Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

VodaCom mmejisahau sana! Mtandao hata wa kutuma sms kwa baadhi ya maeneo ni hamna kabisa! Maeneo ya manyara barabara kutoka katesh kwenda kondoa(dodoma) ni hakuna kabisa mtandao lifanyieni kazi basi
 
Mbona hamjibu watu tunaibiwa helaa mna msaada gani sasa transaction inafanyika bila mtu kujua???
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
mnaonaje mkianzisha hudama za pesa mfano kununua dollar,euro n.k kupitia m pesa..?
 
Habarini wadau!
Nimeamua kuandika hii thread kupendwa kujuzwa na wadau kama vodacom ni wezi au la?

Nimekuwa natumiwa message kila siku ya tusua mapene ya kushinda milioni 100 kila siku na nimekuwa nikicheza mara kwa mara lakini sijawahi sikia mtu anashinda hiyo milioni 100 kila siku kama wanavyojitangaza.

Na kama hamna mshindi wa milioni 100 kila siku, huu si uongo wa kuvutia watu wacheza bahati nasibu huku wao wanakula tu hela. Au ndo kurecovery techniques baada ya kupata loss ya bilioni 350?

Naomba kuwasilisha.
 
Habarini wadau!
Nimeamua kuandika hii thread kupendwa kujuzwa na wadau kama vodacom ni wezi au la? Nimekuwa natumiwa message kila siku ya tusua mapene ya kushinda milioni 100 kila siku na nimekuwa nikicheza mara kwa mara lakini sijawahi sikia mtu anashinda hiyo milioni 100 kila siku kama wanavyojitangaza.
Na kama hamna mshindi wa milioni 100 kila siku, huu si uongo wa kuvutia watu wacheza bahati nasibu huku wao wanakula tu hela. Au ndo kurecovery techniques baada ya kupata loss ya bilioni 350?
Naomba kuwasilisha.
Inatia hofu maana hatujawahi kusikia hata mmoja aliyeshinda hiyo M100, pia hata hao wanaoshinda hizo ndogo wanaandika majina yao kwa mkato tu kwani wanaogopa nini kuyatangaza mbona tangazo la kushiriki wanalitoa kwanini wakwepe kutangaza washindi?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Jana saa kumi na mbili na dakika sita (12.06) nilijiunga kifurushi cha Yakwako Internet cha masaa 24, leo saa nane na dakika thelathini na tatu (8.33) wananitumia sms kwamba kifushi changu kimekwisha muda wake ( sio kimeisha kimatumizi), sasa huu si wizi na utapeli juu ya pesa yangu niliyonunulia kifurushi cha saa 24.

Na nimejaribu kuwasiliana na huduma kwa wateja, nako ushirikiano wao ni zero kabisa.

Yan aisee MB zangu zimenuima kweli!

Voda nyinyi hivi ni lini mtaacha huu wizi na utapeli + uhuni kibao??.
 
Hbari za leo niliishajitoa kwenye huduma ya kupokea matangazo kutoka vodacom kwa ujumbe wa maandishi. Nasikitika kupokea matangazo ya kamari inayoitwa mojabet.
 
Voda, hii tabia si nzuri. Kwa kawaida, huwezi kuingia kwenye huduma ya Sim-Banking kama huna salio la kawaida kwenye simu. Kwa sababu hiyo, sisi wateja wa huduma hiyo hulazimika kununua salio ili tupate huduma hiyo ya benki. Ajabu ni kuwa, ukinunua salio hata la Sh 3,000 baadaye ukaingia kuuliza salio kwenye akaunti yako ya CRDB, na kuishia hapo; zikishapita saa kadhaa ukitaka kupata huduma hiyo hiyo utaambiwa huna salio kwenye simu yako. Swali langu, hizo fedha zinazobaki hupotea kwa muujiza upi? Je, huu si wizi? Naomba majibu.

Manyerere
Hili swali linahitaji majibu ya kina, tena kwa haraka...
 
Back
Top Bottom