Aisee hamna kitu wananikera kama hicho,yaan nikiweka vocha labda niitumie yote kujiunga kitendo cha kujisahau dk 10 lazima wapite nayo,sijawahi kujiunga na hayo mahuduma yao ya PERUZI ila wananilazimishia kwa nguvu,nimeshawalalamikia lkn wap ila ipo siku tuu hili li line nitalitupa au niipumzishe kwanzaVoda mi nakaribia kuacha kutumia mtandao wenu. Kila niwekapo vocha asunuhi nakuta mmeramba. Juzi nimeweka 5000 nikatumia 3500. Iliobaki yote mkachukua. Eti nina huduma ya rafiķi chat. Nawakati mim sijajiunga kwenye ujinga huo. Nimeshawapigia mara kibao, hamtaki. Mmeshachukuw zaidi ya 10000. Nimesema ivi imetosha. Nikija kuibiw tena hata sh 100. Laini yenu natupa. Sitakuja tumia tena lain ya voda.
MATUMIZI MABAYA YA MUDA... SIKU MBILI KUSUBIRI HUDUMA KUSHUGHULIKIWA..Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania