwenye simu yangu nikiweka salio mfano 2000 harafu nikatuma sms 1 baada ya siku mbili nikiangalia tena salio na kuta limebaki 4.51 haya ni mambo ya ajabu kabisa......sasa hivi naanza kutembea na daily na record kila nitapo weka salio na baada ya matumizi mnakwapua kimya kimya
 
Harafu voda com ....nimekuwa nikifatilia salio kwenye simu yangu nikiweka salio mfano 2000 harafu nikatuma sms 1 baada ya siku mbili nikiangalia tena salio na kuta limebaki 4.51 haya ni mambo ya ajabu kabisa......sasa hivi naanza kutembea na daily na record kila nitapo weka salio na baada ya matumizi mnakwapua kimya kimya
Wezi sana hawa jamaa dawa ni kupiga chini laini zao tunalalama kila siku hawajali kabisa
 
Kwema wandugu......naona leo nimepata sms kutoka m-pesa inasema tuma pesa bila makato, naomba wahusika waje waseme n kweli????
 
Hivi voda, mbn hamueleweki?? Mara leo vifurushi vinavyoeleweka, kesho mnapandisha! Kesho kutwa mnashusha! Mbona halotel wanasomeka na tuna lain zao za kudum?

Amueni moja mnapandisha vifurushi au mnashusha?? Tumechoka kuvunja na kusajili upya! Wengine ni wakurya bhana!! GB1 kwa buku mnarudisha au tupite hv!
 
Hivi kweli vodacom nikitaka kubadilishq password yangu ya mpesa sitoweza kutumia mpesa kwa muda wa siku saba

Mana nilikua najaribu kutuma pesa kutoka mpesa kwenda mitqndao mingine kila ikifika sehemu yq namba ya siri nikiingiza inakuja tena ingiza nqmbq ya siri, nikawapigia kuwauliza kulikoni mkanambia kua eti namba za siri zinapaswa kua nne tu sasa kwanza nawaukiza kwanini mliruhusu mwanzo niweke sita kqma mlikuq mnata nne
Pili nikiingia kwenye menu yangu kubadilisha password inakuja invalid PIN

Nawapigia ili nibadilishe password mmenijibu ikiwa nataka kubadilisha password zije nne ni lazima zipite siku saba bilq kutumia mpesa

Nasikitika kua shirika kama vodacoma mnamasoftware enginner vilaza kuahindwa solve issue ndogo kama hii ila wala msijali mana situmii tena mpesa yenu
 
Sema voda nyie mnatuibia na si tunawaibia yaani tuibiana,pesa mlizo nipa kwenye songesha na mpawa ,mupunguze simu na msg za vitisho ningewalipa mda sema utanzania wa kusubiri kitokee na hivyo vitisho ndo kAbisaa
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Habari vodacom nimefanya malipo kwa master card yetu nimakatwa pesa ila sijapatiwa huduma nilio lipia kwenye Skype yangu shida nini.?
 
Habari vodacom nimefanya malipo kwa master card yetu nimakatwa pesa ila sijapatiwa huduma nilio lipia kwenye Skype yangu shida nini.?
Naitwa Mtwale Daudi huduma hii nimekatwa pesa na sijapatiwa nilicho lipia. Vodacom naomba msaada wa kitaaramu kwenu

transactions: 1972021 M-Pesa Mastercard deducted TSH 20000.00 1572021 M-Pesa Mastercard deducted TSH 102000.00 972021 M-Pesa Mastercard loaded .
 
Back
Top Bottom