Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Naitwa Mtwale Daudi huduma hii nimekatwa pesa na sijapatiwa nilicho lipia. Vodacom naomba msaada wa kitaaramu kwenu .
transactions: 1972021 M-Pesa Mastercard deducted TSH 20000.00 1572021 M-Pesa Mastercard deducted TSH 102000.00 972021 M-Pesa Mastercard loaded .

Wasiliana na Skype apo boss ninachoona tatizo halipo Voda coz wao wameisha ruhusu malipo skype ni jukumu lako kuwatafuta skype sasa uhoji wamepokea pesa ila hawajatoa huduma
 
Habari,
Mbona hii visa card hairejeshi sms ya malipo baada ya kulipia kitu mtandaoni?

Alafu customer care tunawapataje?
Mnatupotezea muda sana wakati wa kutaka huduma!
 
Name:
Number: Vodacom
Content:
UPO TAYARI? Kesho tuna Jambo Letu, USIKOSE
Time: 02/12/2021 10:40:14
 
Vodacom siku hizi mbili internet yenu ina shida gani....mbona iko chini kupiliza yaani inapiga mpaka 0.0kb/s kweli wakati nyie ndo mko vizuri Kwa speed.

Tatizo ni nini????
 
Kuna shida kubwa sana,
Pindi unapotaka kuongea na mtoa huduma.

Kama huamini jaribu kuwapigia ili usikie hizo ngonjera zao.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

  • Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
  • Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
  • Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
  • Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
  • Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Mkuu mm ninashida na statement ya till yangu nimejaribu kutembelea voda shop wameniambia niwasiliane na wakala wangu mkuu ilhali simjui nimejaribu kutafuta mawasiliano naye aliye nitengenezea till amekuwa akinichenga sijui mnanisaidiaje kwa hilo
 
Habari waungwana,nataji msaada wa line yangu ya vodacom mpesa,line hii niliuziwa na mtu miaka mitatu sasa imepta ,aliniuzia nikaendelea kuitumia baada ya yeye kufunga bihashara ya huduma za kifedha,sasa aliama mkoa na sina mawasiliano yeyote nae ,sasa juz line yangu imegoma gafla kusoma,sasa nafanyaje ili niiswap wakat mm sina document yoyote ya usajil wa lin hii,naitaji msaada wenu,atanguliza shukuran
 
Leo nimeweka vocha za 1,000 mara tatu kwa mkupuo ilinijiunge kifurushi cha wiki 3,000 kuangalia salio nashangaa nakutana na 2,938 bila maelezo yoyote sijui hio 62 imepotelea wapi.

Nimeweka vocha data nimezima tu muda mrefu kwabla ya kuweka vocha, sajajiunga na huduma yoyote ambayo ingenikata pesa bila idhini yangu.

Kwakweli inasikitisha mtandao mkubwa kama huu kuwa na mambo ya kitapeli kiasi hiki.

Shame on you.
Screenshot_20220316-215704_Messages.jpg
 
Tuwekeeni GB10 kwa TZS 10000 kwa siku 30, na sisi tumudu kununua, sio sasa hadi simba na yanga wakicheza ndio nanunua kwa siku moja, tusaidieni tuwe online masaa mengi tujifunze vingi.
 
Ni namna gani naweza kununua hisa za Vodacom?
Ni Bei gani? Na Minimum inapaswa kuanza na hisa ngapi?
 
Waheshimiwa naombeni msaada,nimekwangua vocha vibaya nimeshindwa kuingiza baadhi ya number,nimejaribu kupiga Customer care sipati msaada ,nafanyaje ili niitumie hii vocha?
 
Back
Top Bottom